
SEHEMU YA AROBAINI NA SITA
Aliongea Sophia akiinuka nakuufwata mlango wa ofisi ile, alipo ufikia akasimama na kumtazama SuzanSASA ENDELEA...
“Poa tutaona” aliongea Sophia na kufunua mlango akatoka nje na kuondoka zake, akiufunga mlango, Suzan akatafakari kidogo, kisha akatabasamu “kumbe ni kweli alituwekea dawa kwenye ile pombe aliyo kuja nayo sikuile, mshenzi sana huyu, sasa hiyo mimba atailea mwenyewe, ngoja nimwamishe kabisa Edgar wangu,” hapo akakumbuka sikuile anajifanya anataka kwenda shambani na Edgar, “mshenzi sana huyu,” alisema kwa sauti ya chini Suzan huku ana chukuwa simu yake toka kwenye mkoba wake na kumpigia EdgarWakati huo Edgar alikuwa ndio ameingia nyumbani, baada yakupak gari akaingia chumbani kwake, kile alicho panga, moja kwa moja aka chukuwa begi lake na kuanza kuhesabu fedha zake, ambazo alikuwa ana zikusanya kwa wakina sophia na mama yake pia na mzee Mashaka, wakati anaendela kuhsabu ndipo alipo isiia simu yake ikiita, mpigaji alikuwa Suzan mama mwenye nyumba, akaipokea “hallow umesha ni miss?” alitania Edgar pasipo kujuwa kuwa bomu limesha lipuka, “sanaaaa mume wangu, vipi umeshafika nyumbani?” aliuliza Suzan kwa sautiambayo Edgar akufahamu kama kuna bomu lime lipuka mida hiyo hiyo
“Ndo naingia vipi nikufwate nini, maana mimi mwenyewe nipo hoi hapa” aliongea Edgar kisha wote wakacheka, “mh! hupo hoi kivipi, mwenzio bado nasikilizia utam wa asubuhi, sasa njoo basi baadae kwenye saa tano hivi ili tukapate chakula cha mchana,” aliongea Suzan akiwa na lengo moja tu, kuwa anatakiwa awe jirani zaidi na Edgar, ili Sophia asiweze kumnyapia, “ok! poa mama saa tani kamili nitakuwa hapo, ila kuna kitu sija kuambie,” ile kusikia hivyo Suzan mapigo ya moyo wake yakastuka kidogo, “nini tena mpenzi?” aliuliza kwa kiholo Suzan, “ujuwe nini mama, siku hizi umekuwa mtamu zaidi, yani kila siku zina vyo enda nakuona unazidi unoga, mpaka natamani kila saa tuwe tuana gongana tu” wote wakacheka kisha wakaagana
Hapo Suzan akatoka ofisini kwake na kuelekea ka manage wake, bahati nzuri hakukuwa na mztu mwingine mle ofisini zaidi ya manage mwenyewe, baada ya kumsalimia Suzan akaanza kumwelezea nia yake ya kuhamia Songea, akitoa sababu zakuwa anaitaji kaka karibu na wazazi wake, akidanganya kuwa ni wazee sana wanaitaji uangalizi wakaribu, “ok! tena una bahati sana kulikuwa namaitajio ya mwasibu huko Songea, ebu andika barua ya maombi wakati mimi na wasiliana na akao makuu kujuwa ama hiyo nafasi itakuwepo bado,” alisema manage, na suzan aka mwelea pia kamaatafanikiwa basi ataomba awapangishie nyumba yae hiliyopo kibamba kwaajili ya wafanyakazi, manage wake akamuunga mkoo kwahilo pia, Suzan akarudi ofisini kwake, akiwa na furaha moyoni mwake, “sasa huyu mshenzi anae mvizia mume wangu atajijuwa na baba yake,” alijiwazia Suzan akiwa anaelekea ofisini kwake
Dada mkubwa wa Edgar alichelewa sana kuamka siku hiyo, na baada ya kuamka akabaki kitandani akiwaza aende nyumbani kwake akachukue nguo zake, maana hakuwa na nguo za kubadirisha zile alizo kuja nazo zilikuwa zime tapakaa damu na hizi alizovaa, alipewa na mama yake, lakini wakati anajishauri kuamka mala akasikia mlango wa chumba chake ukigongwa, “ingia” alikaribisha mke wa bwana Kazole, mlango uka funguliwa akaingia binti wa kazi, “samahani dada unaitwa na mama kuna mgeni wako” alileta ujumbe yule binti wa kazi
