
SEHEMU YA TISA
Baba yake moureen akaishia hapo aliendelea kunitandika baadhi ya sehemu huku kila sehemu mkia huo ulikuwa unanichana na kuniweka Alama kubwa kutokana na mkia huo kuwa na mibamiba.SASA ENDELEA...
"Niuweeeniiiii tuuuu jamani mnasubiri nini niuweeniiii ooooooo aaaaaaaaaaaaaaaaaaa nasema niuweeeeniii"Nilijikuta nikiropoka maneno hayo yalimfanya robert asogee na kumsukumiza kidogo baba yake moureen kisha akanisogelea na kunisika kichwa na kunitandika ngumi kali ya pua nakusababisha damu ziliendelee kunibubujika.
"Leo ni siku ya kukutoa roho umfuate mbwa wako moureen kuzimu na wazazi kwa sababu huna hadhi ya kustahili"robert alinambia huku akiwa katika hali ya kujiamini na kunifanya nichanganyike baada ya kuniambia nimfuate moureen kuzimu hali iliyonifanya niaanze kupata picha ya kuwa Moureen alikuwa kashauliwa.sikutaka hata kuamini huku kwa muda mfupi nikijikuta nikikubwa na msongamano wa mawazo yalioanza kunishambulia katika kichwa changu.kamba niliyofungwa katika mti ikakatwa nakunifanya nidondoke chini sikufungwa kitu chochote lakini nilikuwa sina uwezo wa kukimbia kutokana na vidonda vingi vilivyoninyong'onyesha na kunifanya nibaki namuangalia robert ambaye akanipigisha magoti kisha akatoa bastola yake na kuiweka risasi kisha akaisogeza katika kichwa changu.
"Ee Mungu mimi mja wako ambaye kwa sasa niko hatarini kupoteza uhai wangu bila ya sababu yoyote ya msingi hivi Kwa nini usinisaidie kwa hili.Eebaba Muumba mimi mja wako ambaye nimeuliwa familia yangu ambayo nilikuwa naitegemea na mimi unataka na mimi niondoke katika tumbo la Ardhi hii Aaa fanya miujiza sina wakumtegemea isipokuwa wewe sina ni wewe ndio mwenye mamlaka yakuamua na kama nikifa hapa basi ndio wewe utakaokuwa umepanga na hakuna anayeweza kupangua.Naomba unisamehe madhambi yangu yote niliokukusea najua sijawai kutubu baada ya kufanya madhambi yote lakini leo nakuomba msamaha kwa kuamini uwepo wako Asante." hakika sikuwa na budi ya kusali sala zangu za mwisho kimoyomoyo tena kwa uchungu huku nikakaza macho yangu katika mkono wa bwana robert ambaye nilishuhudi kidole chake kikinyonga taratibu katika kidude cha kufyatulia risasi na kunifanya nizidi kutoa macho.ile anataka kufyatua tuu ghafla kitu kama mshale kikatua katika kidole cha robertson aliyekuwa anakaribia kufyatua risasi katika bastola aliyeshika na kumfanya aiachie bastola ile huku akipiga ukelele kutokana na maumivu ya mshale aliopigwa na kusababisha wote wapigwe na butwaa na kuanza kuangalia mshale huo ulipotekea.wakiwa katika hali ya mshangao ambao hata mimi nilikuwa katika hali hiyo.Mshale mwingine ukatua kichwani kwa mfuasi wa baba yake moureen aliyekuwa pembeni yake na kufa papo hapo hali iliyosababisha...........
