LISEME JINA LANGU (7)

Zephiline F Ezekiel
0
Mwandishi: Pablo

SEHEMU YA SABA
Nikiwa katika tahamaki Macho yangu yakatua kwa robert ambaye wakati huo alikuwa amekombatia na moureen ambaye wakati huo alikuwa katika nyuso za uzuni.baba yake moureen alikuwepo naye akiambata na mama yake moureen aliyekuwa ananiangalia kwa dharau.
"Pablo kama umeshavua nguo hauna budi kuyaoga hahaha.......

SASA ENDELEA...
Maneno hayo aliyesema robert akiwa kamshika kiuno moureen jambo ambalo liliniumiza kiasi fulani jambo ambalo lilionekana katika furaha ya wazazi wa moureen ambao wote walikuwepo wakiwa wananiangalia kwa dharau
"sasa kama nilivyokuambia nataka tucheze kamchezo kidogo hebu James walete haooo" hakikupita hata dakika robert akamuita james ambaye alikuwa na mwili mkubwa wenye mazoezi na kumfanya aonekane kama mcheza mieleka.james akaenda mpaka kwenye mlango ambao ulikuwepo mbali kidogo na mimi na kuingia kisha akatoka na mashine kubwa iliyokuwa nzito kutokana na jinsi alivyokuwa akiiburuta.Macho yangu sawa sawa yakatua katika shangazi yangu akiongozana na mjomba na mwanae ambao walikuwa wamefungwa kamba shingoni kwa kila mmoja ambao wote walikuwa wanaugulia kwa chini chini kutokana na kufungwa vitu vigumu mdomoni.hakika niliumia sana baada ya kumuona hata mtoto mdogo wa miaka nane mtoto wa shangazi naye akiwa anaburuzwa kama ng'ombe huku naye akiwa anatokwa na machozi ambayo yalisababisha na kufungwa kwa kamba hiyo shingoni.
"jamani ee mnaugomvi na mimi kwanini mnawaoneea watu wasiohusika sasaaaaaaaa"nilijikuta nikisema kwa uchungu hali iliyosababisha james aje pale na kunipa ngumi kali sana ya mdomo na kunifanya nitapike damu kutokana na uzito wa ngumi hiyo iliyonipelekea maumivu makali yalionifanya nidondoshe chozi.hakukawa mtu wa kupoteza muda james akaninyanyua kisha akanifunga kamba kiuoni ambayo ilionganishwa mpaka katika mashine ya kuzunguka ambayo pia kamba hiyo iliwafikia shangazi,mjomba na mtoto wa shangazi.kisha mimi nikasogezwa umbali mrefu sana baina ya mimi na familia yangu kisha james akachukua bunduki na kuanza kupiga risasi taa kubwa za humu na kufanya vyupa vingi vikubwa kudondoka kisha na kuwashwa taa zingine kutokana na zile kupasuka na kusababisha kiza kwa sekunde kama kumi hivi.james akapiga makofi ambapo vijana wawili ambao sikujua wametokea wapi pia nao wakaja na mapipa mawili ambayo wakayafungua na kumwanga vyupa vingi vyenye ncha kali katika sakafu kutoka nilipo mimi mpaka kwa familia ya shangazi.hakika kwa muda huo sikuwa naelewa nini nilikuwa namuangalia shangazi yangu na mjomba akiambatana na mtoto wao kwa huruma kutokana na kuwasababishia matatizo ambayo hata siku moja sikuwai kurifikilia katika maisha yangu.akiwa na kipaza sauti ambacho kilishikwa na robert ambaye alianza na haloo haloo ambayo ilinifanya nimuangalie kisha kwa hali ya tabasamu aliyonionyeshea akiambata na wazazi wake ni moureen tu ambaye kwa kiasi kikubwa alionyesha uso wa huzuni wenye simanzi nzito huku akikwepesha macho yake wakati nilipogeuka kumuangalia robert na kisha nikamuangalia yeye.

