JINA: MUUZA UBUYU
SEHEMU YA TANO
ILIPOISHIA...
"Sikujua kama unayajua yote ayo lakini emmy tungefanyaje uku kazi nimesimamishwa kule kwa Ryidia najishikiza tu saa nyingine natoka bila chochote zaidi ya nauli ningefanyaje emmy?
"Hata km hali ya maisha ni ngumu ndo uuze mwili wako"
NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU
SASA ENDELEA...
"Emmy usimtukane mamba kabla ujavuka mto"
"Una maana gani?
Ukimya ulitawala ghafla na hata swali lile alikupata majibu nilianza kulidadavua kwa kina " mmh usimtukane mamba eeh, ina maana hata elibariki anisaidii bure ndo yale yale payback" tayari nilipata jibu, niliwaza sana na kukumbuka kipindi mama akiwa hai aliwahi kusema kitu nakumbuka nilikuwa mdogo kipindi hicho ila bado nina kumbukumbu.
"Jamani wanaume mnaowaona sio watu wa kuwategemea kwasababu wana sura nyingi, mwanaume anaweza akakwambia ukweli au akakudanganya ila silaha yao kubwa ni uongo ni hili kukupata wewe mwanamke kwahiyo love mdogo wangu kuwa makini"
Kauli hiyo aliwahi kumwambia mamdogo love alipochelewa kurudi nyumbani siku hiyo.
******************""""
Siku zilizidi kusogea nikamaliza mtihani wangu wa qualified test (QT) nikaendelea na kazi zangu kama kawaida na jioni nilipata wasaha mzuri wa kujisomea na wenzangu masomo ya form four, kwa kipindi kifupi nilipenda sana somo la histry na kiswahili na nilijitahidi kuyasoma kila siku .
Siku hiyo nikiwa natoka shule eli alinipitia kama kawaida na kunirudisha nyumbani temeke njiani alinieleza mipango yake ya kuendelea na masomo kwa level ya masters ila itakuwa nje ya nchi, kwa upande mmoja ilikuwa ni jambo jema kwani ingenipa nafasi ya kuspend na sam ila kwa upande mwingine niliwaxa nitawezaje kurun maisha hasa upande wa kifedha na wakati huo kuna aina ya maisha flani nilishayazoea km kwenda saloon kila baada ya mwisho wa wiki, kuspend beach kweny maevents makubwa, nilizoea kuvaa na kula vizuri itakuwaje eli akiondoka na ni wazi sam hana kipato cha kukidhi mahitaji yangu na mara zote tumekuwa tukigawana umaskini nikipata nampa mana nilijua najiwekea hazina maana yeye anasomea mambo ya engeenering leo kesho akifaulu nami pia nitawin.
"Emmy... Wee emmy! Vipi mbona kimya ina maana naongea peke yangu"
"Noo baby nilikuwa nakusikiliza ila huo wimbo ndo umenichanganya"
"Yani huu wimbo(darasa-muziki) umekuwa kero bado kupigwa kanisan na misikitini ila ni mzuri nami naupenda sana"
"Yeah yeah ni mzuri elly nishushe hapo basi" nilifika usawa wa mtaa wa nyumbani nikaona anishushe ili nipite kwao na salma angalau nimsalimu.
Akuzungumza kitu ila nilishangaa alianza kupitisha mkono wake kweny mapaja yangu nilimkodolea macho tu kwani nilikuwa sina hisia nae kihivyo japo alivyokuwa anaendelea nilianza kunyevuka taratibu "noooo elly tupange siku ila sio kwenye gari bhn elly"
"Even kushika bby unanikataza na ni kila cku unasema hivyo"
"Hapana elly ila utajisikiaje nijichafue hapa na bado nina safari na humu ni kwenye gari elly bhn"
"Sawa amna shida kesho jipange uamie kwako nilitaka nikusuprise ila nikaona ni bora umwambie kabisa mama mdogo nataka uweke mambo yako sawa nitakufata kesho nikakuonyeshe nyumba yako please please usikatae"
"Wooow! Baby thanks, baby i love you mwaaaaaa"
"Kesho nataka nilale na wewe kwenye nyumba yako"
******************
AFTER ONE WEEK..
Makazi mapya yalinipa shida sana maana muda mwingi nilikuwa getini sikupata hata muda wa kuuza ubuyu kama kule temeke mikoroshini siku hizi mbili tatu nimegombana sana na elibariki kwani nilikuwa natoka na kwenda kushinda temeke narudi jioni, kwanza nilimiss utumbo wa kuku na miguu ya kuku huku ninapoishi hakuna hayo mambo kila kitu supermarket ilikuwa ni shida kuishi huku(kijichi).
"Hallo hey sam nimekumiss upo wapi?
" nipo kwenye gari natoka chuo narudi home"
*please sam nakuomba njoo kijichi ccm ukifika hapo chukua bodaboda uje please"
"Okey sawa nakuja usijari*
Simu ilipokatika nilitabasamu kisha nikaingia kwenye facebook account ya sam nikaanza kutazama picha zake nikawa nafarijika mara nyingi upenda kupiga picha akiwa darasani, maabara, kanisani hana picha za sijui bata la wapi mara wapi kama elibariki, muda huo nilikuwa kwa jirani anaitwa sasha ni kadada flani wa arusha ameolewa na mzungu ndio huyu nimezoeana nae mara zote uko ndo naenda kuuza ubuyu kama siku hiyo nimewahi kutoka shule maana hata kazi nilianza kwenda kwa kujisikia.
" kwani emmy umeolewa shoga?
"Mmh kuolewa bahati shoga, sijaolewa nahudumiwa na bwana tu yeye ndo kaniajiri, ananisomesha na ndio amenipa nyumba hii niishi"
"Kheee ni mpenz wako wa muda mrefu?
*aaah wapi zari nikikusimulia utashangaa ila ntakupa ubuyu kesho ngoja niende uko kwangu maana hata taa sijawasha na giza limeingia hivyo"
"Aya poa mwaya usiku mwema"
Nilitoka pale miguu yote ganzi maana nilikaa pale toka saa tisa mchana hadi saa moja kasoro, sam alipofika alinipigia simu nikamwelekeza na kuongea na bodaboda amlete kwa diwani charles.
Alipofika sam nilifunga geti kabisa na milango ya nyumba nzima kisha tukala pale na mambo mengine yaliendelea ilikuwa palepale kweny kocho tulianza kuvingirishana mpi kwenye zuria chini..
Simu yangu ilianza kuita sikujihusisha nayo mana ilikuwa mbali kidog ikakatika mara ya pili na ya tatu ikaita nikasogea na kuangalia screen jina lilikuwa "sweet mangi" ambaye ni elibariki kimaro nimezoea kumtania hivyo "mmmh sasa nikipokea nitamwambiaje?
Kabla sijapata jibu honi za gari zilisikika getini kwa nguvu moyo ulilipuka paaaaaaa!!!! Sam huyu sam nitamweka wapi???????
Kitete kilinipanda yani hii miguu ilifuka moto sam alikuwa ananitazama nilivyokuwa naweweseka yeye akiwa ana analolijua ila kadri sekunde zilivyosogea alizidi kugundua akaniuliza.
"Nini hivyo sasa?
" sam amekuja mwenye nyumba nitafanyaje mimi?
"Sikia unanipenda?
" sam unajua wazi kuwa nakupenda"
"Basi fata kile nitakacho kwambia sawa?
" sawa"
"Nenda kamfungulie geti usiwe na wasiwasi wowote umesikia?
" sam sasa akikukuta itakuwaje sasa?
"Wewe fata nilichokwambia"
Nilitoka kweli kwenda kufungua mlango nikaamua kuvaa sura yangu ya awali bila kuwa na wasiwasi wowote huku moyoni uoga ulinijaa hakuna mfano.
"Heee bae mambo"
"Mambo ya nini muda wote unanikalisha njee tu ulikuwa unafanya nini hata usinisiikie?
" bae nawe twende ndani kwanza mpenzi mbona unafura hivyo?
Nilimshika kidevu na mkono mwingine nikashika kifua chake, kitendo kila kilimkata kauli kabisa akuongea neno tukaingia ndani.
"Kwani bae unaingiza gari nikufungulie geti?
" aaah natoka sasa hivi leo silali, khe khee kheee hiyo kelele ndani ni nini?
Hata mimi nilishindwa kujibu maana sam alifungulia redio ndani mfano wa kumbe ya sherehe. Tuliingia ndani tulimkuta amevua tshirt amebaki na vest anaangaika na redip km fundi nilishangaa "yani huyu sam khaaa" alipunguza sauti ya redio kisha akaongea.
"Habari za leo mheshimiwa?
" aahsalama tu"
"Sasa dada nadhani kuna machine iliungua hapa na unasikia inatoa kelele kisa kifaa hicho"
"Kheee jamani sasa tunafanyaje fundi?
Nilijibu haraka mno.
" aaaha hii redio hata mwezi haina imeanza kusumbua, kesho tuirudishe si umetunza yale makaratasi ya warranty? Alidakia elly.
