SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA
ILIPOISHIA...
“Amepata mstuko wa moyo”
“Mmmm kwahiyo itakuwaje?”
“Ndio tunamshuhulikia kuurudisha moyo wake kwenye hali yake ya kawaida”
“Sawa dokta kila kitakocho endelea unijulishe kwenye hii namba”
“Sawa”
NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU
SASA ENDELEA...
Nikamuachia daktari namba yangu ya simu kisha nikatoka na kwenda kwenye mgahawa wa karibu na hospitali na nikaagiza chakula na kuanza kula taratibu huku nikitafakari ni nini nifanye juu ya ushaidi wa kumkamata mkuu wa shule.Tv(Luninga) iliyopo kwenye mgahawa Chaneli Ten ikaonyesha habari iliyo wafikia kwa wakati huo(BREAKING NEWS) na kunifanya niache kula na kuitazama kwa umakini.Nikashuhudia jinsi askari wakijitahidi kutuliza fujo zinazo endelea shuleni kwetu huku ofisi za waalimu zikiwa zinateketea kwa moto
“Wanafunzi bado wanaendelea kupambana na askari wa kutuliza ghasia na madai yao makubwa ni mkuu wa shule hiyo kuwaambukiza vijana wa kike wapatao kumi na sita virusi vya ugonjwa hatari wa UKIMWI kimakusudi huku akitumia nguvu katika kulifanya hilo”
Mtangazaji alizungumza huku kamera ikionyesha jinsi wanafunzi wa shuleni kwetu wakiwarushia mawe askari huku wengine wakiwa na mipini ya mejembe na makwanja wakiendelea kupambana na polisi
“Mkuu wa jeshi la polisi amewaahidi wanafunzi hao kufanya kila linalo wezekana katika kumkamata mkuu huyo wa shule ambaye hadi sasa hivi haijulikani yupo wapi.Serikali nini maana ya elimu? Wazazi wanajitolea pesa zao ili watoto wao wapate elimu iliyo bora ila mwisho wa siku hali ndio hii.Tunaiomba wizara ya elimu kuunda tume ya kuchunguza tabia za waalimu hususani katika haya mashule ya watu binafsi.Tutaendelea kuwajulisha kitakacho endelea….Nikikutangazia kutoka Mkoani Arusha mimi ni Upendo John Chanel Ten”
Nikasusha pumzi na kuwatazama watu waliomo kwenye mgahawa huo ni jinsi gani walivyo ichukulia hiyo taarifa ya habari na kila mmoja anaonekana kukasirishwa na kitendo cha mkuu wa shule kufanya jambo la kikatili kama hilo.Nikalipa nilicho kula na kuingia ndani ya gari na safari ya kuelekea shule ikaanza,Nikapitiiza moja kwa moja kwa Madam Mery na nikafika nyumbani kwake nikapiga honi kwa muda nikaona kupo kimya ikanilazimu kushuka kwenye gari na kuligonga geti na kwakupitia uwazi mdogo nikamuona Madam Mery akichungulia kwenye mlango wa kuingilia kwake huku wakiwa na Madam Rukia wakishauriana kuja kufungua huku wakionekana kuwa na wasi wasi.
“Madam ni mimi Eddy fungueni”
“Eddy yupi huyo?”
“Sasa hivi hunijui au?”
“Ahaa Eddy nakuja kukufungulia?”
Madam Rukia akatoka ndani na kuja getini na kunifungulia geti nikarudi ndani ya gari na kuliingiza gari ndani na kushuka na Madam Mery akanifwata huku akionekana kuwa na wasi wasi
“Eddy umesalimika?”
“Ndio ila sijampata mkuu wa shule”
“Sasa si utulie jamani mpenzi wangu”
“Siwezi kutulia hadi nijue muafaka wa mkuu wenu wa shule”
“Eddy jamani huoni kama unajiingiza matatizoni?”
“Maji nimeyavulia nguo acha niyaoge…..Ngoja nielekee shule”
“Shule tena?”
“Ndio”
“Eddy huko unapokwenda kuna vurugu nyingi na askari wanawakusanya wanafunzi wanao fanya vurugu na kuwapeleka polisi”
“Ache iwe hivyo wewe nilindie hili gari sawa”
“Eddy jamani mpenzi wangu nakuomba usiende”
“Madam mimi sasa hivi sio mpenzi wako kutokana tayari wewe umesha olewa na nimjamzito kwaiyo siwezi kuvunja kile alicho kiunganisha MUNGU”
“Eddy ila tambua ya kwamba ninakupenda tena sana”
Madam Mery alizungmza huku machozi yakimwagika huku akining’ang’ania mkono wangu nisiondoke
“Sory Madam ninakuomba uniachie niende na ninakuomba umpende mume wako kama ulivyo nipenda mimi ninakuomba unisamehe kwa hilo siwezi kuwa na wewe”
“Eddy Eddy ndio unaniacha?”
