SEHEMU YA KUMI NA TATU
ILIPOISHIA...
Nilihisi kichwa kinauma nikamuitaji sana kaka rafiki angalau anipigie simu anielekeze cha kufanya maana nilihitaji mfariji kwa wakati huu ila ckuwa nae hivyo kaka rafiki nilihisi ni mtu anayenitakia mema mno.NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU
SASA ENDELEA...
Ujumbe ukaingia niliwahi fasta kuufungua namba ngeni "emmy usirudi kijichi nenda kwa mama temeke" nilijibu
"Kuna nini kwani? Sikuweza kupata tena jibu zaidi ya nusu saa ilipita nikaamua kupiga simu
" namba ya mteja unayompigia haipatikani kwa sasa tafadhari jaribu tena baada, the number..." Nilikata simu kwa hasira
*************
Wakati nafika nyumbani(kwa mama mdogo) nilishangaa watu wakiingia kwenye gari aina ya noah wamembeba mdada aliyeonekana ni mgonjwa sana alikuwa amevaa dela nakumbuka, sikutilia maanani japo watu niliowaona nawafahamu niliendelea kutembea ghafla moyo ukawa mzito nikamsimamisha dada fulani anaitwa mwajuma "samahani kwani yule dada kapatwa na nini?
" haaaaa mwanaharamu mkubwa weee emmy sijawahi kuona mshenzi duniani kama wewe mpaka mama yako anazidiwa anataka kufa wewe ujui unatanua tu na vigari vya kuongwa, chefuuuuuu" aliishia kunishamba niliumia sana kwa yale maneno nikakimbia haraka kuwahi lile noah ambalo mlango wa abiria ulikuwa unafungwa.
Toba yarabi nafsi nilipohitaji kuingia nilipewa maneno ya kashfa ina maana pale mtaani hakuna aliyenipenda hata mmoja "toka tena ukome we mtoto kama umeshindwa kumlea mama yako tuache sisi tutamtunza ndo nyienyie freemason mnatoa ndugu zenu kafara ilo mfanikiwe kimaisha wee emmy wa kuvaa nguo za gharama namna hiyo mama yako hana hata hela ya kula toka sitaki kukuona" nilisimama nikaanza kulia huku nikimkumbuka mama yangu "emmy mwanangu ishi vizuri na wakubwa zako na hata wadogo waheshimu uwezi kujua atakayekusaidia nani, mheshimu mtu bila kujali anamuonekano upi utafanikiwa mwanangu" ni maneno ya mama kabla ajafa nimekuwa nikiyakumbuka ili ili ninalo bambikiwa leo sio.
"Mwajuma ni kweli emmy kamroga mama yake mdogo" nilisikia mnong'ono nikiwa nimesimama pale
"Wee uoni mtaa huu ni nani asiyejua kuwa emmy alikuwa maskini wa kutupwa nakumbuka alikuwa na nguo mbili tu tena gauni na dela muda wote unamkuta emmy na kanga haya ya leo haya kumiriki hadi nyumba, gari na kuvaa minguo ya gharama unafikiri ni nini kama sio ndumba" aliongea mwajuma bila wasiwasi hakujua ni jinsi gani ananiumiza.
"Iki kiama wengu watachomwa moto emmyhuyu alikuwa anakuja kwangu ananiazimisha nguo leo anaringa kisa kigari hicho simpendi huyu mdada hadi kinyaa" aliongea mwanaidi rafiki yangu wa kitambo
Niliendelea kulia hadi kimasi lilianza kunitoka na kichwa nacho kilianza kuniuma.
Niliondoka pale nikasogea hadi nyumbani mlango ulifungwa na funguo hazikuwepo pale nilipokuwa nimepazoea nikija nazikuta, nilimuona mpangaji jirani yetu mama bakari.
"Emmy kulikoni dada?
" shikamoo dada"
"Marahaba poleni ila hali ya mama yako haikuwa nzuri ulikuwa wapi kipindi chote?
Aliuliza mama bakari
" dada mama bakari mimi sijui lolote lile na kusema ukweli natuhumiwa kwa mambo nisiyoyafanya"
" emmy mdogo wangu mtaa mzima umekuwa gumzo wewe unaonekana umemroga mama yako ili upate mali nilivyosikia hivyo niliumia wanadai hata kumsaidia umsaidii chakula tu tuliwekeana zamu hapa kumuhudumia kweli emmy umeamua kufanya hivyo?
*mungu wangu mamdogo unanichumia dhambi bure, angalia mihamala hii nimekuwa nikituma laki kila wiki kweli simjari mama mdogo" nilifungua message na uzuri sikuzifuta sio kwamba nini nilikosa muda na mara ya mwisho aliniomba laki mbili hii niktumia.
