MY SECRET DIARY (11)

Zephiline F Ezekiel
Mwandishi: Michael Mejah

SEHEMU YA KUMI NA MOJA
ILIPOISHIA...
Sasa kwa muda ambao nilikuwa najifanya kumuombea rose kwakuwa yule anayekuja haikuwa rahisi kutuona kwakuwa nilimpa mgongo na isitoshe alikuwa mbali kidogo kutuona haikuwa rahisi sasa kwa muda ule rose aliweza kuvaa vizuri nguo zake na pia mimi nilipata fursa ya kumrudisha kasuku wangu pangoni kisha tuliendelea na maombi kabla ya kumaliza.

NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU

SASA ENDELEA...
B"haya nenda kapumzike nadhani utakuwa sawa"
Tuliongea mimi na rose na kumfanya aliyekuwa pale aamini kabisa kuwa tulikuwa kwenye maombezi kumbe we acha tu. Ile kugeuza shingo alikuwa mchungaji akatabasamu huku akiwa ameweka mikono yake nyuma.

"kazi nzuri sana jacob"

"sifa kwa mungu"

"haya me naenda usiku mwema" aliaaga rose na kutuasha na mchungaji.

"haya rose ubarikiwe"

"amina mchungaji"

Rose alipopotelea nje kabisa nikabaki mimi na mchungaji kisha mchungaji atoa ile mikoño yake nyuma na kunipa dairy ni mfano wa dairy kama yangu.
Nilíipokea kwa kusita sita kidogo ila nilifanikiwa kuishika kiganjani kwangu juu kabisa iliandikwa "MY SECRET DIARY" nilishtuka maana diary zangu zote niliziandika hivyo nilihisi kutetemeka mwili mzima.
"jacob my sin usiogope ebu fungua na ndani uone"
"mchungaji hii diary yangu umeipata wapi?"
"jacob fungua kwanza ndani"

Nilitii amri nikafungua na kutoka gamba la juu paliandikwa JINSI YA KUPATA NGUVU TIMILIFU NA KUUTANUA UFALME WAKO" Nilishangaa sana diary ni kama yangu vilevile ila kilichomo ndani ni tofauti.
***
Kama saa sita na nusu nilikuwa naangalia vile diary mbili zote zimeandikwa my secret diary ila ile ya kwanza niliandika "LIFE AFTER RECEIVE CHRIST IN MY LIFE" Na nyingine iliandikwa "LIFE BEFORE RECEIVE CHRIST" nilitetemeka mwili mzima na nakumbuka kauli ya mwisho pale hallini aliniambia "jacob nataka uwe mtu mwingine" nilijaribu kumuuliza kivipi hakunijibu zaidi aliniambia nijiandae.

"sasa hapa nashndwa kumuelewa mchungaji ana maana gani nipo njia panda" niliwaza na kuwazua kabla sijapitiwa na usingizi.

Nilikuja kushtuka pamekucha nami nilikuwa wa kwanza kuamka pale roöm kwetu yapata saa kumi na moja kasoro nilikumbuka napaswa kwenda morning grory/maombi ya asubuhi. Nilivuta sweta langu pale juu kisha nikawa napiga hatua kuelekea ofisi ya mchungaji.
Nilipofika pale nje taa ilikuwa inawaka ndani ya ofisi na nilienda moja kwa moja na kufungua mlango looo! Alikuwa mchungaji akifanya mapenzi na rose na ni jana tu nimetoka kufanya nae mimi. Nilishangaa sana kiongozi wa dini nae anafanya hivi kweli!!!
Usidanganyike mungu adhihakiwi chochote apandacho mtu ndicho atakachovuna.

Nilitaamaki kwa muda baada ya kumuona mchungaji akiwa anazini na rose mwana maombi mwenzetu nilitokea kumchukia yule mchungaji nikatoka nje kwa hasira na kubamiza mlango kwa nguvu sikujua kilichoendelea kule ndani maana huyo rose hakuniona ila mchungaji.

Nilikutana na spiritual leader/kiongozi wa kiroho wa kike patricia akiwa na joan, pendo, Amina, justina na leah. Wote hawa walikuwa wanakuja kwenye maombi ya asubuhi na wasichana wengne kama kumi na mbili.

"vipi tena kaka mchungaji hayupo?

"patricia we acha tu mchungaji yupo ndani uko?"

"anafanya nini ina maana maombi hamna au?"

"muandaa neno yupo wapi?"

"khaa rose tumemtafuta dom hatujamuona tukajua ameshatangulia"

"patricia hapa cha muhimu twende madarasani tukafanye maombi naona leo ofisini kwa mchungaji haitawezekana"

"mmh madarasani utakuta kuna watu wanajisomea tutakuwa tunawasumbua"

"sawa mungu yupo popote ebu hapahapa tufanye maombi isijekuwa kuamka kwetu kukawa ni bure tu"
***
Maisha yalisonga na nilijitahidi kumkwepa mchungaji nisionane nae lakini nae kumbe alikuwa ananitafuta tulimalize lile jambo kukwepa aibu.

