MUUZA UBUYU (10)

0
Mwandishi: Micky Mejah

SEHEMU YA KUMI
ILIPOISHIA...
Wakati huo naendelea kuperuzi kweny kinote book nikaona jina limeandikwa sammy nilishtuka nikainote down ile namba, mbele kidgo nikaona jina limeandikwa mpango mzima nikalinote pia down.

NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU

SASA ENDELEA...
Nilimuonea huruma elly na kumsihi aache kunywa vile pombekali ila hakunielewa aliendelea kunywa mpk akazima. Nilipata shida kumnyanyua kutokana na kuwa heavy weight(uzito mkubwa) ila nilifanikiwa kumfikisha kitandani kisha nikarudi sebureni kwenye simu yake nikaitazama nione mtu wake wa mwisho kuwasiliana nae alikuwa ni nani? Nilikuta ujumbe kutoka kwa sammy "bro tumejitahidi kumtafuta lakini hatujanikiwa" hapo tu nilianza kupata akili inawezekana huyu sammy ni mhusika katika kumteka nyara sam.
Haikuishia hapo nikaangalia ujumbe wa pili alikuwa ni salma japo alisaviwa sally ila namb yake naijua kichwani "please samahani elly kama umekasirika but nielewe nakupenda nimeshindwa kujizuia" niliumia moyoni hamna mfano kumbe salma anamtongoza elly roho iliniuma na hapo nikakumbuka tulivyokuwa marafiki wa karibu ananifanyia hivi niliona jumbe zake tatu ambazo elly hakuzijibu japo aliziona. Nikafungua sehemu nyingine nikaona jumbe moja ambayo alituma yeye elly kwa mtu ambaye namba zake azikuwa zimekuwa saved "sitaki kusikia huo ujinga anawezaje kutoroka na hapo upo wewe, sammy na julio kweli sitawaelewa" ujumbe huo ulitumwa saa 22:44 usiku ina maana ni muda mfupi tu alipokuwa ametoka kuelekea road kutafuta pombe zake ilibidi ninote ile namba pia kwa jina la unknown guy.
**********************"

Ilitimu saa kumi na moja kasoro bado nilikuwa macho nafikiria mengi sana juu ya sam na ukweli ambao elly anaujua na huyu kahaba ambye ananizunguka na kuact kuwa ni rafiki kumbe mshenzi anayetamani emy aanguke hata leo anipokonye mume. Niliamua kuwa endapo elibariki ataamka asubuhi nimwambie ukweli juu ya sam ila roho inasita maana atajua nimejua siri zake kupitia simu yake na hata ile line ya private number asipoiona atashuku bado nitakuwa sijasave tatizo. Sijui nililala saa ngapi ila nilijikuta nipo kwenye ndoto za hatarimno.

Siku hiyo elly alinichukua na kunipeleka tour moja ndefu ambapo ilikuwa ni ya kutembelea moja kati ya mbuga za wanyama nchini it was just fun journey(ilikuwa ni safari yenye furaha sana) nilipenda sana na haya yote elly alifanya ili tu kuufanya ubongo wangu na akili yangu usimfikirie mwanaume mwingine ila niyeye tu, tulifika mpaka kwenye hotel moja ya kifahari ambayo ufikia watalii ambao asilimia 70% ni outsiders(watalii kutoka nje). Tulispend pale siku ya kwanza ilikatika, sikuya pili yake tulitoka na kwenda umbali mrefu kutoka pale ilipo hotel au mbuga, ilikuwa karibu na waterfall(mteremko wa maji) mbele yetu kulikuwa na mwanaume aliyetupa mgongo akitazama upande ambao maji yanamwagika.
Tulimsogelea mpaka pale elly alipomuita "saaaam" nilishtuka lilipotajwa hilo jina kugeuka alikuwa sam niliyekuwa namuwaza mimi na kumfikiria kwa kipnd kirefu mno "the game is over" sam alijibu hapohapo nilisukumwa kwenye lile bonde kubwa la maji.


"Nooooooooooooo" nilipiga kelele palepale nilianguka kutoka kwenye sofa mpaka kwenye carpert. Nilikaa kwanza nikafikisha macho nikatazama picha yangu ukutani nikiwa nipo na elly nakumbuka siku nilipopiga nae ilikuwa beach moja kigamboni ina sunrise, si ngeni machoni kwangu ila tu ilibadili mwelekeo wa fikra zangu.
"Mmh hii ndoto ina maana gani mungu wangu" nilijiuliza maswali kimoyomoyo "mmh inaonyesha nisipokuwa makini ninaweza kuwapoteza wote wawili kwanini nisiseme ukweli tu" niliendelea kujiuliza maswali moyoni..

