MUUZA MAZIWA (5)
JINA: MUUZA MAZIWA Mwandishi: Gift Kipapa SEHEMU YA TANO ILIPOISHIA... “Ah, mh, a-, u-n-a-j-u-a hi-li ka-ba-ti ni bo-vu” “limeharibika , ooh, mungu wangu!” Penina aliongea huku akilisogelea kabati hiloili kuiangalia sehemu ilipoaribika. “ah, hapana wifi usiiguse hapa nimeitegesha , iache hivyo hivyo mpaka atakapokuja fundi kulirekebisha” NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU SASA ENDELEA... Aliongea Lisa haraka haraka. “okey”[sawa] Aliongea Penina huku akitikisa kichwa kuonyesha kwamba ameelewa. “nataka kuoga wifi” “na kweli manaake umechoka kweli kweli wifi yangu” Aliitikia Lisa haraka haraka kwani alijua huo ndio upenyo wa kumtoa muuza maziwa. Na kweli penina alipoingia bafuni lisa aliufungua mlango wa kabati haraka na kumtoa muuza maziwa , akala chakula haraka na kuanza safari ya kutoka nje ya nyumba hiyo , walipofika kwenye mlango wa kutokea muuza maziwa alimbusu lisa kwa mara ya mwisho , alipomaliza kufanya hivyo alitoka ndani ya chumba hicho na kutokeza koridoni ili atoke n…