SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU
ILIPOISHIA...
Nikaifungua kamba iliyo nielekeza Sheila na kusababisha turubai lililo funika gari lake kufunguka na macho yangu yakakutana na gari aina BMW ambayo tangu niijue Tanzania na kutembea kwangu sikuwahi kuiona MBW ya muundo huuNIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU
SASA ENDELEA...
“Duuuu hii ngoma bei gani?”
“Jamaa wameniambia ni laki mbili na nusu za kimarekani”
“Kudadadeki ni kama Milioni 400 za Kitanzania”
“Ndio maana yake”
“Funguo yake iko wapi?”
“Unataka twende nalo?”
“Ndio”
“Eddy hatuta kamatwa na polisi?”
“Si imesajiliwa kila kitu?”
“Ndio”
“Basi kalete funguo yake”
“Ipo hapo hapo kwa juu kwenye vidude vya kuzuia jua”
Nikafungua sehemu aliyo nielekeza Sheila na kukuta funguo ikining’inia na haraka haraka nikaichomeka kwenye sehemu yake na kuizungusha funguo yake kama ninavyo washa magari ya kawaida ila cha kushangaza gari halikuwaka
“Mbona haliwaki sasa?”
“Kwani ni lako hadi liwake?”
“Ehee hembu njoo unielekeze bwana linawashwa washwa vipi?”
“Eddy mpenzi wangu kama kuwasha unashindwa je kuendesha utaweza kweli?”
“Wewe njoo unionyeshe linawashwa washwa vipi”
Sheila akazunguka upande wa pili na kukaa siti ya pembeni kisha akaminya kitufe chekundu kilichopo pembeni yangu kilicho andikwa ‘VOICE’ kisha akanitazama usoni na kuachia tabasamu
“BMW 007 START”
Nikastuka gari likiwaka na kila kitu kikaanza kusoma kwenye dashboard yake na kujikuta nikibaki ninashangaa
“KARIBU BI.SHEILA KWENYE GARI LAKO BMW 007 JE UNAHITAJI KUELEKEA WAPI TUKUONYESHE RAMANI”
Sauti ya msichana ilisikika kwenye spika za gari hilo na kubaki nikikaa kimya
“Nahitaji kuelekea mkoani Arusha”
“SUBIRI KWA DAKIKA”
Tukasubiri kwa sekunde kadhaa huku nikibaki kimya na kila nilicho kiona machoni mwangu ninakiona kama ni kipya na ramani ikajitokeza kwenye kioo cha ya gari hilo dashboard
“RAMANI YAKO IMEKAMILIKA JE UNAHITAJI HUDUMA NYINGINE”
“Ndio”
“CHAGUA KATI YA HIZI ZIFWATAZO 1.TAZAMA USALAMA WA GARI LAKO, 2.TAZAMA UJAZO WA UPEPO ULIPO KWENYE MATAIRI YAKO, 3.BADILISHA DEREVA 4…….”
“Tatu”
“DEREVA MPYA ATAJE JINA LAKE”
Sheila akanikonyeza na kunifanya nikohoe kidogo huku nikiwa ninafuraha kwani sikuwahi kuona gari kama hilo zaidi kuona gari linalo endana na hilo kwenye filamu za JAMES BOND
“EDDY GODWIN”
“KARIBU BWANA BWANA EDDY GODWIN KWENYE BMW 007 WEKA KIDOLE GUMBA CHA MKONO WA KUSHOTO KATIKATI YA KIENDESHEO CHA GARI”
Nikaweka dole gumba katikati ya mskani ambapo kuna kioo kidogo na mstari mwekundu ukaanza kupita kwenye kidole changu kuanzia chini hadi juu
“UMEFANIKIWA KUWA DEREVA WA BMW 007 NAWATAKIA SAFARI NJEMA NA UENDESHAJI MWEMA”
Sauti ikakata na gari ikaaendelea kunguruma taratibu ikisubiria kuanza kwa safari.Kutokana nina uzoefu kidogo kwenye uendeshaji wa magari haikuwa ngumu.Nikakanyaga taratibu mafuta na gari likaanza kusogea kwenda mbele,nikalitoa kwenye chumba hicho na kulisimamisha pembeni na Sheila akashuka na kuminya rimoti yake na kila kitu kikajifunga na akairudisha ndani na kufunga milango yake kisha akafungua geti la mbele na nikalitoa gari nje na kumsubiria Sheila akimalizia kufunga geti lake na kuingia ndani ya gari
Mwanga wa jua bado haukuwa umeanza kuchomoza ikanilazimu kuwasha taa za gari ambazo zina mwanga mkubwa kupita maelezo.Nikaingia kwenye batabara kuu ya mikoani huku ramani ikinionyesha wapi nielekee.
“Hivi hii gari ina spidi ngapi?”