"jacob mbona unanikimbia sana na siku hizi unafanya mambo bila kunishirikisha"

"mmh mchungaji unajua unanichanganya wewe ndie unayepaswa kurekebisha tabia za watoto lakini unawaharibu me nashindwa kukuelewa"

"hahaha utanielewa tu jacob ebu njoo ofisini tuzungumze kwanza"

Nilikubali na kuingia nae ofisini uku nikimtazama vizuri huyu mchungaji wa kusomea tena chuo cha biblia dodoma na mara zote akisimama kuubiri alikuwa anahubiri upendo na kukemea dhambi hasa uzinzi leo hii anafanya uasherati yani nilimchukia kweli.
"sikiliza jacob wewe bado kijana mdogo ila nataka nikwambie siri moja"

Nilitulia kimya kumsikiliza mchungaji wangu ambaye ndio alikuwa mlezi wangu kiroho kwa muda wote pale shule.

"kuna wakati huwa ni ngumu sana kushinda vishawishi hasa unapojikuta unamfanyia delivarise/uponyaji mwanamke mzuri tena hasa kwa sisi wachungaji tusiooa ni ngumu umenikuta na rose sawa lakini nina mpango wa kumuoa rose na si kumchezea" nilikisa kichwa na hapo nikaanza kumpima huyu mchungaji uwezo wake wa akili.

"kwahiyo hata wewe jacob upo nakuona mungu anakutumia sawa lakini wewe ni kijana ni lazima utajikuta majaribu sasa ili usíingie uko tafuta eeh kabinti kazuri kuwa nacho"

"nimekusikiliza sana mchungaji lakini neno la mungu linasema ole wao wachungaji waovu wanaoshindwa kulikusanya kundi la kondoo bali kulitawanya, mchungaji yafaa nini mtu kuzitii tamaa za mwili na kufanya kitu ambacho ni chukizo kwa mungu? Me sipo tayari kufanya hayo uliyoyafanya wewe kwaheri"
Nilimuasha mchungaji paul na kuondoka hadi darasani nikavuta kiti na kukaa nikiwa natafakari sana juu ya hayo yaliyotokea.
***
Baada ya mwezi mmoja kupita na mimi kutokuwa na mahusiano mazuri na mchungaji mara leo ananisemea kwa walimu mimi simuheshimu mara kwa baba kuwa sasa hivi nimebadilika ni kweli inaweza kuwa kweli lakini halikuwa jambo sahiihi kwa sasa.

Neno la mungu liñasema "dhambi ikitungwa uzaa mimba na mimba ikikomaa uzaa mauti" nilikuwa sifahamu hili lakini siku ambayo wasichana walishtukizwa na kufanyiwa vipimo vya ujauzito hapo ndipo ilipojulikana rose ni miongoni mwa wasichana watatu waliopata ujauzito.

Mahusiano kati ya mimi na mchungaji yalianza kuwa mabaya kwani alianza kunitolea kauli mbaya kwa walimu na mara zote amekuwa akimpigia baba na kumwambia siku hizi nina tabia mbaya simuheshimu wala ibadani sihudhurii sikumjali kabisa na hata kipindi nimeongea na baba nikamwambia asimzingatie kabisa.
Kweli biblia inasema "dhambi ikikomaa utunga mimba na kisha mimba hiyo huzaa mauti" ndicho kilichotokea kwa baada ya mwezi mmoja wasichana walienda kupima mimba na kati yao watatu walikuwa na ujauzito akiwemo rose wote tulikuwa tumbo joto sikujua ni mimi au mchungaji.

MWENDELEZO WAKE.

Sikutulia kipindi ambacho wanatoka kwenye vipimo ili uamuzi mwingine uchukuliwe mimi moja kwa moja nilimfata rose nikamvuta mkono kichochoroni.
"nini lakini jb niache hapa nimechanganyikiwa sijui baba akijua itakuwaje"
"rose ebu niambie hiyo mimba ni ya nani?"
"kusema ule ukweli mimba hii ni yako jb yule mkaka alikuja baada ya yako kuingia"

"hivi rose kwanini wewe ni malaya namna hii ona umeamua kulisambalatisha kanisa sijui tutaonekanaje hapa"

"jb wewe sio malaya? Aznael umemfanyaje na mimi ndo nimekutunzia siri wewe endelea kunitibua mambo yako ntayaweka adhalani wajue ushenzi wako"

"aaah rose uko mbali lakini rose wewe ulijua fika upo katka kipindi kile kwanini uliniseduce/
kushawishi tufanye Vile ona sasa"

"jb sikiliza kuna wakati ambao sisi wasichana yai linapopevuka kwa wakati huo mwili unakuwa na joto kali na unatamani yani uwe na mwanaume karibu na ukishafanya hivyo taap mimba ndo kilichonikuta mimi lakini sawa tu najua ntafukuzwa shule na bila ya uamisho"

"rose niokoe basi baba yangu mchungaji na wanafunzi wote wanajua nitamtia aibu na fedheha"

"wewe rose ebu njoo haraka hapa"

Alitokea mchungaji na kumuita rose huku sura yake imekunjamana kama ramani ya taanzania na mimi nikawa nimesimama palepale.