“Sio kama ninakuacha ila nitakuheshimu kama mwalimu wangu na si vinginevyo”
Nikauachanisha mkono wa Madam Mery kwenye mkono wangu kisha nikaanza kupiga hatua za haraka kuelekea getini
“EDDY TAMBUA NIMEBEBA MWANAO NA MUME WANGU NIMEACHANA NAYE BAADA YA KUJUA MIMI NINAUJAUZITO AMBAO SI WAKE”
Niksimama na kugeuka taratibu huku nikiwa ninamtazama Madam Mery anaye lia huku akiwa amekaa chini akionekana kuwa na uchungu na kunifanya nizidi kuchanganyikiwa
Nikapiga hatua za taratibu na kumnyanyua Madam Mery na kuanza kufuta machozi taratibu kwa kutumia kitambaa changu kisha tukaingia ndani na moja kwa moja tukapitiliza hadi chumbani kwake.Ukimya ukatawala kati yetu huku madam Mery akiendelea kulia chini chini na kichwani kwangu sikuwa na hata wazo la kulizungumza likaeleweka
“Eddy”
“Naam”
“Amini ya kwamba nina kupenda sana japo kuwa kiumri tume tofautana ila moyo wangu umeshindwa kumpenda mwanaume mwengine zaidi yako”
“Acha kuniongopea......nilikuona ni mtu wa maana sana kipindi mapenzi yetu yalipo anza lakini leo hii unaniambia umeolewa tena na mapicha ya harusi yako unayambandika huku ukutani”
Nilizungumza kwa sauti ya ukali kiasi kwamba Madam Mery akawa mpole pasipo kuzungumza kitu cha aina yoyote
“Tena umeona gia yako ni kuniongopea kuwa wewe ni mjamzito,Unadhani mimi nitakubali kirahisi kulea mimba ambayo sielewi mwanzo wake ni upi wala mwisho wake”
“Eddy najua unauchungu moyoni mwako kwa mimi kuolewa.....Ila Eddy mimi sikuwa na jinsi ya kufanya”
“Ahaaaa hukuwa na jinsi ya kufanya kwani wewe ni mtoto mdogo ambaye ulibebwa juu juu na kupelekwa kanisani na kufungishwa ndoa eheee?”
Madam Mery akazidi kulia kwa uchungu huku na mimi hasira ikianza kujaa kifuani kwangu hadi nikajikuta nikianza kutetemeka mikono
“Eddy am sory?(Eddy samahani)
“Samahani yako haiwezi kuchukua nafasi yoyote ndani ya moyo wangu kwasababu hujui ni jinsi gani nilivyo kuwa ninakupenda.....Leo hii unasema umeolewa na mimba ni yangu.Hainiingii akilini hata kidogo”
“Eddy naomba nikuambie ukweli”
“Ukweli kuhusu nini?”
“Eddy kipindi nilipo anza mahusiano na wewe nilikuwa na mpezi wangu ambaye alikuwa Uingereza kimasomo....Alirudi mwezi ulio pita na akanifanyia suprize ya kunivalisha pete ya uchumba na tukafunga ndoa ila...”
“Ila nini sasa kumbe siku zote una kazi ya kuniongopea na kumbe una bvwana wako nje ya nchi.Mbona nyinyi wanawake hampendeki mufwanye nini ili mujue munapendwa.....Wenyewe mukafanya vya kutosha ehee alafu mukajazana mimba leo hii unaniambia Eddy hii mimba ni yako.Si ndio munavyo danganyana”
Nilizidi kuzungumza kwa sauti ya kufoka kiasi kwamba Madam Mery akanyanyuka kwa hasira na kunipiga kibao cha shavu na kuzidi kunipandisha hasira.Nikamshika koo Madam Mery na kumuegemeza ukutani huku nikimuangalia kwa macho yaliyo jaa hasira hadi machozi yakaanza kunimwagika
“MERY NITAKUUA”
“E...ddy we..ee niue nipo...radhi kwa hilo.Mimi siku zote nilijua UMEKUFA NDIO MAANA NIKACHUKUA MAAMUZI YA KUOLEWA”
“Fuc* you”
Nikamuachia madam Mery na kuanza kuvunja picha zilizo tengenezewa frame na kwahasira nikaanza kupiga ngumi ukutani hadi mikono ikaanza kuvuja damu.Madam Mery akapiga hatua moja ya kunifwata nikageuka kwa jinsi ya muonekano wangu tu ilitosha kumfanya asimame kama namba moja asipige hatue nyingine ya pili
“Usinifwate nitakuua”
“Eddy unajiumiza”
“Nimekuambia niache...Sasa hivi huyu unaye zungumza naye ni mfu wa Eddy ila Eddy mwenyewe amekufa mwanzo leo mwisho leo sitaki kusikia unanitafuta”
“Eddy jamani kwanini unanifanyia hivyo au kwasababu ninakupenda,kwa nini unanikatili kiasi hicho unataka huyu kiumbe huku tumboni akose baba?”
