LISEME JINA LANGU (7)
JINA: LISEME JINA LANGU Mwandishi: Pablo SEHEMU YA SABA ILIPOISHIA... Nikiwa katika tahamaki Macho yangu yakatua kwa robert ambaye wakati huo alikuwa amekombatia na moureen ambaye wakati huo alikuwa katika nyuso za uzuni.baba yake moureen alikuwepo naye akiambata na mama yake moureen aliyekuwa ananiangalia kwa dharau. "Pablo kama umeshavua nguo hauna budi kuyaoga hahaha....... SASA ENDELEA... Maneno hayo aliyesema robert akiwa kamshika kiuno moureen jambo ambalo liliniumiza kiasi fulani jambo ambalo lilionekana katika furaha ya wazazi wa moureen ambao wote walikuwepo wakiwa wananiangalia kwa dharau "sasa kama nilivyokuambia nataka tucheze kamchezo kidogo hebu James walete haooo" hakikupita hata dakika robert akamuita james ambaye alikuwa na mwili mkubwa wenye mazoezi na kumfanya aonekane kama mcheza mieleka.james akaenda mpaka kwenye mlango ambao ulikuwepo mbali kidogo na mimi na kuingia kisha akatoka na mashine kubwa iliyokuwa nzito kutokana na jinsi alivyokuwa akiiburuta.Mach…