SORRY MADAM (18)

0
SEHEMU YA KUMI NA NANE
ILIPOISHIA...
“Nyamaza wewe subirini hukumu yenu ya kunyongwa”
“Afande hadi sisi!?”
Nilimuuliza askari kwa mshangao na kuyafanya machozi yaanze kunimwagika
“Tena nyinyi ndio mutakuwa wa kwanza na hiyo minjemba mine itafwatia”

NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU

SASA ENDELEA...
“Acha kumrusha roho dogo wewe hembu tutolee hiyo sura yako kama kisigino chenye magaga”
Jijamaa linguine likamjia juu askari japo amembeza askari kuwa ana sura mbaya ila sura ya jamaa imezidi kwa ubaya kwani imechanwa chanwa kiasi kwamba imekuwa kama mistari ya mipaka kwenye ramani ya Dunia.Askari akaondoka huku akicheka,akili yangu ikaanza kumkumbuka Manka na sikujua kama yupo hai au amekufa na kujikuta nikizidi kutokwa na machozi ya uchungu na nikaanza kumuomba Mungu atende muujiza ili aweze kuyaokoa maisha ya Manka.Mida ya saa tatu asubuhi akaja askari mmoja na kutuita mimi na dereva na kabla sijatoka nikawaaga mijamaa kisha tukamfwata askari na kuingia kwenye ofisi ya mkuu wa polisi wa wilaya na kumkuta mama akiwa amekaa kwenye kiti huku amekasirika kiasi kwamba hata sikuweza kumsalimia

“ Na wewe hapo kichwani umechanika na nini?”
“Shikamoo mama”
“Marahaba ehee ninakuuliza apo umechanwa na nini hapo kwenye paji la uso?”
“Kuna askari jana alinipiga kichwa na ngumi za kifuani”
“Kijana unaweza kuniambia huyu askari yupo vipi?”
“Mrefu hizi mweusi anaitwa Sele”
“Ahaa ok ngoja”

Mkuu wa polisi akanyanyua mkonga wa simu ya mezani kisha akaiweka sikioni na kuanza kuzungumza na mtu wa upande wa pili wa simu
“Nakuhitaji ofisini kwangu haraka”
“Ehee na nyinyi hembu nielezeni imekuaje kuaje hadi mukawa hapa?”
Mama alituuliza na dereva akaanza kuzungumza huku akijing’ata ng’ata na anavyo onekana anamuogopa sana mama.Ikanilazimu nianze kumuelezea mama kila kitu kilicho tukuta ila sikutaka kumumbia majeruhi niliye muokoa ni Manka.Yule askari aliye nipiga jana usiku akaingia ofisini kwa bosi wake na kumpigia saluti na akaonekana kustuka kumuona mama akiwa ofisini humo

“Wewe ndio uliye mjeruhi mwanangu kiasi hichi?”
“Muheshimiwa mwanao ni mkorofi tena sana na anamaneno machafu sana”
“Kwahito ndio ummpige kiasi kwamba amechanika hapo usoni,wewe unajua ni jinsi gani nilivyo pata naye tabu huyu mtoto hadi kufikia hatua hiyo aliyo kuwa nayo?”
“Hapana mama yangu ila ukitaka kuhakikisha mwanao ni jeuri jana nilirekodi kila kitu alichokuwa akinijibisha na mimi”

Afande Sele akatoa simu yake kisha akaweka sehemu sauti zetu tulizo kuwa tuna jibishana jana usiku kuanzia tulipokuwa barabarani hadi tulipofika kituoni.Mama akaachia msunyo mkali huku akinitazama kwa macho makali kiasi kwamba nikajikuta ninaanza kuogopa
“Haya afande asante na samahani kwa kukusumbua……Afande Methew huyu kijana wangu niachie mimi nitamnyoosha tuu tembo hawezi kushindwa na mkonga wake”
“Sawa muheshimiwa waziri nimestuka san akukuona huku kwetu asubuhi asubuhi”
“Aaaa wee acha tuu ni kwaajili ya huyu mjinga mmoja hapa.Haya kachukueni kila kitu chenu na niwakute kwenye gari”

Tukatoka na dereva na kup
fitia mapokezi na kukabithiwa kila kitu kilicho chetu kisha tukaenda kwenye gari la mama ambalo ni gari la kazini kwake.Baada ya muda mama akatoka huku akiwa ameongozana na yule asjari aliye nipiga huku wakiwa wanazungumza kama marafiki kisha wakapeana mikono na kutufwata sisi tulipo na safari ikaanza huku akiendesha dereva wa kazini kwake