"Ndio yapo"
"Mmh haina haja ya kurudisha mana inaonekana mna vifaa vingi hapa kuna pasi, tv, deki, subfaa, amplifier vyote vimeunganishwa bila uwepo wa stablizer ni hata kwa vifaa vyote kuungua na ndio maana leo imesumbua redio ila kesho itakuwa tv au hata amplifer"
"Aaaaha kumbe sasa fundi hiyo stablizer ni shilingi ngapi?
" sijui unataka za nchi gani maana kuna za japan, china, german na england, ila za german ndo venye quality"
"Hiyo ya german ni bei gani?
" hiyo ni laki mbili na nusu"
Nilishuhudia pesa inatoka anapewa fundi sam mimi nilifarijika moyoni ila kabla hawajaelewana simu ilipigwa upande wa elly "ndio mama yeah, ndio ila nipo kijichi now, anhaa basi nakuja" yalisikika maneno hayo.
"Jaman nimepata dharura nadhani mtanipa ripoti mmefikia wapi fundi kazi njema"
"Anhaaa sawa mheshimiwa"
Tulitoka wote nje kisha tukaingia ndani ya gari tukazungumza kidogo.
"Mbona ukuniambia kama fundi amekuja sasa?
" aaha simu yangu ukupokea bae ningefanyaje"
"Sawa hakikisha anakamilisha hapo shika hii hela kama itapelea mtaongeza naomb uende nae dukani maana hawa mafundi hawa wapigaji, na hivi hela imekuwa ngumu tunaziba hiyo mianya ya upigaji"
"Bae nawe umekuwa magu hahaaaa aya byeee"
Nlimchum nikafungua mlango na kutoka nje ya gari. Elly nae aliwasha gari na kugeuza pale tayari kuondoka ila nashangaa aliniita tena.
"Kuwa makini na huyo fundi mpo wawili nyumba nzima onhoo naondoka basi tu"
"Mmmh nawe acha wivu wako me na yule wapi na wapi?
" mnasemaga hivyo hivyo"
"Bwana kwaheri.msalimie mamie".
***********************
" sam wewe ni mshenzi haswaaaa"
"Kwanini unasema hivyo?
" hiyo tactic uliyotumia sikuifikiria na wala ajafanikiwa kujua lolote sema aliniambia kuwa makini"
"Kama kasema hivyo inabidi tuwe makini sisi pia maana anawexa kurudi hata alfajiri"
"Mmh sidhani na wala hana desturi hiyo"
"Me nakwmbia maana naelewa usinipinge na ni kwasababu ameniasha hapa so kuwa makini"
"Tuyaache hayo bhana sam unajua umenitia genye sasa nimalize hapahapa"
Tulianza kama utani mara sebureni tukaenda chumbani akanipa goli moja, wote tulikuwa hoi tumejilaza, nikaona mwenzangu usingizi umempitia nikamuamsha tukaoge napo bafuni akaanza tena kusema ukweli sam anajimudu na hii inatoka na kupenda kufanya kwake mazoezi tofauti na elly yeye ana kitambi mazoezi afanyi mbili tu kalala km pono.
Tuliyapanga mengi na hasa kwa kipindi hiki sam alikuwa anakaribia kumaliza degree ya pili ya mambo ya ukemia sijui hata wanaiitaje kitaalamu. Sam ana maisha magumu sana na ndio maana anajitahid kusoms sio mtu wa bata wala totoz na uhalisia wa maisha yake unashabiiana na wangu japo umri ndo tofauti yetu. Nilimuahidi kumsaidia maana ndio future yangu ipo kwake ila kwa elly ni kujikimu kimaisha tu.
Alinipa ushauri wa namna ya kusoma na kuweza kupangilia ratiba zangu na kuniahidi kunikumbusha kwa kila jambo nilipasalo kufanya on time.
"Baby inabidi niondoke saa kumi na moja kasoro 20"
"Jamani kwanino usiku huo wote?
" yule jamaa anaweza rudi asubuhi niamini mm"
"Sam bhana awezi rudi bhana"
*******************
Nilimkabidhi sam hela yote ile ilikuwa laki tatu na themanini japo sikupenda aondoke muda ule.
"Sam mbona unanifanyia hivyo?
" kwaheri baadae tutaonana njoo ufunge geti"
Niliumia roho ila nitafanyaje yeyw ndo kaamua aliondoka na kuniasha nimejilaza kweny sofa haikuchukua dakika kumi na tano nilisikia sauti ya bajaj njr nikajua sam karudi may be alikuwa ananienjoy kuchungulia dirishani nikamuona elly moyo ulishtuka "kheee my Godness angemkuta sam ingekuwaje?"
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI
KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger
Email: ZephilineEzekiel@Gmail.Com