“380 na ina Turbo”
Ilinibidi nimuulize Sheila kutokana hakuna mishale inayoonyesha mwendo kasi zaidi ya kiio tu kinacho onyesha mfumo mzima wa spidi zinavyo ongezeka kama saa ya kawaida
“Mmmm tumuobe Mungu”
“Kweli mume wangu safari ni ndefu”
Nikaendelea kukanyaga mafuta huku moyoni mwangu nikiwa ninafuraha kuendesha gari kama hili ambalo nahisi ni watu wachache sana walilo nalo Tanzania au hakuna kabisa.Safari ikazidi kwenda mbele huku mara kwa mara nikijipima uwezo wa uendeshaji wa gari kwa mwendo wa kasi kiasi kwamba Sheila akaanza kuniomba nipungunze mwendo.
“Tulia mimi ndio dereva hatuwezi kupata ajali apa najitahidi niifike Segera mapema”
“Eddy lakini muda si upo?”
“Ndio ila najitahi pia kuepukana na trafki”
“Haya dereva”
Safari ikazidi kusonga mbele huku magari madogo na mabasi makubwa nikiyapita japo yapo kwa mwendo wa kasi ila niliyapoteza sana.Hadi ninafika Korogwe tayari ni saa moja na dakika zake na tukaingia kwenye Hotel ya High Way kupata chakula kwani kwa shuguli tuliyo ifanya muda mchache uliopita ni pevu kupita maelezo.Tukaagiza kifungua kinywa na kuanza kula taratibu huku nikiendelea endelea kumtazama Sheila machoni
“Mbona unanitazama hivyo?”
“Ninakuangalia jinsi ulivyo mzuri mpenzi wangu”
“Mmmm muongo wewe”
“Kweli baby”
“Asante kama ni kweli”
“Shei umeliona hilo basi linalo ingia?”
“Ndio”
“Unakumbuka tulilipita wapi?”
“Si tulilipita Kabuku”
“Sasa hivi ndio linaingia hapa na hili ndio basi la kwanza kuondoka Dar kuelekea Arusha”
“Na lilikuwa lipo kasi”
“Ehee ila ndio hivyo tumelipita”
“Ila wewe uendeshaji wako ni wafujo”
Tukamaliza kula na kulipa tulicho kula kabla hatukatoka jamaa mmoja akanifwata na kunipa mkono huku akicheka
“Kaka hongera sana”
“Kwa nini?”
“Wewe jamaa si ndio ulikuwa unaendesha ile gari pale?”
“Ndio”
“Wewe ni dereva.Yaani mimi nilijitahidi kukanyaga mafuta ili nikupate nakukuta hapa”
“Ahaa ile ngoma pale mziki wake tofauti na hizi gari nyingine”
“Mimi ni dereva wa hilo basi hapo”
“Ahaa kumbe wewe ndio tuliye kupita ukawa unatupigia honi?”
“Ndio kaka….Unaelekea wapi?”
“Arusha”
“Kaka naomba uniachie namba zako tunaweza tukawasiliana kama huta jali”
“Powa”
Nikampa dereva namba yangu ya simu kisha na yeye akanipa namba yake
“Ni save nani?”
“Save RAMA”
“Powa utanisave kwa jina la Eddy”
Nikamkuta Sheila ndani ya gari na safari ikaanza na sehemu isiyo na trafki nikaendesha kwa kasi na tukafanikiwa kufika Arusha mida ya saa sita mchana bila ya kusimamishwa njiani na trafki kwani hapa nilipo sina leseni.Tukachukua chumba kwenye hoteli moja ya kifahari na kumuacha Sheila akienda kwenye mizunguko bila ya kutumia gari yake na mimi nikabaki nikiwa nimelala kwa uchovu nilio upata wa kuendesha gari kwa safari ndefu.Nikaamka saa moja usiku baada ya kusikia simu ikiita na kukuta ni Sheila ndio anaye piga
“Mmm vipi?”
“Safi baby mimi nimesharudi nipo hapa chini hotelini shuka huko gorofani basi tuje kula mpenzi wangu”
“Umeagiza chakula gani?’
“Nakusubiria tuagize pamoja”
“Powa ngoja nivae”
“Ulikuwa bado umelala nini?”
“Ndio”
“Fanya basi uje mumwe wabgu ninakupenda”
“Ninakupenda pia”
Nikakata simu na kunyanyuka kitandani huku mwili ukiwa umechoka kidogo,Nikaingia bafuni na kunawa uso ili kuutoa mikunjano ya usingizi kisha nikavaa shati langu vizuri na kufungua mlango.Moyo ukanipasuka baada ya macho yangu kugongana na macho ya Salome akiwa ameshikwa kiuno na mkuu wa shule wakitoka ndani ya chumba tunacho tazamana huku nao wakionekana kukosa pozi baada ya kuniona
Tukatazamana kwa dakika mbili huku kukiwa hakua anayemsemesha mwezanke na gafla nikamshuhudia Salome akilegea na kuanguka chini na kuzidi kumfanya mkuu wa shule kuweweseka.Nikataka kupiga hatua kwenda kuwafwa ila roho yangu ikasita na kujikuta nikisimama huna nikiitoa simu yangu mfukoni
“Wewe kijana njoo unisaidie kumnyanyua mwenzio”
Sikutaka kumjibu kitu chochote mkuu wa shule kwani taratibu nikajikuta hasira zikianza kunipanda
“We….ewe naniii……Eddy njoo basiiii”
“Wewe mzee una mapepo nahisi…..Starehe mule wenyewe alafu unasema mimi nikusaidie”
“Ahaaa kijana usinifanyie hivyo”
“Mpuuzi nini wewe kumbe ndio kazi yako kuwatorosha wanafunzi na kuja kuwamega huku hotelini?”
