MAMA MWENYE NYUMBA (45)

Zephiline F Ezekiel
0
Mwandishi: Mbogo Edgar

SEHEMU YA AROBAINI NA TANO
Kwa upande wa Sophia alikuwa ame jilaza kitandani kwake, chupa za bia za kutosha chini yameza na moja iliyo funguliwa juu yameza

SASA ENDELEA...
Akipanga mchongo wake jinsi ya kutumia fumanizi la jana la Suzan na baba yake, kumpata Edgar, wakati mwingine alivuta picha ya baadae akiwa na Edgar, akama mke na mume huku wapo na katoto kao katakako zaliwa, picha hiyo ilifanya atabasamu kidogo, “we ngoja kesho ndio kesho, kwanza na lialibu kwa Edgar, kisha nakisanua kwa baba, alafu yeye atanipa majibu” aliwaza sophia akiendelea kujimiminia bia, “kuhusu mama, ataelewa tu! sijuwi anamwona mtoto, yani ange juwa mh!”

Masaa yalienda mida ikapita jua likazama, atimae saa moja ..mbili... tatu za usiku.. ndiyo mda ambao bwana Kazole na hawala yake Siwema, walipo ingia nyumbani kwa bwana Kazole mtaa wa mfalanyaki, wakiwa wamelewa sana wakiwa wamesha tumia elfu alobaini na kubaki na elfu sitini, ambazo bwana kazole alikuwa ameazima kwa mzee Kalolo “karibu sana mama, jisikie hupo nyumbani, tena ukiweza kesho amia na mizigo yako,”aliongea bwana kazole, wakiingia ndani huku wana yumba yumba kwa ulevi, “asante baba, mbona mimi ni wako tu!” walikokotana mapaka juu ya makochi yale kizamani, wakajibwaga juu yake, “yeye sianajifanya ameondoka ngoja sasa niweke kitu, maana watu wana semaga, toa kitu weka kitu” alisema bwana Kazole akijizoa zoa kuelekea kwenye TV, kwalengo la kuiwasha, lakini kabla hajaifikia TV maali hilipo, akasikia mlango huki gongwa

“Mh we Kazole, umesikia hodi hiyo” alisema siwema akitaka kwenda kufungua mlango, “we mwamke umesha chelewa, nenda uliko lala jana, mwenzio amesha wai” aliongea bwana Kazole, akiwai kumzuwia Siwema asifungue mlango, akizani ni mke wake, hapana shemeji nimimi Hawetu,” ilisikika sauti ya Hawetu toka nje, ambae walitoka kuachana nae mda mchache huliopita baada ya kuwa wamesha piga bia za kutosha, “hoo! shemeji vipi tena mbona...?” hapo bwana kazole akaufwata mlango nakuufungua, ile anafungua tu! alikutana na ngumi nzito ya usoni, iliyo mtupa chini akifwatia na teke la ubavuni, “mama nakufa” yowe lili mtoka bwana kazole, huku akishuhudia njemba kama tano hivi zikiingia ndani, “hooo! mumewangu jamani, naomba unisamehe” bwana kazole akashangaa akisikia Siwema akiongea maneno hayo, akajuwa amesha fumaniwa, kitu ambacho hakikitegemea nikwamba Siwema ni mke wamtu, maana toka wame anza mapenzi yao alijuwa anakaa chumba kimoja na Hawetu, sasa huyu mume wake kivipi?

Kabla hajapata nafasi ya kuhoji bwana, Kazole alistukia akikanyagwa usoni, “mtaniua jamani” alipiga kelele Kazole, “weeee kimya” jamaa mmoja kati ya wale watatu, alimwambia bwana Kazole huku akichomoa kisu alicho kuwa ame kiweka kiunoni mwake na kumtishia Kzole yani shemeji yake Edgar, hapo bwana kazole akatulia, kilcho fwata ni kumfunga kamba bwana kazole, ikiwa ni mikononi na miguuni, pia waka mziba mdomoni kwa kumfunga nguo, baada ya hapo akawashuhudia wale jamaa waliodai wana kuja kumfumania , wakisaidia na na wakina kidawa kufunga vitu vya mle ndani kama vile anataka kuhama, huku wakiwasiliana na mtu ambae hakumjuwa anausika nini na tukio hili, baada ya dakika chache akapata jibu, ni baada ya kushuhudia gari aina ya fuso liki paki mlangoni kwake kwa kuegesha mlango wa body kwenye mlango wa nyumba yake ya kupanga

