SORRY MADAM (12)

Zephiline F Ezekiel
SEHEMU YA KUMI NA MBILI
ILIPOISHIA...
Manka alizungumza kwa sauti ya kibabe na kunifanya nibaki nikimtazama pasipo kumuunga mkono kwenye mazungumzo yake. Akavuta fumba kubwa la moshi wa sigara kisha akaja kunipulizia usoni na kunifanya hasira zizidi kuongezeka

NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU

SASA ENDELEA...
“Huyo ticha wenu mayange kwangu hapa ana nihanya siku nikimuanzishia mtiti yeye mwenyewe ana bwela……Kuna siku nilimkuta anamkoromea sister kilicho mpata anakijua mwenyewe”
“Manka mpenzi wangu nakumba unifungue basii?”
“Hhaaaaa wewe fala mimi sio mpenzi wako usijidai una gia za uongo uongo alafu ukadhani mimi ni kenge kiasi hicho kugekuwa na semu yoyota ninaye soma naye ungemuuliza kuwa Mamka G. ni nani?”

Manka akamaliza kuvuta sigara yake kisha akatoka chumbani huku bastola yake ikiwa mkononi.Nikaona nikiendelea kujilaza kitandani utakuwa ni ujinga wa karne.Nikajivuta juu kidogo na kuanza kuifungua kamba ya mkono wa kulia kwa kutumia meno japo ninapata maumivu ila nikayapotezea,Nikafanikwa kuifungua kamba kisha kwa haraka nikaifungua kamba ya kumkono wa pili na kumalizia kamba za miguuni kala sijanyanyuka kitandani nikajikuta tunatazamana na Manka huku bastola yake akiwa amenielekezea kwangu.Nikamrukia Manka kabla hata sijamfikia nikstukia kitu chenye ncha kali na chamoto kikipenya ndani ya kifua changu na kuningusha chini

Maumivu makali yakanitawala katika kifua changu nikajishika kwenye kifua changu na kugungua kuna damu zinanitoka ikanibidi niukaze mkono wangu ili kuzuia damu nyingi kuendelea kuvuja katika sehemu risasi ilipoo pita.Manka akaanza kuweseka huku akiwa kama haamini kwa tukio alilo lifanya.Akaitupa bastola chini na kupiga magoti kuangalia eneo aneo alilo nijeruhi kwa risasi
Eddy nilikuwa ninakutania”

Manka alizungumza huku akilia na kuonekana kuchanganyikiwa kwa kitendo alicho nifanyia.Taratibu nikahisi nguvu zikiniishia huku mwili ukizizima kwa kukosa uwezo wa kufumbua machona taratibu nikajikuta hali nzito ambayo sikuwahi kuipata katika maisha yangu ikiutawala moyo wangu

***

Macho yangu yakafunguka na kujikuta Mama akiwa amekaa pembeni yangu huku puani kwangu nikiwa na mashine ya kupulia.Mama alipo niona nimefungua macho yangu akaanza kuliita jina langu na nikamuitikia kwa sauti ya chini
“Mwanangu unajisikiaje?’
Nikataka kunyanyuka ila nikashindwa na mama akanirudisha chini na kugundua kuna bandeji kuwa nimefungwa kwenye kifua changu.Kumbukumbu zinanikumbusha dakika za mwisho nilikuwa na Manka ila kuanzia hapo sikuelewa kitu kilicho enedelea hadi mama akawa pembeni yangu.

“Mama nipo wapi?”
“Mwanangu upo hospitalini?”
“Nani kanileta?
“Ni story ndefu kidogo mwanangu ila kwa sasa pumzinka nitakuadisia ukipata nafuu”

Simu ya mama ikaita akaitazama kwa muda kisha akaipokea na nikamuona sura yake ikiwa imebadilika kidogo na kuwa sura ya hasira
“Ndio ameamka”
Godwin nakuomba unielewe hapa huna mtoto na huyo mwanao aliye mfanyia mwanangu hivi nilazma nimfunge”
“Ahhhh kwahiyo wewe ndio umemtuma amuue mwanangu si ndio?”
“Sasa lazima nimfunge na kumbuka kuwa tangu mwanangu akiwa utotoni hukuwa na mapenzi naye sasa naomba umuache na wala sihitaji urudi uje umuuone”

Mama akakata simu huku akiachia msunyo mkali,sasa sikuelewa anazungumza na nani na kumfokea kiasi hicho
“Mama unazungumza na nani?”
“Ahaaa mwanangu nitakuambia”
Mama alanijibu huku akiwa anatabasamu kisha akanibusu katika paji la uso wangu.Simu yake ikaiita tena na ikamlazimu kutoka nje.Sikutaka kujisumbua mama anamfokea nani niahisi watakuwa ni watu wa serikali anao fanya nao kazi.Mama akarudi na kukaa karibu yangu huku machozi yakimlenga lenga akionekana kuwa na hasira kubwa na tangu nizaliwe sikuwahi kumuona mama akiwa katika hali kama hiyo.

“Mama nipo hospitali gani?”
“Ni KCMC
Mlango ukafunguliwa akaingia mzee wa makamo akiwa amevalia nguo za polisi huku akiw na vyeo vingi
“Habari yako muheshimiwa?”
“Salama vipi mumesha mkamata aliye sababisha hili tukio?”
“Ndio muhesimiwa ila ninashindwa kuelewa kwani mzee ananiambia nimuachie huru ili we……”
“Nisikilize wewe mimi si ndio nimetoa amri yule binti kukamatwa?”
“Ndio”
“Sasa mbona unaniletea Kiswahili.Muwekeni ndani hadi mimi nije sawa”
“Sawa mkuu”
Askari akatoka na kutuacha ndani ya chumba na ukimya ukatawala huku mama akonekana kusongwa na mawazo na mara kwa mara akawa anasunya sikujua kinacho mfanya asunye ni nini.

Nikakaa hospitali kwa wiki moja nikapewa ruhusa japo sikuwa nimepona vizuri.Safari ya kwenda uwanja wa ndege wa KIA ikaanza huku dereva anayemuendesha mama akiwa makini katika uendeshaji wake kutokana Dokta ameniambia nisifanye kazi ngumu wala kupata mitingishiko ya aina yoyote kwani kidonda changu kinaweza kisipone kwa haraka.Tukakuta ndege ya kukodi ikiwa tayari kwa ajili yetu mimi na mama.Tukapanda na dereva akaondoka na gari ya mama na tukaahidiana naye atatukuta nyumbani.Safari ikaanza taratibu huku ndege aina ya Fast Jet tuliyo ipanda ikizidisha kasi kadri tmuda unavyo kwenda tukiwa angani

“Pole kaka”
Muhudumu wa kike wa ndege akanipa pole huku akiniwekea juisi kwenye kimeza kidogo kilichopo mbele yangu
“Asante”
“Muheshimiwa huyu ni mwanao”
“Ndio ni mwangu wa kwanza na wamwisho”
“Aisee mtu akikutizama wala hata amini kama unamtoto mkubwa kiasi hichi”
“Unajua kipindi sisi tulipokuwa tunamaliza kidato cha sita mika ya themanini tulipelekwa jeshini sote na ilitusaidia kuweza kuzilinda afya zetu ni tofauti na hao kina Eddy mtu nikimwambia mwanangu ana miaka 20 haamini”
“Mmmm mama umekosea nina miaka 21”
“Sasa sib ado haijatimia”
“Sasa muheshimiwa nyinyi si mupo huku ngazi za juu kwanini musirudishe sheria ya wanafunzi wanao maliza kuingia jeshini?”
“Ile imerudishwa sasa sijui huku mwanagu kama ataweza kwa maana mmmm”
“Mama wewe unaniona mimi nimeoza sana”
“Wewe hujioni”

Tukacheka sote na safari ikaendelea,haikuchukua mud asana kutua katika uwanja wa ndege wa mwalimu JK Nyerere.Gari ya serikali ikaja kutuchukua na kutupeleka nyumbani maeneo ya Masaki.Nikakumbuka kuna kitu ninakihitaji kukijua vizuri kutoka kwa mama kwani kila nilipohitaji kumuuliza nilijikuta nikisahau
“Mama hivi pale hospitalini nilifikaje?”
“Eddy mwanagu hata hatujapumzika umeanza kwa maswali?”
“Ndio ama nataka kujua?”
“Kavue nguo zako chumbani kwako upumzike kisha wakati wa jioni tutazungumza ngoja mimi niende ofisini jana kuna kazi niliiacha”
“Kwani mama jana ulikuja ofisini?”
“Ndio kila siku nilipokuwa ninakuja hospitali nilikuwa ninalala Dar asubuhi ninakuja kwa ndege jioni au mchana ninarudi kwa ndege”
“Mmmmm mama mbona nyumba ipo kimya dada wa kazi yupo wapi?”
“Nimemfukuza”
“Kwa nini?”
“Nitakuja kukuambia jioni nikitoka kazini”

Mama akaondoka mimi nikaelekea chumbani kwangu,sikukuta kina mabadiliko ya aina yoyote tangu nilipo kiacha ipindi nanakwenda shule.Nikaingia bafuni nichukua taulo na kulichovya kwenye maji na kuanza kujisujgua sehemu ya mwili kwani ndio oga yangu tangu nikiwa huspitalini hii ilisaidia kidonda kuto kuingia maji.Nikamaliza na kurudi kitandani kutokana nimeshiba nikaamua kulala.
Nikaamka mida ya saa moja jioni na kutoka chumbai kwangu na kumkuta mama akiwa anaandaa chakula.Nikamsalimia na kukaa kwenye moja sofa zilizopo katika sabule yetu.

