BIKRA YANGU (4)

0
Mwandishi: Emmanuel F. Kway

SEHEMU YA NNE
ILIPOISHIA...
Ndani ya gari Sabrina aliendelea kulia huku akizidi kumtingisha Catherine ambae wakati huo alikua kimnya sana. Wala haongeoi tena, alikua ame fumba macho yake kama aliye kua amekufa au amelala usingizi mzito, hali ile ili mtisha sana mama yake , alijua kumpoteza Catherine ata poteza kitu muhimu sana chini ya jua pengine ulimwenguni, Catherine alikua ndiye mtoto wake wa kipekee na hakutaka kuzaa mtoto mwingine yoyote Yule, alilia sana hasa alivyo mkumbuka Ramsey , hakuelewa
Nini ange mwambia au ange mfanya nini kama angelikua hai baada ya kusikia mwanae kafa, alilia sana huku akimuomba Mungu asimchukue mwanae sababu bado ni mdogo sana kufa,, hakuacha kujilaumu kwa kitendo cha kumpiga mwanae!,

SASA ENDELEA...
Taxi hiyo haraka haraka ili fika nje ya hospitali iyo ya wilaya na kabla ya taxi kusimama tayari Sabrina alifungua mlango na kuruka nje huku akikimbilia ndani akiomba msaada wa manesi, nao hawa kucheza mbali haraka haraka walitoka na kitanda chenye magurudumu na kumuweka Catherine juu ya kitanda hiko huku kikianza kusukumizwa haraka haraka, ndani ya chumba maalumu, nesi mmoja alikuja na chupa ya dripu na kuitumbukiza ndani ya mshipa wa damu ili maji yaweze kuingia mwilini mwake,

“subiri nje mama”
“kwanini? ni mtoto wangu huyu wa kumzaa”
“ndio tuna elewa huruhusiwi kuingia humu, tuache tufanye kazi yetu wenyewe”
“EEEH MUNGU weeeeee”!
Alilia Sabrina huku akiweka mikono yake miwili kichwani na kupiga piga miguu chini, kitendo cha Catherine kuingizwa ndani ya chumba cha wagonjwa mahututi kina mfanya azidi kuchanganyikiwa sana,
“tsup Dad,”(habari yako baba)”
“nili kwambia nini Enock, usiwe una nisalimia mimi kihuni, na vua hayo mahereni yako masikioni, usilete uma rekani hapa , upo AFRIKA tena Tanzania, usinilete habari iyo tsap tsap yako siitaki, sema shikaamo Baba”
“come on Dad, what is wrong with yah haaah(mbona ivyo baba! Tatizo nini?). Okay okay easy easy Shikamoo BABA”
“namna hiyo marahaba mwanangu, ukiwa una nia mkia ivyo , nitafurahi, I will be proud of you son(nita jivunia kuwa nawewe kijana wangu).”
“okay Dad, see you,(sawa baba tuta onana ) naenda JOB”
“ila una kumbuka kuwa kesho ni siku ya kwenda kumuona mama yako gerezani?”
“ndio nakumbuka hata juzi nilivyo enda THEY TOLD ME THAT,(waliniambia) nita enda kesho,”
“ila mimi sitoenda, sasa sikiliza uki fika ofisini pale mwambie Sakina anitumie laki tano”
“sawa Dad, take care, see you later”(kuwa mwangalifu, nita kuona baadae)”

Yalikua ni mazungumzo kati ya Enock na baba yake mzazi mr, mwasha , asubuhi ya siku iyo wakiwa ndani ya nyumba kubwa ya kifahari, ambayo waliishi wawili tu, yeye na baba yake, hakika bado kulikua na pengo kubwa hapo kati kati MAMA ambae ni jOsephine., Enock aliumia sana kwa kitendo cha mama yake kuwa gerezani, ila hakua na jinsi yoyote ile, sasa hivi ni mtu mzima alielewa fika kabisa kilicho fanya mpaka mama yake awepo gerezani, mara kwa mara alipenda sana kumtembelea mama yake gerezani akimpelekea

chakula na vitu vingine kadhalika, MAMA NI MAMA hata kama akikosea ata baki kuwa mama tu, hiko ndiko kilicho kua ndani ya akili ya Enock,

Baba yake ali mkabidhi kampuni ya NISSAN iliyopo posta ambayo hapo awali ili kua ikiendeshwa na mama yake na yeye leo kuimiliki akiwa kama MKURUGENZI , hakikaa aliiendesha vizuri na kurudi katika hali yake ya zamani,

Akiwa na mabuti yake makubwa huku kichwani akiwa amevaa kofia aina ya chepe iliyo andikwa DOPE aliizidi kudunda na kuliendea gari aina ya JAGUAR na kulitia moto akitoka nje huku baba yake akimsindikiza kwa macho, mavazi yale yali mchukiza sana baba yake, ila hakua na jinsi aliamini ipo siku atabadilika lakini hakujua ni lini.

