
ILIPOISHIA...
...mimi nilikuwa ni daktari wa upasuaji basi nilijumuika na madaktari wezangu kumfanyia baba yako upasuaji chini ya kitovu ambapo tulikuta mirija yake ya uzazi imeharibika na tukashauriana na madaktari wezangu ambao walinishangaa kuniona nina uwezo mkubwa wa kumfanyia mtu upasuaji japo kuwa nilikuwa bado ni mwanafunzi tukaona ni vyema tukamtoa……..”NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU
SASA ENDELEA...
Mapigo ya moyo yakanipasuka na kujikuta nikikaa vizuri kwenye sofa na kumtazama mama ambaye uvumilivyu unamshinda na kujikuta akiendelea kutokwa na machozi.Mama akameza fumba la mate kisha akaendelea
“Tuliishoma sindano mirija yake ya uzazi ili kuwatoa bacteria ambao wangeweza kushambulia mirija hiyo kwa jinsi ilivyokuwa imeharibika.Lakini mwanangu kusema kweli ile sindano haikuwa nzuri kutokana inamfanya mwanaume kukosa uwezo wa kuzalisha mbegu zenye nguvu zitakazo mpelekea mwanaume kumzalisha mwanamke”
Nikajihisi mwili mzimwa kupoteza nguvu kutokana na maelezo ya mama na moja kwa moja hisia za baba niliye naye sasa hivi si baba yangu zikaanza kuutawala moyo wangu na kujikuta nikiwa mapigo ya moyo yakianza kunienda kwa kasi hadi na kwa maumivu ya kifua yanayotokana na jeraha la risasi yakanisababishai kizungu zungu kikali kilichonipelekea kujilaza kwenye kochi na nikaanza kuliona giza kubwa likitawala macho yangu kama ilivyokuwa siku niliyo pigwa rasasi na Manka
Nikafumbua macho yangu na kujikuta nikiwa nimelala kwenye sofa jengine lililopo sebleni huku mama akiwa pembeni yangu pamoja na mzee mmoja ambaye nilikuwa nikimuonaga akija kumtibu mama kipindi akipandwa na presha.Mama akabaki akinitazama huku sura yake ikiwa haina tabasamu wala huzuni
“Kijana unajisikiaje?”
“Afadhali kidogo”
“Kwa sindano niliyo kuchoma itakusaidia na utakuwa sawa kwani ni mstuko mdogo uliupata”
“Eddy nikuletee chakula mwanangu?”
“Ehhee ila usinitilie chakula kingi”
“Inakubidi ule ili nguvu zikurudie mwanangu wewe ujioni mwili ulivyo isha tofauti na ulivyokuwa ukienda shule”
“Sawa mama ila chakula kidogo kitanitosha”
Mama akaondoka sebleni na kuelekea kwenye meza ya chakula na kunipakulia chakula na kurudi nacho nilipo kaa
“Haya nyanyuka sasa nikulishe”
“Mmmm mama nitakula mwenyewe”
“Sawa”
“Muheshimiwa naona hali ya mwanao sasa imekuwa nzuri ngoja niwaache”
“Dokta mbona unakimbia wakati chakula kipo mezani?”
“Muheshimiwa yaani pale uliponipigia simu nilikuwa mezani ninakula kwahiyo hapa nipo sawa”
‘”Jamani dokta kaa basi ule hata vijiko viwili vitatu”
“Muheshimiwa hapa ni sawa na nyumbani kwahiyo siku yoyote nitakuja kula tena na sasa hivi upo wizara yetu ya afya basi ninajisikia faraja kwa hilo yaani ni zaidi ya kula”
“Sawa ila na wewe siku utanialika kwako alafu sinto kula”
“Muheshimiwa sasa huyo yatakuwa ni malipizo kwani si mara nyingi huwa ninakula chakula hapa…….ila nimekumbuka kitu muheshimiwa”
“Kitu gani?”
“Unajua muheshimiwa Raisi alipo kuhamishia kutoka uwaziri wa maliasili na utalii na kuwa waziri wa afya nikaona kidogo kile kilio chetu kitakuwa kimesikika kutokana nitakuwa na fursa ya kuzungumza na wewe pamoja”
“Kilio gani Dokta Amdanil?”
“Mama kwani umehamishwa wizara?”
“Mwanangu siku zote ulikuwahujui?”
“Sijui kwani shule kwenyewe hata TV yenyewe hatutizami?”
“Ehee makubwa hayo sasa ni kwanini hamtizami TV?”
“Waalimu wanatubania”
“Mwanangu siku hizi unakiswahili cha kiuni kubaiwa ndio nini?”
“Hawataki”
“Eheee dokta endelea mwaya kwani huyu mtu akianza kuzungumza hapa hamalizi na sasa unaweza kusema amemeza CD ya mziki”
“Mamaaa!”
