SORRY MADAM (18)
JINA: SORRY MADAM Mwandishi: Eddazaria G Msulwa SEHEMU YA KUMI NA NANE ILIPOISHIA... “Nyamaza wewe subirini hukumu yenu ya kunyongwa” “Afande hadi sisi!?” Nilimuuliza askari kwa mshangao na kuyafanya machozi yaanze kunimwagika “Tena nyinyi ndio mutakuwa wa kwanza na hiyo minjemba mine itafwatia” NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU SASA ENDELEA... “Acha kumrusha roho dogo wewe hembu tutolee hiyo sura yako kama kisigino chenye magaga” Jijamaa linguine likamjia juu askari japo amembeza askari kuwa ana sura mbaya ila sura ya jamaa imezidi kwa ubaya kwani imechanwa chanwa kiasi kwamba imekuwa kama mistari ya mipaka kwenye ramani ya Dunia.Askari akaondoka huku akicheka,akili yangu ikaanza kumkumbuka Manka na sikujua kama yupo hai au amekufa na kujikuta nikizidi kutokwa na machozi ya uchungu na nikaanza kumuomba Mungu atende muujiza ili aweze kuyaokoa maisha ya Manka.Mida ya saa tatu asubuhi akaja askari mmoja na kutuita mimi na dereva na kabla sijatoka nikawaaga mijamaa kisha tu…