MUUZA CHIPS (10) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumamosi, 20 Mei 2023

MUUZA CHIPS (10)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
📖 KUSOMA SIMULIZI
🎬 FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
😂 VIDEO za KUCHEKESHA
📑 MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa
Mwandishi: MoonBoy

SEHEMU YA KUMI
ILIPOISHIA...
"dada yake ndio kamlipia"

"dada yake yupi huyo jamani… We chidi eti nani kakuseidia…. "

Wakati huo huo sarah nae ndio anaingia huku akiwa kashika mfuko mkubwa ulio onekana kujaa chakula..

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
Sasa chidi alipatwa na kigugumizi,.. Mara dokta akajibu kuwa

"huyo dada yake ndio huyu hapa"

Kaka wa chidi aligeuka na kumtazama huyo dada wa chidi,… Sasa chidi anamjua kaka yake huwa hapendi ujinga, na ni mkali haswa…

Sasa ibra akiwa anamuangalia sarah ambae ndio kamseidia kijana chidi,..

"eti wewe ndio umemseidia huyu kijana"

Sasa kwa jinsi sarah alivyo, chidi alihisi kuwa sarah angemjibu kaka yake vibaya,.. Hivyo chidi alimshtua sarah na kumuonyesha kwa ishara ya vidole viwili vya mwisho, yaani kile cha kwanza cha mwisho na cha pili kutoka mwisho, huwa vimepishana sana… Hivyo alipomuonyesha hivyo vidole,… Ndio sarah akagundua kuwa huyo alikuwa ni kaka yake…..

Sasa, sarah kwa uoga alijikuta anashindwa kumjibu kaka wa chidi…. Ule mfuko wa chakula ulimdondoka chini, mana hata kaka wa chidi hakuuliza kwa sauti ndogo… Hivyo sarah alihofia usalama wake… Huku akikumbuka sauti ya ndugu yake Miriam ikisema…

"weee nawe si ungeliacha life uko, utakuja kuseidia mijambazi wewe, shauri lako"

Kaka wa chidi alikuwa akilalama sana kutokana na swala la mdogo wake kuumia ingali hali yao sio nzuri kifedha, mana chidi alipata matibabu ya kutosha na chumba alicholala sio cha kulala kila mmoja, bali ni watu wenye hali nzuri kifedha, hivyo Ibrah alichanganyikiwa sana kwa kuona matibabu ya hali ya juu kana kwamba atawezaje kuyalipa,…….

Dokta alimwambia ukweli kuwa matibabu yote yalishalipiwa, Ibrahim hakuamini kama ni kweli matibabu yalilipiwa,…. Ila kitu kilichomshangaza Ibrahim ni kwamba inasemekana ni dada yao ndio aliemsaidia chidi,.. Ibrahim alitamani sana kumuona huyo dada aliemseidia kijana chidi,…

Punde sii punde sarah anakuja huku akiwa kashika mfuko uliojaa vyakula kwa ajili ya chidi au mgonjwa wake,..

"huyo dada yake ndio huyu hapa"

Ilikuwa ni sauti ya dokta akimwambia ibra kuwa huyo dada yake ndio huyo anakuja,…

Ibrahim aligeuka kwa haraka ili kuweza kumwangalia dada yao anaesadikiwa kuwa ndie mseidizi wa chidi,

"eti wewe ndie uliemseidia huyu kijana"

Ibrahim alimuuloza sarah, lakini aliuliza kwa sauti ya juu na iliomshtua sarah na kukosa umahiri wa kuongea…

Chidi alimwonyeshea kwa ishara kiwa huyo ni kaka yake,.. Sarah alizidi kupata hofu mana akiangalia ule mwili wa kaka wa chidi, alikumbuka maneno ya rafiki yake miriam akisema kuwa

"weee nawe si ungeliacha life uko, utakuja kuseidia mijambazi wewe, shauri lako"

Sarah alipata hofu kubwa sana huku akitamani kuondoka, lakini akapiga moyo konde liwalo na liwe kama ni kuonekana mbaya wacha aonekane tu, lakini keshaseidia maisha ya mtu,

"ndio mimi niliomseidia"

Sarah aliongea huku akiangalia chini kwa uoga…

"Ahsante sana mdogo wangu,.. Undugu si kufanana, Undugu ni kuseidiana… Kiukweli umefanya kitu kizuri kwa mdogo wangu, sina budi hata mimi kukufanya kama mdogo wangu.. Asante sana na mungu akudhidishie"

Kaka wa chidi alimshukuru sana sarah hata sana mwenyewe haamini kama kaka wa chidi angeliweza kumshukuru kiasi hicho, tena mbaya zaidi kamkusanya na kumfanya kama ndugu,..

