SEHEMU YA KUMI NA MOJA
ILIPOISHIA...
Mwajuma Binti Mafujo walikuwepo wengi lakini idadi yao haikuweza kuwafunika wale wasichana wengine wakarimu ambao wangeweza hata kuolewa kabisa.SASA ENDELEA...
Nilianza mchezo wangu wa kuchat naye, mchezo ambao katika maisha yangu nilikuwa nikiupenda sana, hii ilitokana na umahiri wangu wa kucheza na maneno katika kupangilia beti zangu ambazo kwa kweli hata kama
Angekuwa ni msichana mgumu kiasi gani endapo angeweza kunipa nafasi ya kuwasiliana naye kwa njia ya Message (Ujumbe mfupi.) basi ungenihesabia masaa tu! kwani nilikuwa ninauwezo wa kipekee sana katika kumshawishi msichana mpaka abadili mawazo yake.
“Mambo mdada,” nilimtumia ujumbe mfupi hapa ni baada ya kukaa kimya kwa muda wa masaa kadhaa tangu alipoweza kunipigia simu na kama vile nilikuwa nimemtumia ujumbe muda muafaka kabisa mtoto naye akaweza kunijibu bila choyo nikaanza kumchombeza. “Poa Dick yani nina furaha jamani.”
“Furaha ya nini tena?”
“Kwa kuweza kunitafuta nilijua ungenipotezea.”
“Hahaha! Sio kwa kirahisi kiasi hicho ujue wewe ni sawa na jirani yangu.”
“Hilo nalo neno.”
“Japo halipo kwenye kamusi.”
“Hahahaha! Kumbe unavituko hivi.” “Ah! Mbona kawaida tu!.”
“Yani natamani nikuone maana si kwa machombezo yale unayoyaandika mmmh! Kweli wifi anafaidi jamani.”
“Wifi tena.” “Ndiyo.”
“Kwani ulihudhuria kwenye harusi yangu?”
“Hapana.”
“Sasa mbona unanipa mke wa kufikirika?” “Kwani huna mke?”
“Sina.”
“Ah! Basi mpenzi una mpenzi?”
“Ndiyo ninaye.”
“Anaitwa nani?”
“Chombezo.” “Hahaha embu kuwa serious bhanaaa.”
“Kweli sasa nikudanganye iliiweje?”
“Inamaana huna mpenzi na umaarufu wote huo?” “Umaarufu gani?”
“Wa uandishi.”
“Umaarufu na mapenzi ni vitu viwili tofauti kabisa naomba usivichanganye hata kidogo.”
“Kwahiyo huna mpenzi?” “Ndiyo.”
“Nitaamini vipi?”
“Utaniamini tu!”
“Sawa.”
Nakumbuka nilichat nae muda mrefu sana, nilikuwa nikimchombeza mpaka alikuwa hataki kuacha kuchat, naweza kusema hatukuwa na kikomo katika kuwasiliana kwetu, tulichat sana tena sana tu, mahali tulipochoka tulihamia WhatsApp ambapo huko tuliweza kupigiana kupitia ‘Video Call’ na baada ya hapo tuliweza kutumiana picha mbalimbali.
Helena alikuwa ni msichana ambaye hakuwa na muonekana mzuri sana, alikuwa wakawaida tu! lakini alijaaliwa figa namba nane iliyozidi kumfanya kutamanika.
Nilikuwa nimemtamani sana kupitia baadhi ya picha zake alizokuwa amenitumia hata hivyo alikuwa akiishi karibu kabisa na mahali nilipokuwa nikiishi hivyo sikutaka kuwa mwenye papara sana, niliufahamu uchawi wa mambo yale hivyo sikuwa na shaka hata kidogo, niliamini lazima angejileta mwenyewe kwani kwa muda mfupi tu! niliyofahamiana naye tayari alikuwa amejirahisisha kwa kiasi kikubwa.
Niliendelea kuwasiliana na Helena huku akili yangu ikiendelea kumfikiria Precious. Nilikuwa nikimfikiria sana Precious kwasababu alikuwa akinipa pesa, tangu nilipoanza mchezo huu wa kuwachanganya wanawake, alikuwa ndiye mwanamke wangu wa kwanza ambaye alikuwa akinipa pesa,
Alikuwa akinihudumia mahitaji yangu yote muhimu sasa kwanini akili yangu isijishughulishe katika kumfikiria kila wakati. Nilikuwa nikiutumia muda wangu mwingi sana katika kuwa na yeye. Tulikuwa tukienda katika viwanja mbalimbali vya starehe kujirusha, kipindi hicho mume alikuwa bado hajarudi.
