SORRY MADAM (10)

0
SEHEMU YA KUMI
ILIPOISHIA...
“Hivi si nilienda kuoga baada ya kupanda kitandani?”
Sikuwa na kumbukumbu za kutosha kama wakati nilipo panda kitandani kuupumzisha mwili wangu nilikwenda kuoga au usingizi ulinipitia na kuanza kuota vitu vya ajabu.

NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU

SASA ENDELEA...
Nikasimama kwenye mchuruziko wa maji kisha nikaanza kujisugua kila kona ya mwili wangu.Nikamaliza kuoga na nikamuomba Madam anipe msaada wa wa taulo la kujifutia maji.Akampa John na akaniletea bafuni,Nikajifuta maji kisha na kuvaa nguo zangu za shule,sikuwa na jinsi zaidi ya kuzivaa hivyo hivyo japo zina nuka jasho kwa mbali

Nikarudi sebleni na kumkuta John akiwa anaendelea kunywa chai,nikajumuika naye.Tukamaliza kunywa chai.Nikamuomba Madam Rukia anipatie japo pafyumu ili mwili uishiwe na kajiarufu ka jasho ambacho kalianza kunikera

“Ingia ndani kwangu utakuta dressing table utachagua ni pafyumu gani unayo ihitaji”
Nikaingia chumbani kwa Madam Rukia na nikaanza kutafuta ni pafyumu gani nitaweza kupulizia kwa bahati nzuri nikakuta body spry kama yangu.Nikaanza kujipulizia taratibu huku nikiwa nimefungua vifungo vya shati ili niweze kujipulizia katika makwapa vizuri huku nikiwa ninacheza.Mlango ukafungulia na Madam Rukia akaingia na akaanza kunishangaa kwa jinsi ninavyo cheza cheza
“Kumbe wewe na rafiki yako akili yenu ni moja?”
“Kwanini Madam?”
“Kinacho kuchezesha chezesha hapo wewe ni kipi wakati wezako tunakusubiri?”

Nikanyamaza kimya,Madam Rukia akapiga hatua na kunifwata na kuanza kunifunga vifungo huku akinitazama usoni
“Mery anaonekana ana faidi”
“Ana faidi nini?”
“Ahaaa hakuna kitu”

Hapa ndio nikaanza kupata picha ya swali alilo niuliza Madam Rukia kipindi tunaokota mayai.Alipo niuliza kuwa mimi ni mtaalamu nikajua moja kwa moja watakuwa wameadisiana na Madam Mery kila kitu tulichokuwa tunakifanya.Tukatoka huku mimi nikiwa nimetangulia mbele na kumuacha akiufunga mlango wa chumbani kwake

“Haya hapo kila mmoja wenu abebe tray tatu tatu na mutembee kwa uangalifu musije mukaziangusha”
Safari ya kwenda kwa Madam Mery ikaanza huku njia nzima John akiwa anatupigisha story zisizo na kwichwa wala miguu.Tukafika nyumbani kwa Madam Mery na tukakaribishwa na kaka Lucka,Kutokana nimekuwa mwenyeji katika nyumba hiyo nikazipeleka tray mayai hadi jikoni na kurudi sebleni

“Broo Madam yupo wapi?”
“Yupo ndani kwake amepumzika kwani ametoka kunywa dawa muda si mrefu”
Tukakaa kidogo mimi na John tukaaga na kurudi zetu shuleni na kumuacha Madam Rukia akizungumza na kaka Lucka.Njiani tukaingia katika mgahawa mmoja na kuagiza chakula ili kuyaweka matumbo vizuri
“Eddy kuna kitu nataka nikuulize?”
“Niulize?”
“Hivi huyu Madam Rukia wewe unamuonaje onaje?”
“Kivipi?”
“Ni mlaini au mgumu kama mtu akimtoke?”
“Best hilo nalo jipya kwa hiyo unataka kwenda kumtokea Madam Rukia?”
“Ndio mwangu yaani nikimuangalia kwa jinsi mapigo yake anayo tupia mimi mwili mzima unanisisimka”
“Jitahidi”
“Nijitahidi na nini?”
“Ahaaa wewe si unamtaka….Jitahidi katika kumtogoza”
“Laiki Madam mwenyewe kauzu kama nini”
“Ndio maana nakumbia jitahidi”

Tukamaliza kula na kurudi shuleni,kwa jinsi tulivyo shiba hatukuwa na hamu ya kufyeka tukatafuta sehemu yenye kivuli cha mti mkubwa tukakaa huku tukivuta vuta muda wa wanafunzi wengine kutoka darasani
“Eddy hembu nimbie ukweli jana Salome ulimla au hukumla?”
“Sasa John best yangu unataka kusema kwamba sijamla Salome au?”
“Inawezekana ukawa umekwenda kupiga naye story tuu chooni alafu unanishangaa mimi niliyekwenda kuomba tochi”
“Best najua huto niamini ila kusema ukweli jana Salome nilimla japo alizimia baada yaw ewe kuanza kuuvuta uvuta mlango wa kuingilia chooni”

