SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE
ILIPOISHIA...
Sheila akasimama kwa muda akionekana akishangaa na akaanza kupiga hatua za kuja sehemu nilipo huku akionekana kupandwa na hasira.Cha kwanza alicho kifanya Sheila ni kutuachanisha mikono mimi na Salome kisha akamgeukia Salome
“Malaya wa kiarusha kumbe wewe ndio unachukua mabwana za watu si ndio”
NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU
SASA ENDELEA...
“Sheila ninakuomba unisikilize”
“Weee Eddy nyamaza huwezi ukaniweka nje kule mimi kama roboti kumbe upo na Malaya zako huku”
Sheila akamshika Salome nywela na kuanza kumtingisha tingisha huku akipiga makofi na ikanilazimu kumshika Sheila kwa nyuma na kumuachanisha kutoka mikononi mwa Salome ambaye kwa kiwewe akaanguka chini.Tukiwa tunageuka ili nimpeleke Sheila katika chumba tulicho fikia gafla mlio wa bunduki ukasikika na huku macho yangu yakikukutana na macho ya mkuu wa shule akiwa ameishika bastola yake huku ametuelekezea sisi.Nikaanza kuhisi maji ya moto yakiaanza kuvichoma viganja vyangu na taratibu nikanza kwenda chini baadaya ya mwili wa Sheila kuniegemea na kunizidi uzito
Hadi ninakaa sakafuni nikaona damu nyingi zikimwagika kifuani mwa Sheila huku akitetemeka kwa woga
“Eddy ninakufa mume wangu”
“Huwezi kufa baby”
Nlizungumza huku nikimziba kwa nguvu Sheila kwenye jeraha lake na nikaamshuhudia mkuu wa shule akianza kukimbia akipita katikati yetu.Nikanyanyuka kwa haraka huku mikono ikiwa na damu nyingi na kuanza kumkimbiza,kabla sijamfikia askari wawili wenye bunduki wakatokea mbele yetu na kutuomba tusimame.Nikasimama huku nikitazama nyuma na kumuona Salome na watu wengine wakitoka kwenye vyumba vingine wakimuhudumua Sheila aliye lala chini.Mkuu wa shule akanyanyua mikono juu huku akiwa ameishika bastola yake
“Hilo ndio jijambazi lililo mpiga risasi mke wangu”
Askari wakanisikiliza na kumfunga pingu mkuu wa shule na mimi nikarudi kwenye kundi la watu walio mzunguka Sheila.Tukasaidiana na watu wengine na tukashuka chini kwa bahati nzuri hoteli hiyo ina gari la wagonjwa aina ya Landcruzer za zamani zenye mkonga mweusi.
“Salome nenda nao mimi ninakuja na gari kwa nyuma”
Salome akaingia kwenye gari pamoja na meneja wa hoteli kisha mimi nikaelekea kwenye maegesho ya magari na kuingia kwenye gari letu tlilo kuja nalo.Nikaingiza funguo na kuminya batani nyekundu kama alivyo fanya Sheila asubuhi kilicho andikwa ‘VOICE’
“BMW 007 START”
Gari halikuwaka nikarudia kuzungumza tena kama mara nne halikuwaka nikujikuta nikilipiga piga kwenye mskani kwa hasira huku nikitukana na kuwafanya watu walio karibu nami kunisogelea huku wakiwa wananishangaa.Nikafungua mlango kwa hasira na kuufunga na kukuta watu wakiongezeka huku kukiwa na jamaa mmoja akinipiga piga picha kwa kamera na anaonekana ni mwandishi wa habari kutokana na kitambulisho alicho kivaa dhinoni na kuning’inia kwenye kifua chake.Nikamsogelea mtu anaye nipiga picha na kumpokonya kamera yake na kuitupa chini na kuaanza kuikanyaga kanyaga na kusabiabisa mtafaruku mkubwa huku jamaa akionekana kupandwa na hasira akitaka kunipiga ila watu wakawa wanamzuia wengine wakimlaumu kwa umbea wake anao ufnya
“Mimk muandishi wa habari hawezi kunivunjia kamera yangu”
“Na wewe ni mbea imekuaje kupiga piga watu wa watu usio wajua”
“Haykuhusu na wewe”
“Sio hayanhusu ingekuwa mimi ni huyo chalii hapo ningekutia vitasa vya kutosha”
“Jaribu”
Vurugu zikaongezeka na polesi waliopo eneo la tukio wakatuchukua mimi na mtu niliye mvunjia kamera na wakatupeleka kwenye moja ya kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi
“Kwanini ulivunja kamera”
Askari mmoja aliniuliza swali huku nikiwa nimekaa kwenye kiti pembezoni mwa meza kubwa kiasi iliyopo kwenye chumba cha mahojiano
“Nisikilize bwana afande……Mimi sijui jamaa ana maana gani ya kunipiga mimi pichaa”
“Hata kama hutakiwi kuchukua sheria mkononi huoni umemnyima jamaa haki kama muandishi wa habari?”
Afande kuna maswala ya haki na mengine ya kipuuzi……Haiwezekanai mimi mpenzi wangu apigwe risasi na ninajitahidi kwenda kuwafwata hospitali eti anakuja mtu kunipiga piga picha hivi niakili kweli?”
“Na wewe unahusika kwenye tukio la binti kupigwa risasi?”
“Sijakuelewa unavyosema nimehusika?”
“Wewe ndio uliye mpiga risasi”
“Acha bangi maswali ya kiseng* mimi siyataki umenielewa wewe afande na kama umekosa cha kuzungumza muite mkuu wako mimi ndio nitazungumza naye na si wewe”
Askari akaanza kucheka huku akinyanyuka kwenye kiti alicho kikalia na kuanza kunizunguka huku akipiga makofi ya kejeli
“Bwana mdogo jua upo kwenye mikono ya dola na ukileta mchezo utakwenda kunyea debe”
“Hivi wewe unadhani nitanyea debe kirahisi rahisi…..Na huyo fala niliye mvunjia camera yake nenda kamuulize ameinunua kiasi gani nimlipe”
“Hujanijibu swali langu la awali?”
“Sawali gani?”
“Umehusika kwenye tukio la ujambazi lililo tokea hotelini”
“Sasa wewe naona unanichanganya ni hivi nikiendelea kuzungumza mimi mutaniweka ndani kwa maana ninajijua.Sasa siwezi kukujibu chochote hadi mwanasheria wangu aje hapa na sinto ongea na wewe kenge nitazungumza na mkuu wako”
“Kijana ninaona hunijua wewe”
Askari alizugumza huku akiviminya minya vidole vyake na vikaanza kutoa mlio watu wenyewe hukiita kitendo hicho ni kuvunja koda.Akanisogelea na kunishika shati langu na kunivuta jua hadi nikasimama kabla hajanipiga kofi mlango ukafunguliwa na akaingia mkuu wa polisi na kumfanya jamaa kuniachia
“Mjomba vipi tena mbona hapa saa hivi?”
Mkuu wa polisi alizungumza na ninavyo kumbuka nilisha wahi kumuona hospitalini kipindi nimepigwa risasi na alikuwa ni rafiki yangu ambaye aliweza kunipa taarifa za kumkamata Manka na mara nyingi alikuwa pia akizungumza na mimi
“Ni hawa vijana wako mjomba wananisumbua sumbua”
“Ispekar ninakuomba utupishe”
“Sawa mkuu”
Askari akatoka na kutuacha tumasimama ndani ya chumba hicho
“Haya niambie mjomba ni yapi yaliyo kukuta?”
“Mjomba bwana nilikuwa pale hotelini kuna tukio limetokea la mchumba wangu kupigwa risasi sasa nimekwenda kwenye gari letu kuna jamaa akaanza kunipiga piga picha kutokana nina hasira nikampokonya jamaa kamera yake na kuivunja ndio hawa vijana wako wakanileta hapa”
“Ahaaa wapumbavu kweli….Unajua nilipigiwa simu kuwa mkuu wenu wa shule amempiga risasi binti mmoja hotelini sasa nikajua basi yeye ndio yupo humu anahojiwa ndio maana nikaingia mara moja ili nimpatie dhamana kutokana yule ni kama kaka yangu”
“Mjomba huyo usimpatie dhamana kwani amempiga risasi mchumba wangu”
Mkuu wa polisi akashusha pumzi huku akionekana akifikiria cha kufanaya kisha akanitazama kwa sekunde kadhaa na kuzungumza
“Sasa mmjomba ni kwanini hujakwenda shule?”
“Mjomba leo ndio nimetoka Dar nimekuja na mchumba wangu ili arudi na gari home na mambo yamekuwa kama hayo unayo yaona”
“Huyo mchumba wako mama anamjua?”
“Mama hamjui na ninavyohisi mama atakuwa amesha ondoka na kwenda nje ya nchi”
“Ahaaa twende hospitali”
Tukatoka na mkuu wa polisi na kuwafanya askari wengine wakiwa wanashangaa akiwemo yule askari aliyekuwa akinihoji maswali ya ajabu ajabu.Jamaa niliye mvunjia kamera yake alipo niona akanyanyukwa kwenye benchi alilo kaa na kunifwata kwa hasira na kabla hajanifikia askari wengine wakamuwahi
“Namdai kamera yangu huyo na nyinyi munamuachia”
“Sema hiyo kamera yako ni bei gani nikulipe sasa hivi?”
