MAMA MWENYE NYUMBA (47)

Zephiline F Ezekiel
0
Mwandishi: Mbogo Edgar

SEHEMU YA AROBAINI NA SABA
“Hongera Suzan umefanikiwa, una uamisho wa kwenda Songea, unatakiwa ulipoti ndani ya siku saba, sasa fanya makabiziano ya ofisi ukimaliza upewe form ya uamisho”

SASA ENDELEA...
Aliongea manage huku aimkabidhi barua toka makao makuu ya benk yao, hapo Suzan akaachia tabasamu moja matata sana, “asante mungu kwa kufanya kila nianalo lipanga liede sawa,” alisema Suzan akipokea barua huku boss wake akitoka ofini, na kupishana na monika, “dada Suzan mdogo wako,”aliongea suzan kwa pupa hisiyo na mfano, Suzan akamtazama Monica kwa hasira, pasipo kusema lolote, “dada suzie Edgar amekamatwa kwa nguvu na watu flani hivi” aliongea tena Monica, baada ya kuona Suzan amwelewi

Hapo Sophia akastuka kidogo, “unasemaje monica?” aliuliza Suzan akisimama na kumsogelea Monica, “wakati natoka kwenye chai, nikamwona Edgar anangia hapo nje yupo na gari lako, nikasema nimkimbilie nika msalimie, mala ghaafla likaja gari moja hivi naliona mala nyingi hapa benk, lika simama waka shika na kumfwata Edgar ambae alikuwa bado yupo kwenye gari ameshika simu mkononi, wakamnyanganya simu na kumvuruta wakingia nae kwenye gari lao,” alimaliza kusimulia Monica, Suzan akajihisi kuchanganyikiwa, “gari la nani tena hilo” alijiuliza Suzan kwa kunong’ona “hen heee! nime kumbuka unakumbuka juzi kuna mzee ulikuwa unasalimiana nae pale bar,” Suzan akaitikia kwa kichwa, “basi gari lake ndo lina fanana na la yule mzee”

Hapo Suzan alijiona akilegea na kuona giza usini mwake, na kizunguzungu kikitawala kichwa chake, kisha taratibu akajikuta akienda, huku Monia akijaribu kumdaka pasipo mafanikio “da’ suzie , da! Suzie,” aliita Monica akimtikisa Suzane, lakini Suzane akuitikia, hapo Monica aka timua mbio kutoka nje na kuomba msada kwa wenzake, nao wakaja haraka na kujaribu kumwamsha Suzan pasipo mafanikio, wakaona bola wampeleke hospitali iliyopo jirani, nao waka mpeleka kwenye hospitali ya Dr Stellah, shangazi yake Jayde, (msome kwenye mkasa wa SHANGAZI ANATAKA utakuja baada ya huu Mungu akijaalia) wakitumia gari la kwake yeye mwenyewe Suzane, ambae alikuwa amekata moto ajitambui

Walipo fika pale hospital, walipokelewa haraka sana, na mgonjwa ambae ni Suzan akaanza kuchukuliwa vipimo kuakikisha kama mapigo ya moyo yana fanya kazi, maDr walipo jilizisha kuwa mapigo ya moyo wa Suzan yana dunda, waka sema mgonjwa anaitajika kupumzika, mpaka fahamu zitakapo mjia, basi Suzan aka pelekwa kwenye chumba ambacho alitakiwa kulazwa, akalazwa kwenye kitanda maalumu kwaajili ya wagonjwa wasio jitambua kama yeye, akaja Dr Stellah na kutoa maagizo kuwa mgonjwa apimwe, kwanza kama anatatizo jingine au kitu chochote mwilini mwake, kabla ya kumtundikia drip za dawa mbali mbali, ambazo zingemsaidia kumwongezea uwezo wa kurudisha fahamu, hapo mala moja vipimo vikaanza kuchukuliwa ikiwemo na vipimo nya ultrasound, hk wafanyakazi wenzake wakiondoka wakimwacha Monica akimuuguza Suzan, akipanaga kuto mwambia mtu yoyote kilicho tokea, mpaka Suzan atakapo amka, maana hakujuwa undani wa tukio lile, akichukulia ni kama watu wanao fahamiana