“Sasa alizimia nini?”
“Mawazo na fikra zetu zote tulijua ni mwalimu au mlizi”
“Eheee Eddy cheki yule demu pale anayeshuka darasa la kidato cha nne”
“Ndio ana nini?”
“Basi unaambiwa yule demu hapa shule hajawahi kuliwa na boy hata mmoja”
“Kwa hiyo?”
“Sasa ndio una nishushua au?”
“Sio nakushushua wewe John sasa hivi umeshaanza tabia ya kupenda penda unakuwa kama chiriku”
“Haya basi nisamehe mimi niliye kuonyesha huyo demu”

Tukaendelea na mazungumzo ya kawaida hadi muda wa saa nane na nusu watutu kutoka madarasani tukajumuika nao kwenda mabwenini kuadilisha nguo.Nikavua suruali yangu ya darasani pamoja na shati la shule na kuvaa suruali ya kushindia pamoja na tisheti.Nikatoka na kwenda darasani kuchukua madaftari yangu ambayo ninahitaji nirudi nayo
Nikakutana na Salome akiwa ameongozana na Claudia wakielekea katika Cantin ya shule kununua chakula.Nikasalimiana nao kisha Claudia akachukua vyombo alivyokuwa amebeba Salome na kutangulia mbele na kutuacha mimi na Salome tukiwa tumesimama

“Salome nikuulize kitu?”
“Niulize”
“Unauginjwa wa kuzimia?”
“Hapana mpenzi wangu ila jana nilijikuta tuu nina legea na kuisgiwa nguvu na jinsi ulivyokuwa ukiniita nilikuwa nikikusikia ila nikawa niashidwa kukujibu”
“Basi nilidhani una ugonjwa huo ili tufanye mchakato wa kukutafutia dawa”
“Mbona dawa ninayo?”
“Dawa gani?”
“Si hiyo nanilio yako”
“Nini?”
Sote kwa pamoja tukajikuta tunaanza kucheka na kuwafuanya watu wengine kutushangaa
“Ehee munakwenda kununua nini?”
“Chipsi na maandazi”
“Powa ngoja basi nikupe hela na mimi uninunulie samaki kamongo watano”

Nikajipapasa mfukoni nikastuka sina walett na nikakumbuka nimeiacha kwenye suruali yangu ya shule na kwa bahati mbaya nimeicha juu ya kitanda changu kwani nilitaka niifue nikirudi kuchukua madaftari
“Mbona umestuka hivyo?”
“Walett yangu ipo kwenye suruali yangu ya darasani na hapo nilipo iacha mmmm”
“Basi nenda kaiwahi wasije wakakuibia.Nitakununulia hao samaki sawa baby?”
“Powa”

Nikaachana na Salome na kuanza kukimbia kuelekea bwenini huku akili yangu kuwa ikiwazia simu aliyonipa baba kwani ni simu ya gharama.Nikafika katika chumba chetu sikukuta mtu kwani watu wengine wamekwenda kuchukua chakula cha kwanza kukifunua ni begi langu la nguo na kuingiza mkono chini kwenye nguo cha kushukuru nikaikuta simu yangu kidogo mapigo ya moyo yakanitulia.Nikaichukua suruali yangu na kuikuta wallet ndani ya mfuko wa nyuma wa suruali.Nikaitoa haraka na kuifungua,Mapigo ya moyo yanakipasuka baada ya kukuta pesa zote hakuna zaidi ya shilingi hamsini iliyo baki na sikujua hata imeingiaje kwenye wallet yangu.

Nikafungua zipu ya pembeni ambapo pia ninahifadhia hale ndogo ndogo za noti,nako pia sikukuta kitu zaidi ya karatasi ambayo sikujua ni nani aliye iweka.Nikaitoa na kuiangalia vizuri nikakuta imechongwa kwa urefu wa sawa na noti ya shilingi elfu kumi huku ikiwa imechorwa picha zinazo onekana katika noti hiyo huku ikiwa na maandishi makubwa yaliyo andikwa kwa wino mwekundu yanayosomeka ‘PESA HALALI YA MALIPO YA SHILINGI ELFU KUMI’ huku ikifwatiwa na tarakimu iliyo chorwa kwa ukubwa huku ikipinda pinda ya 10,000/=

Nikajikuta nikianza kucheka mwenyewe huku nikirudia rudia kuisoma karatasi niliyo ikuta
“Oya Emma hujamuona mtu aliye ishika suruali yangu?”
“Hapana ndugu ndio ninarudi hivi kutoka class kwani vipi…?”
“Mwanangu wamesha niliza na cheki wameniachia kikaratasi tuu”

