SEHEMU YA KWANZA
“Mume wangu leo nataka kukiri jambo moja
kwako, naamini litakukera sana lakini naanza
kuomba radhi nikiwa chini ya miguu yako, ”
alisema Zainabu akimwambia mume wake ,
Masalanda. ..
“Ipi hiyo? Mbona unanitisha mke wangu, mwaka
wa tatu sasa tangu tumeoana hujawahi
kuniambia hivyo .”
“Oooh ! Siku zote nilikuwa nafikiria namna ya
kukwambia mume wangu .”
“Sasa niambie basi .”
Zainabu alianza kuporomosha machozi na
kumfanya mume wake huyo kushangaa na
kukifikiria zaidi hicho kitu ambacho kimemfanya
mkewe aamue kukisema...
NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU
“Labda ameamua kuachana na mimi sasa
anashindwa kuniambia ?” aliwaza Masalanda .
“Utanisamehe kweli mume wangu ?”
“Nitakusamehe mke wangu, we niambie tu.”
“Unajua ... unajua wakati unanioa nilipokwambia
nilizaa mtoto akafa na nikawa sipati mimba
nilikudanganya mume wangu ... ”
“Ooo! Kumbe hukuwahi kuzaa kabisa?”
“Hapana, ila... ”
“Ila nini mke wangu hebu kuwa muwazi jamani!”
“Nina mtoto... ”
“Hee! Una nini ?”
“Nina mtoto mume wangu, nisamehe sana
sikukwambia nilikuficha kwa sababu nilijua
utaniacha wakati nakupenda sana mume
wangu,” alisema Zainabu huku akiendelea kulia.
Kwa mbali , Masalanda alianza kumuonea
huruma mkewe . Ni kweli walioana ukubwani
sana kwani Masalanda alikuwa na mke akafariki
dunia na mpaka kifo mwanamke huyo hakuwahi
kumzalia mtoto.
Wakati anakutana na Zainabu, aliamini atadumu
naye kwa sababu wote ni watu wazima tayari.
Aliamini kwamba kwa sababu alishazaa mtoto
akafa , basi watamtafuta mtoto wao kwa kudura
za Mungu mwenyewe.
“Zainabu, ” aliita Masalanda akitumia sauti ya
unyonge.
“Abee .”
“Hebu nijibu maswali yangu kadhaa
nitakayokuuliza.”
“Sawa .”
“Huyo mtoto ana umri gani ?”
“Miaka ishirini na moja .”
“Anaishi wapi ?”
“Yupo kwa shangazi yake, Tanga.”
“Anaitwa nani?”
“Mwaija .”
“Baba yake yuko wapi?”
“Alishafariki dunia , si nilikwambia. ”
“Hebu fanya mpango aje hapa, tumlee sisi . Mimi
nitakuwa baba yake.”
Zainabu alishtuka kusikia agizo hilo la mumewe
kwani siku zote , shangazi wa mtoto huyo
amekuwa akimwambia afanye juu chini
amchukue binti yake kwani ameanza
umachepele, anahofia asije akapata ujauzito
akiwa nyumbani kwake ikaonekana amemtuma .
“Kweli mume wangu?”
“Kweli , imetoka moyoni mwangu , sina kinyongo
na wewe. ”
Zainabu aliachia tabasamu kavu huku akijifuta
machozi kwa kanga. Mumewe alimkumbatia,
akampiga busu wakakaa sawasawa .
***
Ilikuwa siku ya tatu, Mwaija alikuwa ndani ya
basi la Raha Leo lenye maandishi nyuma
yanayosomeka; Tanga wadeka. Kila mara
alimtumia meseji mama yake akimjulisha
alipofikia. ..
“Mama sasa tunapita Segera .”
Mama yake alimjibu sawa , akamtakia safari
njema.
Moyoni Mwaija alikuwa na furaha iliyopitiliza ,
alitaka sana kuishi na mama yake, hasa
akizingatia kuwa anaishi katika Jiji la Dar es
Salaam ambalo aliambiwa lina kila aina ya raha
na karaha !
Alipofika Chalinze , mama yake alianza safari ya
kutoka Kigogo kwenda Ubungo kumpokea binti
yake huyo ambaye ilikuwa inamuuma sana kuwa
naye mbali .
Basi lilifika, Mwaija akashuka, mama akashtuka
moyoni maana mara ya mwisho alimuacha akiwa
na miaka kumi na nane . Alimshangaa kumuona
amenenepa, amenawiri , ametakata ile mbaya.
Kikubwa zaidi alimshangaza nguo alizovaa.
Mwaija alivaa suruali ya kubana, wenyewe
wanaita skintaiti na t- shirt juu. Kwa umbo
alilokuwa nalo Mwaija , kila mwanaume
alimuangalia kwa uchu wa mapenzi. ..
“Ha mama jamani ,” alichangamka Mwaija na
kumkumbatia mama yake kwa furaha. ..
“Shikamoo mama.”
“Marahaba mwanangu, lakini Mwaija hizo nguo
kweli ni za kuvaa mbele ya watu , si za kulalia
hizo?”
