MAMA MWENYE NYUMBA (69)

Zephiline F Ezekiel
0
Mwandishi: Mbogo Edgar

SEHEMU YA SITINI NA TISA
“Nyie visilani ondokeni sie tuendelee na sherehe zetu za kukaribisha mkwe wangu,” alisema mama huyu kisha akaelekea kwenye mlango wanyumba kubwa akifwatiwa na wageni wake

SASA ENDELEA...
Naaaam maisha yalianza hivyo kwa Suzane baada ya kufika Songea, ilikuwa nizaidi ya changamoto, baada ya kushuhudia ndoa ya wifi yake na bwana kazole ikivunjika huku wifi zake wakirudi kwa mama yao na kuomba msamaha, wakati huo huo mzee Magige na vijanawake waliamishwa sehemu mbali mbali, huku mzee Magige mwenyewe akiamishiwa Tabora, ikiwa ni msaada wa RPC akiwaokoa kwa kesi ya uvamizi wa hotel

Ilisha pita miezi saba na week kadhaatoka Suzane aamie Songea licha yakufungua ofisi zao binafsi za usanifu wamajengo na kununua nyumba yao na mashamba makubwa ambayo wali weka mifugo mingi sana kuanzia kuku bata ng’ombe mbuzi nk. pamoja na kuongeza gari jingine moja aina ya Toyota wish, pia Suzane alichukuwa likizo ya mwaka na kwenda Iringa kwa wazazi wake kumtambulisha mume wake mtarajiwa, wakiongozana na mzee Ngonyani kama mshenga, posa ilipokelewa, vizuri bila pingamizi, Suzane aliendelea kuwasiliana na Joyce huku akimtumia fedha za matumizi kila mala, akuruhusuwa kuwasiliana na Edgar, Joyce ambae na yeye ujauzito wake uliendelea kukua vizuri pasipo matazo yoyoye alikubariana na shalti la kuto kuwa siliana na Edgar

Edgar aliendelea na shughulizake za kutengeza ramani za majengo makubwa ya serikali na taasisi binafsi, pia alijitaidi sana kumwonyesha upendo wa hali ya juu mke wake, na kumfanya suzane au mama kijacho ajisikie furaha muda wote, tatizo la Edgar aliendelea kuwasiliana na Rose kwa siri ambae alikuwa ni fafiki mkubwa wa Suzane na Seline ambae ali wakutanisha Suzane mwenyewe, pasipo kujuwa kuwa Rose na Edgar ni wapenzi wasiri

Siku moja suzane akiwa katika matazamio ya kujifungua, alikuwa ame kaa sebuleni huku Edgar alikuwa jikoni ana mkaangia mayai, mala Suzan akaona simu yake ikiita, akaitazama iliuwa namba ngeni, akaipokea, “hallow habari” alisalisalimia Suzane mala baada ya kupokea simu, “mambo Suzie,”ilisikika sauti ya kike upande wapili, aikuwa ngeni masiikioni mwake, akajaribu kuikumbuka niyanani “poa habari za wapi?” aliuliza Suzane kwa mtego, pengine ange nge fahamu ninani, “haaaa! best ume nisahau, Sophia hapa, habari za Songea” hapo mapigo ya moyo ya Suzane yaka ongeza speed kwa mstuko, lakini akajikaza, “safi tu za dar,?” aliongea Suzane akihisi kijasho chembamba kiki mtoka, “huku safi nilitaka nikujulishe mambo mamwili, mwenzio nime pata mtoto wakiume, pia mama yupo Hospital amejifungua mtoto wa kike,”

Taarifa hiyo ya Sophia aiku mstua sana Suzane, japo ilimshangaza kidogo, “he ina maana mama alikuwa mjamzito?” aliuliza Suzane wakati huo Edgar alikuwa anakuja sebuleni na saani ya mayai ya kukaanga na grass mbili za maziwa, “ndiyo tume pishana siku moja kujifungua, sasa nilikuwa naomba uni saidie kitu kimoja” alisema Sophia, “wala usijari best, sema tu nikusaidie nini?” aliongea Suzan akitaka Edgar asijuwe anaongea nanani, “msaada mdogo tu best, nitafutie nyumba, nime amishiwa Songea mjini” kiukweli hapo Edgar ambae alkuwa ajuwi Suzane anaongea na nani akashangaa mpenzi wake akikata simu na kuiweka kwenye kochi, akajishika tumbo na kiuno huku akikunja sura, kuonyesha kuwa alikuwa katika maumivu makali.“mume wangu nipeleke Hospital”