Nikampa Emmanuel kikaratasi na akaanza kukisoma naye akajikuta akianza kucheka hadi machozi yakawa yanamwagika
“Mwanagu Eddy jamaa wamekukomoa”
“Weee acha tuu”
“Wamekuibia bei gani?”
“Laki na ishirini”
“Duuu best ilikiwaje na wewe ukaacha wallet kwenye suruali?”
“Si unajua kusahau sahau”
“Daaa pole ndugu yangu ngoja wanachumba waje tuwatangazie”
“Alafu walivyo na roho za ajabu….Walet yangu wakairudishia kama walivyo ikuta”
“Alafu wenye mtindo wa kuiba na kuandika vikaratasi ni O Level kwani juzi asubuhi niliona dogo mmoja analia huku naye akiwa ameshika kikaratasi kama chako”

Hamu hata ya kukaa shule ikaanza kunipotea gafla huku mawazo yakianza kunitawala ni jinsi gani nitaaishi bila pesa na kila mwanachumba niliye muuliza akasema hajui.Na mbaya zaidi John naye amefulia kupita maelezo na kwa kipindi cha wiki mbili anakula kwa kupitia mfuko wangu

“Mwanangu Eddy ndio tumesha fulia hivi”
“Weee acha kaka yaani hapa nachanganyikawa na mbaya zaidi mzee atakuwa amesafiri”
“Mmmm best hata shibe ya chipsi tulizo zila pale kibandani imesha kwisha”
“Nimekumuka kitu”
“Kitu gani”
“Mwalimu wa ni zamu ana pesa zangu”
“Mwalimu gani kwani waalimu wa nidhamu wapo wengi”
“Sir Mayange”

“Doo yule nilimuona anaondoka zake na kale kajipiki piki kake”
“Kwake ninapajua”
“Sasa itakuwaje?”
“Itanibidi nitoroke niende kwake muda wa nyinyi mukiwa assemble ya jioni”
“Hato kuzingua?”
“Si dhani nitamuambia ukweli kwani sasa hivi muda wa ruhusa si muesha pita?”
“Ndio”
“Itanibidi nivae nguo za nyumbani”

Nikasubiria muda wa saa kumi na moja kufika nikavaa nguo za nyumbani pamoja na kofia kubwa aina ya bushori wakati wezangu wakienda mstarini jioni mimi nikarika ukuta na kwenda nyumbani kwa Mwalimu Mayange.Kwa mwendo wa kujificha ficha nisionewe na waalimu ikanichukua kama nusu saa kufika nyumbani kwa mwalimu Mayange.Nikagonga na mlango wake ukafunguliwa na msichana kwa makadirio ya umri ni kama miaka 25.Ikanilazimu kumsalia ila hakitikia salamu yangu zaidi ya kunijibu powa

“Sir Mayange nimemkuta?”
“Ametoka kwenda kutafuta majani ya Ng’ombe”
“Ninaweza kumubiria?”
“Ndio unaweza kumsubiria ila siwezi kukuruhusu kuingia ndani pasipo kukujua wewe ni nani na una shida naye gani?”

Ikanibidi kuivua kofia yangu aina ya bushori kwani ninahisi ndio inampa wasiwasi wa kunihisi mimi ninaweza kuwa mtu mbaya kwani kwa mkoa wa Arusha una waalifu wengi
“Mimi ninaitwa Eddy ni mwanafunzi katika shule anayo fundisha nimekuja kuchukua pesa za matumizi”
“Sasa mbona umevaa hivyo kama jambazi umetoroka?”
“Ndio”

Nikaanza kujiuliza mbona huyu msichana ana maswali mengi kiasi kwamba anaanza kunipa mashaka ya kuto zipata pesa zangu.Akanikaribisha ndani na nikakaa kweye kochi moja na macho yangu kuyaelekezea katika TV inayo onyesha miziki ya wamarekani weusi huku naye akikaa katika kochi jengine akinitahdimini

“Wewe hapo shuleni kwenu unasoma kidato cha ngapi?”
“Cha tano?”
“Mchepuo gani?”
“Sayansi”
“Ahaaa nilikudanganya mwaya shemeji amekwenda kwenye kikao cha harusi pamoja na dada yangu hapa kurudi hadi saa mbili usiku kama utaweza endelea kumsubiria”
“Sawa kutokana nina shida itanilazimu kusubiri hata kama ni asubuhi itabidi nikae hapa hapa”
“Sasa kama unasema utalala hapa hapa je shuleni kwenu itakuwaje?”

“Nitajua cha kufanya ila kutokana wanarudi basi itanilzimu kukaa hapa hapa niwasubirie”
“Ahaaa ila vipi masomo?”
“Kidogo tunajitahidi tahidi”
“Mimi ninaitwa Manka ninasoma kidato kama chako na nipo sayansi”
“Sasa wewe mbona upo nyumbani”
“Kidogo kuna ishu Fulani hivi ilitokea katika shule ninayo soma ikatulazimu tufunge shule”

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI

KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)