MUUZA UBUYU (9)

Zephiline F Ezekiel
Mwandishi: Micky Mejah

SEHEMU YA TISA
ILIPOISHIA...
Nilimshangaa maana si kwa kujibaraguza kule ila sikuwa na time nae nilimkatalia tu. Na kumbuka hapo nilikuwa nafikiria nimpate mtu wa kuishi nae kijichi anisaidie hata usafi maana nyumba ni kubwa mno na nipo alone(mpweke) nilipoona zile dalili za salma niliogopa kumsogeza karibu na nyumbani kabisa.

NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU

SASA ENDELEA...
TURUDI KWENYE UHALISIA (OFISINI KWA WILLIAM NA JIMMY)..

"Kumbe ndivyo ilivyokuwa? Willy unaona this is the game for real willy(willy huu ni mchezo kabisa)"
Alihamaki Jimmy

"Yeah ila kuna vitu vya kunote pia, sasa unasema mtu wa mwisho kuwasiliana nae alikuwa ni salma? Aliuliza william

" ndio"

"Na mpenzi wako huyo mwingine(,elibariki) uliachana nae muda gani?
Aliendelea kuuliza willy

" kwakuwa ilikuwa ni jioni na mimi na elibariki muda mwingi tulikuwa close aliniambia ndani ya siku mbili hizi atakuwa busy kuna mambo anafatilia ila baada ya hizo siku atanitafuta hapo ndipo nikapata upenyo wa kumtafuta sam tukaja hapa sasa nikiwa najiandaa nakuja nilimjulisha salma haya yote"

"Asante sana kwa kutuambia ukweli sasa emmy tunakuahidi kulifatilia hili jambo ila tunakuomba kuwa mvumilivu sana na usimwambie mtu juu ya hili maana wewe utakuwa hatiani na sisi pia"
Alinitahadhari william.

"Sawa nimekuelewa kwahiyo polisi nisiende?

" emmy hili suala tuachie sisi, sisi ndo tutajua tuanzie wapi na tuishie wapi cha msingi mawasiliano"
Aliongea willy.

"Napenda kukukaribisha tena kupata huduma zetu pia tunakupa ofa ya kutembelea hapa bure kwa six months pia tutakupa kiasi kidogo cha fedha kwa usumbufu uliojitokeza na pole ya kumpoteza mpnzi wako"
Aliongea jimmy kwa bashasha.

"Sawa nashukuru"

"Ukitoka hapo nje kwa cashier(mhasibu) utachukua mzigo wako au kama una account tunaweza kukuingizia bank kabisa"

"Wote kwangu ni sawa tu"
************************

TURUDI KWA CINDY NA EMMY.

"Daah emmy pole mwaya story yako inasikitisha sana"
Aliongea cindy.

"Ndo hivyo imeshatokea nitafanyaje?

" sasa vipi hao wakina jimmy walifatilia hilo jambo la kumpata sam? Na nini elibariki alitambua jambo lolote?
Aliendelea kuhoji cindy.

"Dah shoga we acha tu mambo yalizidi kunisumbua kichwa"
***************

(ENDELEA NA EMMY FEED BACK KWA CINDY)..
Nilitoka pale hotelini nikapokea kiasi cha shilingi milioni nne kwa ajiri ya usumbufu na pole huku nikihadiwa jambo lile kufatiliwa kwa kina.

Niltoka pale hotelin nikapitia bank nikakuta imefungwa hivyo nikabidi niingize gari sheli nikajaza mafuta ya elfu20 kisha nikaanza safari ya kuridi nyumbani, nilipofika mtoni kwa aziz ally nikaingia kushoto kwenye supermarket ya al jazeela nichukue baadhi ya vitu na niulizie fedha za mzigo uliwahi kuletwa pale.

"Karibu dada emmy"
Mhudumu alinikaribisha maana nilikuwa nimezoeleka sana pale.

"Asante mambo naona mpo"

"Tupo karibu mwaya"
Alijibu yule mhudumu anaitwa zenabu.

"Hivi Zenabu nawadai nyinyi"

"Yeah ila bosi alikuja hapa jana akaasha maagizo"
Aliendelea zenabu.

"Mmh maagizo yapi?.

" anasema uache account number ya bank ili tuwe tunafanya malipo kwa bank au tigo pesa ama airtel money"

Nilimuandikia akaunti namba yangu kisha nikachukua vitu pale maziwa ya kopo(nido), penertbarter, mikate, siagi, sukari 5kg, tambi pakti4, mchele kg10, cocoa na juice za pineaple kisha nikafanya malipo nikawa natoka wakati natoka kuna mkaka ambaye ni customer care(mhudumu) alinisaidia ile mizigo kuingiza kwenyr gari. Nikiwa sina ili wala lile nilisikia naitwa "emmy weee emmy" haikuwa sauti ngeni masikioni mwangu niligeuza shingi kutazama daaah alikuwa saleh mpnz wangu wa zamani tulisoma nae shule ya msingi.