Nilikumbuka elly amelala ndani na muda si mrefu ataamka kwenda kwa job hivyo ilibidi niamke kumchemshea maji ya chai na kumkaangia angalau mayai pindi atakapoamka apate kifungua kinywa kabla ajaondoka kwa muda ule nilikuwa nimewahi sana(saa 12) ila nalikuwa nahitaji angalau nikasome maana siku mbili hizi sikufanikiwa kufika kabisa darasani.
Nilifanya kila kitu mpk mambo yalipokaa sawa niliingia chumbani nimuamshe elly akaoge tuondoke mapema.

Nilishangaa ambapo sikumkuta mtu nikajiuliza " huyu ameenda wapi na jana alilewa" nilipata wasiwasi nikatoka nje ya nyumba gari yake haikuwepo ikiashiria ameondoka nilirahumu mno kuwa mbali naye ila uzuri nina zile namba, sasa tatizo nitapata wapi mtaalamu wa kuongea kiswahili kama cha kichagga kama elibariki ili nitumie kuongea na wale watu ambao tayari niliikuwa na namba zao. "Nitapata akili nikishafika shule" nilijiandaa nikanywa chai na selesi moja tu nikavaa vizuri nakumbuka siku hiyo nilivaa skin jeans, simple nyeupe, blauzi nyeupe kiujumla nilipendeza kama nilivyojiona kwenye kioo kwani siku zote hakidanganyi.

Sikutumia muda mrefu kudrive maana kutoka kijichi mpaka kurasini nilitumia dakika 20 tofauti nikiwa peke yangu. Nilimtafuta mtu wa kuongea lafudhi ya kichagga ila nimalize utata kwangu na nijue kilichotokea uko nyuma.
*************

Muda mrefu ulikatika sikumuona elly kibaya aliondoka bila hata kuaga ila nakumbuka moja kati wale watu watatu aliniambia ukweli juu ya sam story ilikuwa hivi:

Kuna dada anaitwa salima alinipiga simu siku hiyo nilikuwa nipo na elibariki, tulikutana kama bahati nilikuwa naingia kwenye ukumbi wa ddc keko ndipo nilikutana na elobariki. Tuliongea mawili matatu ndipo alipopata simu kutoka kwa mdada salma alitoa maelezo mengi ila alionysha ni mtu mwenye kutaka kitu kwani alipomaliza ya moyoni akasema "please usijisahau" niliacha nafasi ya yeye elly anisumulia kama angehisi kufanya hivyo.

Wakati huo ndipo tulimkamata kijana huyo sam ambaye alichukiwa sana na elibariki kitendo kile kilisaidiwa na yule dada salma ambye alikuwa ni mtu pekee tuliyekuja naye.

"Mmh mlipitaje mlangoni" ilibidi niulize swali(emmy)

"Kuna mtu anaitwa Romney ni mtaalam wa it ndiye alitusaidia tukaja pale hotelini tukiwa na dawa za kupoteza fahamu ili tumchukue sam"

"Ina maana gani kufanya hayo yote na faida yake?
Emmy akauliza tena.

" ni mambi ya bosi wetu na wivu juu yako emmy"

"Sam yupo wapi sasa?"

Baada ya muda mrefu kupita nakumbuka kipindi flani nilipanga njama ya kumtorosha sam kuelekea handeni tanga kisha halale pale siku moja aende mombasa kenya kwa mama mkubwa wangu ili kujikinga mauaji maana elibariki alipanga kumuua na kumzika porini kuua ushahidi yani hapa nilipo cna maelewano na elly na wale wengine pia wanahesabika kama walimtorosha sam.
*************"

Niliumia roho ila sikukata tamaa baada ya kuongea na yule mkaka na kuniahakikishia sam yupo na namba zake pia anazo naweza kuwasilian naye. Huo ndio kama ulikuwa mwisho wa kuongea na yule kaka nilikuwa nilikuwa nipo temeke nakumbuka baada ya kurudi kuja kumuona mamdogo aliyekuwa mgonjwa muda huo nilitumia muda mwingi kuchat nilipita kichochoro kimoja nilikuwa naelekea dukani ghafla nilisikia naitwa pale pale niligeuza shingo nilikutana kitu kama flapeni usoni.....


Nilisikia maumivu makali usoni baada ya ile flampeni kutua usoni kwangu niliita sauti ya juu kisha nikapoteza fahamu palepale.
*****************

TURUDI KWA EMMY NA CINDY.
(Mpenzi msomaji napenda kukumbusha kuwa simulizi yote unayosoma huko nyuma ni hadithi ya emmy kwa rafiki yake cindy)..