Sarah alifurahi sana kwa kitendo cha ukarimu alichokifanya kaka yake na chidi

Basi chidi alipewa chakula na kuanza kukila, Kiukweli hakuwahi kula chakula kama hicho, yaani katika vyakula bora Kiukweli hicho ni bora sana kwake mana pia ni kipya katika mdomo wake,

Wote wawili walikuwa wakiendelea kumuangalia huku dokta akisema

"nadhani jioni tunaweza kumruhusu kwasababu tayari tumeshampatia dozi hivyo baadhi ya majeraha yatapona akiwa nyumbani"

"tunashukuru sana dokta"

Alikuwa ni Ibrahim akimshukuru dokta kwa kutoa ruksa mapema, mana akiendelea kukaa hapa afu siku mdada wa watu akashindwa kuendelea kulipia huduma itakuwaje mana sio ndugu yake bali ni mpita njia tu,

Ghafla simu ya Sarah inaita, kuangalia jina alikuwa ni ndugu yake miriam,

"haloo miri"

"wewe sarah, asubuhi subuhi yote hio umetoka umeenda wapi wewe"

"nilitoka kidogo shosti"

"aahhh basi njoo twende kazini"

"aahh tangulia tu"

"sarah, Sarah, Sarah.. Umepatwa na nini lakini"

"nakuja basi Nisubiri… "

"aaaaaaaa, basi nimeshakumbuka kumbe upo huko kwa huyo jambazi lako"

"ndio"

"na takukaba mwenyewe huyo we jipendekeze tu"

"nakuja bwana miri acha hizo"

"nakusubiria hapa nje"

Sarah alikata simu kisha akawaaga akina chidi na kaka yake, alitoa pesa kiasi cha shilingi elfu 50

"aahh samahani kaka, naomba nitoke kidogo, na hii hapa mtaitumia kama kuna chochote cha kununua"

Sarah aliongea hivyo huku akimkabidhi Ibrahim pesa hio

"asante sana mdogo wangu, mungu akudhidishie zaidi na zaidi… "

"usijali kaka angu….. Chidi mi naenda"

"lakini si utarudi, au ndio mazima ivo"

"yaani kuacha kuja ni sawa na kuacha kula wiki nzima jambo ambalo haliwezekani"

"sawa.. Asante sana dada sarah"

"usijali chidi"

Saraha hakupenda chidi aanze kumuita dada japo umri wao huenda wakalingana au chidi akamzidi kama mwaka au miaka miwili tu,.. Hivyo sarah hajapenda kwasababu anahisi chidi akimpa heshima kubwa sana, atashindwa kufanikisha lengo lake,… Hivyo chidi hatakiwi kumueshim sarah kwasababu sarah ana hisia tofauti na kijana chidi, sema chidi hajui tu,…

Baada ya sarah kuondoka kaka wa chidi ndie aliekuwa na mdogo wake karibu, ndugu wawili wakiwa pamoja, ila kaka wa chidi ni mwanaume anayejiheshim sana hivyo huwa hapendi ujinga wa hapa na pale,

"ivi Rashid? Ulifanya nini mpaka kufika hapa hospitali"

Ibrahim alimuuliza mdogo wake, mana toka aje hajapata nafasi ya kumuuliza vizuri

"mmhhh kaka… Kiukweli sijui ni kwanini huu mji una ukorofi kiasi hiki"

"kwanini useme hivyo"

"yaan wakati nashuka tu kwenye gari, kulikuwa kuna mwizi anakimbizwa na polisi, yule mwizi alinipamia na kunifanya nidondoke chini.. Sasa polisi walipokuja wakajua ndio mimi… Aisee walinipiga, mpaka wanakuja kuujua ukweli kuwa sio mimi, nilikua nimeshaumia… Kuna polisi alinipa pesa ili nikajitibu, lkini sasa hospitali siijui ilipo, na wewe sijui ningekupataje… Ikabidi ile pesa niinunulie simu, ndio nikawa nakupigia mpaka nikakuelekeza kwenye bango la koka kola, hapo ndio huyo dada akaja kuniulizia mambo supermarket nikamjibu sijui lakini aliponiangalia sura akagundua nina majeraha… Ndio akaniseidia na kunileta hapa… Ni hivyo tu kaka hakula lingine"

Chidi alimsimulia kaka yake jinsi ilivyokuwa mpaka kufika hapa, Ibrahim alichoka kwa kusikia hivyo, ila haikuwa na budi mana uwezo wao wa kimaisha ulikuwa bado ni mdogo hivyo hawawezi kushtaki kwa kupigwa pasina kosa,..

