BABU G (7)

Zephiline F Ezekiel
BABU G (7)
JINA: BABU G Mwandishi: Eliado Tarimo SEHEMU YA SABA ILIPOISHIA... “Unatakiwa ufanye pambano la nguvu ambalo litamfanya akukumbuke maisha yake yote..” Mara alinyanyuka pale alipokuwa amekaa akaingia jikoni na aliporudi alikuwa na mizizi hata sikujua ni mizizi ya nini. Alinipa na kuniambia nitafune. Nilisita kidogo lakini sikuwa na jinsi nilianza kutafuna. Haikuwa michungu kama nilivyotarajia la hasha ilikuwa na ladha ya utamu utamu. Babu G hakuishia hapo baada ya muda aliniletea kikombe klichojaa dawa ingine ya kienyeji . NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU SASA ENDELEA... Alinambia ninywe ili nipate hamu ya kufanya lile tendo siku hiyo. Sikuweza kubishana na mzee huyu mimi nilimwamini sana hivyo nilikunywa. Niliona mabadiliko kidogo ya moyo na nikajua lazima dawa hiyo imeanza kufanya kazi. Mapigo yaliongezeka na kijasho chembamba kilinitoka. “Sasa mjukuuu wangu tuendeleee na somo kidogo maana hli litakusaidia sana siku za mbeleni. Unataka nieendelee kukueleza habari za …