“Eddy hicho kinywa chako kichafu umekianza lini na nani aliye kufundisha matusi?”
“Hakuna mama”
“Kwa hiyo siku hizi wewe umekuwa hadi unawatukana askari wa watu si ndio?”
“Mama wao walipo anza kukutukana wewe ndi…..”
“Ndio na wewe ukaamua kuwatukana….Unajua Eddy sishindwi kukuweka ndani hadi hicho kichwa chako kikae sawa…Unaljua hilo?”
“Likini mama wao ndio chanzo mimi nilikuwa ninarudi kuchukua sijui PF nini huku ili nikamtibu majeruhi tuliye muokoa sasa wao ndio wakaaanza chockochoko hadi wakanilaza ndani”
“Na wewe Hamisi kwa nini ulimuachia huyu mwehu aendeshe gari kazi imekushinda?”
“Hapana mama nakuomba unisamehe”

“Sasa ni hivi itabidi ukanionyeshe huyo majeruhi wanu aliye wachanganya hadi mukajikuta munafanya vitu vya ajabu”
“Mama si wewe uendee tuu”
“Niende wapi?”
“Dar”
“Tena tukitoka kwenda kumtazama huyo mgonjwa wenu sote tunarudi Dar ukanieleze huo utumbo wako ulio ufanya”
“Sawa je na gari tulilo kamatwa nalo lipo wapi?”
“Limesha pelekwa nyumbaini”
“Na nani?”
“Eheee usinihoji hoji maswali yako ya kijinga sawa?”
“Sasa mama hilo ni swali la kijinga?”
“Eddy mwanangu hembu niache kichwa changu kitulie”

Kila tulivyo zidi kuifika Zahanati tuliyo mpeleka Manka jana usiku moyo wangu ukaawa unapoteza amaini kisi kwamba nikaanza kuhisi hali yahatari kichwani mwangu.Tukafika kwenye Zahanati na madaktari walipo muona mama wakaanza kuhaha kwani wanadhani amekuja kwa ajili ya kuwakagua.Mtu wa kwanza kukutana naye ni mganga(daktari) mkuu wa Zahanati hiyo
“Huo ndio utaratibu wenu wa kazi?”
Mama alizungumza huku akimshika shati huku likiwa limejikunja kunja kama limetafunwa na ngombe kisha likatwemwa

“Ha….haapa muheshimiwa”
“Na koti la kazi lipo wapi?”
“MMmmm lilipo ofisini?”
“Sasa hivi saa ngapi na muda wa kuripoti kazini ni saa ngapi?”
Daktari akaanza kubabaika babaika huku akijikuna kuna nywele zake zilizokosa kupitiwa na kitana kwani zimejinyongorota kiasi kwamba ni shida tupu

“Daktari mzima huna hata saa ya mkononi,pili haupo smart kimavazi unazani huyo mgojwa ukikuona wewe si ugonjwa wake unaweza kuongezeka kutokanan na uchafu wako,tatu unaonekana ndio unatoka kuamka mida hii na bado unanuka pombe kiasi kwamba unatia kinyaa.Sijui hata huo udaktari umeupataje”
“Hapana muheshimiwa”
“SNikimaliza unione”

Mama akamuacha daktari na kuafwata wananchi walio kaa kwa wingi kwenye foleni isiyo sogee kiasi kwamba wagojwa wamechoka sana. na foleni hiyoAkawasalimia wananchi na wakamuitikia kwa furaha kisha akaanza kuwahoji mwaswali,nikapata upenyo wa kwenda katika chumba alicho ingizwa Manka jana usiku na nikajikuta wasi wasi wangu ukizidi kuongezeka hii ni baada ya kumkuta Manka hayupo ndani ya chumba hicho

Nikabaki nimesimama huku sielewi ni kitu gani nifanye nikageuka kiunyonge na kukutana na daktari tuliyemkuta jana usiku akiwa anatembea mwendo wa kasi sikujua ni wapi anapoelekea ikanibidi nimsimamishe
“Daktari vipi”
“Salama mdogo wangu nakomba tuzungumze baadaye mimi ngoja niondoke hali imeshakuwa mbaya”
“Sijakuelewa dokta?”
“Kuna waziri wa afya amekuja hapa tayari dokta mkuu ameshapigwa chini wewe nakuomba tuondoke kama vipi njoo tuzungumze nyuma huku”

Nikatoka huku nikicheka kimoyo moyo na kusema laity anegejua huyo mtu anaye mkimbia ni mama yangu wala asinge zungumza na mimi
“Ehee kijana shida yako ni nini?”
“Dokta jana nilileta mgojwa hapa mida wa usiku alipatwa na….”
“Ohooo nimekumbuka huyo mgonjwa wako tumemsafirisha kuelekea katika hospitali ya K.C.M.C”
“Hali yake ikoje?”
“Si nzuri sanaa na kama tungembakisha hapa angetufia bure…..Kijana hembu nakuomba uniache niende kwani huyo mama namuona anakuja huku”