“Hamna mama, ndiyo fasheni yenyewe ya siku
hizi. Mama upo Dar es Salaam lakini hujui
mitindo?”
“Mimi sidhani kama nitapenda mwanangu , hata
baba yako niliye naye siamini kama atakukubali
kwa mavazi haya . Hapa natamani nikupeleke
wapi sijui ukabadili nguo ndiyo twende
nyumbani.”
“Jamani mama , basi nimekuelewa , twende tu
nyumbani nitavaa kanga nikifika. ”
Walianza safari ya kwenda nyumbani Kigogo .
Moyoni mama Mwaija alikuwa anaomba
mumewe achelewe kurudi nyumbani ili wao
watangulie kufika na Mwaija abadili nguo haraka
sana.. .
“Hivi na huyo shangazi yako ina maana alikuwa
hakuoni unavyovaa ?”
“Alikuwa ananiona . ”
“Sawa ? Akawa anakuacha tu unaharibika
hivihivi?”
Mwaija hakujibu swali hilo alihisi halimuhusu
yeye zaidi ya shangazi yake .
Kufika nyumbani, mlango ulikuwa wazi ...
“Mswalie mtume, keshafika huyu , sijui itakuaje?”
alisema moyoni mama Mwaija , wakaingia ndani .
Sebuleni alikaa Masalanda , alipomuona Mwaija
akashtuka.. .
“Karibuni. ..karibuni sana. ”
“Asante , shikamoo, ” alisalimia Mwaija huku
akikaa kwenye kochi kwa adabu .
“Marahaba, za safari?”
“Nzuri .”
“Karibu sana, karibu mwanangu, ” alisema
Masalanda huku akimkazia macho Mwaija na
kumshangaza mkewe kwani uchangamfu
ulikuwa mkubwa tofauti na alivyofikiria.
“Asante sana . Naamini wewe ndiyo baba
mdogo?” aliuliza Mwaija .
“Hapana! Huyo ni baba yako , mambo ya baba
mdogo yanatoka wapi saa hizi hapa ?” alikuja juu
mama Mwaija .
“Sawa , baba!”
“Ni mimi mwanangu .”
Mwaija alifurahia mapokezi hayo kiasi kwamba
alijikuta akifurahi sana tofauti na alivyotaka
kuamini hasa baada ya kushuka stendi Ubungo.
Mwaija alioneshwa chumba chake cha kulala.
Akaingiza mizigo yake ndani , akakiangalia
chumba hicho kisha akakipenda sana.
***
Ilikuwa usiku wa manane, Masalanda aliamka na
kuanza kumuwaza Mwaija . Aliwaza tangu
alipomwona jioni ile akitoka Tanga ...
“Asante , shikamoo. ”
“Marahaba , za safari?”
“Nzuri .”
“Karibu sana, karibu mwanangu. ”
“Asante sana . Naamini wewe ndiyo baba
mdogo?”
Masalanda akazinduka kutoka kwenye mawazo
ya jioni, akasema mwenyewe moyoni . ..
“Anaonekana binti mchangamfu halafu ana akili
kichwani. Ana heshima zake f’ lani. Yale mavazi
ndiyo ya watoto wetu wa siku hizi. ”
Wakati Masalanda akiwaza hayo , mkewe
alishtuka na kugundua kuwa mumewe hakuwa
amelala. Akajua ana mawazo kwani anamjua
vizuri ...
“Baba Mwaija ,” aliita mama Mwaija kwa kutumia
jina la binti yake.
“Naam.”
“Nahisi kama una mawazo sana ?”
“Hapana. Sina mawazo .”
“Kama unayo niambie tu. Unajua binti yetu kaja
kama ulivyomuona mavazi yake , nilimwambia
yale si mavazi ya kuvaa humu ndani , akasema
atajirekebisha kwa hiyo tumvumilie kidogo mume
wangu.”
“Sijayashangaa mavazi mimi , mabinti wetu mjini
siku hizi ndivyo wanavyovaa , sidhani kama kuna
namna.”
“Sasa mawazo ni ya nini ?”
“Nawaza biashara zangu naona kama haziendi
sawasawa kama zamani .”
“Mungu atakusaidia mume wangu, biashara
ndivyo zilivyo , leo nzuri kesho ni mbaya sana .”
“Sawa , nashukuru pia kwa dua zako .”
***
Kule chumbani, Mwaija alikuwa akichati na jamaa
yake wa Tanga mjini anaitwa Seif Mabanda ya
Papa. Licha ya kwamba ilikuwa usiku lakini yeye
hakuona tabu ...
“Mwenzio nimekuja kwa mama Dar , sipo Tanga ,
hajakwambia Mwanakombo?”
“Sijasikia. Unarudi lini ?”
“Mh ! Sijui kama nitarudi tena huko . Mama
hataki.”
“Kwa hiyo ina maana umenimwaga?”
“Jamani sijakumwaga , siku mojamoja we njoo
huku Dar . ”
“Mi sijawahi kufika Dar itakuaje?”
“Mi nitakuelekeza.”