“Utaendelea kuishi huku Tandale mpaka lini?” aliniuliza Precious siku moja tulipokuwa kwenye gari tukirudi nyumbani majira ya usiku tukitokea Ambiance Club iliyokuwepo maeneo ya Sinza Afrika Sana. Wakati huo nilikuwa nimeiweka simu yangu Silence (Kimya) ili nisiumbuke kwani nilifahamu fika muda huo Helena alikuwa akinitafuta hivyo kuhofia usumbufu niliamua kuiweka kimya.
“Unaniuliza mimi?” nilimuuliza huku nikijifanya mwendawazimu nisiyeelewa lolote.
“Sasa kwani naongea na nani?”
“Kwa kweli bado sijajua kuwa nitahama lini halafu kwanza sina mpango huo.”
“Kwanini?”
“Nakipenda sana chumba changu.”
“Unajua huwezi kuishi pale siku zote itabidi uhame ukatafute chumba au nyumba sehemu nyingine.”
“Unazungumzia nyumba au chumba?”
“Vyovyote ila itabidi uhame pale.”
“Pale napapenda kwasababu mwenye nyumba Mke wake anaurafiki na mama yangu kwahiyo pale swala la kodi kidogo inakuwa kitonga sasa unaniambia maswala ya kuhama kwa kazi ipi kubwa ninayoifanya au unataka niumbuke?”
“Dick wewe ni mtunzi mzuri sana wa Machombezo kuna siku ndoto yako itatimia na amini kipaji chako kitabadilisha maisha yako.”
“Maisha yenyewe ndiyo haya tunaishi kwa bahati mbaya nitawezea wapi mimi.”
“Hahahaha!”
“Unacheka.”
“Hapana ila usijali kuna mambo nayaweka sawa yakikamilika nitakuhamisha pale mimi sipendi unavyoishi pale halafu unajua pamekaa kiuswahili sana.”
“Sasa ulitaka pakae kiuzunguni sana.”
“Hahahaha! Embu usinichekeshe mimi subiri nitakufanyia mpango.”
“Unasema kweli?”
“Kweli kwani mimi nakutaniaga?”
“Nitajuaje kama ndiyo utani umeanza leo.”
“Hahahaha!”
Precious alikuwa ni mtu wa kucheka kila wakati, nilifahamu kitu kikubwa alichokuwa akikipenda katika maisha yake ni kucheka, alikuwa akipenda furaha katika maisha yake. Niliitumia nafasi ile kuwa naye katika kujivika vazi la uchizi kisha nikawa najaribu kujifanya katuni za Tom na Jerry ili aweze kufurahi kila wakati na kweli nilifanikiwa katika hilo. Nilikuwa nikiutumia muda wangu mwingi wa maongezi katika kuwa wa uchekeshaji ili asichoke au kujutia kuwa na mimi.
Kwenye gari tulizungumza mambo mengi sana. Safari yetu haikuwa na umbali mkubwa sana ila kutokana na mwendo wa taratibu aliyokuwa akiutumia uliweza kuirefusha safari yetu hiyo ambayo niliitumia katika kuzungumza naye mambo mengi sana ambayo mengine yasiyojulikana.
“Dick unajua ninapokuwa na wewe najihisi mwenye furaha kila wakati,” aliniambia Precious huku akiwa bize na usukani wake, macho yake yalikuwa makini kukitazama kioo cha mbele ya gari kwa wakati huo.
“Kwanini?” nilimuuliza huku nikijikuna kichwani hata hakukuwa na kitu kilichokuwa kinaniwasha kwa wakati huo, nilikuwa najifanyisha.
“Sijui niseme vipi ili uweze kunielewa ila wewe fahamu hivyo,” aliniambia huku akiendelea kucheza na usukani wake.
“Unajua kila mwanadamu ana mtindo wake ambao ndiyo anautumia katika kuishi. Binafsi nina mtindo wangu na wewe unamtindo wako lakini kitu cha kushangaza mtindo huu mtu huwezi kujiona mwenyewe mpaka watu wakutazame, waishi na wewe ndiyo wataweza kuufahamu.”
“Unamaanisha nini?”
“Namaanisha kuwa wewe ndiye ambaye umeona kitu cha tofauti kwangu hivyo unatakiwa uniambie ili na mimi nijue,” nilimwambia kisha nikampa nafasi ya kujieleza, kwanza alianza kwa kujikoholesha halafu akaanza kusema,
“Unajua mume wangu kuna vitu hana sijui nisemeje lakini kuna baadhi ya vitu nahisi hanifanyii mimi kama mke wake.”
“Kama…”
“Napenda kufurahi sana lakini hanifanyi nifurahi muda wote yuko bize na kazi zake akirudi nyumbani unakuta amechoka analala, muda mwingine unakuta najisikia kufanya mapenzi lakini anakuwa hafanyi kama vile ninavyotaka mimi. Tangu nilipoanza kuwa na wewe umekuwa mwanaume ambaye unanifanyia vitu vyote hivyo hata vile ambavyo nilikuwa sivijui umekuwa ukinifanyia na ndiyo maana nakuambia kuwa unanifanya nakuwa mwenye furaha kila wakati.”