Dokta alizungumza huku akichungulia chungulia kupitia mlango tulio tokea nje huku akianza kupiga hatua za haraka kuelekea kwenye njia ya kichochoro iliyopo karibu na Zahanati hiyo.Nikarudi ndani huku nikiwa nawaza ni nini nifanye ili mama aweze kunielewa kama ni kuenda shule niende siku hiyo hiyo.Mama akamaliza kuzungumza na madaktari pamoja na manesi alio wakuta

“Ehee wee huyo mgonjwa wako yupo wapi?”
“Wamesema wamemuamisha hospitali”
“Nani kasema?”
“Waulize hao madokta hapo”
“Eti kuna mgonjwa aliletwa jana amepata ajali?”
“Ndio muheshimiwa”
“Ahaa bahati yako haya jamani tekelezeni yale niliyo waambia ni bora mupoteze kazi nyinyi kuliko kupoteza nguvu kazi ya taifa kwa vifo vinavyo sababishwa na uzembe wenu na kuanzia sas hivi Kiongozi mkuu atakuwa huyo hapo bwana nani vile?”
“Bwana John Henry”
“Ok bwana John ndio atakuwa kiongozi wenu kwa muda hadi pale wizara itakapo leta mtu daktari mwengine sawa jamani”

Madaktari na Manesi wakamuitikia mama kisha akaagana nao pamoja na wananchi kisha tukaingia ndani ya gari na safari ya kurudi nyumbani ikaanza.Tukafika nyumbani mida ya saa saa nane mchana.Wakanishusha getini kisha mama akaelekea kwenye mishuhuliko yake.Mida ya jioni mama akarudi huku akionekana amechoka nikamsalimia na moja kwa moja akaenda chumbani kwake na kulala.Nikakaa nyumbani kwa siku mbili na bila ya kuzungumza na mama kuhusiana na swala la kurudi shule

“Eddy shule unakwenda lini?”
Mama aliniuliza baada ya kupita mbele yake nikitokea nje huku yeye akiwa amekaa sebleni akitazama taarifa ya habari ya saa mbili usiku
“Mama nakusikilizia wewe?”
“Unanisikilizia mimi hivi una akili kweli mwanangu?”
“Sasa mama kuzungumza hivyo ndio mimi sina akili?”
“Nakuona bado una akili za kitoto.Sasa anaye soma ni mimi au wewe?”
“Ila kumbuka mama wewe ndio uliye niruduisha nyumbani”
“Nilikurudisha iliakili yako ikae sawa.Na sijui hiyo PCB yako unaisoma vipi?”
“Mama mimi Genius”
“Mmmm genius uwe wewe,kesho shule na uondoke na gari ya kwanza uwahi kufaika shuleni?”
“Mama siwezi kusafiri ijumaa”
“Pumbavu wewe usiniletee ujinga nimekuambia kesho alfajiri nikitoka kwenda kazini ninakuacha ubungo sawa”
“Ila mama hizi safari zako za kustukiza huwa sizipendi kama nini”
“Upende usipende kesho shule”

Kama alivyozungumza mama safari ya kurudi shule ikaanza na akaniacha stendi ya mabasi ya Ubungo mida ya saa kumi na moja asubuhi kisha yeye akaelekea ofisini kwake sikujua ni kwanini siku hiyo amewahi sana kwenda ofisini.Nlicho kifanya ni kutafuta nyumba ya wageni(gest house) iliyo karibu na stendi kwa bahati nzuri nikapanda chumba nikaingia na kulala hadi mida ya saa tatu asubuhi kisha nikarudi stendi na safari ikaanza kwa kutumia basi Dar Express na katika siti niliyo kaa nipembeni yangu kuna msichana amavalia baibui ninja na ningumu kuweza kuiona sura yake.Hatukusemeshana chochote kiasi kwamba safari nzima kila mtu akawa kimya,kwa bahati mbaya tukakuta ajali ya roli mbili zimegongana maeneo ya Wami kiasi kwamba ikatuchukua muda mrefu kukaa barabarani tukisubiria gari hizo kuja kuondolewa kutokana zimeifunga barabara na hapakuwa na uwezekano wa magari kupita

“Aisee hii ajali inatuchelewesha”
Msichana niliye kaa naye alizungumza na kunifanya nimtazame kwa muda kisha nikamjibu
“Wee acha tuu yaani nilisaa la tatu tumekaa hapa na hiyo foleni hapa hadi tuimalieze ni shughuli”
“Ndio tatizo la nchi yetu kukitokea jambo kama hili basi wahusika wataanza kujivuta vuta usishangae hapa tunakaa zaidi ya masaa kumi”
“Kweli na hapa mtu huwezi kusema utahairisha safari kwani nyuma yetu kuna foleni mbele huko ndio usiseme”

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI

KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)