
SEHEMU YA KUMI NA NNE
ILIPOISHIA...
Nikastuka kusikia mama akizungumza kitu kama hicho huku akiwa analia kwa uchungu na kunifanya na mimi kujawa na hisia za huzuni na taratibu machozi yakaanza kunitoka,Kutokana na hali yangu ya kuumwa sio nzuri sana ikanilazimu kukaa katika ngazi ya juu huku nikiwa nimeuegemea ukuta na kuendelea kuwasikiliza mama na daktariNIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU
SASA ENDELEA...
“Muheshimiwa unataka kuniambia huyu kijana si mtoto wa mzee?”
Kabla daktari hajajibiwa swali lake na mama simu yake ikaita,akaitoa na kupokea na kumfanya mama akae kimya
“Ajali ya basi gani?’
“Majeruhi 34?’
“Ninakuja ninakuja sasa hivi”
“Dokta ni ajali ya basi gani?”
“Basi la Msulwa Express limegongana na roli la mbao maeneo ya maili moja”
“Eheee wamekufa watu wangapi?”
“Watano ila majeruhi nao wana hali mbaya kiasi kwamba hali ya vifo itaongezeka wakati wowote na majeruhi wapo hospitalini kwetu”
“Duu poleni.Haya mwaya Dokta nikuache ukatumikie majukumu yako”
“Sawa muheshimiwa hali ya mgojwa wangu itakavyo endelea utanijulisha”
“Sawa nahisi atakuwa amelala”
“Haya kama atakuwa bado yupo macho utamuambia mimi nimesha ondoka”
“Hakuna shaka juu ya hilo”
Nikasikia mlango wa kuingila sebleni ukifunguliwa na kufungwa nikajua moja kwa moja dokta atakuwa ameondoka.Mama akanza kupandisha ngazi akaanza kupata wasi wasi baada ya kuniona nimekaa katika ngazi huku machozi yakinimwagika
“Eheee mgonjwa bado hujalala na unalia nini mwanangu?”
“Mom who is my father?”(Mama baba yabgu ni nani?)”
Mama akabaki kimya huku akinitazama akionekana kuto kulitarajia swali kama hilo nililo muuliza.Akapanda ngazi na kukaa ngazi niliyo kaa mimi
“Eddy my son i will tell you tomorrow now your supporse to relax”(Eddy mwanangu nitakuambia kesho sasa hivi unatakiwa upumzike)
“Momy i can’t relax because i don’t know who is my real blood father”(Mama siwezi kupumzika kwasababu simjui baba yangu wa damu)
Nilizungumza kwa hasira huku machozi yakinimwagika na kumfanya mama aniegemeze kichwa changu kwenye bega huku akinibembeleza
“Eddy my son do you love me?”(Eddy mwanangu unanipenda mimi?)
“I love you mother but i need know the truth”(Nakupenda mama ila nahitaji kujua ukweli)
“Ok my son am happy to hear that you love me.I need you to listen me very carefull”(Sawa mwanangu ninafuraha kusikia kuwa una nipenda.Nahitaji unisikilize vizuri kwa umakini)
“Ok mom am listen up”(Sawa mama nina kusikiliza)
“Now is night give me a chance to go and prepair my some of the office work and tomorrow after i came back i will give you good explaination and i will tell you who is your real father”(Mwanagu sasa hivi ni usiku,nipe nafasi ya kwenda kuandaa baadhi ya kazi za ofisini kwangu na kesho nitakapo rudi nitakupa maelezo mazuri na nitakuambia nani ni baba yako)
Mama alizungumza huku akinifuta machozi kwa kutumia kiganja chake na kunifanya nizidi kulia kwa uchungu
“Mama sitaki tena nimesema sitaki nahitaji kumjua baba yangu ni nani kwa jinsi ninavyo ona hauto shindwa kusema mimi sio mwanao wa kumzaa”
Nilizidi kuzungumza kwa hasira iliyo changanyikana na uchumgu na nikaanza kujihisi upweke ambao nikaanza kuufananisha na mtoto aliye kosa wazazi wote awili
“Eddy what are you say?”(Eddy unasemaje?)
“Yeah you can tell me that your not my mother”(Ndio unaweza ukanimbia kuwa wewe sio mama yangu)
Nlizungumza kwa hasira nikastukia kofi likitua shavuni mwangu kutoka kwa mama na kumfanya anyanyuke kwa hasira na kuelekea chumbani kwake na akaubamiza kwa mguvu mlango wa chumbani kwake.Nikamfwata na kumkuta akiwa amelala gubi gubi kitandani kwake huku akiwa analia taratibu nikakaa kitandani na kumgusa mgongoni
“Momy am sory i d…”(Mama samahani si……)
“Eddy leave me alone now”(Eddy ondoka na uniache peke yangu sasa hivi)
“Mom am sory i din’t mean to say that words”(Mama samahani sikuwa na maana ya kusema maneno yale)
“Eddy do you whant me to die?”(Eddy unahitaji mimi nife?)
“No mamy”(Hapana mama)
“Your father comfused me and you too so if you need me to die kill me now”(Baba yako ananichanganya na wewe pia.Sasa kama unataka mimi nife niue sasa hivi)
Mama alizungumza kwa hasira huku akiuchukua mkono wangu mmoja na kuuweka kwenye koo lake ili nimkabe afe nikajikuta nikiogopa na mwili mzima ukianza kutetemeka kwani sikuwahi kumuona mama katika hali ya hasira kiasi kwamba anataka mimi nimuue
Machozi yakaanza kunitiririka kwa wingi huku moyo wangu ukijawa na maumivu ni kwanini nilizungumza kitu kama kile,nikautoa mkono wangu koo ni mwa mama na kumkumbati na kukiweka kachwa chake begabi mwangu na kuanza kumbembeleza taratibu.
“Eddy mwangu kwa nini unataka kuwa kama huyu baba yako?”
“Mama ninakuomba unisamehe sio kusudio langu kuzungumza hivyo”
Nikaendelea kumbembeleza mama taratibu hadi akanyamaza na taratibu usingizi ukaanza kumpitia baada ya muda kidogo akalala,Nikachukua shuka lake na kumfunika vizuri kisha nikatoka ndani ya chumba chake huku nikizima ta ya chumbani kwake na kushuka gorofani na kukaa kwenye sofa huku maneno ya mama akiwa anazungumza na dokta yakaaza kunirudia taratibu katika akili yangu huku yakiwa yanapita kama kanda wa video aina ya VHS.Kitu kinacho niumiza kichwa sana ni nani baba yangu na kitu kingine watu wengi wanasema ninafanana sana na baba yangu
“Au mama atakuwa amechoka ndio maana akazungumza hivi?.........ila hata kama ni kuchoka itakuwaje akamwambia daktari mtu asiye husika katika familia yetu?”
Nikaendelea kujiuliza maswali yasiyo na majibu kiasi ya kujikuta taratibu nikiaanza kupitiwa na usingizi na kujikuta nikilala kwenye kochi.Nikaanza kuisikia sauti ya mama kwa mbali ikiniita taratibu huku akionekana akiomba msaada,Nikayafumbua macho yangu na kuuta mlango wa kuingilia hapa sebleni nikatazama nje na kukuta bado kuna giza jingi.Nikanyanyuka kwa haraka na kwenda chumbani kwa mama nikakuta mlango wake ukiwa wazi nikaingia na kukuta kuna mwanaume yupo juu yake akimkaba huku kichwani kwake akiwa amevaa maski(Kinyago).Nikachukua chombo cha dogo kilichowekewa uwa la pambo na kwenda kumpiga nalo la kichwani na akaangukia kwa pembeni baada ya kuniona mimi akachomoka na kukimbia sikumjali zaidi ya kumuangalia mama kama yupo sawa au laa.Mama akanyanyuka huku akiwa anakooa huku akiwa amejishika koo.
“Mama unajisikiaje?”