Alisema Suzane huku akiendelea kujishika tmbo na kiuno upande wa mgongoni, “vipi tena Suzane, kuns nini?” Edgar aliongea kwa huku akionekana kustushwa na tukio lile, “chukuwa lile begi langu lenye vitu vya kujifungulia twende unipeleke Hospital Eddy, uuuwwwwiiiiiii jamani mimi leo” hapo Edgar akamnyanyua mpenzi wake utazani mtoto mdogo, akamwingiza ndani ya gari, kisha akarudi ndani na kuchukuwa ule mkoba ambao mke wake aliununua mwezi mmoja uliopita, na fedha kiasi cha laki tano, alafu akaichukuwa simu ya mke wake akaizima kisha akaenda kwenye gari, hapo safari ya Hospital ikaanza, huku Edgar akipiga simu kwa mama yake na pia kwa Selina na Rose ambae sasa alikuwa rafiki wa karibu wa Suzane

Saa nane mchana ndani ya Hospital ya Pelamiho iliyopo nje ya mji wa Songea, ndani ya mji mdogo wa pelamiho, ndani ya Wadi moja ya VIP, walionekana ndugu jamaa na marafiki wa Edgar na Suzan, wasio pungua ishilini, huku wengi wao wakiwa wame valia sale za wafanyakazi wabenk, na zawadi zao mikononi, walikuwa wamezunguka kitanda cha wagonjwa, kilicho laliwa na Suzane ambae alionekana akiwa amemshika mtoto mikononi mwake, kila mmoja akimsifu mtoto yule kuwa kiume kuwa ni mzuri,, kwa maana hiyo Suzane alijifunguwa salama kabisa mtoto wa kiume aliepewa jina la Eric.

Licha ya kuwepo kwa watu kama mzee Haule na mke wake, mzee Ngonyani kijana Milinga Shemeji yake Edgar, Seline na Rose, lakini dada zake Edgar alikuwepo mmoja tu ambae ni yule dada mkubwa aliekuwa mke wa bwana Kazole, wale wengine awakuwepo, kwani bado walikuwa na kitu mioyoni mwao, japo mwenzao alikuwa amegutuka toka upumbavuni, wao waliendelea kumchukia Edgar na mke wake wakidai anamajivuno anajiona sana nk. Siku ya pili mchana, Suzane aliluhusiwa na kurudi nyumbani, wakiwa ndani ya gari wanarudi nyumbani, mtoto akiwa ame pakatwa na suzane mwenyewe licha ya uweo wa binti wa kazi mle ndani ya gari, ndipo Edgar au baba Eric akakumbuka jambo, “hivi kabla ya kushikwa na uchungu ulikuwa unaongea nanani kwenye simu?” aliuliza Edgar, “haaaaa naomba usini kumbushe tena ebu ngoja kwanza naomba simu, Yangu ” alisema Suzan akionyesha kuingiwa na unyonge wa ghafla

Edgar akampa simu Suzane, Suzane akaiwasha maana toka jana Edgar aliizima simu kuofia kusummbuliwa kwa mama mzazi “yani huyu mshenzi anataka namie Nachingwea” alisema Suzane huku akitafuta ile namba ngeni iliyo mpigia jana, alipo ipata akaipiga, na baada ya mda mfupi ika pokelewa, “hahahahahahaaa niambie best” alipkelewa na sauti ya Sophia iliyo ambatana na kicheko, nikicheko kilicho kuwa kelo kwa Suzane, “eti ulisema unaamia wapi?” aliuliza Suzane bila kuitikia salamu ya Sophia, “hahahahahaaa wacha unikatie simu best, hahahahahahaha” Sophia aliendeleza kicheko ambacho kili mwambukiza Suzane na yeye akajikuta akicheka, kicheko kilicho ambatana na hasira, “besti nilikuwa naakutania, siwezi kukufanyia hivyo wangu, kilichobaki tulee watoto,” kauli hiyo ili mfanya Suzane aachie tabasamu la matumaini

“Ahsante Sophi kweli ume amua kitu kizuri, na mimi nimesha jifungua mtoto wa kiume” alisema Suzane sasa akionekana kurudi katika hali yake ya kawaida, “fungua data ni kutumie picha za mwanangu na mdogo wangu, yani mtoto wa mama” alisema Sophia, “ok poa ila mwambie mama miezi mitatu mbele tuna tarajia kufunga ndoa, huku huku Songea” alisema Suzane, siyo kwamba ali mshangaza Sophia peke yake, alimshangaza na Edgar pia, ambae akuwaza kama kuna kufunga ndoa, hapo wakaagana na kukata simu, “Afadhari, dah! alitaka kuni changanya huyu kichaa” alisema Suzane akimwambia Edgar, ambae mda wote alikuwa anaendesha gari huku akifwatilia maongezi ya mke wake, “nani huyo sophia?” aliuliza Edgar, 

NAOMBA SAPOTI, KUNA MATANGAZO(ADS) YANAJITOKEZA KWENYE APP YETU, LIMOJA LINAJAA KWENYE KIOO CHAKO JINGINE LINANG'ANG'ANIA HAPO CHINI KABISA, BONYEZA JAPO MARA 2 AU 3 KILA UKIFUNGUA SIMULIZI HIYO ITANIPA NGUVU YA KUENDELEA ZAIDI NA SIMULIZI ZETU🙏🙏

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO



USIKOSE SEHEMU YA SABINI

Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)