JAMANI BABA (1)

Zephiline F Ezekiel
JAMANI BABA (1)
JINA: JAMANI BABA Mwandishi: Beka SEHEMU YA KWANZA “Mume wangu leo nataka kukiri jambo moja kwako, naamini litakukera sana lakini naanza kuomba radhi nikiwa chini ya miguu yako, ” alisema Zainabu akimwambia mume wake , Masalanda . .. “Ipi hiyo? Mbona unanitisha mke wangu, mwaka wa tatu sasa tangu tumeoana hujawahi kuniambia hivyo .” “Oooh ! Siku zote nilikuwa nafikiria namna ya kukwambia mume wangu .” “Sasa niambie basi .” Zainabu alianza kuporomosha machozi na kumfanya mume wake huyo kushangaa na kukifikiria zaidi hicho kitu ambacho kimemfanya mkewe aamue kukisema... NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU “Labda ameamua kuachana na mimi sasa anashindwa kuniambia ?” aliwaza Masalanda . “Utanisamehe kweli mume wangu ?” “Nitakusamehe mke wangu, we niambie tu.” “Unajua ... unajua wakati unanioa nilipokwambia nilizaa mtoto akafa na nikawa sipati mimba nilikudanganya mume wangu ... ” “Ooo! Kumbe hukuwahi kuzaa kabisa?” “Hapana, ila... ” “Ila nini mke wangu hebu kuwa muwazi jamani!” “Nina mtoto... ” “…