SORRY MADAM (31)

Zephiline F Ezekiel
SORRY MADAM (31)
JINA: SORRY MADAM Mwandishi: Eddazaria G Msulwa SEHEMU YA THELATHINI NA MOJA ILIPOISHIA... “Wewe dogo lazima nikutafute tuu sehemu yoyote na nilazima nikuue” Jamaa alizungumza huku akishikwa na baadhi ya watu,sikutaka kumjibu kitu cha aina yoyote zaidi ya kuelekea kwenye chumba ambacho nilimuona Manka akiingizwa kabla sijakifikia madaktari wawili wakanizuia NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU SASA ENDELEA... “Huwezi kuingia humu ndani?” “Kwa nini?” “Hichi ni chumba cha wagonjwa mahututi haturuhusu mtu wa aina yoyote kuingia humu hususani wewe ambaye umetuchafulia hewa ya hospitli” Daktari mmoja alizungumza huku akinitazama kwa macho makali kiasi kwamba nikajikuta nikibaki nimemtazama.Nikatoka nje na kuifungua simu yangu sehemu ya Internet na kuingia kwenye mtandao wa google na kuanza kuitafuta habari ambayo nimeiona kwenye Tv,Nikaingia kwenye tovuti ya BBC Swahili na taarifa ya kwanza kuikuta ni ambayo inahusiana na kupotea kwa ndege ambayo hadi wanakwenda mitamboni hawaku…