Baada ya kufika ofisini anaendelea na shughuli zake za hapa na pale, jioni ilivyo fika aliwasha gari na kuondoka akirejea nyumbani, siku hiyo jioni

kabla ya kufika nyumbani alipita katika moja ya SUPER MARKET na kuta futa chakula kizuri kwa ajili ya kesho ampelekee mama yake gerezani,.

alinunua burger, pizza na vingine vingi akiamini kua mama yake ata weza kufurahi sana, baada ya kumaliza hapo alitoka na kuingia ndani ya gari na kuondoka zake, alifika nyumbani, kwa kua kulikua hakuna hata mlinzi ili mbidi ashuuke na kufungua geti, aliirudi ndani ya gari na kuliingiza gari ndani katika moja ya maegesho ya magari.
.
Ukimnya ulio tawala alijua kua baba yake ameshalala tayari ivyo hakutaka kumsumbua alipitiliza mpka chumbani kwake na kuji mwagia maji, baada ya hapo alijitupa kitandani huku akiwaza kesho ita kavyvo kua.

Kulivyo kucha kama kawaida alimsalimia baba yake na kumuaga huku akiwa na vifurushi mikononi vya chakula alivyonunua jana yake, alivaa miwani yake nyeusi na jins nene huku chini alivaa mabuti
makubwa ya njano, shingoni alikua na mikufu ya dhahabu na hereni pia, unge bahatika kumuona ungesema hakua

mtanzania alikua ni mmarekani mweusi pengine unge mfananisha na P.DIDY mwimbaji wa marekani , jinsi alivyo chonga nywele zake zika shuka chini yaani timberland na kuchora O , hakika alikua kijana mmoja wa kuji tunza sana na kuji penda sana, alikua mrefu kama baba yake Mr, Mwasha alikua na rangi ya chocolate, sura yake ili kua pana kidogo,, macho yake ya ukali aliridhi kwa baba yake, na vingine alichukua kwa mama yake, kama pua na mashavu,

Aliingia ndani ya gari na kukanyaga klachi na kuweka mkono wake juu ya gia , ambapo alisogeza mpka kwenye herufi R na gari hilo aina ya BENZ kuanza kurudi nyuma taratibu, alivyo ridhika alirudisha kwenye gia nambari moja na kuanza kulitoa gari nje taratibu, alishuka na kufunga geti alivyo hakikisha kila kitu kipo sawa, aaliirudi ndani ya gari na kuondoka kwa safari moja tu kuelekea MAGEREZA YA Segerea ambapo siku iyo ilikua maalumu kwa ajili ya kuwaona wafungwa, ndugu jamaa na marafiki siku hiyo hujumuika na kwenda kuwaona watu wao waliio kua gerezani.

Dakika chache baadae alikua tayari kafika maeneo ya magereza na kushuka huku akiwa na mifuko ile ya chakula,
“nataka kumuona MY MOM(mama yangu).
Alimuongelesha askari mmoja aliye kua mapokezi,
“ana itwa nani”?
“Josephine David MWASHA,”
“subiri kidogo”
Askari Yule alipekua pekua mafaili yale yaliyo kua pembeni yake na kumuangalia Enock,
“kijana”?!
“yes”
“Mama yako ulisema ana itwa Josephine Mwasha”?
“yap ndio,”
“samahani kwa usumbufu, masaa mawili yaliyo pita amewahishwa hospitali ya taifa Muhimbili, ana hali mbaya sana,”
“whaaaaaaat, (nini)?… I don’t understand (sielewi).. aan aumwa nini yupo hospito gani? ”)
“kapelekwa MUHIMBILI hakika bado hatu jajua aise lak….”

Kabla ya kumalizia kuongea tayari Enock alianza kuli kimbilia gari lake alilo kuja nalo, alizama haraka haraka na kulitia moto, aliweka gia namba moja na kukanyaga mafuta, gari lili toka kasi na baada ya sekunde kadhaa tayari gia ilikua namba tano kuashiria kua Gari ili kua katika mwendo wa kasi sana, alitembelea gia iyo na kupangua baada ya kuona kona ila ailivyoiakata alirudisha gia namba tano, kwa kua ilikua ni siku ya jumapili hakukuwa na msongamano wa magari, tayari alikua maeneo ya upanga na sasa hivi alikata kona na kuzunguka round about ya Muhimbili, aliweka gari pembeni na kushuka haraka haraka,

Alienda moja kwa moja mapokezi, haikua shida kumpata MAMA yake sababu alijielezea kuwa alikua ni mfungwa,

katika kugeuga aligongana kikumbo na mwanamke mmoja ambae alikua hamfamu na wote kudondoka chini,
“sorry”(samahani)!”
Aliinuka haraka haraka na kutimua mbio ambapo huko alielezwa kuwa ndipo mama yake alipo. Kweli alipo fika ndani ya wodi hilo alimkuta mama yake akiwa mwenye pingu mkono mmoja ambayo ili fungwa kwenye kitanda, huku pembeni yake kukiwa kuna askari akiwa na SMG ,
“mwanangu naumwa sana”
“Mama utapona. Every thing is gonna be okay , TRUST me MOM, I love you MOM, (kila kitu kitaenda sawa, niamini Mama, nakupenda Mama).