Taalifa za kuanguka kwa Suzane zilimfiia manage wa Suzan, mwanzo manage alizani kuwa ni matatizo ya kifamilia ndiyo yanayo mchanganya Suzan, akikumbuka kuwa leo hii mapema alimwambia kuwa anaitaji kuamia Songea kutokana na jukumu la kuwatunza wazai wake, “wacha tumsaidie aende haraka huko Songea, akipaa nafuu aje achukuwe form yake ya uamisho, maana nazani atokuwa na deni lolote”aliwaza manage akikagua kwenye computer yake, akikagua mambo yanayo muusu Suzane, alipo lizika akanyanyua mkono wa simu ya mezani na kupiga, “hee hallow, ebu andaa form ya suzane ya uamisho, kamahiyo barua ilivyo sema, usiandike tarehe kwanza,” kisha boss akakata simu

Kiukweli Suzan alistuka sana, alipo sikia kuwa Edgar ametekwa, na moja kwa moja akajuwa kuwa mtekaji ni mzee Mashaka na si mwingine, na kama mzee Mashaka ndie aliemteka Edgar, wahiyo mzee huyu amesha fahamu mchezo mzima, na wakumweleza ukweli ni mwanae Sophia, mstuko mkuba ulimpata Suzan na kuanza kuona kuzungu zungu, huku mwili hukikosa nguvu na kuona macho yake yakitanda giza nene, na kuanguka chini kisha taratibu akaanza kuona manga usoni kwake ukianza kujitokeza, na lile giza likitoweka, mala akaanza kuon taswila ya eneo aliopo, kadri sekunde zilivyo enda ndivyo alivyoweza kujitambua kuwa yupo ndani ya chumba kimoja chenye kuta nyeupe, zenye picha mbali mbali, zilizo ashilia kuwa ni hospital, akajitazama alikuwa ametundikiwa drip akaangalia pembeni, akamwona Monica ame kalala kwenye kitanda kingine kilichopo jirani yake, akakumbuka atamala yamwisho alikua nae ofisini akimsimulia kukamatwa kwa Edgar na watu watatu, wakiwa na gari la mzee Mashaka, hali ya nje ilionyesha kuwa ni usiu sana

Hapo alijikuta machozi yakimtanza machoni mwake, “sijuwi yupoje jamani?” alisema Suzane kwa sauti ya chini iliyo ambatana na kilio, sauti iliyo mfikia Monica pale kitandani, akaamka na kumsogelea Suzane alipo lala, “afadhari umeamka, yani umelala toka jana saa tano mpaka sasa hivi” aliongea Monica na kuangalia saa kwenye simu yeke, ilsha timia saa tisa za usiku, inamana Suzane alizimia muda mrefu sana toka saa tano asubuhi mpaka saa tisa za usiku “simu yangu hipo wapi?” aliuliza Suzane, na monica aka chukuwa simu kwenye mkoba wa Suzan na kumpatia, Suzane akaitazama aikuwa na missed call wala sms akatafuta namba ya simu ya Edgar, alipo ipata akaipiga na simu ikaanza kuita, iliita kidogo ikapokelewa

“Hallow mke wa mzee Mashaka hapa naongea, nikusaidie tafadhari” hapo Suzan alistuka kidogo akaitazama ile simu labda alikosea kupiga namba ile, lakini jina lilikuwa ni mpangaji mpya, ilikuwa ni auti ya mama sophi, akionyesha mwenye uchovu na usingizi Suzane akajiuliza “inamaana sophia na mama yake ndio wame mteka Edgar?” akaiirudisha simu sikioni, “mimi suzane, samahani mama naomba kuongea na Edgar tafadhari”aliongea Suzan kwasauti tulivu na ya pole pole sana, hapo alihisi kabisa mama sophi akipatwa na mstuko, baada ya kuachia mguno “we mtoto una wazimu, Edgar nitakuwa nae ipi huku?, au ume changanyikiwa?, au ulikuwa una mpigia huyu hawala yako?” Suzane alisikia sauti ya mshangao ya mama Sophia iliyo changanyika na hasira, wala hakushangaa maneno yake maana alisha juwa kuwa mambo yamesha bumbuluka

“Utakosa vipi kuwanae kama simu yake upo nayo” hapo mama Suzan akasikia tena mguno mwingine, kisha kika pita kimya kidogo, “nasema naomba uniambie Edgar yupo wapi?” sasa Suzan aliongea kwa sauti ya juu kwa ukari sana, “sikia Suzie, atamimi sielewi hii simu nime ikuta kwenye gari la mume wangu, nipo nae hapa hospital hajitambui, maana leo mchana yeye nawenzake walivamiwa kwenye gari nakushambuliwa na mtu ambae mpaka sasa hajajuliana, yeye na wenzake wawli wapo hapa hospitali ya tumbi huku kibaha, na wenzake mmoja amepoteza maisha,” taalifa hiyo ili mstua sana Suzan, “hapana mama hapana, mwambie mume wako amwachie Edgar” aliongea Suzan kwa sauti ya ukali kama mwanzo akiwa ayaamini maneno ya mama Sophia

