MAMA MWENYE NYUMBA (7)
JINA: MAMA MWENYE NYUMBA Mwandishi: Mbogo Edgar SEHEMU YA SABA ILIPOISHIA... Akainuka, na kwenda, kuichukua simu yake kwenye mguo aliyokuwa ameitundika kwenye msumali ukutani, akaitoa na kuangalia kwenye kioo, akaona kweli kuna messeji imeingia tena mbili, akafungua akaona zote zinztoka kwa mama mwenyenyumba SASA ENDELEA... Mapigo yamoyo yakaenda mbio, kwani alikumbuka alichokuwa anatakiwa kufanya, yakwanza iliamndikwa hivi “Eddy vipi umekumbuka dawa?” nayapili ilisema hivi “mbona hujibu au hauna salio?” hapo hapo kwakuogopa kumkasilisha mama mwenye nyumba , Edgar alivaa kandambili nakuchukua yale mafuta na tishet akaanza kutoka nje tishert mkononi, akaanza kuvaa akiwa njiani Akiwa na kanga yake moja bado amejilaza kwenyekochi, baada ya kutuma sms mbili bila majibu, Suzan akawa ameanzakuingiwa na uzuni, lakini ghafla akasikia hodi, akaenda na kufungua mlango kwaharaka pasipo kukumbuka kuwa mguu wake unauma, naam alimwona kijana Edgar, akiwa amevalia bukta yake ambayo alimwonanayo asubuhi, na…