MUUZA UBUYU (7)

Zephiline F Ezekiel
Mwandishi: Micky Mejah

SEHEMU YA SABA
ILIPOISHIA...
Kwa kipindi kile chote watu wote walishajua juu ya mahusiano yangu na sam sio km zamani nilikuwa naingia kwa kujificha.
*********************

"Unawaza nini emmy?
Sam aliniuliza wakati tunakula

NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU

SASA ENDELEA...
"Sam unajua kwa kiasi kikubwa nilikuwa namtegemea elly economically kwa sasa ndio nimeingia advance(form five&six per one year) kule wanahitaji ada na mambo ya chakula pia plus nauli bby kichwa kinaniuma" niliongea uku machozi yakinitoka.

"Baby sorry najua ni jinsi gani unajisikia nakuomba usiumie nipo kwa ajiri yako wiki hii nitapata mkopo na pia najiandaa kwenda field nitakuwa na hela kiasi nadhan itakufaa kujisukuma siku mbili tatu hizi tukifanya mpango wa muda mrefu, sawa baby?
Aliongea uku amenikumbatia na kunifuta machozi yangu.

" sawa bby nashukuru kwa kunifariji maana kichwa kinaniuma nataka ndoto zangu zitimie bby ila najua mapito aya ya muda mfupi"
Mara simu yangu iliyokuwa chaji ikaita nilinyanyuka nikaenda kuichukua kweny screen lilisomeka jina la Rafika.

"Hello! Mambo shosti"

"Poa niambie emmy".

" poa vipi wazima uko?

"Mmh wazima ila tumekumiss huku wateja pia wanaulizia emmy muuza ubuyu yupo wapi shosti umenogewa na bwana hata kaxi basi"

"Hamna Rafika masomo yamebana sana ila nitakuja"

"Eeeh bosi(elly) siku hizi amekuwa mkali yani jambo dogo anamaindi kuna nini mamie?

" mbona hamna kitu nitaengea naye nimuulize"
Sikutaka kumwambia kuwa mimi na bosi wake tumegombana tuliongea mengi ya udaku wa kazini ba best yangu huyu uku tukikumbushiana mengi pale wananiita emmy muuza ubuyu kutokana na tabia yangu ya kuwapa watu umbea mwepesi mwepesi..
Hapo kidogo nilipata furaha ukiplus na sam kunipetipeti nilienjoy kidogo.
*****************

Nilifanikiwa sana na ubuyu wangu ambao nilikuwa nautengeneza na kuusambaza kweny supermarkets na wauzaji wa rejareja ni ushauri ambao niliupata kwa mama mmoja anaitwa mama aikaeli ambaye yeye anafanya biashara ya kuuza crips na tambi kwny supermarkets ndiye aliyenipa hili dili na nilianza kwa mtaji wa laki 3 na usafiri kama 3'7.

Nilimchukua salma rafiki yangu akawa ananisaidia kwa nyakati za jioni nikienda shule yeye alikuwa anakusanya hela kweny supermarkets zote tulizokubaliana ktk malipo ya wiki, siku na hata mwezi kwa ujumla ndani ya miezi miwili ya ile biashara niliweza kupata faida laki sita kwa mtaji wa laki tatu kwangu ilinipa hamasa kubwa kwani hapo kabla sikuiona hii fursa. Siku hiyo jioni nilikutana salma alikuwa ananipa ripoti ya biashara tuliketi kweny kibanda cha maziwa tukawa tunazungumza.

"Dah emmy nimechoka mno kwa mizunguko hii"

"Leo muddy bajaj kakushusha wapi?


"Niambie vipi wale sumàri wamekupa hela yetu?

" amenipa laki na nusu kasema ijumaa itakamilisha"

"Yani ni wasumbufu wale sumari nitafatilia mwenyew na wananijua vizuri na wale wa al jazilla pia awajakamilisha"

"Hivi emmy ilikuwa kuwa mpk umepata hii network kubwa hivi supermarkets kubwa vile mamie?

" niliamka asubuhi sana nilimuaga sam kuwa naelekea mjini nilijaribu kwenda kariakoo shimoni lengo langu niulizie fursa ya kupata angalau biashara ya kufanya kwa mtaji nilikuwa nao wa laki nne kila niliyemwelezea aliniambia kwa mtaji huo uwezi kufanya biashara ya kuweza kusurvive kariakoo nilizunguka sana shimoni nikakuta na mama mmoja anaitwa mama aikaeli yule mama nilimwelezea ndio akanipa mbinu ya kuuza ubuyu mtamu kweny supermarket ila ilinibidi niwe na vifaa vya kutengenezea kwa mtaji nilionao ningeanza taratibu kwa kununua ubuyu na rangi pia alinipa vifaa ambavyo alikuwa anavitumia hivi unavyoviona kwa makubaliano ya kumlipa taratibu taratibu"

"Kheee emy una bahati wewe dah"

"Sio bahati tu salma hata juhudi zangu za kutoka km mtoto wa kike kuzunguka mule kariakoo kulikojaa wanaume wengi namna ile si rahisi"

"Sasa mama ulipomueleza alikuelewa tu bila shida?

" no salma it was not easy ilibidi nimueleze mimi ni yatima nadaiwa kodi ya nyumba na mambo turuki uwezi amini alinipenda sana hadi chakula alininunulia na ana binti wake pia rika kama letu hilo ndio linisaidia pia"

"Wewe ni superwomen na kila ninapopita nauliziwa emmy emmy nawaambia emmy ni pacha wangu"
****************

Nilifanikiwa kwa kiasi kikubwa rafiki yangu cindy uwezi amini kwa miaka muda mrefu nilikaa bila kumtafuta elibariki sikujua ni nini kilitokea japo kule nyumbani kijichi nilikuwa naenda kufanya usafi na mambo mengin na nyakati nying nilikuwa nalala pia.

Kumbe katika kipindi chote elly alipokuwa kimya alikwenda south africa kimasomo kwa miezi tisa nililijua siku hiyo ambapo nilipeleka makusanyo ya fedha benk nakumbuka mara ya mwisho nilikuwa na milioni nne kweny akaunti yangu cha ajabu nilipoingiza zile laki tatu nilizokuwa nazo nikashangaa kuona salio langu ni milioni 14 tanzanian shilingi nilishanganyikiwa "ooh my God ni nani kaniingizia pesa kweny akaunti yangu, au sam? No sam ni juzi nimetoka kumtumia laki mungu wangu"

"Hello, enhee sam eti umeniingizia pesa yeyote kweny akaunti yangu?

" hapana sijafanya hivyo" wakati naongea na ile simu kuns simu iliingia "okey kata kuna mtu ananipigia nitakupigia baada ya"

"sorry ebu kata kuna simu inaingia nitakupigia baada ya" Kweli sam alikata na mimi wakati huohuo nilitoa simu masikion na kuitazama simu inayoingia ilikuwa ni namba ngeni nadhani zile code si za hapa nchini nilipata wasiwasi sana akili yangu ikanituma au kuna mtu kachukua namb zangu fb ndo huyu ananipigia. Nilitafakari pasipo kupokea simu mpk ilikatika.

Niliweka simu kwenye hand beg yangu kisha nikatafuta bajaj inipeleke nyumban kwangu kijichi. Kweli haikupitq muda bajaj ikaja tukaanza safari kwa mtu ambaye alimuona emmy miezi kumi nyuma awezi kuamini akiniona leo kwani nilibadilika sana kimuonekano na kadri siku zinavyozidi kwenda nazidi kuwa mcharo/kung'ara na kikubwa zaidi mimi ni muangaikaji sipendi kukaa bure kumtegemea mwanaume. Kuna mteja alinipigia simu alikuwa anahitaji mzigo ni mkaka ambaye nimetokea kuzoeana nae sana huwa ananitaniq mno.

'Niaje emmy muuza ubuyu!

"Niambie janu mzee wa mipango"

"Poa agent wa shilawadu nasikia wewe ndio unawauzia ule ubuyu mtamu ambao ukila unatoa ya moyoni"

"Hahaaaa janu wewe nakuona unakula tu ubuyu"

"Umejuaje? Nilikuwa sipendi ubuyu ila toka nimeupata ubuyu wa emmy basi napenda ubuyu mno niambie ninaweza kupata mzigo"

"Unataka wa mifuko au wa kilo"

"Fanya unipe wa kilo nataka kilo nane"

"Sawa usijari nitakuletea ofisini kwako kesho saa nne"

Maongezi yalikatika nikiwa bado nacheka tu mimi nipo social na napnda sana kuihudumia jamii yangu na ndio maana nina ndoto za kusomea sheria niwasaidie wanawake wenzangu hasa vijijini.
*************

Baada ya kumaliza shughuli zangu zote kiukweli nilikuwa nimechoka ila ilinibidi nisome vitu viwili kabla sijalala kwanza nimalizie kukisoma kitabu cha "i will marry when i want" na nifanye maswali tuliyotolewa na mwalimu ya topic ya "rise of democracy in europe" history2.

Nilifanikiwa kujibu yale maswali yote ila nilishindwa kumalizia kusoma ile play ya "i will marry" kutokana na kuanza kusinzia, "mmh ila huu usingizi jamani ndio kwanza ni kitabu changu cha pili kusoma bado novels bado poetry nikizembea nitafail bure inabidi nijikaze mno" wakati najitafakari niliamua nilale hivyo nilienda kuchukua simu niliyoiweka kweny chaji muda mrefu kidogo nikaiwasha..

Haxikupita dakika tano ile namba ikaingia tena "jamani huyu nani mbn sielewi itakuwa ni yule aliyeniingizia milion kumi kweny akaunt yangu au freemason? Nitamwambia haitoe hela yake" nilipokea kwa ujasiri

"Hello nani mwenzangu"

"Emmy mambo"
Nilipigwa na bumbuwazi ghafla sauti ya elibariki kimaro au sweetmangi sikuamini.
"Vipi mbona kimya?

" hapana nakusikiliza"

"Naomba sahau yaliyopita bby, niambie masomo yanasemaje?

" namshukuru mungu"

"Nimekuingizia hela kweny akaunti yako na kuna gari nimekuagizia kutoka japan nimeshaikatia kila kitu kwa hapi nchini mimi nipo south africa uko nitarudi mwisho wa mwezi huu nakuomba kuwa makini*

" wow! Nashukuru baby asante" nilitepeta mwenyewe niliposikia gari na milion kumi juu umaskini ndo nauasha taratibu na tena hizi shughuli zangu nahitaji mno gari.

"Ngoja nakutumia picha za hiyo gari whatsapp halafu nakuomba urudi kijichi ile ni nyumba yako na nilikutoa temeke makusudi sipendi upate shida emmy"

"Asante honey"

"Jitahidi usome hiyo milioni kumi nimekutumia ufungue biashara sio unaishiwa hata hela ya kuweka mafuta kweny gari au kufanya service"

Niliona ni muujiza mkubwa kwangu elly huyu hata sijui ana akili gani ila ananipenda sana tatizo kwangu ni sam nae ana mipango ya ndoa na mimi soon atakapomaliza masters yake ya mambo ya ukemiia atakuwa na kazi nzuri na yenye kipato kizuri tu.
*****************

Nilikosa majibu ya kufanya maana hawa wanaume wawili wananiumiza kichwa sam nae alikuwa anamaliza field wikii hii tulipanga twende kwao kumsalimia baba yake tumpelekee na zawadi angalau aanze kula matunda ya kuzaa. Ila sasa mimi sam atanitambulishaje kwa baba yake?

Wakati huohuo mwalimu wa language one aliingia darasani akawa anaendelea kufundisha topic ya writing skills nilikuwa nampenda maana nilikuwa namuelewa mno na test zake nilikuwa nafaulu kuliko mwanafunz yeyote mule darasani. Kamwe sikuwahi kufikri kama nitakuja kuikosa amani kwa sasa ila jambola mapenzi ndio ulikuwa mtihani mkubwa kwangu.
*******************

Nilitoka dar na basi la asubuhi ili niwahi kufika morogoro mapema ambapo ndipo tulipanga tukutane sam hivyo nilipofika morogoro terminal sam alikuja kunipokea kisha tukapanda jingine costa kuelekea kweny mashambaya sukari tuliani huko.

Kupenda ni kitu cha ajabu sana elly pamoja na kunisaidia kote kule sikuwahi kwenda kwao hata siku moja na huku wazaz wake wapo dsm ila nimeenda morogoro kwao na sam, baba mkwe alikuwa mzee lakin wa makamo alikuwa bado ana nguvu zake uwezi amini alilima shamba kubwa mno na kupanda miwa, maboga, karanga.

"Karibu sana mama"

"Nashukuru sana"

Tuliongea sana na ninashoshukuru tulienda jumamosi isingeweza kuathiri shule na biashara pia alitoa nasaha zake na kukua ana kiona mbali/hekima alituhasa tujue ni njia gani njema ya mafanikio ya kupita ili tusije kupoteza malengo na ndoto zetu akatupa simulizi za zamani alipokutana na mke wake/mama sam.

"Yeye alikuwa darasa la pili(mama sam) mimi nilikuwa darasa la nne tena nikiwa kaka mkuu pale nilikuwa safi suruali safi, raizoni yangi inang'aaa mabinti wengi walinipnda ila mama yenu nilikuwa namtania siku moja nitakuoa monica kalikuwa kanacheka tu ila nilipomaliza shule nilienda nairobi kusoma huku nyuma nikasikia anataka kuolewa na jamaa mmoja mfanyakazi serikalini na anapesa zake niliamua kuandika barua nikamkumbushia ile ahadi ndo unaona hawa wakina sam leo maana nilimpenda monica na sikutaka kumpoteza japo sikuwa na pesa kama yule jamaa ila nilikuwa na msimamo na nilijua kusimamia ahadi zangu wewe jiukize kenya airway kuna warembo wangapu niwaache nimfatilie binti wa kijijijni?"

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI

KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger

Chapisha Maoni