“Sawa nakuja” alisema mke wa bwana Kazole na yule binti akatoka kisha dada yake Edgar akaamka na kujiandaa kwa kunawa uso pekee kisha akatoka kwenda kusikiliza wito, naam ile anatoke zea Sebuleni aka kutana uso kwa uso na mume wake, akiwa amevimba usoni vibaya sana, pembeni yake akiwa amekaa jirani yao wa kule mfaranyaki, pamoja na wazazi wake, yani mzee haule na ke wake, “karibu shemeji” alikaribisha mke wa bwana kazole akimkaribisha yule Jirani yao, “asante sana shemeji” aliongea, dada ake Edgar akaa karibu na mama yake, “haya mwanangu nazani umemwona mumeo jinsi alivyo?” aliongea mzee Haule
“Nikweli nime mwona” aliitikia mke wa bwana Kazole, “nakuomba umsiklize mwenzio anachosema” alimaliza mzee Haule kisha bwana Kazole akaanza kusimulia kilicho mtokea jana usiku, akidanganya kuwa baada urudi kwenye matembezi yake usiku akiwa peke yake, ndipo alipo vamiwa na wezi na kupolwa kila kitu mle ndani pamoja nafedha, ikiwa pamoja na yeye kupigwa vibaya sana na wezi hao, kiukweli bwana Kazole aliiweka vizuri story yake kiasi kwamba ikawa ya kuuzunisha, na ili muuzunisha kila mtu mle ndani, kisi kwamba ata msa maha kwake ulikuwa ni mwepesi, aka karibishwa na kuelekezwa chumbani kwa mkewe, pamoja na mzee Haule kumkabidhi shilingi laki moja wakanunue nguo yeye na mkewe, akiahidi kuwa saidia kuanza upya
Ina mana auna simu? maana nime kutumia ujumbe toka usiki kimya, yani bahati yako baba yako alipanga kutoka saa nne, vinginevyo usinge mkuta” mama sophia alikuwa anaongea na mwane mala baada ya sophia kufika nyumbani hapo, “yani mama huwezi amini, sms nimeiona asubuhi, sina ata dakika wala sms, na mpaka sasa sijaweka vocha, hivyo utaniazima simu yako niwataalifu kazini kuwa nitachelewakidogo” aliongea Sophia wakati huop baba yake alikwa anatoka chumbani amesha jiandaa kwa kutoka, “shikamoo baba,” alisalimia Sophia, “malahaba mwanangu, ongera sana mama yako ame nidokeza kidogo, nashukuru kwa kuniletea mjukuu” aliongea baba Sophia huku anakaa kwenye kochi, na mke wake anasimama na kuacha simu mezani, na kuelekea chumbani akienda kujiandaa ili ampeleke Sophia kufwata gari lake aana alikuja na gari la mama yake
“Ok niambie mwanangu huyo mkwe ni waukweli lakini?” aliongea mzee Mashaka, na Sophia akaona hiyo ndiyo nafasi pekee ya kuli kologa na kusababisha mvurugano ambao uta mtoa Edgar kwa Suzan, “mh! baba nae, kuna kijana mmoja hivi ni mpenzi wa yule rafiki yangu Suzan ana itwa Edgar, anaekaa nae kwake” kusikia hivyo moyo wa mzee Mashaka nuu uchomoke, kiukweli hapo hakuweza kuskumbuka alikuwa anaongea nini na mwanae, “ok! sawa .. ok! tuta ongea baadae” mzee Mashaka aliongea hivyo akionekana kabisa amechanganyikiwa
Sophia alimwona baba yake akiinuka nakuelekea chumbani, kisha akatoka haraka haraka na begi lake mkononi, “mama yakoanaoga, akitoka mwambie nime toka nitarudi mapema” aliongea mzee Mashaka akifungua mlango na kutoka nje, dakika chache lika sikika gari lake liki washwa, na kuondoka, sophia aka jipiga kifuani, “tuone sasa kama patakalika huko” alisema Sophia akichukua simu ya mama yake na kuifungua, kisha akatoa simu yake na kutafuta namba za simu za manage wake wa tanesco, alipo zipata akiaziandika kwenye simu ya mama yake na kuipiga, baada ya mda mfupi ili pokelewa kisha akaongea na boss wake , akimambia kuwa atachelewa kidogo, maana amepata taalifa kuwa ,mama yake anaumwa sana hivyo amepitia kumwona kidogo
Alipo maliza hilo akakumbuka kuwa haja wasiliana na Edgar, akaona bola atumie simu ya mama yake kumpigia Edgar, Sophia aka bonyeza namba za Edgar ambazo alikuwa ameziifadhi kichwani, passipo kuangalia kwenye kioo chasimu akabinyeza sehemu ya kupigia, simu ikaanza kuita, iliita sekunde chache ikapokelewa, “niambie mke wetu, pole sana kwa kuumwa jana” Sophia alistuka na kuitoa simu sikioni mwake akaitazama kwenye kioo, jina liliandikwa saloon, akakata simu, akizani kuwa amekosea na kuupigia mchepuko wa mama yake, safari hii akaichukua simu yake na kuitazama namba ya Edgar, kisha akaiandika kwenye simu ya mama yake kwa umakini sana, huku mapigo ya moyo yakimwenda mbio
“Naomba ile ya kwanza niwe nime kosea,” alijisemea Sophia huku akimaliza kubonyeza namba za Edgar kwenye simu ya mama yake, lakini jina lilikuja Saloon, hapo aka waza sekunde chache kisha akaipiga tena, lengo likiwa ni kusikiliza sauti ya mpokeaji, safari hii haikuchelewa kupokelewa, “niambie mmama mbona una kata simu au mzee yupo” kiukweli ilikuwa ni sauti ya mpenzi wake Edgar, wakati anawaza amjibu nini Edgar, mala akasikia sauti ya vishindo vya mama yake akitokea chumbani kuja sebleni, akakata simu faster na kuifuta ile namba ya edgar kwenye orodha ya watu waliopigiwa, “haya twende mwanangu,” aliongea mama sophi, na Sophia akainuka na kuongozana na mama yake huku akimpatia simu yake, “umesha wataalifu?” hapo Sophia aliitkia kwa kichwa maana ange toa sauti inge ambatana na kilio
Mzee Mashaka akiwa mwenye jazba kali, aliendesha gari lake mpaka magomeni kagera njia panda ya kwenda mbulahati, akaingia kufwata njia ya kwenda mbulahati, huku anwasiliana na jamaa yake mmoja hivi, akidai anaitaji vijana wawili wakazi, akisisitiza wawe na uwezomzuri wa kumwazibu mtu, baada ya kutembe kwa kilomita mbili mbele mzee Mashaka akaimamisha gari wakaingia vijana wa tau walio shiba utazani myule bouncer wa diamond kisha safari ikaanza, akipiga u turn kurudi aliko toka
Ilisha timia saa tano kasolo midaambayo Edgar aliacha shuguli zake za kupanga vizuri fedha zake ambazo aliamini zita msaidia kufungua ofisi ya Sanaa aliyo somea, watakapofika Songea na mpenzi wake Suzan, akaandika mahesabu yake kwenye ki note book chak na kukiweka mfukoni pamoja na peni yake, hapo aliingia ndani ya gari la Suzan na kuanza safari ya kwenda mbezi kwa mpenzi wake kama walivyo panga, wakati anasubiri kuingia bara bara kuu, akamwona Joyce akija mbio huku anamwita, “Edgar nisubiri kidogo” aliongea Joyce huku akongeza mwendo kumfwata, “nita kuja kwako baadae” aliongea Edgar akiondoa gari, Joyce alitabasamu akionyesha kulizika na jibu la Edgar
Kiukweli bwana kazole alishangaa maendeleo ya mzee Haule, maana pale je alikuta duka kubwa na jinsi alivyo iona ile nyumba, ilikua tofauti na alipoiacha sikuile alivyo mkaba mzee Haule ambae ni baba mkwe wake, “hapa lazima ni niondoke na faida” aliwaza bwana kazole
Saa tano kasolo mzee Mashaka na watu wake watatu walikuwa wanakaribia kibamba ccm, ndpo alipo liona gari la Suzan likielekea mbezi, huku ndani yake akiwa Edgar peke yake “huyo huyo., amepita hapo, aliongea mzee Mashaka akitafuta sehemu nzuri ya kugeuza, akapiga u turn na kuanza kuli fukuzia gari la Edgar
Wakatii huo Suzan alikuwa ofisini akifanya kazi zake, huku akisubiri majibu ya barua yake ya kuomba uamisho, mala akaingia manage wake, “ongera Suzan umefanikiwa, una uamisho wa kwenda Songea, unatakiwa ulipoti ndani ya siku saba, sasa fanya makabiziano ya ofisi ukimaliza upewe form ya uamisho”
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

USIKOSE SEHEMU YA AROBAINI NA SABA
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com