LISEME JINA LANGU (9)
JINA: LISEME JINA LANGU Mwandishi: Pablo SEHEMU YA TISA ILIPOISHIA... Baba yake moureen akaishia hapo aliendelea kunitandika baadhi ya sehemu huku kila sehemu mkia huo ulikuwa unanichana na kuniweka Alama kubwa kutokana na mkia huo kuwa na mibamiba. SASA ENDELEA... "Niuweeeniiiii tuuuu jamani mnasubiri nini niuweeniiii ooooooo aaaaaaaaaaaaaaaaaaa nasema niuweeeeniii"Nilijikuta nikiropoka maneno hayo yalimfanya robert asogee na kumsukumiza kidogo baba yake moureen kisha akanisogelea na kunisika kichwa na kunitandika ngumi kali ya pua nakusababisha damu ziliendelee kunibubujika. "Leo ni siku ya kukutoa roho umfuate mbwa wako moureen kuzimu na wazazi kwa sababu huna hadhi ya kustahili"robert alinambia huku akiwa katika hali ya kujiamini na kunifanya nichanganyike baada ya kuniambia nimfuate moureen kuzimu hali iliyonifanya niaanze kupata picha ya kuwa Moureen alikuwa kashauliwa.sikutaka hata kuamini huku kwa muda mfupi nikijikuta nikikubwa na msongamano wa mawazo yalioanza k…