Aliendelea kumfariji Mama yake alivyo geuza shingo alimuona Mwanamke aliyemgonga kikumbo yupo pembeni yake, na alipo simama pembeni yake alikua Amelala binti wa kike
“Mwanangu Catherine utapona, samahani kwa niliyo kufanyia”

Sabrina aliiongea maneno yale na kumfanya Enock amuangalie msichana Yule aliye kua kitandani, na wote kugonganisha macho yao na msichana Yule aliye kua kitandani yaani Catherine…

BAAADA ya madaktari kukaa kikao kidogo ndani ya chumba kidogo na kutoka na majibu ambayo yaliwa ogopesha sana wana aamua kufanya mipango ya kumuamisha hospitali iyo kutokana na uhaba wa vifaa , Catherine siku ya pili sasa alikua bado haja zinduka kitandani hii ni kutokana na ubongo wake wa nyuma kuumia vibaya mno, iisingekua kumuwahisha hospitali wenda ange poteza uhai wake kama sio kupata ugonjwa wa kupooza milele, madaktari wa hospitali ya taifa ya MUHIMBILI walipewa taarifa juu ya ujio wa msichana huyo ambaye alikua bado mdogo sana kupoteza maisha yake, hawa kutaka jambo lile litokee, ivyo wali fanya kazi kwa kina sana ili kuokoa maisha ya Catherine.

Gari la wa wagonjwa tayari lilkua nje likipiga kelele za king’ora , baadae kidogo Catherine anaingizwa ndani ya gari hilo na safari ya kuelekea hospitali ya taifa kuanza, huku nyuma mama yake akiwa pembeni yake, picha ya Ramsey siku ya kifo chake ina zidi kuji rudia rudia, sababu ili kua ni kama siku iyo,

Gari hilo tayari lili fika hospitalini hapo na Catherine kupatiwa matibabu ya haraka sana, baada ya siku nne kupita hali yake ilizidi kuwa nzuri na kurejewa na fahamu jambo lile lili mfurahisha sana mama yake , ila bado roho ilimuuma sana kwa kitendo cha kumpiga mtoto wake, hakuwa na jinsi zaidi ya kuji shusha na kumuomba msamaha akiwa yupo kitandani hospitalini pale,

“mamii nisamehee mwanangu”
alizungumza mama yake.
Catherine aligeukia upande wa pili na kumuona askari mmoja aliye shika mtutu huku juu ya kitanda kuna mwana mke ambaye alikua na pingu pembeni yake alimuona mwana ume aliye vaa hereini, alizidi kuwaangali bila kumsemesha mama yake,
“mama usijali wewe ni mama yangu, najua ulifanya vile ili kuni fundisha . haina haja ya kuniomba msamaha, naomba unisamehe mimi”
Catherine aliiongea kwa utulivu sana huku bado macho yake yakiwa malegevu kutokana na dawa alizo pewa, dripu ilizidi kushuka taratibu ndani ya mshipa wa mkononi,
Kadri siku zilivyo zidi kwenda ndipo Catherine hali yake ilizidi kua njema, mwishowe aliruhusiwa kwenda nyumbani baada ya hali yake kuwa sawa kabisa,
Juma moja lili pita bila ya kwenda shule kutokana na mama yake kuma kataza mpaka hali yake itakapokua sawa kama hapo awali, kweli hali yake ilizidi kuwa nzuri na baadae kurudi shule ili kujuimika na wana funzi wenzake ambao walionekana kumchangamkia sana alipo fika shuleni,
“cate ulikua na tatizo gani mbona shule ulikua huji”?
“nilikua naumwa Rose, “.
“nini tatizo”?
“malaria tu”
“pole sana umepona lakini”?
“nime pona tayari, vipi mmefikia wapi Geography, utaniazima madaftari yako nianadike notes za nyuma”
“sawa, ila Adam bado anakuomba uwe girlfriend wake”
“lakini si nilisha kwambia Rose mimi siwezi kua nae”
“nakuomba muonee huruma binamu yangu”
“hapana siwezi”
“kwani Catherine, una boy au”?
“wala sina”
“Sasa kwanini una mkatalia binamu yangu, ana kupenda kweli”
“muda wangu bado”
“bado kivipi sasa?, kwani huja wahi kusex na mwana ume mpaka useme bado”?
“sijawahi,”
“mmmh mimi nabisha”
“kama una bisha basi, ila ukweli ndo huo”

KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)