"Vipi emmy mambo? Alinisalimia saleh pemben akiwa na marafiki zake.

" poa wapi hiyo?

"Nimetoka chuo hapo TIA(UHASIBU)"
aliongea kwa kujidai kweli.

"Wow! Hongera kweli noe umeamua kusoma maana nilisikia story zako mara ulipelekwa shule uganda ukatoroka, kenya napo ukafukuzwa ila nafurahi kusikia unaendelea na shule"

"Aah waongo tu hao mashilawadu tu me sijafanya yote hayo"

Kabla sijamjibu yule kaka customer care aliniita "dada emmy tayari"

"Nashukuru kaka"

"Karibu tena"

Alipoongea vile nilibonyeza lock kwenye gari kitendo kilichomshangaza saleh na rafiki zake.

"Emmy its your?(emmy ni lako?)

" its mine saleh why not?(ni langu saleh kwanini isiwe?

Tulizungumza mengi akaniomba namba yangu nikampa na kwakuwa nilikuwa na haraka niliagana nae nikampa hela ya soda (30000) kisha nikawa nageuza gari nikamsikia akiwaambia rafiki zake.

"Ebhanaa kweli haya maisha hayana formula huyu demu nimeshamto**** sana na kwao nakujua temeke mikoroshini anaishi na mama yake mdogo dah eti leo ana mkoko(gari)"

"Hahaaaa saleh mwanamke sio mwenzio yeye ana mtaji wewe una nini, cha msingi pasua hiyo hela kati kwa kati tukapige viroba" aliongea rafiki yake wa pili.

"Weee boya kweli unataka hela usiyoifanyia kazi mimi ni huruma zangu nikupe au nisikupe" alijihami saleh.

"Haaa wewe umeifanyia kazi gani?
Aliuliza rafiki yake wa pili aliyekuwa kimya.

" mimi nilimtomb*** vizuri hivyo nimeasha mhuri wangu na kwa taarifa yako mimi ndo nimetoa bikra kwa huyo demu unayemuona"

Sikutaka kusikiliza zaidi nikaingiza gari barabarani hapo kichwani nilinote vitu viwili vikubwa kutoka kwa wanaume "kwanza wengi wao wanapenda miteremko wamkute demu ana mali zake ili wafanye matanuzi ti, pili wanatuchukulia wanawake sisi ni dhaifu sana kwao hasa kwa wale wanaotutoa bikra" niliona ni mawazo ya kijinga ya wale vijana na wengi wao wanakula kwao hivyo hawakuwa na mawazo ya kutafuta maisha zaidi ya kupiga viroba(pombe za mifuko ie zed).

Nilipofika nyumbani niliwasha simu yangu(baada ya siku mbili kuwa off) ziliingia message nyingi mno na mimi ni mvivu kujibu message kwa sababu message nyingi ni za wanaume kukutongoza tu tena wengine ni watu na heshima zao na wengine ni hawa ninaofanya nao biashara, walimu, wanafunzi wenzangu basi ni uchafu. Unajua msichana ukiwa na kipato angalau kama mimi hivi emmy wanaume wengi watakuja ili mradi wapate unafuu wa maisha na wale mabosi zangu ambao nafanya nao biashara wao ni tamaa za kingono wakiona mwanamke mzuri wanamtamani na ndio maana rushwa ya ngono maofisini ni ngumu kuisha kutokana na aina ya mabosi tulionao.
Nikiwa napika jikoni simu yangu iliita nikajifuta mikono na kitaulo ili nipokee alikuwa ni salma.

"Yes salma"

"Mambo vipi emmy?
Ilisikika sauti ya salma

" poa niaje?

"Poa upatikani wangu siku ya pili hii uns nini tena'

" nilikuwa na shida flan ndogo tu lakini, vipi ulifatilia pesa za madeni?

"Aah pole mwaya, ndio nilifatilia kote na jana tulitengeneza mxigo mpya" alijibu salma.

Ahaaaa sawa kesho tutaonana basi"

"Sawa ila nina shida ya laki naomba nisaidie"

"Kheeee jamani salma unapeleka wapi hela juzi nimekupa elfu themanini salna shoga yangu hatuendi hivyo"

"Sio hivyo nina shida hapa sina hata mia"

"Sawa nakutumia"

Nilikata simu nikawaza juu ya salma "unajua salma anataka kuiga maisha yani sijui kwanini ajifunzi kutoka kwangu mimi bank nina karibu milioni 20 ila uwezi kunikuta nafanya matumizi ya ovyo ika yeye atataka ajionyeshe ana hela ikitoka nguo hii yumo hii yumo na hapo hajui km najua anahonga wanaume dah! Alafu kanidanganya kaenda al jazella kumbe ni uongo hajaenda subiri tutachukiana tu maana si kubebana huku na amesahau juzi kasababisha hasara ya laki mbili kunidanganya kaporwa hajui yote nayajua, mimi emmy najua maisha ya kila namna na sitabiriki ni samaki wa maji chumvi au maji baridi sasa we muache anikariri kama samaki wa maji baridi atashangaa ya karne"
Niliongea kama mwendawazimu. Mara sweetymangi(elibariki) nae akapiga nilifikiria kuipokea simu ila nilipokea tu.

"Mambo bae"

"Poa sweetymangi wangu"

"Emmy ulikuwa wapi jana na leo?
Aliuliza kwa ukali.

Kitendo cha elly kuniuliza kwa hasira kilinishangaza na huku mwanzo tulianza kwa kuongea vizuri tu.

"Mbona unaniuliza kwa hasira hivyo?

" emmy wewe ni mchumba wangu na mke wangu ni lazima nikuulize" alijibu

"Jifunze kumsomà mtu yupo kwenye mood/hali gani ndipo uonyeshe hisia zako sipendi kufokewa elly na unajua hivyo"

Ukimya ulitawala simu ikiwa bado hewani nami sikutaka kujipendekeza nikakaa kimya tu. Wakati huo chakula kilikuwa karibu na kuiva ikabidi niiache simu pembeni na kuweka loudspeker kama hataongea nimjibu. Elly nae ni jeuri mno na nililijua hilo kipndi kile nilipomkosea akakaa muda mrefu bila kunitafuta nami nilipoomba sana msamaha bila kusamehewa niliamua kukaa kimya na shughuli zangu. Wanaume wengi upenda kunyenyekewa na wanawake na kujiona wao ni superior(bora) nasisi kutuchukulia km inferior(dhaifu) mimi sijawahi kuwa muumini wa dini hiyo mara zote napenda mwanaume hajue msimamo wangu kama tutawexana sawa km hatoweza ni sawa pia.
********************

Nilikaa mezani nikawa nasoma zangu geography maana nilichukua mchepuo wa HGL kwani tokea mwanzo niliyapenda sana masomo haya matatu na kuyafanya vizuri mno. Topic ya map(pratical geography) ni topic pekee ambayo mimi uipitia sana na ile ya physical geography. Nilishangaa kuona mlango unagongwa nilishtuka mno maana ilishafika saa nne na kule kwetu kijichi mida hiyo kunakuwa kimya mno ikabidi nifikirie mara mbili. Nikafungua mlango nikatoka mpaka getini nikauliza 'nani mwenzangu?

"Funguaa' ilisikika sauti ya elibariki.

" mmmh haya"

Niliguna kilichomfanya aje usiku ule nikahisi uenda alidhani sipo nyumbani au niko na mwanaume maana hana wivu yani anawexa kukunusa hata jasho haone umekumbatiwa huko utokapo au kwa namna yeyote ile. Akunisalimia akapita ndani mimi nikafunga geti kabla sijamalizia akaniita "weee usifunge geti fungua natoka muda si mrefu"

"Elly unaenda wapu usiku huu?

" we niambie gari yako ina mafuta?

"Elly jmn ndio unaenda wapi unajua sikuelewi"

"Emmy unaniumiza sana"
Aliongea hivyo akiwa anaingia ndani ya gari nilimshangaa nje kaasha gari yake anaondoka na yangu niliweza kumuona jinsi gani kavulugwa maana sikioni alikuwa anatoa maji kweny vile vitundu nilitetemeka kwani nilihisi mengi hasa hili la sam nikajua uwenda amelifahamu au kalisikia mahali.

"Bae niingize gari ndani?

'Nakuja" alijibu na kuondoka.

Niliingia ndani ya gari yake ili niipaki ndani. Nilifanya hivyo kisha nikarudishia geti, nilirudi tena ndani ya gari nikawasha taa na kuanza kuchukuza kwenye dashbody nikafanikiwa kuona kijitabu kidogo km kinote book nikakichukua na kukifungua kurasa zake niliona majina ya watu wengi na namba zao za simu hadi salma niliiona namba yake na kikubwa nilifanikiwa kuipata line ya tigi ambayo ni private number nikaichukua wakati huo naendelea kuperuzi kweny kinote book nikaona jina limeandikwa sammy nilishtuka nikainote down ile namba, mbele kidgo nikaona jina limeandikwa mpango mzima nikalinote pia down.

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI

KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger

Chapisha Maoni