“Laki tatu”
Nikafungua waleti yangu na kuanza kumuesabia pesa anayo ihitaji na kabla sijailipa mkuu wa polisi akanizuia
“Huyo mpiga picha ndio mwenye makosa muwekeni ndani hadi nirudi na nimkute ….Twende mwaya mjomba”
Tukatoka nje na kuingia kwenye gari analo tembelea mkuu wa polisi huku likiendeshwa na askari mwengine na haikuchukua muda tukafika kwenye hospitali aliyo pelekwa Sheila ambayo ni hospitali ya kanisa la katoliki na kumkuta Salome akiwa amekaa kwenye benchi huku akilia na alipo niona akanikimbilia na kunikumbatiaa na kuzidisha kilio na kunifanya nianze kuchanganyikiwa na kuhisi Sheila atakuwa nimempoteza
“Sheila yupo wapi?”
Salome akanionyesha kwa ishara ya kidole chumba alichoingizwa Salome na nikamuachia na kupiga hatua za kwenda kuingia kabla sijafika manesi wawili wakanizuia
“Samahani kaka hiki ni chumba cha oparesheni haruhusiwi mtu yoyote kuingia humu ndani zaidi ya madaktari”
“Mpenzi wangu anaendeleaje lakini?”
“Madaktari wanajitahidi kuyaokoa maisha yake tunakuomba uwe mpole na mtulivu”
“Ila si atapona na kuwa mzima kama zamani”
“Ndio”
Nilizungumza huku machozi yakinimwagika nikatafuta sehemu na kukaa juu ya viti vilivyopo katika kordo ya kuingilia ndani ya chumba hicho.Mkuu wa polisi akanifwata na kuniaga
“Mjomba nitakuja asubuhi kuangalia hali ya mgonjwa inaendeleaje mimi ngoja niende nikashuhulikie hili swala”
“Sawa mjomba”
“Ila usije ukamjulisha mama hili swala mimi nitalishughulikia hadi mwisho”
“Asante mjomba”
Mkuu wa polisi akaondoka na kuniacha nikiwa nimejiinamia,Salome akatoka kwenye kiti alicho kaa na kuja kukaa kando yangu huku na akilia kichini chini.Hatukusemeshana kitu chochote zaidi ya kila mmoja kuwaza anacho kiwaza yeye mwenye.Nikanyanyuka na kukaa upande mwengine wa viti na kumfanya Salome unyanyuka na kuja kukaa karibu yangu
“Salome rudi ulipokuwa umekaa”
“Eddy samahani kwa kilicho tokea”
“Nimekusamehe ila sihitaji ukae karibu yangu”
“Ndio Eddy ninalijua hilo ila ninakuomba tafadhali nikae karibu na wewe”
“Ukae aribu na mimi….Mfwate basha wako ukakae naye ila sio mimi sawa”
Nilizungumza kwa sauti ya juu na kuwafanya manesi na baadhi ya watu waliopo eneo tulilo kuwepo sisi wakitutizama kwa mshangao
“Eddy”
“Eddy jina langu…..Ila Salome ninakuomba ukakae sehemu uliyo kuwepo na sihitaji kukuona hapa”
Salome akazidi kulia kwa uchungu kiasi kwamba akazidi kunikasirisha,nikasimama na kuelekea nje kupata upepo japo kuna baridi ila mwili wangu umetawaliwa na joto kali.Salome akanifwata sehemu niliyo kaa huku akilia
“Eddy ninajua kuwa unanichukia kwa sababu nimekuwa chan…..”
“Nyamaza kwani tatizo lako wewe ni nini?”
“Nakuomba unisamehe”
“Haya nimekusamehe nenda zako sasa”
“Eddy usinifukuze kama mbwaa kumbuka kuwa mimi ninakupend……”
“Malaya wewe unanipenda mimi……Niachie unafki wa kiseng* seng*,Wewe si nisuper star wa shule basi tembeza mbaliga zako nenda shule aua unataka nikuchomeshe kwa askari?”
“Hapana”
“Powa nakuomba unipotezee”
Salome akanyanyuka kiunyonge nyonge na kubaki akiwa ananitazama huku akionekana kama anahitaji kuzungumza kitu ila anashindwa na kuanza kutembea taratibu
“Unashangaa shangaa nini wewe?”
“Mmmmm”
“Njoo”
Salome kapiga hatua hadi sehemu niliyo kaa na nikanyanyuka taratibu na kufungua waleti na kutoa noti mbili za elfu kumi na kumpa Salome
“Nenda zako shule na sihitaji nikuone hapa”
“Wewe utakuja?”
“Hilo halikuhusu wewe nenda zako”
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI
KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger
Email: ZephilineEzekiel@Gmail.Com