PENZI LA DADA (8)
JINA: PENZI LA DADA Mwandishi: Khamis Kambi SEHEMU YA NANE ILIPOISHIA... "Hapana usijali ntapanga mwenyewe" "usiwe mbishi John" "haya basi nguo nnazobeba ni hzo hapo wewe ziweke tu! kwenye begi" Coleen akasema"ok" NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU SASA ENDELEA... Basi akazipanga kisha akamaliza na kuniambia "John tayari lala mapema kesho tutaondoka asubuhi sana" sikupinga lakini kwa mawazo niliyokua nayo nilijua usingizi nisingeupata kirahisi", basi baada ya Coleen na Sweet kuondoka mimi nikaendelea kufikiria la kufanya huku nikipiga simu tena hotelini kuulizia kama angalau naweza pata chuMba kimoja cha akiba lakini vyote niliambiwa vilikua tayari vimejaa kwani kulikua na harusi ya muigizaji maarafu JOHN PREY kwahyo kulikua na wageni mbalimbali waandishi wa habari pia waigizaji wengine jibu hilo lilitosha mimi kugundua hii ilikua ni lazima hoteli iwe imejaa basi ikabidi nikubaliane na hali halisi kisha nikaamua bora nilale. asubuhi n…