MUUZA UBUYU (13)
JINA: MUUZA UBUYU Mwandishi: Micky Mejah SEHEMU YA KUMI NA TATU ILIPOISHIA... Nilihisi kichwa kinauma nikamuitaji sana kaka rafiki angalau anipigie simu anielekeze cha kufanya maana nilihitaji mfariji kwa wakati huu ila ckuwa nae hivyo kaka rafiki nilihisi ni mtu anayenitakia mema mno. NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU SASA ENDELEA... Ujumbe ukaingia niliwahi fasta kuufungua namba ngeni "emmy usirudi kijichi nenda kwa mama temeke " nilijibu "Kuna nini kwani? Sikuweza kupata tena jibu zaidi ya nusu saa ilipita nikaamua kupiga simu " namba ya mteja unayompigia haipatikani kwa sasa tafadhari jaribu tena baada, the number..." Nilikata simu kwa hasira ************* Wakati nafika nyumbani(kwa mama mdogo) nilishangaa watu wakiingia kwenye gari aina ya noah wamembeba mdada aliyeonekana ni mgonjwa sana alikuwa amevaa dela nakumbuka, sikutilia maanani japo watu niliowaona nawafahamu niliendelea kutembea ghafla moyo ukawa mzito nikamsimamisha dada fulani ana…