Lile gari lilikuja na vijana wengine wawili, ambao walijiunga na wakina Hawetu, nakuanza kubeba vitu vyote na kuvi pakiza kwenye gari, mwisho wasiku alisachiwa mifukoni akachukuliwa na ile elfu sitini iliyobaki, kisha wale jaamaa pamoja na wakina Siwema waka ingia kwenye gari nakuondoka zao wakiwa wame beba kila kitu mpaka nguo za bwana kazole na mkewake, wakimwacha bwana kazole akiwa na nguo alizo bakiwa tu! huku ndani ya nyumba mkionekana kama nyumba mpya ambayo bado aija anza kukaliwa na mtu, kiukweli bwana kazole hakuamini macho yake japo alikuwa amelewa lakini alianza kulia kilio cha kimya kimya, nimachozi tu ndiyo yaliyo onyesha kuwa huyu mtu alikuwa analia

Usiku huo nyumbani kwa mzee mashaka mambo yalikuwa moto moto, asa baada ya kupiga mechi yapili usiku huo, “mke wangu huja niambia kama una mfahamu huyo kijana, aliempa Sophia ujauzito” aliuliza mzee Mashaka akiwa kitandani na mke wake, “sikuwai kumwuliza, ila ngoja nimpigie ili kesho aje alete gari na uweze kuongea nae” aliongea mama sophia huku akichukuwa simu yake na kutuma ujumbe kwa mwanae Sophia, akitumia ujanja mume wake hasione anacho kiandika, “kuhusu ujauzito nime furahi sana mwanangu tena, jitaidi huyo Edgar uishi nae, kwa namna yoyo teile, pia kesho mapema njoo na gari langu, na baba yako anataka kuongea na wewe” akaituma kwa Sophia, baada ya hapo kila moja akajiweka tayari kulala akiwa na furaha tele moyoni, mzee Mashaka alifurahi kupata vitu ambavyo hakutegea kama mke wake angekuwa anaviweza, “sina haja ya kuangaika sasa, nitabaki na Suzan na mke wangu tu,” wakati mzee Mashaka akiwaa hayo, mkewake aliwaza yake, “sasa huyu mtoto atalelewa na mzee Mashaka, Edgar yeye atakuwa anamkuza mwanae tu!, huyu sophi ni kimbelembele chake mwenyewe, ata akiolewa nae kanisani, siwezi kumwacha yule mtoto, navile anavyo juwa kuing’ang’ania kum..”

Siku ya pili saa kumi nambili asubuhi, watu wakiwa katika pilka za kwenda makazini, ndipo jirani mmoja ambae jana aliona pilika pilika za kuamisha mizigo, akijuwa labda jilani yake anataka kuhama, nayeye kwakuona bwana Kazole ameamua kuhama bila kuaga, akaamua kutulia bila kwenda kumwuliza kulikoni, mida hiyo alikuwa anapita mbele ya nyumba ya bwana kazole, na ndipo alioona kuwa mlango hupo wazi, alipo angalia akaona kama kuna mtu mle ndani amelala chini, akachungulia vizuri na kumwona bwana Kazole akiwa amefungwa kamba na kuzibwa mdomo, “haaaa kumbe alivamiwa”

Siku hiyo ya jumatatu Suzan alimwomba Edgar ampeleke kazini kwa gari kisha aludi nalo nyumbani, maana kwa muda walioishi pamoja, Suzan alifanikiwa kumfundisha mpenzi wake kuendesha gari, na akaweza vizuri tu, saa moja nanusu walikuwa wameshafika maeneo ya benk ya wananchi, Edgar alisimamisha gari kisha Suzan akampiga busu Edgar akisha akashuka toka kwenye gari na kuelekea kwejengo la ofisi huku Edgar akigeuza gari na kuondoka zake, wakati Suzan anaufikia tu! mlango wajengo la benk, akastuka akiguswa begani, akageukakumtazama aliemgusa, “dada Suzie, mbona huja mwambia Edgar aje anisalimie?” alikuwa ni Monica, hapo Suzie akabaki ame tabasamu, “unge nistua ninge mwambia aje akusalimie basi utamwona jioni,” alijibu Suzan huku wakiongozana kuingia ndani, yani nimependa mnavyo ishi na kaka yako, yani mnachumiana wenyewe” aliongea Monica wakati Suzan anaingia ofisini kwake, wote wakacheka, Suzan akaingia ofisini kwake na kurudisha mlango, akimwacha Monica akienda sehemu yake ya kazi

