NIFANYE NAMIMI KAKA (10)

0
Mwandishi: Juma Hiza

SEHEMU YA KUMI
ILIPOISHIA...
Niliamini nilikuwa tayari nimeshampoteza Evadia katika maisha yangu, katika maisha ya simulizi na chombezo ambazo nilikuwa nikiziandika, niliamini sikutakiwa kumuona tena Evadia msichana ambaye kwa kweli alikuwa na uzuri wa kipekee sana na laiti kama ungepata bahati ya kukutana naye naamini ungeyasahili maneno yangu kwa kukubali kuwa alikuwa ni mzuri haswaa.
SASA ENDELEA...
Sikutaka kuendelea kujilaumu pale kitandani, niliamua kumpigia simu lakini hakuwa akipokea, niliendelea kumpigia na mwisho alikuwa akinikatia. Nilizidi kuwa katika wakati wa mawazo sana hasa baada ya kugundua kuwa nilikuwa nimemkosea sana Evadia.

Nilimpigia simu Mick yule rafiki yangu mkubwa sana ambaye nilikuwa nikisaidiana naye mambo mengi na mara baada ya kumpigia aliweza kupokea.
“Niambie mzee wa totoz,” aliniambia mara baada ya kupokea.
“Ndugu yangu we acha tu!”
“Niache nini sasa?”
“Yule mtoto ameingia kingi mwenyewe.”
“Duh! We noma kaka kwahiyo umeshajilia vya utamu.”
“Nadhani unanifahamu vizuri huwa sicheleweshagi lakini kuna tatizo.”
“Tatizo?”
“Tatizo gani?”
“Nimefanya naye mapenzi kwa kumlazimisha.”
“Kivipi?”
“Hakuwa amepanga kufanya mapenzi na mimi.”
“Kwahiyo alikuja magetoni kuimba taarabu au?”
“Hapana kuna mchezo nilimchezea.”
“Mchezo gani?”
“Nilizihack akaunti zake na niliamua kutumia njia hii ili aweze kuja geto kwa lengo la kumtatulia tatizo lake na kweli aliweza kuja.”
“Kwahiyo kumtatulia tatizo ukamtatua kweli.”
“Dah! Mtoto kaniona mimi sio kabisa ameondoka lakini anaonekana kukasirishwa sana na kitendo nilichokuwa nimemfanyia.”
“Dah!”
“We acha tu ndugu yangu.”
“Sema Dick wewe sio wa kulilia wanawake kwani huyo mmoja akiondoka kuna nini, utakuwa umepungukiwa na nini wakati kila siku wanawake wanazidi kujigonga kwako.”
“Tatizo sio hilo.”
“Tatizo sio hilo ni nini sasa?”
“Hivi umemuona au unazungumza tu.”
“Wazuri wangapi bhana umekutana nao?”
“Mick baadae.”
“Hahaha! Haya bhana naona mtoto amekuchanganya,” aliniambia na huo ndiyo ulikuwa mwisho wa mazungumzo yetu kwenye simu.

Nilizidi kuwa katika wakati wa mawazo sana, sikuwa najua nilitakiwa kufanya nini kwa wakati huo ili niweze kumrudisha Evadia katika hali yake ya usawa aliyokuwa nayo mwanzo, nilikuwa nimemkosea tena nilikuwa nimemkosea kikubwa sana.

Wakati nikiendelea kuwaza na kuwazua ghafla! Ukaingia ujumbe kwenye simu yangu, haraka niliufungua, ulikuwa ni ujumbe kutoka kwa Precious na alikuwa ameniandikia hivi;
“Mbona umenibadilikia ghafla! Jamani Dick, hutaki kuwasiliana na mimi tena wala hutaki kunijulia hali kabisa au kwa kuwa umeshanijua mwili wangu? Ok basi mimi nilikuwa nakujulia hali. Mchana mwema nakupenda sana.”