"Mungu wangu!" Cindy alionyesha kushtuka kutokana na kusikia hivyo.

"Basi nikajikuta nipo hospitali ila nikiwa na maumivu makali sehemu za paji la uso"

"Enhee emmy story yako inavutia sana natamani kujua ilikuwaje?

Kabla hawajaendelea na simulizi emmy alinyanyuka akaenda kwenye friji akachukua juice na glass mbili ambazo aliweka juice na kurudi tena sebureni.

" enheee endelea na story" cindy alionysha kuwa na shahuku kubwa na ile simulizi.

"Shoga unapenda ubuyu wewe" aliongea emmy.

"Hahaaa sio hivyo nataka nijifunze mengi kutoka kwako" aliongea cindy.

"Aya mwaya kunywa na juice basi tuendelea leo si wikiend tutaongea mpk uchoke wewe"
************

Nilirejea nyumbani baada ya kupata nafuu, cha kushangaza sikuwahi kumjua aliyenifanyia lile tukio, angekuwa kibaka simu yangu na pesa zangu angechukua lakini haikuwa hivyo, nakumbuka siku hiyo ni salma ndiye aliyenifata hospitali na kunisaidia.

"Mamie tunapanda daladala au" aliuliza salma.

"Nooo tukodi bajaj mamie" niliketi pembeni yeye akatoka mbali kidogo kuulizia dereva bajaj kama tungeweza kupata usafiri, kusema ule ukweli sikuwa na imani hata punje ya kumuamini huyo salma sema nilijikaza tu kuongea nae ila ni mtu niliyemtoa moyoni kabisa hasa nikikumbuka yale matukio ya nyuma kitendo cha kuwa na mawasiliano na bwana wangu elibariki na kuunda njama ya sam kukamatwa hiyo tu iliniogopesha na niliamini ipo siku ataniua kabisa " na nina wasiwasi atakuwa ni yeye kanipiga na flampeni usoni, kweli mfadhili mbuzi" nilikatishwa mawazo yangu baada ya bajaj kuja mpk pale nilipokuwa.
*************

Siku zilikatika tukiendelea na ukaribu na salma kiasi kwamba wasiwasi juu yake ulianza kupotea, kuna wakati nilimuona kama mtu aiyetumwa kwa mpango flani na inawezekana ni kuniua hivyo sikutaka kabisa nimpe nafasi mno lakini yeye alikuwa akimbiliki kama kalio na chupi yani.

Taratibu nilianza kujenga imani nae kwani alinieleza mambo yake na matarajio yake kimaisha, nilikumbuka tulipotoka toka miaka3 tumekuwa wote mpaka leo hii 19/20 tumedum ya kupewa taarifa kuwa atakuwa huko kwa auty yake yule aliyenisimulia ile simulizi ,,,††††

Siku zilizidi kusonga nikiwa ni mtu mpole sana na nakumbuka kuna siku nikikawakumbuka wale watu wa kule hotel ambayo waliniahidi kuwa nami kwa kila hatua ni mimi ndye niliwasahau kwa kipindi hiki ila nilipanga ratiba ya kuonana nao kesho yake.

Ilipotimu asubuhu nikijiandaa na kumjulisha jimmy na william kuwa nitapita pale, ila nilipanga kukutana na mtu mwingine pia ila kibiashara zaidi maana biashara yangi ilinipa umaarufu wa haraka na kunifungulia wigo mpana ktk ufanisi wa kazi pia.
*****

"Emmy wewe una pass ya kusafiria? Aliuliza jimmy baada ya kuanza kikao

" hapana sina" nilijibu kwa kutingisha kichwa kabla ya kutoa sauti.

"Unajua elibariki anafanya biashara gani?aliuliza willy

," ndio anauza maduka na pia ana saluni zake" nilijibu kwa kujiamini.

"Sawa kuna mambo bado tunapeleleza tutakupa ripoti ya siku hizi mbili, sawa dada" alihoji willy

"Sawa nashukuru".

Nilitoka nikiwa mnyonge kwani nilitegmea mengi kutoka kwa wale jamaa ila ckukata tamaa ile safari yangu ya kwenda kenya bado nilikuwa naiandaa kwani kilichokuwa kinakwama ni anuania za sehemu niendako na yule jamaa anayedai/aliyesema sam yupo pia hakupatikana hewani. Nilijitupa kitandani nikiwaxa mengi ila nilishangaa willy akinipigia nikapokea haraka sana kwani nilijua kutakuwa na mpya.

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI

KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)