"ebu rose nakuomba usinitaje ntaumbuka mimi mtu mzima nisaidie nakuahidi tukitoka hapa ntakuoa"

"fyooo we kumbe una akili uniharibie maisha kisha uniambie utanioa mimi nimekuja kutafuta mume shule sasa jiandae mimi nikifukuzwa shule na wewe hauna kazi shenzi"

Rose aliondoka pale na mimi nikabaki uso kwa uso na mchungaji ambaye alikuwa best yangu sana sana zamani kabla ya mambo haya kutokea. Aliangalia kwa kitisho sana.

"wewe unanifatilia sana sasa subiri utaona usidhani naondoka hapa ukajua sitakupa kuna watu wangu nimewaasha hapa mpuuzi na mapembe yake wee"

Nilibaki mwenyewe pale na nilimshukuru mungu sikumjibu kitu chochote hadi alipoondoka. Nikiwa nimesimama pale nachezea tai yangu mara nikasikia kengele imegongwa palepale nikajua ni kuhusu kufukuzwa shule kwa watu yani nilitetemeka sana. Ilikuwa cabinet yote ya shule na mkuu wa shule ndo alikuwa anahutubia wote tulikuwa kimya kama tupo gwaride.

"shule yetu imejengwa kwenye misingi ya dini na hata sheria zetu pia sasa endapo utakwenda kinyume na maadili yetu hapa hautakuwa rafiki yetu tena. Ni kosa la jinai kama katiba ya nchi inavyosema mwalimu au mfanyakazi yeyote kumpa mimba mwanafunzi pia hapa shule utakutwa hatiani endapo utakutwa na mahusiano kati yako na mwalimu au mwanafunzi kwa mwanafunzi hivyo napenda kuwatangazia wanafunzi wafuatao si wanafunzi tena wa shule ya st. Laurance"
Moyo ulipasuka paah nikajua shule ndo basi.

Ndugu mpenzi msomaji tunaomba radhi kutokana na simulizi hii kuchelewa kutokana na sababu za hapa na pale. Sasa tusonge mbele na historia ya kijana jacob.
**
Haikuwa hali ya kawaida pale shule kwa matukio kama yale ya wanafunzi kufukuzwa shule kisa ujauzito lakini siku hiyo mambo yalikuwa ni tofauti.
Tukiwa bado assemble/mstarini wazazi wa watoto waliofukuzwa shule kwa ujauzito walikwisha fika na kutukutia assmble wakati mkuu wa shule pastor michael mugarura akiwataja hao wanafunzi watatu yani jessica male, upendo mongi na rose kimario moyo ulipasuka kama radi pindi rose anatoka mbele nikajua kwa vyovyote vile mambo yanaweza kubadilika.

"jamani nyie wasichana mnaona jinsi wanaume walivyokuwa wabaya haya sembuse mmoja kati ya hawa kapewa mimba na hao wanaume miöngoni mwenu mnachotakiwa ni kuwa makini haswa mmenielewa?

"ndiooøoooo"

"nadhani tumemaliza kama kuna jipya nadhani tutawajulisha au walimu wenu watakuja kuwatangazia"

Tulikuwa tunajiandaa kuondoka hapo nikawa napumua na kusema "asante mungu" mara tukaitwa tena. "jamani rudini kuna mwenzenu anataka kuwaambia neno" Wote tulirejea mimi nikiwa nyuma kujificha nisije kuonekana akasimama rose kwenye umati wa wanafunzi 2500 akaanza kuongea kwa kwikwi.

"Jamani me napenda kuwashukuru wanafunzi wenzangu kwa upendo wenu hasa team ya maombi mlikuwa msaada mkubwa kwangu, roho inaniuma kuwaasha lakini siwezi kuzirudisha siku nyuma nalia mie kwa kutokuwa na msimamo hadi mchungaji emma aliponilaghai na kunipa mimba hii najuta mie leo nawaasha wenzangu, jamani nawahasa someni yasiwakute kama yaliyonikuta mimi na kibaya zaidi kaniambukiza na ukimwi kwani niliomba nifanyie kipimo hicho pia eeh yesu wangu"

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI

KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger

Chapisha Maoni