“Umekunywa zile dawa za kutuliza maumivu?”
“Hapana?’
“Kwa nini wakati unatakiwa kuzinya kila jioni?’
“Mama sib ado sijali.Nikila nitameza”
“Unanjaa nikupakulie chakula?”
“Mmmm nitakula baada ya kuzungumza na wewe”
“Eddy yaani mwanangu ukishikilia bango kitu yaani hadi kikamilike”
“Ila mama hiyo tabia si nimeridhi kwako”
“Kwenda zako mimi sina tabia za king’ang’anizi kama wewe”

Mama alizungumza huku kija kukaa karibu yangu na kuanza kukichunguza kidonda changu kikiwa ndani ya bandeji kubwa iliyo zungushwa nusu kufua na kufungiwa kwa mgongoni
“Alafu hicho kidonda ukikitia maji kitachelewa kukauka”
“Sijakitia….eeeha mama kwanza swali langu la mimi nimefikaje pale hospitalini ujanijibu hadi leo?”
“Pale hospitalini ulipelekwa na wasamaria wema ambao walikuokota pembezoni mwa mto huku ukiwa umevalia suruali ya jeansz na ulikuwa kifua wazi.Kwa mashuhuda nilio zungumza nao katika kituo cha polisi waliseama ulitupwa mida ya saa kumi na moja asubuhi na binti aliyekuwa na pikipiki”
“Sasa ikawaje?”
“Kuna bibi alikuwa yupo na mmjukuu wake wa kiume walikuwa wakielekea shamba ndio wakakuona pembezoni ya mto huku mtu waliyemuona akiwa anakimbia na piki piki……Unamjua mtu huyo?”
Swali la mama likaniweka njia panda huku nikijiuliza maswali ni nini nimjibu mama kwani nikisema nina mjua ataniuliza ni nani na nikisema simjui atasema nilikuwa ni wapi ninatoka wakati wa usiku

“Ninamjua”
“Ahaaa basi baada ya watu hao kukuwahisha hospitalini kwani hali yako ilikuwa mbaya sana ikawalazimu madaktari wapewe namba ya baba yako na mmoja wa waalimu aliyedai dai ni shemeji wa yule binti kisha baba yako ndio akanipigia mimi”
“Alafu mama nilikusikia kama ukibishana na simu kuwa kuna mtu alimtuma yule binti aniue?”
Mama akakaa kimya huku akinitazama kwa macho yaliyo jaa masikiiko na kwa mbali machozi yakaanza kumlenga lenga
“Mwanangu kuana historia ndefu sana unatakiwa kuijua ila kwa kipindi hiki nakuomba usome kwa juuhudi sana na uaache michezo”
“Mama na hisoria gani?”
“Utakuja kuijua tuu”
“Mama nataka kuijua kwani mama una mtoto mwengine zaidi yangu wa kumwambia mambo yanayo familia yetu”

Mama akanitazama kwa macho yaliyo jaa uchungu na machozi yakaanza kutapakaa kwenye uso wake na kunifanya na mimi nimpokee kwa machozi yalio anza kunichuruzika na kwa mistari mistari kwani mara ya mwisho kumuona mama analia ni miaka kumi iliyopita siku ya kifo cha mama yake.
“Eddy nakuoba uwe na moyo na koo la kuvumilia hiki nitakacho kuambia kwani kinahitaji moyo wa ujsiri na nisiri ambayo sijawahi kumuambia mtu wa aina yoyote zaidi yako na ninakuambia hivi kwa sababu wewe ni mwangu wa pekee”
“Niaimbie mama”

“Eddy nilikutana na baba yako kwenye ajali moja ya basi iliyotokea kipindi mimi ninaelekea chuo katika kumaliza mafunzo ya mwisho ya udaktari.Katika ajali ile watu wengi walijeruhiwa na kama sijakosea ni watu wawili tuu walipoteza maisha.Mimi nana mshukuru Mungu sikupata majeraha makubwa zaidi ya michubuko midogo midogo ila kwa upande wa baba yako yeye alipata majeraha makubwa sana katika maeneo ya kiunonina kutokana mimi nilikuwa ni daktari wa upasuaji basi nilijumuika na madaktari wezangu kumfanyia baba yako upasuaji chini ya kitovu ambapo tulikuta mirija yake ya uzazi imeharibika na tukashauriana na madaktari wezangu ambao walinishangaa kuniona nina uwezo mkubwa wa kumfanyia mtu upasuaji japo kuwa nilikuwa bado ni mwanafunzi tukaona ni vyema tukamtoa……..”

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI

KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger

Chapisha Maoni