Wakati huo alikwa anaingia muuguzi, ni baada ya kusikia sauti ya Suzan, “sikia Suzane, yani hapa tunapo ongea mzee Mashaka yupo hoi amevuja damu nyingi sana, ukiachilia kupigwa vibaya sana pia ametobolewa nakitu chenye ncha kali kwenye shavu lake, yani amevunika mguu kabisa, hivi navyo kuambia tupo hapa toka mchana, ameibiwa fedha nyingi sana” Suzan alitulia akimsikiliza mama Sophia huku Monica na muuguzi wakimtazama, Suzan ambae alionekana kuanza kupunguza jazba, “samahani dada, naomba upumzike kwanza mpaka asubuhi ndipo ufanye mawasiliano mengine, maana unaitaji kutuliza akili” aliongea yule muuguzi akiichukuwa simu toka kwa Suzane nakuikata, Suzan akamtazama monica, “una uakika kuwa Edgar alichukuliwa na watu watatu kwenye gari ulilo sema?" aliuza Suzane akiwa bado amemtazama Monica,

“ndiyo da Suzie, nalikumbuka sana lile gari, isitoshe nimesha liona mala kadhaa likija benk” alijibu Monica, na kumfanya Suzane aanze kuwaza “sasa Edgar atakuwa wapi?” alijiuliza kimoyo moyo, “mh! lakini....” hapo Suzane alikumbuka siku ile yapat miezi mitatu nyuma, alipo mwona Edgar akipambana na mwendesha boda boda pale kibamba, “inawezekana kweli?” ali maanisha Edgar kupambana na watu watatu ongeza mzee Mashaka, maana alikuwa na uakika kuwa lazima Sophia amesha bumbulua kila kitu, sababu alikuwa anafahamu yote kuhusu yeye Suzane, na uusiano wake na baba yake na Edgar, “mtoto wa watu sijuwi atakuwa wapi saa hizi”

Wakati Suzan anajiuliza kuwa Edgar atakuwa wapi, kumbe mwenzie alikuwa mbali sana akiitafuta Songea

Ilikuwa hivi, baada ya kumwona Joyce anamfwata Edgar alijuwa kuwa mschana huyo ana hamu ya dud utu! nasiyo kingine, maana ilisha pita karibia week hawaja peana mambo, akaamua kumdanganya kuwa atamtafuta baadae, kisha yeye akaondoa gari na kuelekea zake mbezi aliko itwa na Suzan wakapate chakula cha mchana wahehe wanaita lunch, aliendesha gari mpaka maeneo ya benk akasimamisha gari kisha akatoa simu yake, nakuanza kuandika ujumbe kwa Suzan akimtaalifu kuwa amesha fika, lakini kabla haja maliza kuandika ujumbe huo, akashangaa watu watatu wanaume walioshiba, wakizunuka gari lake na kusimama kwenye milango ya mbele, na mmoja akafungua mlango wa dereva alio kaa yeye, nakumnyanganya simu

“Dogo tulia, husilete fujo ya aina yoyote zaidi ya hao utaumia vibaya sana” alisema yule alie mnyang’anya simu. kisha akamshika mkono na kumvuta kuelekea kwenye gari ambalo Edgar alilitanbua kuwa ni la mzee Mashaka, nandio gari ambalo alisha wai kuliona malakadhaa mtaani kwao, kabla ya kumfahamu mzee Mashaka mwenyewe, nandio gari pekee lililowai kumwagia maji machafu, pia ndilo gari pekee ambalo mwenye gari amesha mpatia fedha nyingi sana zaidi ya million sita, na ndilo gari pekee ambalo mwenye gari hilo amesha mfanyia zambi kubwa ya kutembea na mke wake hawala yake na mtoto wake, ikiwa na kutumia fedha nyingi sana za milikiwa gari hilo, kupitia nyumba ndogo yake na mke wake, “yametimia kama yalivyo nenwa, mke wamtu sumu” alijisemea Edgar kwa sauti ya chini kama ananong’ona, wakati mlango wa katika wa gari ukifunguliwa na kusukumiwa ndani, hapo jamaa mmoja aka kaa kusho kwake na mwingine kulia kwake moja aka kaa mbele na mzee Mashaka ambae ndie aliekuwa anaendesha gari, kitendo bila uchelewa gari likaondolewa “mzee simu yake hii hapa”

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO



USIKOSE SEHEMU YA AROBAINI NA NANE

Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)