MAMA MWENYE NYUMBA (69)
JINA: MAMA MWENYE NYUMBA Mwandishi: Mbogo Edgar SEHEMU YA SITINI NA TISA ILIPOISHIA... “Nyie visilani ondokeni sie tuendelee na sherehe zetu za kukaribisha mkwe wangu,” alisema mama huyu kisha akaelekea kwenye mlango wanyumba kubwa akifwatiwa na wageni wake SASA ENDELEA... Naaaam maisha yalianza hivyo kwa Suzane baada ya kufika Songea , ilikuwa nizaidi ya changamoto, baada ya kushuhudia ndoa ya wifi yake na bwana kazole ikivunjika huku wifi zake wakirudi kwa mama yao na kuomba msamaha, wakati huo huo mzee Magige na vijanawake waliamishwa sehemu mbali mbali, huku mzee Magige mwenyewe akiamishiwa Tabora , ikiwa ni msaada wa RPC akiwaokoa kwa kesi ya uvamizi wa hotel Ilisha pita miezi saba na week kadhaatoka Suzane aamie Songea licha yakufungua ofisi zao binafsi za usanifu wamajengo na kununua nyumba yao na mashamba makubwa ambayo wali weka mifugo mingi sana kuanzia kuku bata ng’ombe mbuzi nk. pamoja na kuongeza gari jingine moja aina ya Toyota wish , pia Suzane alichukuwa likizo ya mwaka na kwend…