SORRY MADAM (31)

0
SEHEMU YA THELATHINI NA MOJA
ILIPOISHIA...
“Wewe dogo lazima nikutafute tuu sehemu yoyote na nilazima nikuue”
Jamaa alizungumza huku akishikwa na baadhi ya watu,sikutaka kumjibu kitu cha aina yoyote zaidi ya kuelekea kwenye chumba ambacho nilimuona Manka akiingizwa kabla sijakifikia madaktari wawili wakanizuia

NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU

SASA ENDELEA...
“Huwezi kuingia humu ndani?”
“Kwa nini?”
“Hichi ni chumba cha wagonjwa mahututi haturuhusu mtu wa aina yoyote kuingia humu hususani wewe ambaye umetuchafulia hewa ya hospitli”

Daktari mmoja alizungumza huku akinitazama kwa macho makali kiasi kwamba nikajikuta nikibaki nimemtazama.Nikatoka nje na kuifungua simu yangu sehemu ya Internet na kuingia kwenye mtandao wa google na kuanza kuitafuta habari ambayo nimeiona kwenye Tv,Nikaingia kwenye tovuti ya BBC Swahili na taarifa ya kwanza kuikuta ni ambayo inahusiana na kupotea kwa ndege ambayo hadi wanakwenda mitamboni hawakujua ni wapi ilipo.Nikajikuta nikizidi kuchanganyikiwa na kuanza kuzungumza mwenyewe

“Ila mama mimi nilikuwambia usiende ila wewe umejifanya mbishi unaona sasa yaliyo kukuta”
Nilizungumza huku machozi yakinimwagika,Nikaingia kwenye taksi nilio kuja nayo na kumuomba dereva anipeleke kwenye hospitali aliyolazwa Sheila
“Kaka mbona unalia?”
“Ahaaa hakuna kitu kaka”
“Hapana una ndugu aliye fariki nini hapo hospitalini?”
“Hapana ila kuna mambo yangu binafsi tuu”
“Sawa kaka ngoja nikuwashie redio usikilize muziki upunguze mawazo”

Dereva wa taksi akawasha redio ya gari yake na tukaanza kusikiliza nyimbo kwenye stesheni moja ambayo sikujua ni stesheni ya wapi.Mara gafla miziki ikakatishwa na kukaja taarifa ya habari na sauti nzito ya muandishi wa habari ikaanza kusikika vizuri masikioni mwangu

“TAARIFA KUTOKA IKULU ZINASEMA NDEGE ILIYOBEBA VIONGOZI WA NCHI YA TANZANIA YA SHIRIKA LA KLM IMEPOTEA KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA NA INASADIKIKA KUWA IMETEKWA NA MARUBANI HAO AMBAO WAMEZIMA MITAMBO YA RADA INAYO ONYESHA SEHEMU AMBAZO NDEGE HIYO HUPITA.
WAZIRI WA MAMBO YA NDANI ANAWAOMBA WANANCHI WAWE WASIKIVU KWANI UMOJA WA MATAIFA WAMETUMA NDEGE ZA KIJESHI KWENDA KUIFWATILIA NDEGE HIYO”

Nikajikuta nikijifunga mdomo huku machozi yakizidi kunimwagika na sura yangu nikaiinamisa chini na sikutaka dereva aelewe ni kitu gani kinacho endelea
“Ahhh acha watekwe bwana kwa maana wamezidi kula pesa za serikali.Watu wanakaa na kujaziana matumbo yao na sisi wananchi wa hali ya chini tanazidi kufa kwa tabu kila siku vitu vinapanda bei”
Maneno ya dereva Taksi yakazidi kuumiza moyo wangu huku hasira ikinipanda na kujikuta nikiyang’ata meno kwa nguvu ili kuizuia hasira yangu na mbaya zaidi katika maisha yangu mimi ni miongoni mwa watu wagonjwa wa hasira na siku zote huwa nikikasirika ninaweza kufanya maamuzi ambayo yatapelekae baadaye kujutia