"Sasa Basi umeona vyupa hivyo Pablo kama unataka Kuikoa Familia yako Unatakiwa upite hapa katikati ya vyupa hivyi kwa dakika kumi lakini tena haraka haraka kama ukichelewa kumbuka na mashine ile itajinyonga nyonga kama unakwenda kwa mwendo mdogo utasababisha familia yako akianzia Shangazi yako atanyongwa na kamba hiyo akiambata na wanaofuta sirudiii" hakika hali ya kuchanganyikwa ikachukua nafasi yake huku kutoelewa maana ndio ilikuja kabisa katika kichwa changu na kunifanya nishangae kwa kuangalia urefu wa sehemu na vyupa vingi vilivyokuwepo hapo.nikiwa katika hali ya kupigwa butwaa nikashtulia na kofi zito la uso na kunifanya nitoe miguno ya maumivu kutokana na uzito wa kofi hilo kutoka kwa james
"Simamaaaaaaaa"sauti ya kukoroma yenye ukali kutoka kwa james ndio kilikuwa kishawishi cha mimi kusimama na kwa kufumba macho haraka haraka nikwangalia akina shangazi na kwa kujiamini nikaanza kutembea katika vyupa hivyo haraka haraka.
"aaaaaaaaaaaaaaaaa uuuuuuu mamaaaaaa"hakika nilipata maumivu makali sana kutokana na kukanyanga vyupa kimoja chenye ncha kali sana na kutokeza kwa njee katika mguu wangu wa kulia na kunifanya niiiname kwa kuugulia jambo ambalo lilinigharimu kwa sababu kuniama kwangu mimi kulisababisha shangazi yangu akabwe sana na kamba mpaka kusababisha kuchana plasta alizibwa nayo mdomoni na kutokana na maumivu ya kamba hiyo iliyosababisha kuanza kutoa ulimi njee huku akitoa macho kwa sana.na kunifanya nisikwe na uoga uliosababisha nisimame na kutaka kutembea lakini kutokana na maumivu makali nikajikuta nikidondoka.
"Noooooooooooooooo....

Nilimshuhudia shangazi akitoaa macho ukiambatana na ulimi alioutoaa nje kisha nakuianama huku akiwa amesamama kutokana na mnyororo ule aliofungwa ambao ulinifikia mpaka mimi kiunoni.Hakika sikuwa nala kufanya nguvu za kusimama ziliniishia kabisa huku nikiwa nimepiga magoti nilisikia kelele za Mume wake shangazi akiambatana na mwanaye mdogo wakitapatapa kutokana na kukabwa sana na mnyororo nilijitahidi kutaka kunyanyuka kwa sababu hatima yao ipi mikononi mwangu lakini Miguu yangu ilikataa kata kata niliendelea kulia kwa uchungu kutokana sikuwa na uwezo wa kuwaokoa tena.

"Dady Noooo stop it dadyyy!!!(baba hapa basi baba) sauti ya moureen nikaisikia ikichanganyika na kilio cha nguvu kilichonisababisha nitake kugeuka lakini nilishindwa.kelele za vibao vikali nilivyofikia vilidhihirisha kabisa alikuwa anapigwa Moureen ambaye baada ya vibao hivyo sikumsikia tena moureen akipiga kelele.Nilipo rudi kuwaangalia Mume wako shangazi na mwanae walikuwa washamfuata shangazi wote walikufa kifo kilichosababisha na mimi huku nikishuhudia kwa macho yangu.mwili wangu ukaanza kutetemeka kwa hasira kali za hali ya juu machozi yalizidi kunitiririka na kuogesha mwili wangu huku majasho nayo yakichukua nafasi katika mwili wangu huku nikiwa nimekang'ata meno yangu kwa hasira iliyonifanya nikunje ngumi.Nguvu za ghafla zikaingia katika mwili wangu nakujikuta nikinyanyuka ghafla na kuanza kuwageukia baba yake moureen aliyekuwepo na mke wake,robert akiwa kamkumbatia moureen ambaye wakati huo alikuwa analia kimyakimya wakiambata na mabody guard wake wanne.Kwa mwendo wa kukimbia nikaanza kuwafuata jambo ambalo liliwastua wote huku mabody guard wale nne wakianza kujiandaa vyema.mikononi nilikuwa sijafungwa kitu mnyororo niliofungwa ulikuwa kiuoni lakini haukunipa shida kukimbia huku nikiwa nawafuata na huku nikikanyaga vyupa bila hata ya kusikia maumivu.nikajikuta nikimrukia body guard yule alinipiga vibao vya kuniamsha na kumng'ata katika shingi yake kwa nguvu huku yeye akinisambulia kwa ngumi nzito ambazo maumivu yake sikuyasikia.body guard yule alijitahidi sana kufurukuta lakini nilimzidi nguvu kwa kumng'ata sana mpaka kuanza kumtoa damu shingoni kwake na kumfanya adondoke na kuaga dunia.Nikaanza kumsogolea robert ambaye wakati huo alikuwa hana la kufanya wakati huo alibaki akiwa anashangaa Baada ya kuniona nikiwa katika hali ile hakika nilikuwa kama nimechanganyikiwa huku nikiwa na damu mdomo baada ya kumng'ata mmoja katika ya mabody guard wa robert