“Kwani mmefanikiwa kupata watoto?”
“Hapana.”
“Kwanini?”
“Nafikiri muda wetu bado.”
“Kwani mna muda gani katika ndoa yenu?”
“Mwaka mmoja.”
“Duh!”
“Nini?”
“Aisee hii ni hadithi ya kipekee nilikuwa sifahamu kabisa hili.”
“Hahaha! Umeshaanza mambo yako,”
Aliniambia kisha akanipiga kibao cha kimapenzi kilichozidi kuniweka karibu naye sana. Wakati huo tulikuwa tayari tumefika Tandale kwa Tumbo lakini usiku wa siku hiyo hakutaka kuutumia kulala na mimi, alidai kuwa mume wake karibuni alikuwa anakuja hivyo kuna mambo ambayo alikuwa anaenda kuyaweka sawa, alichofanya ni kunihesabia kiasi kidogo cha pesa kisha akanikabidhi na kutoweka eneo lile.
Nilipoingia katika chumba changu kitu cha kwanza kabisa nilichoamua kukifanya ni kuiangalia simu yangu ambayo nilikuwa nimeiweka Silence (Kimya). Nilikutana na messages (Ujumbe) kumi pamoja na Missed Call (Simu zisizopokelewa) thelathini.
Nilipotoa Pattern ya simu yangu niliingia moja kwa moja katika uwanja wa messages, nilianza kuzisoma moja baada ya nyingine humo niliweza kukutana na ujumbe wa Helena ambaye alikuwa akilalamika kwanini nilikuwa sipokei simu yake, nilikutana pia na ujumbe wa baadhi ya mashabiki waliyokuwa wakiyasifia machombezo
Yangu lakini sikutaka kuamini pale nilipokutana na ujumbe uliyokuwa umetoka kwa Evadia msichana ambaye nakiri ni kweli nilimkosea sana lakini kutokana na kusumbuka kumuomba msamaha na kutoweza kunikubalia niliamua kuachana naye, sikuwa mtu wa kuwanyenyekea wanawake. Alikuwa amenitumia jumbe nne ambazo kila moja nilipokuwa nikiisoma kwa kweli nilijisikia furaha isiyokuwa na kifani.
“Dick mambo?”
“Mzima wewe?”
“Dick!”
“Mbona hupokei simu zangu?”
Hizi zilikuwa ni jumbe nne ambazo alikuwa amenitumia Evadia. Kila nilipokuwa nikizisoma nilijikuta nikitabasamu, sijui ni nini kilichokuwa kimemsibu mpaka akaamua kunitafuta katika siku ile. Hakika nilijisikia kuwa na furaha isiyokuwa na kifani.
Macho yangu yalitamani kutazama walau yaupe nafasi mdomo uweze kusoma jumbe nyingine ambazo zingeweza kunifariji kwa wakati ule, sikutaka kumjibu Helena kwani niliamini hakukuwa na mada nyingine kati yetu zaidi ya mapenzi, niliamini kwa vyovyote vile lazima angeweza kujileta mwenyewe katika himaya yangu.
Nilitamani kufahamu ni nini kilichokuwa kimetokea kwa msichana huyu ambaye tayari akili yangu ilikuwa imeanza kumsahau. Msichana ambaye ni siku chache tu! nilitoka kumuudhi kwa kitendo nilichokuwa nimemfanyia, kitendo cha kumuingilia kimapenzi bila ya yeye kuridhia japo hakuweza kuleta kukurukakara za hapa na pale lakini ni wazi kwa kitendo kile hakikuwa sahihi kumfanyia.
Nilijutia kosa langu na ndiyo maana niliamua kumuomba msamaha kwa wakati ule lakini hakuweza kunikubalia zaidi ya yote ndiyo kwanza alikuwa akinichukia.
Nakumbuka kwa wakati ule nilikuwa tayari nimeshamuondoa katika Program ya kuzihack akaunti zake, nilikuwa nimezitoa kwani kitu nilichokuwa ninakitafuta nilikuwa nimeshakipata.
Niliamua kumjibu na huo ndiyo ukawa mwanzo wa kuukaribisha uwanja wa mazungumzo marefu kati yetu.
“Niambie Eva.”
“Safi tu! Dick mzima wewe?”
“Mimi mzima hofu kwako.”
“Niko poa.”
“Unauhakika?”
“Ndiyo niko poa kwanini umeniuliza hivyo?”
“Hamna nimeuliza tu! kwani nimefanya kosa?”
“Hapana, uko wapi?”
“Niko nyumbani.”
“Mbona ulikuwa hupokei simu yangu?”
“Nilikuwa bize kidogo kwani kuna nini?”
“Kuna kitu nataka kukuambia.”
KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA