UTAMU WA MCHEZO (7)

Zephiline F Ezekiel
UTAMU WA MCHEZO (7)
JINA: UTAMU WA MCHEZO Mwandishi: Micky Mejah SEHEMU YA SABA ILIPOISHIA... Nilipomaliza kuoga nilinyoosha vizuri kanzu yangu nikachukua na suruali yangu nyeusi nikavalia kwa ndani na sendo zangu nilizonunuliwa na dada cleme mwezi mmoja uliopita nazo nilipigilia kwani nilijua fika ukimfatisha dada cleme basi nitamkosa mtoto salha ambye siku ya kesho saa tisa mchana anaƶndoka kwenda india huko kurudi mpaka baada ya mwezi. NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU SASA ENDELEA... Nilijipulizia body spray yangu kisha nikageuka upande wa pili kwenye kioo na kujitazama nikaona kuna kasoro kwenye nywele zangu nikachukua wese nikajipaka kabla ya kupitisha kitana "sasa hapa nipo fit tatizo kutoka hapa yani ndipo lilipo tatizo lakini lazima niende" Nilipiga hatua kadhaa kabla sijafikia mlango wa chumba changu, nilitazama kitasa kama kilikuwa kigeni kwangu na nilikishka kwa tahadhari kubwa kabla sijakibinya na kufungua mlango taratibu nikapenyeza kichwa kisha kiwiliwili na kuru…