Baada ya kuusoma ujumbe wake aliyokuwa amenitumia niliamua kuufuta, sikutaka kuwasiliana naye kabisa kwani kwa wakati ule akili yangu ilikuwa ikimfikiria Evadia msichana ambaye nilihisi kumkosea sana.

Ni kama vile ilikuwa haitoshi kunitumia ujumbe mfupi, alianza kunipigia simu. Sikutaka kuwasiliana naye hata kidogo hivyo sikutaka kuipokea simu yake kwa wakati ule. 

Ilikuwa ikiita mpaka ikawa inakata. Baada ya kunipigia simu mara tatu bila kumpokelea, aliamua kunitumia ujumbe mwingine, ilinibidi nimjibu kwani nilianza kuhisi usumbufu kwa wakati ule.
“Mbona hupokei simu yangu?”
“Samahani nilikuwa mbali na simu.”
“Kwani uko wapi?”
“Niko nyumbani.”
“Kweli?”
“Ndiyo.”
“Uko na nani?”
“Niko peke yangu.”
“Kweli?”
“Ndiyo.”
“Nitaamini vipi?”
“Utaamini vipi kivipi?”
“Kuwa uko peke yako.”
“We niamini kuwa niko peke yangu.”
“Sawa ila…”
“Ila nini?”
“Mbona kama umebadilika sana.”
“Kivipi?”
“Umebadilika tu!”
“Sio kweli mbona mimi nipo sawa tu.”
“Nakufahamu umebadilika sana.”
“Huo ni wasiwasi wako tu! sijabadilika ila muda mwingine unakuta hadithi zinanifanya nakuwa bize sana na ndiyo maana nakuwa sikutafuti kwa wakati.”
“Lini umenitafuta.”
“Ndiyo maana nakwambia nakuwa bize sana mpaka nakosa muda wa kukutafuta ila nakukumbuka sana.”
“Nikuulize kitu.”
“Niulize.”
“Unanipenda.”
“Swali gani hilo unaniuliza.”
“We nijibu kwanza.”
“Ndiyo nakupenda.”
“Nataka leo nije kulala kwako.”
“Uje kulala kwangu?”
“Ndiyo.”
“Na mumeo?”
“Hayupo.”
“Yuko wapi?”
“Amesafiri ameenda Dubai kikazi.”
“Kwahiyo.”
“Mimi nataka kuja leo kwako.”
“Sawa haina tatizo ni wewe tu.”
“Sawa nakupenda.”
“Nakupenda pia.”

Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa Precious kuanza kulala nyumbani kwangu kwa uhuru kama vile alikuwa mke wangu wa ndoa kitu ambacho hakikuwa kweli, alikuwa ni mke wa mtu.

Alikuwa akiutumia ule usemi usemao ‘Paka akiondoka basi panya hutawala.’ Alitawala kwelikweli baada ya mume wake kusafiri kikazi na kila alipokuwa akija kulala nyumbani kwangu sikuwahi kumuacha salama, nilifanya naye mapenzi usiku mzima.
“Unaandika hadithi gani?” aliniuliza usiku mmoja tulipokuwa tumelala, wakati huo alikuwa akinipetipeti.
“Kuna chombezo naliandika kesho linatakiwa kuwa tayari maana washabiki wananisumbua sana.”
“Wanakusumbulia nini?”
“Ninavyochelewa kuwatumia.”
“Mmh!”
“Nini?”
“Mimi naona wivu.”
“Wivu wa nini sasa?”
“Si hao wasichana wanaokusumbua mitandaoni, nahisi unawakubalia.”
“Mimi nimezungumzia habari za wanawake hapa au kuhusu Chombezo.”
“Hata kama lakini mimi naona wivu sitaki usiwe unachat nao mimi sipendi,” 

Aliniambia huku akiwa amekilaza kichwa chake kifuani mwangu, alikuwa akideka kwa wakati ule jambo ambao lilinifanya nianze kuingiwa na hasira.

Precious alikuwa ni mke wa mtu ambaye nilianzisha mahusiano na yeye hapa ilikuwa ni baada ya kukutana na kufahamu kuwa alikuwa ni miongoni wa mashabiki waliokuwa wakizifatilia chombezo zangu mitandaoni.

