MTAA WA TATU (1)

Zephiline F Ezekiel
MTAA WA TATU (1)
JINA: MTAA WA TATU Mwandishi: Hafidhi J Ikram SEHEMU KWANZA Ndani ya nyumba moja hivi, kuna kelele ziliweza kusikika. kelele ambazo bila shaka mpigaji atakuwa kapandisha mashetani. “niachee"......uuwiiiiiiii huyu mchawi Nimesema tokaa!!!... ndani ya nyumba hiyo milango yote ilifungwa si uwani wala barazani, Wakati nyumba hii kelele za Binti aliyepandisha mashetani zikisikika, Nyumba nyingine kulikuwa na sauti ya vicheko, sijui wanacheka nini, nyumba nyingine kulikuwa na sauti ya vilio sijui wanalia nini. Nyumba nyingine kulikuwa na ugomvi baina ya vijana wawili kila mmoja akisema “Matrida ni wangu mimi" Katika purukushani kukuru kakala baina ya vijana wale mmoja kati yao akadondoka chini huku akipaza sauti jamani...." Nakufaa".....kumbe mwenzake alitoa kisu na kuanza kumchanachana. Yote yanatokea ndani ya kitongoji kimoja, kitongoji ambacho kipo nchini Tanzania jijini Dar es salaam , kinaitwa Mtaa wa tatu Mtaa ambao Ni zaidi ya sodoma na gomora watu wanaishi kama wanyama, Wengi wa vijana…