MAMA MWENYE NYUMBA (46)
JINA: MAMA MWENYE NYUMBA Mwandishi: Mbogo Edgar SEHEMU YA AROBAINI NA SITA ILIPOISHIA... Aliongea Sophia akiinuka nakuufwata mlango wa ofisi ile, alipo ufikia akasimama na kumtazama Suzan SASA ENDELEA... “Poa tutaona” aliongea Sophia na kufunua mlango akatoka nje na kuondoka zake, akiufunga mlango, Suzan akatafakari kidogo, kisha akatabasamu “kumbe ni kweli alituwekea dawa kwenye ile pombe aliyo kuja nayo sikuile, mshenzi sana huyu, sasa hiyo mimba atailea mwenyewe, ngoja nimwamishe kabisa Edgar wangu,” hapo akakumbuka sikuile anajifanya anataka kwenda shambani na Edgar, “mshenzi sana huyu,” alisema kwa sauti ya chini Suzan huku ana chukuwa simu yake toka kwenye mkoba wake na kumpigia Edgar Wakati huo Edgar alikuwa ndio ameingia nyumbani, baada yakupak gari akaingia chumbani kwake, kile alicho panga, moja kwa moja aka chukuwa begi lake na kuanza kuhesabu fedha zake, ambazo alikuwa ana zikusanya kwa wakina sophia na mama yake pia na mzee Mashaka, wakati anaendela kuhsabu ndipo alipo isiia sim…