Alikuwa ni mfanyabiashara wa kujitegemea, maisha yake yalikuwa ni mazuri kwa ujumla, hakuwa na shida ya pesa ndogondogo na kila alipokuwa na mimi hakuacha kunipa pesa, alikuwa akinipa pesa mpaka nikawa siamini kama 

Nilikuwa nimepata bahati ya kukutana na mwanamke aliyekuwa na pesa kiasi kile, shida yake kubwa kwangu ilikuwa ni kufanya mapenzi tu! na alikuwa akinipa kiasi chochote cha pesa nilichokuwa nikikihitaji, alinipa bila kujali lolote kwani kile alichokuwa akikihitaji kutoka kwangu alikuwa akikipata.
“Unataka kiasi gani cha pesa?”aliniuliza asubuhi moja tulipokuwa tumeamka, usiku wa siku hiyo tulikuwa tumetoka kufanya mapenzi.
“Pesa tena?” niliuliza huku nikiyatumbua macho yangu, nilikuwa siamini kile nilichokuwa nakisikia kwa wakati ule kwani hazikuwa zimepita siku chache tangu alipokuwa amenipa pesa kwa ajili ya matumizi madogomadogo yaliyokuwa yakinitatiza.
“Ndiyo pesa nikupe kiasi gani ambacho kitakutosha?” aliniuliza tena.
“Ni wewe tu mimi siwezi kukupangia.”
“Unajua usiku umeniridhisha sana unastahili pongezi kwa kweli, wewe ni dume haswaa tena dume la mbegu.”
“Ponge....” kabla sijamaliza kusema sentensi niliyokuwa nimedhamiria kuitamka kwa wakati ule Precious aliweza kunikata kauli, hapa ni baada ya kuitoa pochi yake akatoa kiasi cha pesa ambazo aliweza kuzihesabu na kunikabidhi shilingi laki tano, akanibusu kisha akaniaga na kuondoka. Nilibaki kinywa wazi huku nikiwa siamini hata kidogo kile nilichokuwa nikikishuhudia kwa macho yangu.-

Precious aliondoka na kuniacha mule chumbani huku nikiendelea kushangaa, nilikuwa siamini kama kweli alikuwa amenipa kiasi kile cha pesa ambazo aliniambia kuwa zilikuwa ni za matumizi madogomadogo.

Hakukuwa na kazi kubwa niliyokuwa naifanya kwake au biashara yoyote kubwa niliyokuwa nikiifanya kiasi kwamba aweze kunilipa kiasi kile cha pesa tena katika siku moja.

Kuna watu maofisini wengine ni wasakatonge wanahangaika mitaani usiku na mchana kuitafuta hata japo shilingi elfu moja wanaikosa lakini mimi ndani ya asubuhi moja ile kuamka tu nakumbana na kiasi kile cha pesa ambazo zilikuwa ni kama pongezi kwa shughuli ya usiku kucha niliyokuwa nikiifanya juu ya kifua cha mke wa mtu ambaye alitokea kulewa na penzi langu kiasi cha kuwa chizi kabisa.

Nilichoamua kukifanya kwa wakati ule ni kuchukua Laptop yangu kisha nikaingia mtandaoni

Facebook pamoja na Instagram ambapo nikaweza kupost machombezo yangu mawili ambayo yalikuwa yakipendwa sana, yalikuwa yakifuatiliwa sana na idadi kubwa ya watu ambao walionekana kuyapenda kupitiliza, kila siku yalikuwa akinipa mashabiki wapya. Machombezo hayo moja lilikuwa ni CHUMBA CHA MASAJI ambalo nilikuwa nikilipost Facebook na lingine lilikuwa ni NITABAKI NA WEWE TU! 

