LISEME JINA LANGU (6)

Zephiline F Ezekiel
0
Mwandishi: Pablo

SEHEMU YA SITA
Ilikuwa sauti ya moureen niliyosikia hakika nilivyochoka nilijikuta nikiikata simu hiyo kutokana na ukweli kwamba nilishajichokea na maisha lakini ile naikata tu messeji ikaingia kwa uvivu nikaiangalia na kukuta ni ile namba iliyonambia nisali sala zangu za mwisho na kunifanya moyo wangu tena uanze kudunda kwa kasi ya ajabu na kuchoka kabisa.kwa simanzi zito nikajikuta nikiifungua huku nikiwa na uoga kabisa wa kuisoma hiyo messeji iliyosomeka

SASA ENDELEA...
"PABLO PABLO,UNAVYOFIKIRIA UNAWEZA UKANIZIDI AKILI HATA MIMI SASA BASI NATAKA UCHAGUE MOJA KUUA WEWE AU SHANGAZI YAKO NA FAMILIA WASIO NA HATIA HAHAHAHA CHAGUO NI LAKO" hakika macho yangu hayakuweza kuamini messeji ile iliyotumwa niliendelea kuisoma kwa kuirudia kama mara kumi hivi huku akili yangu haukataka kuamini kabisa kwamba mtego uliobaki nilikuwa siponi kabisa.Kwa haraka haraka nikamlipa mwenye bajaj na kushuka kutokana na kufikia karibu na maeneo ya nyumbani kwa shangazi nilitembea kwa tahadhari kwa kujifificha mpaka pembezoni kabisa karibia na nyumba ya shangazi.
"Eee Mungu wangu!!!!"nilijikuta nikilalamika baada ya macho yangu kutua kabisa katika nyumba ya shangazi huku njee magari kumi meusi yakiwa yamepaki nje ya nyumba yake.nilijikuta nikikata shauri ya kwenda lakini kabla hata sijanyanyua kwato zangu Nilimshuhudia robertson Mugalula akitoka ndani ya nyumba ya shangazi akiwa anasindikizwa na bodyguard zake wakiwa wamemkamata shangazi na mumewe aliambatana na mtoto wake wa kiume na kuingizwa ndani ya moja kati ya magari yale kumi meusi kisha nikaona vumbi tu likitumika baada ya magari hayo kuondoka kwa kasi ya ajabu............

Hakika nilijikuta nikiganda kama mtu aliyepigwa shoti kali sana mwili wangu uliokuwa umelowa jasho ndio ulizidi kumiminika majasho ambayo licha yakuwa hali ya hewa ni ya kawaida isiyoleta joto lakini mimi nililowa mwili mzima.Hali ya kukamatwa kwa shangazi yangu na familia yake ilileta gumzo mtaani hapo ambapo hakuchukua hata nusu saa Majirani walijaa na kila mtu akiwa anasema lake.Akili katika kichwa changu haikuweza kusoma chochote kila njia nilikuwa nikiifikiria ya kuweza kujikwamua katika hili nilikuwa sipati jibu.Siku sita kutoa machozi aliyokuwa yakinitiririka katika mashavu yangu huku nikiwa siamini kabisa kama Mapenzi ndio yalikuwa tatizo.Nikiwa katika dimbwi zito la mawazo simu yangu ya mkononi ikaita tena na kuingalia nakukuta Jina la moureen likitokea katika screen ya simu yangu nilijitutumua na kuiweka sikioni kwa hali ya unyonge
"Hey upo wapi moureen"
"baby ulitoka salama ba.."
"upo wapi??"
"nipo njiani naelekea home"
"basi njoo mitaa ya nyumbani mara moja sasa hivi"
"mm lakini..."
"lakini nini do you love me..njoo mara moja"
"love you baby nakuja"nilijikuta nikihema baada ya kumaliza na moureen ambaye nilimuambie aje nyumbani.Akili yangu ilishavurugika nakukubali liwalo na liwe kichwa changu kilikuwa kishapata usumbuzi wa tatizo hilo huku mawazo ya kuwapata shangazi na familia yake ndio ilichukua nafasi yake.niliamini sitaweza kumpata shangazi yangu bila moureen.Haraka haraka nikaenda duka la madawa na kununua dawa ya usingizi kisha haraka haraka nikachukua bodaboda ambayo kwa haraka ikaweza kunifikisha Mtani kwetu ambapo sikuweza kwenda katika nyumba yangu niliyopanga kutokana na kuogopa kupatikana kirahisi na robert mugalula.nikaenda dukani na kununua maji ambayo nikaweka ile dawa ya usingizi kisha nikaenda sehemu ambayo nilimwambia moureen aje hapo.Macho yangu yakatua katika gari kali jeusi la moureen ambalo mara ya kwanza nilitaka kukimbia kwa kuangalia vibaya labda linaweza likawa la kundi la akina robert lakini kutokana na kumjua vizuri niliweza kumtambua kupitia kioo cha gari yake.bila ya kuchelewa moureen akafunga breki na kufungua mlango wa gari yake na kuniruhusu mimi kupanda nikaingia na ukaribisho wa mabusu mazito na moureen ambaye aliyeonekana kuumisi sana mchezo huo ambayo kwa wakati huo sikuwa na hamu nao.mkononi mwangu nilikuwa nimeshika chupa yangu ya maji ambayo kwa taratibu nikapa maji hayo moureen