"Hebu mdhibitini huyo.."robert aliwaamrisha mabody guard wake ambao wakati huo walikuwa wanatetemeka kwa uoga kutokana na hali ambayo ilisababisha mama yake moureen akiambatana na baba yake kukimbia.sikuwa na muda wa kupoteza nikaanza kuwatandika mabody guard wale kwa ujuzi ambao mpaka sasa nikikumbuka uga natabasamu mpaka kupelekea wote kuwazimisha.kisha nikaanza kumsogelea robert ambaye baada ya kuona wafanyakazi wake washashindwa akachomoa bunduki kwa lengo la kunipiga jambo ambalo nililiona nakuanza kumvamia nakuanza kuigombea bunduki aliyoshika huku kila mtu akitumia nguvu zake.tukiwa katika harakati za kugombania ghafla mlio wa risasi ukasikika na nilipoangalia ilikuwa ni risasi iliyonipata mimi sawa sawa katika tumbo hali ambayo ilinifanya nitulie na kuanza kuangalia damu zilizokuwa zikinibubujika katika tumbo langu
"Hahaha sasa niwakati wakusali sala za mwisho kwa sababu ni muda wa kukumaliza"robert alisema Maneno yale huku akiwa ameniwekea bunduki kichwani baada ya mimi kupiga magoti na kuanza kushikilia sehemu niliyopigwa risasi hiyo.
"One!!!,twoo!!!three"huku akihesabu robert ile anataka kufyatua risasi tu kitu kizito mfano wa chuma ukasikika ukilia katika kichwa chake na kumfanya atoe ukelele wa maumivu makali na kumfanya adondoke chini kwa maumivu huku akiidondosha bunduki ile na kuanza kuugulia.niliangalia na kumuona moureen akiwa kashika chuma lile akiashiria kuwa ndiye yeye aliyempiga na kuanza kunisogelea kisha akanikombatia akiwa analia.nikiwa nimekombatiwa ukungu mweusi ulitanda katika macho yangu uliosababisha nizimie na kutojua kinachoendelea.

Hali ya baridi iliyosababishwa na kiyoyozi ndio iliniamsha na kunifanya nianze kuangalia huko na huku Nilijikuta nikiwa ndani ya gari ambalo pembeni mwangu alikuwepo moureen ambaye alikuwa ameshalala katika gari hilo.Kumbuku ya yaliotokea yalinijia katika kichwa changu na kunifanya nishike sehenu niliyopigwa risasi na kukuta bandeji kubwa iliyofungwa kiustadi na kiujuzi wa hali ya juu.kukuru kakara zangu zilisababisha nijitoneshe vidonda vya miguuni nilivyojikata na vyupa vile na kunifanya nianze kupiga kuugulia kwa kunung'unika kutoka na maumivu makali ya vidonda hivyo.Kumbukumbu ya yaliotokea kwa familia yangu ikibainisha kifo cha shangazi na familia yake ilinijia kichwani kwangu na kunifanya nianze kulia kilio kikubwa kilichomshtua sana moureen Niliyemshtua kutoka usingizi kutokana na kilio kikubwa nilichokuwa natoa
"Am sorry sana Pablo halikuwa kusudio Langu ni familia yangu mimi nakupenda sana"hakika siku na jibu la kumjibu moureen nilibaki tu nikilia Mapenzi bana sikuwahi hata siku moja kuja kutarajiwa kuwa yatakuja kunitesa kiasi hicho na kusababisha vifo vya familia yangu wakiwa hawana hata hatia.sikuhitaji kumchikia moureen lakini familia yake Niliichukia na huku kimoyomoyo mawazo ya kulipiza kisasi ndio ilikuwa fikra mpya katika kichwa changu.

"pablo haina haja ya kulia sasa inabidi tuanze kupambana na familia yangu ambayo inatutafuta kwa lengo la kutuuua kumbuka nafanya hivi kwa ajili yako nawageuka familia yangu na kuwa upande nafanya hivi sababu Nakupenda Pablo Nakupenda"maneno hayo aliyasema moureen akiwa machozi yanamdondoka katika mashavu yake.Nilimsogelea na kumkombatia huku na mimi Nikiwa nalia kisha wote tukajikuta tukianza kunyonyana denda zito lenye majonzi ya furaha ndani yake.ghafla simu ya moureen ikaita na alipoangalia Akaona namba ya Baba yake akaipokea na kuweka loudspeaker ili tusikie wote.

"WEWE NI MWANANGU NA KAMWE HAUWEZI KUNIKIMBIA MIMI NAPENDA KUKWAMBIA NIKUKAMATA WEWE NA HUYO MBWA WAKO VICHWA VYENU HALALI YANGU".......

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO



USIKOSE SEHEMU YA NANE

Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)