***
Asubuhi Masalanda aliomba kupikiwa chai ili
anywe kabla ya kwenda kwenye biashara zake. ..
“We Mwaija ,” aliita mama.
“Abee mama. ”
“Hebu mpikie chai baba yako sasa hivi .”
Chai ilipikwa ingawa mama Mwaija alishangaa
sana kwani haikuwa kawaida kwa mumewe
kunywa chai asubuhi pale nyumbani.
Baada ya dakika kumi na tano tu, chai ilipelekwa
mezani. Mwaija alibeba kwenye sinia akiwa
ndani ya kanga moja. ..
“Loo !” alihamaki moyoni Masalanda lakini
Mwaija hakusikia.
“Shikamoo baba.”
“Marhaba Mwaija , hujambo mwanangu ?”
“Sijambo baba sijui wewe umeamkaje?”
“Mimi mzima wa afya, nakuhofia wewe na
uchovu wa safari.”
“Nimeamka sawa baba .”
“Haya tumshukuru Mungu wetu. ”
“Ni kweli baba.”
Wakati Mwaija anaondoka, ‘mzigo’ nyuma
ulionekana unavyosumbuliwa na kutembea hasa
ikizingatiwa ile kanga moja tu na umbo la Mwaija
sasa!
“Hivi huyu binti ndiyo nini hivi ?” alijiuliza
Masalanda huku macho yake yakimtoka pima
wakati Mwaija anafuata maji ya kunawa .
“Chai tayari wewe?” mama mtu aliuliza kutokea
uani ambako alikuwa akifagia.. .
“Tayari mama.”
“Weka na maji kama nilivyokuelekeza kila kitu
jana usiku .”
“Sawa mama .”
Baada ya mumewe kuondoka ndipo mama
Mwaija alibaini kuwa , mumewe alikuwa
akihudumiwa huku binti yake akiwa ndani ya
kanga moko , ilimuuma sana!
“We Mwaija .”
“Abee .”
“Wakati unamhudumia baba yako chai ulivaa
hivyo?”
“Ndiyo mama .”
“Ha ! Ha ! Haaa ! Yaani kweli unavaa hivyo mbele
ya baba yako Mwaija ? Hebu jiangalie kwanza.
Ona! Hii mikalio yako ulitaka aione siyo?”
“Hapana mama , ila ... ”
“Ila nini ? Au unataka baba yako aingiwe na ibilisi
juu yako siyo ?”
“Hapana mama , mimi sikujua kama kwa kuvaa
hivi baba anaweza kuingiwa na ibilisi .”
“We hivyo ulivyovaa unaona ni sawa siyo?”
“Ulivyoniambia ndiyo nimegundua si sawa sasa .”
Mama alimwangalia bintiye kwa macho makali
kwa karibu dakika moja nzima huku Mwaija naye
akishindwa kuondoka na kusimama palepale.. .
“Nisamehe mama.”
“Usirudie tena, sawa ?”
“Sawa mama .”
“Haya , kaendelee na kazi zako .”
***
Shughuli zilikuwa haziendi sawa kwa Masilinde.
Kila baada ta muda alivuta picha ya Mwaija. ..
“Yule binti, daa ! Ni shida kwelikweli. Au kuishi
mbali na mama ndiyo kawa vile ? Sasa ni kuvaa
gani vile mbele ya baba ’ake ?”
***
Jioni Masilinde aliporudi nyumbani alimkuta
Mwaija, mama yake alikwenda kudai pesa zake
kwa watu aliowakopesha vitenge .. .
“Shikamoo baba.”
“Marhaba Mwaija , mzima ?”
“Mi mzima baba, pole sana kwa kazi.”
“Nimepoa . Mama yuko wapi?” aliuliza baba mtu
huyo huku akikaa kwenye sofa...
“Alisema anakwenda kudai madeni ya vitenge
sijui.”
“Ooo! Ni ile biashara yake.”
“Nikupikie chakula baba?”
“Hapana, kama kuna juisi naombeni. ”
“Ipo ,” alisema Mwaija huku akienda kuifuata hiyo
juisi...
“Mh !” aliguna Masilinde akimwangalia Mwaija
alivyovaa jioni hiyo. Alivaa gauni fupi , magoti yote
yalikuwa nje huku miguu yenye umbile la chupa
za bia ikionekana vizuri sana na kumfanya
baba’ake azidi kung’ata ulimi .
“Karibu juisi baba .”
“Asante sana mama. ”
Wakati Mwaija anaondoka kwenda kuendelea na
shughuli zake , Masilinde alimtolea macho pima
huku akitingisha kichwa . ..
“We Mwaija .”
“Abee baba .”
“Njoo hapa. ”
Mwaija alirudi haraka ...
“Hebu kaa hapo .”
Mwaija alikaa...
“Hivi hizo nguo zako za ajabuajabu unazovaa
hapa kwangu una maanisha nini? Nani
kakwambia hapa ni hosteli ?”
“Samahani baba, sikujua kama nitakukwaza .”
Mara mama yake aliingia ...
“Afadhali umekuja mama Mwaija ... ”
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI
KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger
Email: ZephilineEzekiel@Gmail.Com