MAMA MWENYE NYUMBA (45)

Zephiline F Ezekiel
MAMA MWENYE NYUMBA (45)
JINA: MAMA MWENYE NYUMBA Mwandishi: Mbogo Edgar SEHEMU YA AROBAINI NA TANO ILIPOISHIA... Kwa upande wa Sophia alikuwa ame jilaza kitandani kwake, chupa za bia za kutosha chini yameza na moja iliyo funguliwa juu yameza SASA ENDELEA... Akipanga mchongo wake jinsi ya kutumia fumanizi la jana la Suzan na baba yake, kumpata Edgar, wakati mwingine alivuta picha ya baadae akiwa na Edgar, akama mke na mume huku wapo na katoto kao katakako zaliwa, picha hiyo ilifanya atabasamu kidogo, “we ngoja kesho ndio kesho, kwanza na lialibu kwa Edgar, kisha nakisanua kwa baba, alafu yeye atanipa majibu” aliwaza sophia akiendelea kujimiminia bia, “kuhusu mama, ataelewa tu! sijuwi anamwona mtoto, yani ange juwa mh!” Masaa yalienda mida ikapita jua likazama, atimae saa moja ..mbili... tatu za usiku.. ndiyo mda ambao bwana Kazole na hawala yake Siwema, walipo ingia nyumbani kwa bwana Kazole mtaa wa mfalanyaki , wakiwa wamelewa sana wakiwa wamesha tumia elfu alobaini na kubaki na elfu sitini, ambazo bwana kazole alik…