"Kheeee kweli jamani mimi juzi hiyo ya.laki mbili aliniomba nimuandikie ujumbe hali yake ilikuwa mbaya"
"Sijui nifanyaje roho inaniuma kusingiziwa, ona message hii hapa namlazimisha aje kukaa pale kwangu unaona alichonijibu.
" mimi nimeshazoea maisha yangu ya temeke, ukitaka wewe mchukue rafiki yako salma uishi naye" ilisomeka hivyo
"Sasa napata picha emmy kuna kitu kinaendelea kati ya mama yako na baba mwenye nyumba na mama yako, na hii nakwambia siri mwisho niliwahi kumuona yule mkaka bonge akiwa nae(elibariki)'
Nilijikuta natokwa na machozi mama bakari alinitazama nikamuona nae machozi yakimtoka akanikumbatia kwa nguvu na kuniambia kwa sauti ya chini sana "emmy mdogo wangu usilie ndio ukubwa huo dada nakuomba wasamehe bure"
"Dada inauma kumbe kila nikipita hapa mtaani naonekana kituko hivi kweli mamdogo anaweza kunifanyia unyama huu"
"Emmy ebu kaa chini nikwambie jambo"
Niliamua kumsikiliza mama bakari nikachukua kigoda na kuketi huku nikimtazama usoni, nae alikaa kwenye mlango wake na kuanza kuongea huku mimi nikiwa bado namtazama ni nini anataka kuniambia.
"Emmy kama kusingiziwa wewe sio wa kwanza, kupitia shida emmy wewe sio wa kwanza na hata kusalitiwa wewe sio wa kwanza, emmy katika maisha yangu nimejifunza kusamehe mpaka hapa unionapo nimetendewa mengi nimesamehe nawe msamehe mama yako" aliongea mama bakari ila bado sikumuelewa kwangu yalikuwa ni maneno ya kawaida.
"Hivi kweli mama mdogo katembea na elibariki kabisa? Niliuliza kwa jazba
" tulia basi emmy mbona hivyo tunaongea wawili tu mbona hivyo"
"Mama bakari nakuheshimu wewe tu ila kile nitakachomfanyia hatasahau ngoja" niilizidi kutoa kilicho moyoni huku kifuani nilihisi kitu kama kiungulia.
"Hivi emmy wanaume unawajua kuliko mimi? Emmy usinione hapa nimepitia mengi kwenye mapenzi nimetendwa na hawa viumbe wanaitwa wanaume nilijuta kupenda niliwachukia wanaume nilimchukia hadi baba mzazi"
"Kheeeeeee" nilishangaa aliposema alimchukia hadi baba mzazi
"Usishangae emmy ndivyo ilivyokuwa"
"Ilikuwaje dada"
****************
FEEDBACK YA MAMA BAKARI KWA EMMY.
(KUMBUKA KUWA HII BADO NI SIMULIZI YA YALIYOMKUTA EMMY AKIMSIMULIA RAFIKI YAKE HIVYO TUWE MAKINI).
Nikiwa msichana mdogo(darasa 6) baba yangu alifukuzwa kazi aliyokuwa anaifanya katika shirika la reli tazara katika mkoa wa tabora. Kipindi hicho tulikuwa tunakaa kota za railway officers. Maisha yalibadili pindi tu tulipoama pale railway kota.
Kipindi kifupi kile mama alianza kufanya biashara ndogo ndogo za kuuza nguo kwenye gurio na mnadani, mimi fatuma(mama bakari) kila niliporudi shule nilikuwa naenda kumsaidia mama katika kuuza biashara yake, mambo yalizidi kubadilika hasa baba alipoanza kunywa pombe kitendo kilichopelekea fedha zote alizolipwa na shirika la reli kumalizika kwa pombe na wanawake..
Nilipomaliza darasa la saba sikubahatika kufaulu kuendelea na elimu ya sekondari hivyo rasmi nilijiingiza kwenye shughuli ndogo ndogo za kuuza vitafunwa na jioni kumsaidia mama mnadani siku zikazidi kwenda, ikafikia kipindi nikavunja ungo na kujiona sasa nimekuwa maana nilichelewa kuvunja ungo tofauti na rafiki zangu. Mara zote mama alikuwa akinihusia usafi(mwili na mazingira) maana tayari nilikuwa mwanamke na kikubwa zaidi juu ya kujiheshimu na kikubwa alinihusia juu ya kuwaogopa viumbe wanaoitwa wanaume.