Wafuasi wengine waanze kumkimbiza baba yake moureen aliyekuwa kaganda baada ya kupata na kama mshangao baada ya kuona mfuasi wake wa pembeni kupigwa mshale wa kichwa na kudondoka papohapo.wengine wakamfuata na kumnyanyua robertson ambaye alikuwa bado anaguliwa maumivu ya kupigwa mshale wa mkono lakini kabla hata hawajaondoka naye mishale miwili ilitua katika miguu ya wale wafuasi wa robertson ambao walishafanikiwa kukimbia nakujikuta wakimuacha robertson ambaye baada ya kusikia wafuasi wake akilalamika akajikuta mwenyewe akikaza mwendo na kutaka kukunja lakini mshale mwingine wa bega mkampata na kumfanya atoe ukelele mwingine lakini hakuweza kusimama.niliendeleaa kushangaa huku nikiendeleaa kuwaangalia wafuasi wa robertson waliopigwa mishale miguuni ambao wote kwa pamoja wakati huo walikuwa wanaugulia kwa kutoa kelele za maumivu huku wote wawili wakiangaika kuichomoa mishale hiyo iliyopenya katika miguu ya kila mmoja huku kila mmoja akipigwa mguu wa kulia.nikiwa bado natafuta ni nani aliyekuwa akirusha mishale hiyo kwa kugeuka nyuma lakini kabla hata sijageuka upande mwingine mishale miwili tena ikapita tena juu ya kichwa changu na kuwapata wale wafuasi waliokuwa wakiugulia maumivu, mishale ya kichwa kila mmoja na kusababisha wote wafe hapo hapo.ghafla nikaguswa bega kwa nyuma na mkono ulionekana mgumu kutokana na kuniumiza pale aliponigusa kisha nikageuka na kumuangalia aliyenigusa ambaye macho yangu yakagonga katika jamaa aliyeonekana mzungu kabisa kwa macho huku akiwa kavaa kofia kubwa iliyofunika sura yake.nilimuangalia sana huku naye akiwa ananiangalia mimi pia mdomo wangu ulikuwa mzito sana kunyanyua mdomo kuongea na kujikuta nikiendelea kumuangalia mzungu huyo ambaye akanishika shika maeneo ya bega na kupandisha kwenye shingo yangu nakunibonyeza sehemu katika shingo ambapo baada ya kunibonyeza giza nene likatanda katika macho yangu na kuzimia hapo hapo.Nilishtuka na kujikuta nikiwa nimelala katika chumba chenye mwanga hafifu huku ni kibatali tu ndio nilikiona kikiwaka.jitahada zangu za kuamka ziligonga mwamba baada ya kujitonesha mwenyewe vidonda vyangu mgongoni na kunifanya nitoe ukelele wa nguvu na kuhema juu juu.nikamshuhudia mzungu huyu aliyekuwa mzee akija pale pale kwangu nakuniangalia kisha akachukua maji maji yaliokuwepo kwenye chupa na kuanza kunimwagia katika vidonda vyangu vilivyokuwepo nyuma ya mgongo na kunifanya nianze kuugulia tena kwa maumivu hali iliyomfanya hata yeye awe ananiangalia kwa kunikazia macho..
"Kijana unaitwa nani??"
"naitwa pa..blo"
"nyanyuka hebu jitahidi kunyanyuka"nilijikuta nikiingia msangao baada ya mzungu huyo mzee kuongea kiswahili fasaha kabisa huku nikifuata ushauri wake wakunyanyula kwa shida huku nikimuangalia mzee huyo ambaye naye alikuwa bize akaniangalia kwa ujasiri.
"Pablo mimi naitwa Gardner thomas ni mtalii ambaye nilikuja huku bagamoyo kutoka kwetu switzland sikufanikiwa kurudi baada ya ndugu zangu niliokuja nao kuuawa na sisi kuporwa dhahabu ambazo tulizinunua kwa kiasi kikubwa sana Mimi ni mzee licha sio mzee sana ni mimi ambaye niliweza kukimbia nakuanzisha maisha yangu hapa porini vp kwani wewe una tatizo gani.". nilimuangalia mzee gardner kwa muda kisha bila ya kuficha nikaanza kumueleza hali iliyonikuta mwanzo mwisho na kumshukuru kwa kuniokoa maisha yangu ambayo nilihisi yalikuwa hatarani kukatika.
"Usijali utakaa hapa mpaka utakapo pona kisha nitakusaidia kuweza kulipiza kisasi kwa wale wote waliokutendea ubaya." hakika baada ya gardner kunambia vile nilifarijika sana huku nikiendelea kummiminia shukrani za dhati kabisa mzee huyo.siku sita kudondosha chozi kila nilipokuwa namkumbuka moureen kutokana na kauli yake aliyoitoa robert kuwa moureen alishakufa niliendelea kuombeleza mwenyewe huku mzee gardner kuendeleza kunifariji kwa kunipa moyo huku akiendelea kunipa tiba mbadala ya vidonda vyangu.hakika siku zilichomoka na kufika mwezi ambapo kwa kutumia dawa za mitishamba vidonda vyangu vilipona kabisa tuliishi maisha ndani ya pori tukitegemea vyakula vya wanyama kama sungura na ndege kama njiwa waliokuwa wapo wengi katika pori hilo.hali yangu iliendelea kumridhisha gardner ambaye akaanza kunipa mazoezi yakurainisha viungo kwa lengo la kujiweka sawa kisha nakuniahidi kunifundisha kupambana na watu kwa lengo la kwenda kulipiza kisasi kwa wale wote walionikosea.roho ya chuki ikazidi kuniingia huku kila nikikumbuka yaliotokea nilijikuta nikishikwa na hasira za ajabu............
Mazoezi ya kukimbia umbali mrefu msituni na kuruka ruka baadhi ya mawe yaliowekwa na mzee gardner yalizidi kuniweka katika hali nyingine tofauti ya ukomavu wa mwili wangu kwa muda mchache nikajikuta nikiingiza vitu vingi katika mwili wangu zilivyonisaidia kuniweka sawa kupita kiasi.kuendelea vizuri kwangu vizuri katika mazoezi kulizidi kumfurahisha sana gardner ambaye alianza kidogo kidogo kunifundisha jinsi ya kukabiliana na adui.
"Kila kitu unachotaka kukifanya lazima uwe na nia nacho je mpaka sasa ushawai kupigana na mtu yoyote pablo."
"No mzee sijawai sikumbuki labda utotoni kwangu ila ukumba huu sijawai ooo nilishawai baada ya kushuhudia tukio la shangazi yangu kufa kama nilivyokuambia kwamba nilipata hasira iliyozidi kipimo na kujikuta nikiwazamia baadhi ya wafuasi wake robert na kuwauwa laki..."
"Ooo basi nikuambie kitu hebu attack me(nivamie mimi)"
"Eeeee unasema??
"Nivamie kijana anza kunishambulia kama unapigana na adui" mzee gardner aliniambia na mimi bila ya kusita nikajikuta nikimvamia mzee huyo na kuaanza kurusha ngumi nzito nzito zilizopanguliwa vikali kwa ustadi wa juu kisha mzee huyo akanipiga mtama na uliosababisha nidondoke.
"Simama attack me haraka kumbuka familia yako iliyouwawa kikatili kumbuka ulivyotaka kuuwawa kumbuka kwa ushampoteza mchumba wako uliyempenda kupitiliza." hakika maneno hayo ya mzee gardner yalinipandisha mori na kujikuta tena na simama na kuanza kumvamia lakini nilikuwa narudisha chini kwa mtama kila ninapojaribu kumvamia mzee huyo.alionekana kama mzee sana lakini alikuwa vizuri sana na kusababisha mimi kumvamia karibia mara hamsini lakini sikufanikiwa hata kumpata hata kidogo na kujikuta nikirusha ngumi kibao zilizokwepa kwa ufundi kisha nakudondosha.
"Nahisi utakuwa utumii akili unajua kupigana na mtu unatakiwa utumie akili huyu anakujaje anaendaje umenielewa"
"Yes nimekuelewa"
"Na kitu kingine angalia balance yako ya mwili kisha msome adui yako anakufuata vipi kamwe katika miongoni mwa sheria za kumpiga adui yako wewe unatakiwa umfuate sio yeye akufuate wewe hivi ushawai kuangalia ngumi alizokuwa anapiga tyson"
"ndio"
"sasa ngoje niaanze kukufundisha" hakika maneno ya gardner yalinijenga sana kisaikolojia na kujikuta nikienda naye sawa sawa katika kila zoezi alilokuwa akinipa.Ndani ya siku saba tu nilijikuta nikiwa nimeivaa na kuanza kupamba naye mzee gardner ambaye alifurahishwa sana na kiwango changu cha upiganaji.hakika hali ya kutaka kulipiza kisasi ilizidi kuniingia katika kichwa changu huku maneno ya mzee gardner yalizidi kunishawishi kulipa kisasi.hakika mzee huyo hakuishia hapo pia alinifundisha jinsi ya kutumia mishale kulenga shabaha zoezi ambalo niliweza kuliweka kichwani kwa muda mfupi sana na kunifanya na mimi niweze kulenga shabaha kali.Siku moja mimi nikiwa nyumbani mzee gardner siku hiyo alienda porini zaidi sehemu aliniokoa mimi kwenda kuchukua dawa zake za mitishamba ambazo mara nyingi alikuwa anapendeleaa kuzitumia.nikiwa peke yangu mimi niliendelea kufanya mazoezi yakujiweka sawa kama nilivyozoea kisha nakuamia upande wa mishale na kuanza kulenga lenga vitu vilivyokuwepo hapo nje kama miti huku nikijitahidi kulengesha sehemu ambayo nilikuwa najisikia kulengesha.ghafla nikiwa katika zoezi hilo nikaanza kusikia majani yakianza kuchakarika huku na huko na kuashiria kuwa kuna kitu kibaya kinakuja bila ya kulaza damu nikaanza kujiandaa kwa kuweka mishale yangu sawa huku mwingine nikiuweka sawa kwenye upinde na kuvuta kabisa na kusubiri kinachotokea ili nifyatue.Macho yangu kakuta na mzee gardner aliyekuwa akikimbia kwa kasi na kunifanya mimi nizidi kuwa na hofu kubwa iliyosababisha nipigwa na butwaa la nguvu.
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

USIKOSE SEHEMU YA KUMI
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com