“Sasa si ndio ujuwe kuwa kuwa mume wangu we uliona wapi kuwa mtu anamchumu kaka yake mdomoni?” aliwaza Suzan akiiweka vizuri vitu vyake na kukaa kwenye kiti chake cha ofisini, baada ya kukaa aikupita ata dakika tano, akasikia mlango wa ofisi yake ukigongwa, “ingia” alikaribisha Suzan, mlango ukafunguliwa akaingia Sophia, huku tabasamu likiwa lime tawala usoni kwake, moyo wa Suzan ukalipuka ‘paaa’, kumbe basi Sophia aliamka asubui na kukuta sms toka kwa mama yake, ikimpongeza juu ya ujauzito na ikimtaka apelike gari mapema ikiwa pamoja na kuongea na baba yake juu ya ujauzito ule, lakini alishindwa kujibu sababu hakuwa na kifurushi chochote hivyo akapanga atajiunga baadae ila ataenda tu kwao kukutana na wazazi wake, lakini akaona bola apitie kwanza ofisini kwa Suzan akaongee nae kuhu su Edgar, “mambo Suzie, hatuonani siku hizi” alisalimia Sophia huku akikaa kwenye kiti kilichopo mle ofisini

“Safi tu! naona hupo busy mwenyewe siku hizi” wali ongea hli nalile huku bado Suzan akijuwa kuna bomu lina fwatia, “hen hee!, niambie wangu maana asubuhi kama hii, siyo mchezo, lazima kuna inshu” aliongea Suzan akimtazama Sophia usoni, kweli wangu, nina mambo mawili madogo yakuelewana, ila uelewa wako uta fwanya yasiwe makubwa” aliongea Sophia nakumfanya Suzan ajuwe kinacho endelea, ni kuhusu yeye kutembea na baba yake mzee Mashaka, “mh! best mbona unanitisha, kuna nini tena?” aliuliza Suzan, hapo Sophia akafunguka, “kwanza kabisa ngugu yangu, licha yakuishi vizuri kama ndugu, kumbe una tembea na baba yangu, kiukweli hilo swala lime niuma sana, nime shindwa kukufanyia kitu kibaya kwkuwa wewe ni rafiki yangu, ila yule mwanamke ulie mkutanae baba nili mpasua kichwani kwa chupa,” hapo Sophia akatulia nakumtazama Suzan ambae aliuwa ame inammisha kichwa chini, akaona ime mkolea, akaendelea, “pili unakumbuka mwanzo ulinitabulisha Edgar kuwa ni mpangaji wako,?” Suzan akakubari kwa kutisa kichwa, “basi mimi nika tembea nae,ata nilipo kuja kuja kugundua kuwa ni mpenzi wako, sikuwa na lakufanya” maneno hayo yalimstua sana Suzan nusu mapigo ya moyo wake ya simame

“Sophia naomba uniachieEdgar wangu tafadhari sana Sophia” aliongea Suzan akimtazama Sophia huku machizi yakianza kumlenga lenga machoni mwake, “lakini Sizie, tatizo ni ujauzito nilionao, mimi nakuomba tukubaliane jambo moja” aliongea Sophia, “ok! sawa kuhusu uja uzito siyo tatizo, wewe niachie, Edgar wangu, mimi nita mle mwanao” alisema Suzan akitoa kitambaa kwenye mkoba wake na kuji futa machozi yaliyoanza kutililika mashafuni mwake, “tatizo siyo kulea, wewe mwenyewe una juwa kuwa nina uwezo wakulea atamwenyewe, ninacho taka mimi ni baba wa mtoto, naomba uniachie Edgar, pamoja kukuaidi kukutunzia siri yako na baba, pia nita kupachochote unacho kitaka” alionea Sophia akimkazia macho Suzan

“Sophia kama ni baba yako kiukweli toa nime anza kuwa na Edgar sikuwa na mpango nae nanilikuwa natafuta sababu ya kuachana nae, naile juzi niliipata, kwahiyo mimi na baba yako hatupo pamoja tena, pia baba yako alini baka kwa kuni nywesha pombe toka tupo chuoni, kama wewe ulivyo mbaka Edgar kwakutuwekea dawa kwenye pombe” hapo Sophia akastuka kidogo, maana ulisha pita mda mrefu tokea afanye kitu hicho, hakutegemea kama itabainika kuwa alifanya hivyo, akabaki kimya kabisa, “kwa hiyo Sophia nakuomba niachie mume wangu” aliongea Suzan kwa sauti ya msisitizo, ambayo ili mfanya Sophia ajuwe kuwa mwenzie hakuwa nautani, “unazani kulahisi tu naweza kukubari kumkosa Edgar?”.......

Aliongea Sophia akiinuka nakuufwata mlango wa ofisi ile, alipo ufikia akasimama na kumtazama Suzan

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO



USIKOSE SEHEMU YA AROBAINI NA SITA

Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)