Wakati huo tukija huku kwa akina sarah na miriam, Sarah alimkuta ndugu yake miriam akiwa anamsubiria hapo nje kwao,

"ivi hilo jambazi lako lipoje lipoje, mana linakuchanganya mno"

Alikuwa ni miriam akimuuliza sarah kuwa huyo mtu wake aliomseidia akiwa kaumia yupoje yupoje mpaka kufika hatua ya kukurupuka asubuhi subuhi kwenda kumjulia hali,

"we hakuusu hata kama ni jambazi si langu"

"utapotea wewe sarah, fata watu na heshma zao"

"wewe huyo wako mwenye heshma yuko wapi"

Miriam alitulia kimyaa baada ya kiambiwa kuwa mbona yeye hana wa heshma wala mwizi, yaan yeye yupo yupo tu hana mpenzi wala nini,

"hata kama, lakini usipende kiasi hicho"

"bwana wewe twende"

Basi sarah na miriam waliondoka na kwenda zao kazini, hatujui kazi wanayofanya lakini inaonekana ni watoto wa watu waziyo haswa, yaani kama ni vigogo basi hawa ni vigogo haswa….

Tukirudi huku hospitalini kwa akina chidi na kaka yake, walikuwa wakipiga stori nyingi sana za kijijini kwao,

"tukifika nyumbani nataka unipigie stori shem langu, mana naskia ulifumaniwaga wewe"

Alikuwa ni Ibrahim akimwambia mdogo wake kuwa wakifika home ampe stori ya mke wake yule salma,

"sawa nitakusimulia tu broo"

Jioni inafika ikiwa ni mida ya saa 11 jioni ndani ya muda na sarah nae huyo, wala hakuchelewa,..

"ooohh karibu mdogo wangu"

Alikuwa ni Ibrahim akimkaribisha sarah kwa furaha,..

"asante shkamoo kaka"

"marahaba ujambo sarah"

"sijambo….. Chidi mambo?"

"poa vipi hali"

"safi tu, unaendeleaje now"

"naniskia poa"

"ok… So nadhani leo ndio siku ya kutoka ee"

"ndio na tulikuwa tunakusubiria wewe"

"ok… Twendeni niwapeleke"

Sarah aliwapakia katika gari yake na kuondoka hospitali hapo, chini na kaka yake hawaamini kama hospitali wametoka bila kudaiwa hata shilingi ya pesa,…

Mioyoni mwao walikuwa wakimshukuru mungu pamoja na sarah, mana kwa maisha yao yalivyo wasingeweza kulipia huduma za pale hospitalini….

Kwakuwa chidi hajawahi kufika kwa kaka yake hivyo hajui hata wanapoelekea, ila Ibrahim yeye ndio alikuwa akimwelekeza sarah Mpaka wakafika katika nyumba aliokuwa akiishi Ibrahim,… Ibrahim hakuwa amejenga bali alikuwa kapangisha vyumba viwili vya pamoja (.. Dabo Rumu..) na ilikuwa nzuri yenye umeme na kila kitu, Kiukweli kwenye upande wa chumba kidogo alijitahidi kiasi flani kwani hata sarah aliona ni kawaida tu,…

Walifika ndani wakaweka mizigo yao na dawa za chidi huku chidi akiwa kakaa katika sofa…

Ghafla Ibrahim anapokea simu na haijulikani aliokuwa akimpigia ibra..

"haloo…. Ok, nakuja basi sasa hivi"

Aliongea hivyo huku akiwa mtu mwenye haraka haraka baada ya kupokea simu hio,

"jamani naombeni niwaache kidogo"

Ibrahim alimuaga mdogo wake pamoja na sarah kuwa atarudi muda si mrefu..

"sawa kaka, ila hata mimi sikai sana nitaondoka"

"sawa nashukuru kwa wema wako, na nina furaha kwakuwa umepajua nyumbani hivyo tutaendelea kutembeleana"

"ahahaha sawa kaka usijali"

"sawa sawa…. Sasa chidi narudi muda si mrefu sawa"

"sawa broo"

Ibrahim aliondoka huku nafsi ya sarah ikiwa na furaha baada ya kaka yake kuondoka,

"alijuaje kuondoka"

Alinisemea kimoyo moyo huku nae akikaa katika sofa

"chidi"

"naam"

"unajiskiaje for now"

"aahhh nipo freshi sema hii michubuko tu ndio bado haijakauka"

"usijali utapona"

Kimya kilipita cha kama dakika moja hivi huku sarah akionekana kuangalia chini, kana kwamba hakuwa na stori zingine tena,..

"chidi, mi nataka kuondoka"

Sarah aliuvunja ukimya kwa maneno hayo, huku chidi akimjibu kuwa

"sawa, nisalimie huko nyumbani kwenu"

"sawa…. Lakini ndio naondoka ivyo"

Sarah aliendelea kuaga kila mara kana kwamba chidi alitakiwa kufanya kitu kama mwanaume lakini chidi hakuwa akilifahamu hilo, hivyo alibaki kuwa kimya muda wote,

"chidi jamani, mi naondoka eti huna la kuniambia"

Chidi bado alikuwa mzito kujua ishu inayomfanya sarah aage age kila mara,

"sarah, we nenda tu, kama ni pesa tunayo wala usijali"

INAENDELEA...

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni