SORRY MADAM (14)
JINA: SORRY MADAM Mwandishi: Eddazaria G Msulwa SEHEMU YA KUMI NA NNE ILIPOISHIA... Nikastuka kusikia mama akizungumza kitu kama hicho huku akiwa analia kwa uchungu na kunifanya na mimi kujawa na hisia za huzuni na taratibu machozi yakaanza kunitoka,Kutokana na hali yangu ya kuumwa sio nzuri sana ikanilazimu kukaa katika ngazi ya juu huku nikiwa nimeuegemea ukuta na kuendelea kuwasikiliza mama na daktari NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU SASA ENDELEA... “Muheshimiwa unataka kuniambia huyu kijana si mtoto wa mzee?” Kabla daktari hajajibiwa swali lake na mama simu yake ikaita,akaitoa na kupokea na kumfanya mama akae kimya “Ajali ya basi gani?’ “Majeruhi 34?’ “Ninakuja ninakuja sasa hivi” “Dokta ni ajali ya basi gani?” “Basi la Msulwa Express limegongana na roli la mbao maeneo ya maili moja” “Eheee wamekufa watu wangapi?” “Watano ila majeruhi nao wana hali mbaya kiasi kwamba hali ya vifo itaongezeka wakati wowote na majeruhi wapo hospitalini kwetu” “Duu poleni.Haya mwaya Dokta n…