“Mama nini wakati huo ndio ukweli”
“Kweli hali yake imekuwa nzuri uchangamfu kidogo umemrejea………Muheshimiwa mimi ombi langu naweza kusema nimaombi yangu pamoja na madaktari wengi…..Muheshimiwa hembu naomba kidogo mishahara yetu muifikirie kwa mara nyingine kwa maana kodi kila kukicha inaongezeka na ukitazama mishahara haipandi”
“Hilo ndio nitalipa kipaumbele tukirudi bungeni mwezi ujao na wala usiwe na mashaka na hilo”
Nikanyanyuka na kujiweka pensi yangu ya michezo vizuri na kuwafanya mama na Dokta wakinitazama
“Unakwenda wapi?”
“Toilet”(Chooni)
“Hizo ngazi za gorofani upande taratibu usije ukaanguka na urudi umalizie chakula chako”
“Mama nimeshashiba”
“Nimekuambia urudi uje kumalizia chakula chako”
“Sawa mama Eddy”
Nikaondoka na kuwaacha mama na daktari wakiendelea kuzungumza mambo yao ya kikazi,nikaingia katika chumba changu kilichopo gorofani na moja kwa moja nikaingia katika choo kilichopo ndani ya chumba changu na kujisaidia haja ndogo.Nikakumbuka kwenye kabati la chumbani kwangu kuna simu yangu ambayo niliiacha kipindi ninakwenda shule nikatoka chooni na kufungua kabati langu na kuaanza kuchangua vitu na kuanza kuitafuta kwani katika sehemu niliyo iweka haikuwepo.Nikatafuta zaidi ya dakika tano sikuuiona ikanibidi nitoke chumbani kwenda kumuuliza mama ila kabla sijashuka kwenye ngazi nikasikia swali la daktari na kunifanya nisimame na kuyasikiliza mazungumzo yao pasipo wao kuniona
“Yule dada wa kazi amekwenda wapi?”
“Yule niliamua kumrudisha kwao kwani amenivurugia familia yangu”
“Kivipi?”
“Dokta yaani ni makubwa sana yaani watu wa nje wanapo ona mtu uanishi katika jumba kubwa magari mazuri wanahisi haya ndio maisha mazuri ila kusema kweli dokta yaani ingekuwa sio haya majukumu ya kiserikali ningeondoka nchini na mwanangu kwenda kuishi mbali na Tanzania”
“Muheshimiwa kwa nini umezungumza hivyo wakati Mungu amekujalia kila kitu katika maisha”
“Ndio amenijalia kila kitu katika maisha ila sio amani katika ndoa yangu…..Daktari ninakuambia hivi kutokana wewe ni sawa na kaka yangu na mamo mengi umekuwa ukinishauri ila hata hili nahitaji unishaur kutoka kwako”
“Kwani kuna kitu kibaya kilicho tokea kati yako na mzee?”
“Ndio tena ni kikubwa sana ambacho kinaninyima usingizi kila nikikifikiria……Si nilikuwa masomoni kwa kipindi kirefu kidogo”
“Ndio”
“Basi huku nyuma nilimuacha huyu kijana wangu yule binti wa kazi na mzee”
“Ndio”
“Wakati nikirudi nchini sikutaka mume wangu atambue kitu chochote…..Nilifika hapa Tanzania mida ya saa saba usiku na pia sikutumia gari yangu kohofia dereva wangu anaweza kumuambia mume wangu kuwa ninarudi”
“Sasa ni kwanini hukutaka mzee ajue?”
“Nisikudanganye dokta kwa jinsi nilivyokuwa nikimpenda baba Eddy basi kama kuna kitu chochote kibaya kitakuwa kanamtokea basi mimi moyo wangu hujikuta na wasi wasi sana kiasi kwamba hata kama anakuwa na safari ya muhimu huwa nina mzuia asiende na akibaki ujue kuna tukio baya litatoke sehemu aliyokuwa anahitaji kwenda…….Basi miezi mine nyuma hali hiyo ikawa inanisumbua sana kiasi kwamba nikaanza kuwa na mashaka kuwa kuna kitu mume wangu atakuwa anakifanya ambacho ni kinyume na makubaliano ya ndoa yetu……..Basi niliingia hapa usiku kama saa nane kasoro hivi kwa kutumia taxi ya kukodi hadi askari wa getini akanishangaa.Sikustuka kutokana ni kawaida ya nyumba yangu kuwa na ukimya,nilipitiliza moja kwa moja hadi ndani kwangu…..Dokta huwezi amini yaani nilimkuta Baba Eddy akiwa amelala na yule binti”
“Weeeee…..!!?”
“Ndio dokta na mbaya zaidi juu ya kitanda changu nilicho kinunua kwa pesa yangu”
“Yule binti kumbe anatabia chafu kiasi hicho?”
“Dokta weee acha tuu hapo ndipo nikaamini ule usemi wa mfadhili mbuzi kuliko binadamu kwani anamaudhi.Na ninamshukuru Mungu ile siku presha yangu haikupanda”
“Sasa hapo ndio naanza kupata pichaa”
“Picha gani dokta?”
“Mwezi uliopita yule binti alikuja pale hospitalini kwangu”
“Alifwata nini?”
“Ndio nakuja huko ulipo niuliza……Alikuja kwa lengo nimtoe mimba?”
“Mimba…..!!?”
Mama aliuliza kwa sauti ya juu hadi na mimi nikstuka nilipo simama na kunifanya niwachungulie na kumuona mama akiwa amekaa katika kochi lake nililo muacha huku akimtazama dokta kwa umakini
“Ndio alikuwa na ujauzito wa mwezi mmoja na nusu”
“Sasa hiyo mimba atakuwa ameipataje pataje wakati mume wangu hana uwezo wa kumzalisha mwanamke?”
“Ehhee mbona uwezo huo anao tuu wakumzalisha mwanamke?”
“Dokta mbona unanichanganya na wewe…..Mimi ninazungumza hivyo kutokana mimi nilihusika katika oparesheni ya mume wangu kipindi amepeata ajali na tulimchoma sindano ambayo asinge weza kumzalisha mwaanamke wa aina yoyote,K?umbuka hata mimi nilikuwa ni daktari?”
“Ndio nalitambua hilo kuwa wewe ni dokta ila hichi ninacho kuambia mimi nina uhakika kutokana miezi mitano hivi ya nyuma kuna madaktari wa wachina walikuja pale hospitalini kwetu wakijishuhulisha na maswala ya wanaume walio na tatizo kama hilo unalo lisema.Mzee alikuja kunitembelea ila hakujua kama kuna huduma hiyo ya kupima wanaume inatolewa pale hospitalini.Katika mazungumzo yatu nikamtania kiutani utani akapime na yeye ili ajue kama ana uwezo au hana…….Alipo pima kama ulivyo sema wewe kuwa hana uwezo wa kumzalisha mwanamke ndivyo majibu yake yalivyo kuwa.Kutokana wezetu wachina wapo mbele kwa taaluma hiyo basi wakamfanyia upasuaji mdogo akarekebishwa katika mirija yake akapewa dawa na akapona kabisa”
“Ndio akaamua majaribio yake ya kama amepona ua hajapona ndio akaamua ayachukulie kwa mtoto wa watu?”
“Kwa hilo hata mimi sijui….Basi yule binti alinibembeleza sana niweze kuitoa mimba aliyo kuwa nayo kwa akili za haraka haraka nikajua mimba amepewa na vijana wako wa kazi…..Ila nikaja kupata mashaka zaidi pale binti siku ya pili alipo nijia na milioni tano ili nimfanikishe kumtoa mimba”
:Na wewe ukamtoa?”
“Sikudhubutu ukiachilia mbali maadili yangu ya kazi hayaruhusu daktari kumtoa mwanamke mimba pia hata imani ya dini yangu hairuhusu jambo hilo”
“Ehee ikawaje?”
“Nilimfukuza akaondoka akiwa analia.Nikachukua jukumu la kuwasiliana na mzee nikakutana naye ila mimi kama dokta kwa jinsi mzee alivyokuwa akinijibu nikaanza kupata mashaka ila nikaja kuachana nalo kutokana nilijua mzee atalifanyia kazi”
“Kwa nini na wewe usinipigie simu ukanieleza hilo swala?”
“Muheshimiwa niliogopa kutokana wewe upo masomoni na isitoshe ulikuwa unakaribia kipindi cha mitihani”
Mwili wangu ukashikwa na ganzi iliyonifanya nitulie sehemu nilipo huku machozi yakinilenga lenga sikuamini kama baba anaweza kutembea na msichana wa kazi na mbaya zaidi msichana wa kazi maisha ya kwao sio mzuri kabisa na ndugu zake wanasomeshwa na kwa pesa ya mama
“Muheshimiwa futa machozi silie”
“Dokta inauma mwanaume niliye mwamini na kumuinua kimaisha leo hii ananifanyia kitu kama hichi”
“Muheshimiwa hizo ni changamoto za maisha”
“Hapana dokta huo ni upumbavu tena upumbavu ulio pindukia yaani pia nashukuru sijazaa na huyu mwanaume”
Nikastuka kusikia mama akizungumza kitu kama hicho huku akiwa analia kwa uchungu na kunifanya na mimi kujawa na hisia za huzuni na taratibu machozi yakaanza kunitoka,Kutokana na hali yangu ya kuumwa sio nzuri sana ikanilazimu kukaa katika ngazi ya juu huku nikiwa nimeuegemea ukuta na kuendelea kuwasikiliza mama na daktari
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI
KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger
Email: ZephilineEzekiel@Gmail.Com