SORRY MADAM (27)
JINA: SORRY MADAM Mwandishi: Eddazaria G Msulwa SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA ILIPOISHIA... “Amepata mstuko wa moyo” “Mmmm kwahiyo itakuwaje?” “Ndio tunamshuhulikia kuurudisha moyo wake kwenye hali yake ya kawaida” “Sawa dokta kila kitakocho endelea unijulishe kwenye hii namba” “Sawa” NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU SASA ENDELEA... Nikamuachia daktari namba yangu ya simu kisha nikatoka na kwenda kwenye mgahawa wa karibu na hospitali na nikaagiza chakula na kuanza kula taratibu huku nikitafakari ni nini nifanye juu ya ushaidi wa kumkamata mkuu wa shule.Tv( Luninga ) iliyopo kwenye mgahawa Chaneli Ten ikaonyesha habari iliyo wafikia kwa wakati huo(BREAKING NEWS) na kunifanya niache kula na kuitazama kwa umakini.Nikashuhudia jinsi askari wakijitahidi kutuliza fujo zinazo endelea shuleni kwetu huku ofisi za waalimu zikiwa zinateketea kwa moto “Wanafunzi bado wanaendelea kupambana na askari wa kutuliza ghasia na madai yao makubwa ni mkuu wa shule hiyo kuwaambukiza vijana wa kike …