Nilikuwa nikiyakumbuka mahusia ya mama kwani pamoja na kutongozwa sana na wanaume bado nilikuwa na msimamo, siwezi sema nilikuwa sipendi la hasha nilipenda ila niliogopa mama akijua yale nitakuwa matatizoni hivyo nilizidi kujitunza mpaka nilipofikia miaka 17 ambapo ndio nilipokutana na changamoto nyingi kutoka kwa mzazi wangu wa kiume/baba. Kuna kipndi tulikuwa na mama tunachelewa kurudi nyumbani kutokana na biashara kule sokoni baba alikuwa anamtukana sana mama mbele yangu matusi ya nguoni nilikuwa naumia mno ila sikuwa na jinsi maana nilikuwa mtoto tu kwao.
"Una akili kweli we mwanamke yani mwanao unampeleka kujiuza? Yani kujiuza wewe haitoshi mpaka unamuuza hadi mwanao shenzi sana wanawake ndio maana mimi nasema wanawake wote wasen*** tu" alikuwa akitoa kauli hizo kila siku japo muda tuliokuwa tunarudi ni saa moja jioni tu.
Kutokana na ile hali mama alianza kupata presha na miguu ilianza kujaa maji kiasi kwamba ukibonyeza unaasha alama, kwa mazingira hayo isingekuwa rahisi kufanya biashara hivyo mimi nilisimamia kila kitu nilijikuta nachoka mno maana asubuhi sana namke nikande ngani nipike chapati, maandazi kisha nichemshe chai kwa ajiri ya kwenda kuuza sokoni. Biashara nikimaliza hiyo saa tano asubuhi narudi kuandaa chakula nyumbani na kurudi tena sokoni kuuza nguo mnadani. Kuna wakati nilikuwa nadhurumiwa na wateja wakorofi mda mwingine wanaondoka na hela zangu ila bado sikuchoka maana bila hizo kazi familia yangu haitaishi.
Siku hiyo nikiwa narudi kutoka mnadani nimechoka hoi kuna kijana anaitwa jose alinisimamisha njiani namfahamu ni jirani yetu kwa mama haule nyumba ya tatu kutoka nyumbani. Alikuwa ananipenda muda mrefu huyo jose kipindi hicho yeye alikuwa mwanafunzi wa kidato cha sita mimi ndo kama hivyo nilikuwa mdada tu wa nyumbani. Nilikuwa nampenda jose ila nilimuomba anitunzie heshima yangu tusifanye mapnzi hadi tutakapo kuja kuoana(nilikuwa bikra) alinishika mkono akanipusu na kunikumbatia hapo ghafla baba akatokea nilimuona jose akikimbia kuelekea porini mimi niligombezwa na kupigwa fimbo kama mtoto njia nzima huku nikipewa vitisho "nakwambia utanikoma malaya mkubwa kama mama yako"
Tulifika nyumbani akamwambia mama maneno ya uongo eti amenikuta nafanya mapenzi porini mimi nilishindwa kujitetea mama nae alizidi kunisema nikakosa amani moyoni na tangu siku hiyo baba alianza mambi ambayo sikuyaelewa mara aje chumbani kwangu au aje bafuni nikioga(bafu la makuti) akijifanya kajisahau nilikuwa nikikaa peke yangu nalia mno.
Nilifanikiwa kupata laki moja ambayo ilimuwezesha mama kupata matibabu na kuhudhuria mazoezi kila asubuhi. Jumapili asubuhi ni siku ambayo mama alianza kwenda hospitali yeye mwenyew mimi nilikuwa nje nafanya usafi wa vyombo na kufagia mazingira nikasikia naitwa ndani.
"Fatuma njooo" ilikuwa ni sauti ya baba
Nilirudi ndani kwenda kumsikiliza akaniruhusu niingie chumbani kwake na hapo ndipo aliponikamata na kunichania nguo na kunibaka nilipiga kelele ila sikupata msaada mithili ya kilio cha samaki. Alitumia zaidi ya masaa manne mpka kufanikiwa kunifanyia kile kitendo maana mna wote tulipigana ila baadae alinikaba na kunixidi nguvu, niling'ang'ania chumbani sikutaka kutoka ila mama akirudi anikute palepale.
"Fatuma twende uku" aliongea kama mtu
"Samahani we mwanaume niache unachohitaji kingine kutoka kwangu ni nini? Wanawake siku zote ni dhaifu umetumia nafasi hiyo kunifanyia hivyo ulivyofanya nakuahidi sikuwahi na sitawahi kuwa na baba kama wewe ustahili kuwa baba na raana hii itakusumbua maisha yako yote mpaka unakufa" niliongea maneno kwa uchungu nikatoka chumbani.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI
KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger
Email: ZephilineEzekiel@Gmail.Com