“Kijana wangu nakuomba basi…Njoo basi hata tumbebe tumuingize ndani”
Nikapata wazo la haraka nikaingia upande wa kamera kwenye simu yangu aina ya HTC kisha nikaanza kuwapiga picha Salome na mkuu wa shule kitendo kilichozidi kumpagawisha mkuu wa shule
“Wewe si Malaya sasa nautangazia ulimwengu mzima waone kitu ulicho kifanya na huyo mwanafunzi wako”
“Haki ya Mungu wewe mtoto lazima nikufunge”
“Unasemaje wewe boya?”
“Lazima nikufunge”
“Sasa ili unifunge vizuri nampigia simu waziri wa elimu sasa hivi tuone kama nitafungwa mimi au wewe?”
“Acha kunitaisha wewe”
Mkuu wa shule alizungumza huku akimnyanyua Salome na kurudi naye ndani walipo toka na kabla hawajafunga mlango na mimi nikaingia.Mkuu wa shule akamuweka Salome kitandani na kinigeukia mimi huku akicheka
“Unajua kijana mimi ndio nimetangulia kuliona jua kabla yako…..Naomba hiyo simu?”
“SITAKI HUNA HADHI YA KUWA NA SIMU KAMA HII”
Nikazidi kumpiga picha kila hatua anayo ifanya nikaona haitoshi nikaanza kumrekodi video
“Eddy nimekuambia ninaomba hiyo simu”
“Sitaki”
Mkuu wa shule akapiga hatua hadi kwenye kitanda na kukaa akimtazama Salome nikapanda juu ya sofa ili niwarekodi vizuri kwa juu
“Endelea kumchezea chezea nywele”
“Kubabak* wewe mtoto nitakuua”
Mkuu wa shule alizungumza huku machozi yakimlenga lenga na macho yake kuwa maekundu mithili ya mtu alite vuta bangi.Mkuu wa shule akainama kama anafunga kamba za viatu vyake na gafla akanyanyuka huku akiwa ameshika bastola kwenye mkono wake
“Utatoa simu hutoi”
Nikakaa kimya huku tukio la Manka kunishikia bastola likanijia kichwani na kuanza kulifananisha na tukio la mkuu wa shule kunishikia bastola na kuufanya mwili wangu kunitetemeka
“Nakupa sekunde 30 jifikirie unanipa simua au nikifumue kichwa chako”
Mwili ukaendelea kunitetemeka huku mkuu wa shule akionekana hana masihara na kitu anacho kizungumza.Nikamuona Salome akinyanyuka taratibu kitandani huku akijishika shika maeneo ya kichwani mwake.Akabaki ameshangangaa kumuona mkuu wa shule akiwa ameshika mbastola huku akiwa amempa mgongo.Nikamkonyeza Salome na kwa haraka akamsukuma kwa nyuma mkuu wa shule na akaangukia kwenye meza ya kiio hadi ikavunjika na bastola yake ikaangukia mbali. Nikamshika mkono Salome na kumyanyua kitandani kabla hatujatoka Salome akarudi alipo angukia mkuu wa shule anaye lia lia kwa maumivu aliyo yapata
Salome akaanza kumpiga mateke ya kwenye makalio mkuu wa shule huku akionekana kuwa na hasira
“PUMBAVU WEE……SHENZII……MTU MZIMA HUNA HAYA MALAYA MKUBWA WEWE….”
“Salome twende bwana”
“Huyu mzee mshenzi”
“Sawa tutazungumza mbeleni”
Nikamshika mkono Salome na tukafungua mlango na kutoka njee kitendo cha kupiga hatua mbili mbeleni huku nikiwa nimemshika mkono Salome nikakutana na Sheila akiwa yupo kwenye mwendo wa haraka akija sehemu tunayo tokea. Sheila akasimama kwa muda akionekana akishangaa na akaanza kupiga hatua za kuja sehemu nilipo huku akionekana kupandwa na hasira.Cha kwanza alicho kifanya Sheila ni kutuachanisha mikono mimi na Salome kisha akamgeukia Salome
“Malaya wa kiarusha kumbe wewe ndio unachukua mabwana za watu si ndio”
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI
KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger
Email: ZephilineEzekiel@Gmail.Com