"moureen unaonekana una kiu hebu kunywa maji haya kidogo"
"jamani umejuaje nipe"sikutaka kuchelewa nikayafungua yale maji yenye dawa ya usingizi nakumpa moureen ambaye kwa taratibu akaanza kunywa pole pole na kuyanywa mpaka nusu huku akiniangilia kwa macho ya kurembua.
"hivi pablo nataka uniambie kwani kule hotelini ilikua....." kabla hata hajamalizia sentensi moureen akashika kichwa chake na kuanza kulalamika na hakuchukua hata muda usingizi mzito ukampitia.bila ya kupoteza muda nikaliwasha gari lake na kuanza kuliendesha huku mkononi nikichukua simu yangu nakuanza kutafuta namba ya robert Mugalula kisha nakuipiga ambayo kwa muda kidogo ikaita kisha ikapokelewa
"kijana pablo kumbuka una masaa ishirini na nne tu ya kuchagua kujisalimisha ili familia yako isiendelee kuteseka au unaweza ukaacha na tutakuleta maiti."
"Na mimi nakuambia hivi ugomvi ni mimi na wewe na kama utaiachia familia yangu basi na mimi nitamuua moureen ambaye nipo naye kwa mikono yangu."
"unasemaje kijana??".hakika nikakata simu kwa kujiamini na huku macho yangu nikimuangalia moureen ambaye wakati huo alikuwa yupo katika usingizi mzito kabisa.nilianza kuliendesha gari hilo kwa uangalifu na kwenda kulipaki sehemu ya kujificha huku na mimi nikilala humo humo ndani ya gari.hakika hali ya hofu ikaanza kunitanda baada ya kushika simu ya moureen na kukuta messeji nyingi za mapenzi baina yake na robert jambo ambalo liliniumiza sana moyo wangu.simu katika simu yake zilikuwa zikiingia kwa wingi na kunifanya niingiwe na hofu ikifuatiwa na simu yangu ambayo katika mida ya saa nne ikaingia messeji iliyozidi kuninyong'onyesha

"KIJANA KUMBUKA KWAMBA UTAPOINGIA KATIKA MIKONO YETU KICHWA CHAKO MALI YETU"maneno hayo yalinitia hofu huku nikibaki kujiamini tu na kuzidi kumuomba mungu aniwezeshe kuipata familia yangu.usiku mzima mimi na moureen ambaye kwa wakati huo alikuwa bado yupo katika usingizi tulila na katika mida ya saa mbili asubuhi nikaamka na kuanza kuelekea chuo kwa kutumia usafiri wa wake.lakini kabla hata sijafika moureen akashtuka na kujishangaa akachukua simu na kuangalia saa zilizoambata na missed call na messeji na kunifanya niwe na hofu baada ya kuniangalia kwa hasira.akachukua chupa ya maji aliyokunywa na kuinusa kisha kwa hasira akanipiga nayo.
"Pablo ndio umefanya nini sasa??"
"moureen sikia nikwambie...ya.."
"yani wewe wa kunifanyia mimi hivi Pablo unaninyesha dawa ya usingizi ili nilale na wewe mpaka...aaa sasa mbona umenitafutia matatizo nitaenda kusemaje nyumbani eee pablo nijibu..aaaa nakuomba shuka kwenye gari yangu."moureen alisema maneno yale kwa uchungu huku akinikunja shati langu kwa hasira kubwa kisha akafungua mlango la gari lake na kuanza kunifukuza hakika nilijaribu kumuelewesha lakini bado alikuwa mkali na hakutaka kusikiliza chochote.

"Nakuambia toka masikini wewe"maneno yale yaliotoka katika kinywa cha moureen yaliniumiza na kunifanya nitoke huku nikiwa na mawazo.lakini ile naangalia tu gari la moureen likiondoka kwa kasi ghafla macho yangu yakakutana na robert ambaye sura yake ilikuwa imekunjamana kwa hasira kali.nikiwa katika harakati za kuanza kukimbia nilisikia mlio wa pikipiki ambapo baada ya kugeuka nikaona pikipiki ikija kwa kasi karibu yangu na kufanya niikwepe lakini ile naikwepa tu nikapigwa rungu kubwa la kichwa na dereva huyo wa pikipiki na kuachia mlio mkali wa maumivu kisha mdogomdogo nikaenda chini na kiza kinne kikachukua nafasi yake katika mboni ya macho yangu.

"oooh aaaaaaaaaaaaa" fahamu zilizirudi na huku maumivu ya kichwa kuchukua nafasi yake nakufanya nitoe ukelele wa miguno.macho yangu yalitua katika mataa taa yaliokuwepo ndani ya jumba hilo lililonipa shauku kubwa la kunyanyuka kwa sababu mpaka muda sikujua nipo wapi.nikiwa katika harakati za kurudisha kumbukumbu zangu zilizopotea wakati huo ghafla maji ya baridi yaliokuwa na barafu barafu yakatua kabisa katika mwili wangu na kunifanya nipige ukelele kutoka na baridi kali nililoanza kulisikia huku kumbukumbu ya yaliotokea nyuma yakija kabisa katika kumbukumbu zangu.nikanyanyuka haraka haraka lakini nikajikuta nikirudishwa chini na kamba ambayo ilioanza kufungwa na kuzunguka kiuoni changu.nikiwa katika tahamaki Macho yangu yakatua kwa robert ambaye wakati huo alikuwa amekombatia na moureen ambaye wakati huo alikuwa katika nyuso za uzuni.baba yake moureen alikuwepo naye akiambata na mama yake moureen aliyekuwa ananiangalia kwa dharau.
"Pablo kama umeshavua nguo hauna budi kuyaoga hahaha.......

DOGO ANAHITAJI MAONI YAKO, NDIO ANAANZA HIVYO BONYEZA PLAY KISHA SUBSCRIBE CHINI YA VIDEO NA BAADA YA KUTAZAMA VIDEO MPE COMMENT YAKO KAMA USHAURI KWENYE SANAA



USIKOSE SEHEMU YA SABA

Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)