“Baba yake si huyo anaye toka uingereza.....Ni mara mia ungenidanganya basi kuwa hiyo pete uliyo ivaa nip ambo lakini kabisa unalipanua domo lako EDDY NIMEOLEWA”
Madam Mery akazidi kulia kwa uchungu na nikazidi kumuona ni muigizaji kwa maana kipindi cha mwisho kufanya naye mapenzi alilazwa hospitali kwa madai ya kuumwa ugonjwa wa malaria
“Eddy siku tuliyofanya mapenzi ndipo nilipata mimba ya huyu kiumbe chako tumboni na wala sio mimba ya mume aliye niona”
“Ahaaa kwahiyo unataka mtoto akizaliwa awe na rangi za Uingereza uingereza si ndio”
“Eddy Eddy”
‘Eddy nini...kama mimba ni ya kwangu basi mumeo kaja kamalizia ukarabati wa rangi ya mtoto”
“Eddy nyamaza sasa kumbuka mimi pia ni mwalimu wako”
“Usinge nivulia nguo kama wewe ni mwalimu wangu......Sasa ni hivi sihitaji tena uhusiano na wewe sawa?”
Nilizungumza kwa hasira huku nikipiga hatua za kuufwata mlango wa kutokea ndani ya chumba.Kabla sijaufikia Madam Mery akalishika shati langu kwa nyuma huku akilivuta hadi baadhi ya vifungo vikakatika nikageuka kwa hasira na kurusha ngumi iliyotua tumboni Madam Mery na kumfanya atoe ukulele mkali huku akijikunja na mikono yake ikiwa imelishika tumbo lake
“Eddy Unaniua?”
Madam Mery alizungumza na kuanguka chini na damu zikaanza kumtoka mdomoni,Hasira yote nikajikuta ikiniisha na nikipiga goti moja chini na kumtazama na Madam Mery na kumkuta akihema kwa shida kama mtu mwenye ugonjwa wa pumu,Gafla mlango wa chumbani ukafunguliwa na akaingia Madam Rukia na baada ya kumuona mwenzake yupo chini akaanza kupiga makelele huku akiwa anakimbilia sebleni.Nikanyanyuka kwa haraka na kutoka nje na kumkuta Madam Rukia akiminyana kuufungua mlango wa kutoka nje.Nikamshika kiuno na kumnyanyua juu juu na kumtupa juu ya sofa
“Unataka kufanya nini?”
Nilizungumza kwa sauti ya juu kiasi kwamba hadi mimi mwenyewe nikajishangaa kwani katika maisha yangu sikuwahi kuzunguamza kwa sauti ya namna hiyo
“Eddy umemuua Mery”
“Acha ufala una uhakika amekufa”
“Ohooo Mama weee Eddy umeuaa ohooo majirani.......”
Nikamuwai kumziba mdomo Madam Rukia anaye waita majirani wamsaidie na nikachukua vitambaa viwili vya makochi na kumsokomeza navyo mdomoni kisha nikavua mkanda na kuifunga mikono yake kwa nyuma.Kisha nikamnyanyua na kumuweka begani na kabla sijatoka njee nikasikia sauti ya Madam Mery akiomba msaada.Nikatoka hadi nje na kufungua buti ya gari na kumuingiza Madam Rukia na kwa uzuri nikakuta kamba ya manila ambayo nikaitumia kwa kumfunga miguuni
“Ukileta upumbavu nitakwenda kukutupa sehemu usiyo ijua na sitaki using** sawa wewe Malaya”
Madam Rukia akaitika kwa kutingisha kichwa akiashiria amenielewa ninacho kizungumza,Nikaifunga buti ya gari na kurudi ndani na kumkuta Madam Mery akiburuzika chini huku akiwa amelishika tumbo lake na damu zikiendelea kumtoka mdomoni.Nikanyanyua na kumuingiza ndani ya gari nikafungua geti na kulitoa gari nje kisha nikalifunga na kurudi ndani ya gari na kumpeleka Madam Mery katika hospitali ya mkoa.Manesi wakampoke Madam Mery na kuanza kumuhudumia nikabaki nikiwa ninajilaumu kwa kitendo nilicho kifanya.
“Wewe ndio uliye mleta huyu mgonjwa?”
“Ndio”
“Nifwate ofisini”
Nikaongozana na Mzee mmoja aliye valia koti jeupe na tukaingia ofisini kwake na nikakaa kwenye kiti nilicho kikuta na yeye akakaa kwenye kiti chake
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI
KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger
Email: ZephilineEzekiel@Gmail.Com