Ambalo nilikuwa nikilipost Instagram na machombezo yote yalikuwa yakifuatiliwa sana, naweza kusema tangu nilipokuwa nimeanza kazi yangu hii ya uandishi wa machombezo haya ndiyo yalikuwa machombezo bora, machombezo yaliyowahi kunipa umaarufu mkubwa sana hasa katika mitandao ya kijamii, kila kona jina langu la 

Kaka Dick au Dick Mapenzi lilikuwa likifahamika, hakukuwa na mtu ambaye alikuwa hanifahamu. Kila siku simu yangu haikuacha kupigiwa na namba ngeni, nilikuwa nikipigiwa sana na namba ngeni mpaka kuna wakati nikaanza kuhisi usumbufu.
“Kaka Dick napenda sana machombezo yako yani pindi niyasomapo huwa nahisi msisimko wa hatari hongera sana,” ilikuwa ni sauti nyororo ambayo ilikuwa ikizungumza kwa upande wa pili mara baada ya kupokea simu, ilikuwa ni namba ngeni kwa wakati huo.
“Asante sana ila hujaniambia unaitwa nani?” 

Nilimuuliza kwa sauti ya utulivu, hapa ni baada ya kugundua kuwa mpigaji wa simu alikuwa ni msichana ambaye alijaaliwa sauti nzuri sana ya kuvutia.
“Oooh, naitwa Helena napenda sana kusoma machombezo
yako,” alijitambulisha Helena kwa sauti ya ukarimu.
“Nashukuru kukufahamu.”
“Asante sana Kaka Dick hivi unaishi wapi?” “Mimi niko Dar.”
“Hata mimi niko Dar wewe uko sehemu gani?”
“Tandale.”
“Wooo, Tandale?”
“Ndiyo kwani vipi?” “Kumbe ni jirani yangu kabisa mimi mwenyewe niko Tandale.”
“Mimi niko kwa Tumbo na wewe
je?”
“Mtogole.”
“Duh! Haya karibu Magetoni.” “Kwani unaishi geto wewe?”
“Ndiyo.”
“Kwani hauna wazazi?”
“Ninao.”
“Sasa kwanini hauishi nao?”
“Katika maisha kuna kipindi kinafika inabidi mtu ukajitengenezee maisha yako hata ndege nao kuna kipindi kinafikia wanatengena na kila mmoja anaenda kutengeneza kiota chake au na hilo pia mgeni?”
“Hapana ila ni vizuri sana nimependa kwa kuwa umekuwa kijana wa kitofauti sana.”
“Kwanini?”
“Ni vijana wachache sana ambao wanakumbuka kama hayo unayoyazungumza na kuyafanyia kazi.”
“Ni kweli.”
“Nafurahi sana kuzungumza na wewe Dick yani nilikuwa natamani sana siku moja kukusikia japo sauti yako kumbe una sauti nzuri hivyo.”
“Hahahaha! Mbona unanipaka mafuta juu ya shati?”
“Hahahaha! Kweli tena.” “Hahahaha haya bhana.”
“Baadae.”
“Poa poa,” nilimjibu kisha akakata simu.

Nilianza kucheka mwenyewe maana nilifahamu fika kama ni swala basi alikuwa tayari ameingia kwenye anga za Simba, ilikuwa ni vigumu sana kuweza kutoka salama, ni lazima angeliwa nyama.

Nimewahi kutembea na wasichana wengi sana, nimejaribu kuwasikia sauti zao nyororo tena wengine walikuwa na sauti nzito mbaya lakini sauti ya 

Helena msichana ambaye alijitambulisha simuni hakika ilikuwa na utofauti mkubwa sana, kuna kitu cha ziada nilihisi kilikuwa kimeongezeka. 

Moyo wangu ukaanza kutamani penzi hata kabla ya kumuona msichana mwenyewe alikuwa amefananaje, niliishi Tandale kwa muda mrefu sana, nilikuwa nawafahamu baadhi ya wasichana waliyokuwa wakiishi humo, kwa kweli walikuwa wamejaaliwa japo akina

Mwajuma Binti Mafujo walikuwepo wengi lakini idadi yao haikuweza kuwafunika wale wasichana wengine wakarimu ambao wangeweza hata kuolewa kabisa.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)