“Vizuri mwangu fungua hiyo droo yangu ya kabati na unitolee bastola yangu”
Nikafanya hivyo na kuitoa bastola yake kisha mama akanyanyuka kitandani na kuvaa raba zake za kufanyia mazoezi na taratibu tukaanza kutoka ndani kwa umakini wa hali ya juu huku na mimi nikifwata kwa nyuma.Tushuka chini na kutoka nje kabisa ambapo kwa safari hii mlango umefungwa.Tukazunguka nyumba nzima kutazama kama kuna usalama kwa bahati nzuri kuna usalama.Tukaelekea getini ambap hukaa askari ila hatukumkuta na wala hapakuwa na kitu chochote kinacho ashiria kuna tatizo lililo tokea katika eneo hilo
“Eddy kimbia kaniletee simu yangu ndani”
Nikaaza kujikongoja kongoja huku nikipiga hatua za haraka nikaamini kuwa mama amesahau kuwa mimi ni mgonjwa.Nikapanda ngazi kwa mwendo wa haraka kidogokitendo cha kushika kitasa cha mlango wa kuingilia chumbani kwa mama nikasikia milio mitatu ya risasi ikitokea nje.Nikabaki nikiwa nimesimama huku miguu yote ikiwa inaaza kuishiwa na nguvu kuingia ndan kuchukua simu ya mamai nikawa ninataka kutoka nje nikawa ninataka.Nikaaona hakuna haja ya kuingia ndani kuchukua simu moja kwa moja nikakimbilia jikoni na kuanza kukitafuta kisu ila sikkukiona zaidi ya kuona Umma wa kulia chipsi,nikiona unanitosha kwends kupambana na kito chochote bitakacho kutana nacho nje
Nikafungua mlango na kujikuta mapigo ya moyo yakianza kumienda mbio huku wasiwasi ukiinza kuukamata mwili wangu kwani katika sehemu nilipo muacha mama sikumuona,Nikajikuta ninaaza kupata kiwewe cha miguu kila nikijaribu kusogea mbele ninajikuta ninasheindwa sasa sikujua ni woga ndio unachania kwani sikujua ni wapi mama yupo.Nikiwa bado nimesimama nikasikia mlio mwengine wa risasi ukitokea nje ya geti kwa mstuko nusu nijikojolee kwani sikujua huo mlio ni nani aliye pigwa nao kwani kipindi nipo mdogo mara kwa mara baba alikuwa akinifundisha jinsi ya kutambua milio ya risasi pale inapokuwa imempiga mtu au kumkosa na moja kwa moja mlio nilio usikia nikajua moja kwa moja risasi iliyo lia imetua kwenye mwili wa mwanadamu
Nikajikaza kiume na kuunza kupiga hatua za kwenda nje ila kwa umakini huku uma wangu nikiwa nimeushika kwa umakini wa hali ya juu huku nikiwa makini kwa chochote kutacho jitokeza huku mwili mzima jasho lilinimwagika.Nikafungua geti dogo taratibu huku nikiwa nimetanguliza kichwa,Nikamkuta mama akiwa amesimama na askari kama watano wakiwa na bunduki zao mikonini huku kukiwa na mtu mmoja akiwa amelala chini huku mwili wake ukiwa unavuja damu nyingi.Nilicho kikumbuka kwa haraka haraka ni nguo alizo zivaa mtuu huyo na kukumbuka ni yule mtu niliye mpiga na bakuli la dongo lililo kuwa na uwa la pambo.
“Alafu bado kijana mdogo sana”
“Ndio huyu nahisi ametuwa na mtu wa humo ndani kwako kwa maana haiwezekani ajiamini kiasi kwamba ya kujua moja kwa moja chumani kwako”
“Hilo usemalo litakuwa na ukweli ndani yake”
Mama akaendelea kujadiliana na askari wanaolinda eneo tunalo ishi akiwemmo na askari wetu huku mama akimshushia lawama askari wetu ni kwa namna gani mtu anaingia ndani pasipo yeye kufahamu,askari wengine wakaja na gari lazo na kuchukua maiti huku wakimchukua askari wa getini kweyu kwenda kumuhoji maswali
***
Mama akamfungulia kesi ya mauaji Manka huku lengo lake kubwa ni Manka kwenda kufungwa kifungo cha maisha,Siku ya kesi kusikilizwa ikawadai huku mahakamani kukiudhuriwa na watu wachache baadhi yao wakiwemo ndugu wa upande wa Manka akiwemo dada yake na pamoja na mwalimu Mayange.Tangu tukiwa nyumbani mama niweze kuzungumza kitu kitakacho muhukumu Manka.Ila moyoni mwangu nikaanza kuhofia endapo atasema tulifanya mapenzi itakuwa aibu kwangu na mama yangu.Watu wakiwa wanaaza kuingi ndani ya chumba cha mahakama mimi nilikaa nje huku nikimdanganya mama kuwa kuna mtu nina mpigia simu na muda si mwingi nitaingia ndani.Alipo ingia nikaelekea katika sehemu yenye mtuhumiwa na kawaonga kila askari elfu hamsini na walikuwa wanne ili wanipe nafasi ya kuzungumza Manka ambaye kwa wakati wote sura yake ilijaa machozi na huzuni hadi na mimi nikajikuta nikiwa na huzuni moyoni mwangu
“Eddy nakuomba unisaidie katika kesi hii wewe ndio kiongozi wangu wewe ndio unaweza kuzizima ndoto zangu katika maisha yangu……..Eddy sikukusudia kukuua na wala sikuwa na lengo baya la kukudhuru yote yalitokea kwa sababu ninakupenda Eddy na sikujua ni jinsi gani ya kukushawishi ili unipende nilidhani utanichezea na kuniacha”
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI
KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger
Email: ZephilineEzekiel@Gmail.Com