SORRY MADAM (10)

Zephiline F Ezekiel
SORRY MADAM (10)
JINA: SORRY MADAM Mwandishi: Eddazaria G Msulwa SEHEMU YA KUMI ILIPOISHIA... “Hivi si nilienda kuoga baada ya kupanda kitandani?” Sikuwa na kumbukumbu za kutosha kama wakati nilipo panda kitandani kuupumzisha mwili wangu nilikwenda kuoga au usingizi ulinipitia na kuanza kuota vitu vya ajabu. NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU SASA ENDELEA... Nikasimama kwenye mchuruziko wa maji kisha nikaanza kujisugua kila kona ya mwili wangu.Nikamaliza kuoga na nikamuomba Madam anipe msaada wa wa taulo la kujifutia maji.Akampa John na akaniletea bafuni,Nikajifuta maji kisha na kuvaa nguo zangu za shule,sikuwa na jinsi zaidi ya kuzivaa hivyo hivyo japo zina nuka jasho kwa mbali Nikarudi sebleni na kumkuta John akiwa anaendelea kunywa chai,nikajumuika naye.Tukamaliza kunywa chai.Nikamuomba Madam Rukia anipatie japo pafyumu ili mwili uishiwe na kajiarufu ka jasho ambacho kalianza kunikera “Ingia ndani kwangu utakuta dressing table utachagua ni pafyumu gani unayo ihitaji” Nikaingia chumbani…