“Unajua hawa vionngozi wetu wamezidi kutunyanyasa hapa utakuta walikuwa wanakwenda kula bata na hao Marubani wamewapatia kweli kwa maana ni washenzi sana”
Dereva alizidi kuzungumza huku akiongeza sauti ya redio ili asikilize majina ya viongozi sita waliomo ndani ya dege hiyo huku wengine wakitokea Kenya.Jina la mama yangu likwa ni lasita katika kutajwa na kumfanya dereva taksi kuanza kucheka

“Haaa huyu mama naye yuopo.....Kweli Mungu hapendi dhambi kuna siku bwana alikuwa na dereva wake sasa kwa bahati mbaya nikamchomekea kwa mbele ile barabara ya kuingilia K.C.M.C nilikuwa namuwahisha mgonjwa hospitalini.Ahaaaa alikwenda kunilaza polisi hadi siku anaondoka Arusha ndio wakaniachia......Tena hao watekaji kama wanajua wamfanye wa kwanza kufa kwa maana yule mama roho mbaya sana”

Maneno ya dereva yakazidi kunipandisha hasira hadi mwili mzima ukaanza kunitetemeka huku misuli ya mwili wangu ikikaza na kujikuta nikikunja ngumi na kuipiga kwenye sehemu niliyokuwa nimeinamisha kichwa na kusababisha kifuniko chake kuchangukuka
“Aiiseee inakuwaje chalii wangu mbona unanaribia gari yangu,”
“Funga bakuli lako”

Nilizungumza huku meno yangu nikijitahidi kuyang’ata kwa nguvu kwani kiwango cha hasira kinazidi kuongezeka huku mapigo yangu ya moyo yakienda kwa kasi huku jasho likinimwagika
“Haa wewe vipi umearibu gari yangu unaniambia ninyamaze....Kama umechanganywa na mambo yangu ndio unizingu mimi na utalipa tuu”
“Funga bakuli lako nitakuua”
“Wewe fala kweli nani umuue?”

Dereva alizngumza huku akipunguza mwendo wa gari,Nikakishika kwichwa chake kwa nyuma na kukigongesha kwenye mskani mara tatu mfululizo na nikasababisha gari kuanza kuyumba na likatoka barabarani na tukajikuta likiingia kwenye mtaro na kulalia upande wa dereva huku kichwa changu kukichanwa na kioo kwenye sehemu ya paji la uso na damu zikaanza kunijaa usoni,Sikutaka kumuangalia dereva taksi anaendeleaje na nikaanza kujitahidi kuufungua mlango wa gari na watu wakaanza kukusanyika na kunisaidia katika kuufungua kwa kwa nje na kunitoa ndani ya gari.Kutokana na wenge nikataka kuondoka eneo la ajali ila wakanizuia huku wakinikalisha chini kiulazima
“Jamani musimzunguke mpeni hewa ajisikie vizuri”

Jamaa mmoja alizungumza huku akiwasogeza watu wanao nishangaa,dada mmoja akaanza kunifuta damu zilizo samba usoni kwangu na sikujisikia maumivu ya aina yoyote
“Begi langu lipo wapi?”
Niliwaauliza watu na mtu mmoja akaniletea begi langu na kuliweka sehemu niliyokaa,Nikawaona wakijitahidi kumtoa dereva taksi ambaye sikujua kama amekufa au laa,
“Jamani tumuwahisheni hospitali”
“Nipo salama”
“Kaka umeumia damu zinakutoka bado”
“Zitakata zenyewe”
“Dada huyo mnamsemesha hapo akili sio zake cha msingi ngoja kuna teksi imekwenda kuchukuliwa tumpeleke hospitali”

Simu yangu ikaanza kuita na dada aliyekuwa akinifuta damu akaanza kunisaidia kuitoa mfukoni na akanionyesha namba ambayo kwa ukungu ulio nitawala machoni mwangu sikuweza kuigundua kwa haraka
“Ipokee”
Dada akaipokea na kuisikilizia huku akiwa ameiweka laud speaker
“Eddy upo wapi mume wangu mbona makelele?”
“Samahani dada yangu”
“Wee ni nani unaye ipokea simu ya mume wangu?”
“Mimi ni masamaria mwema mume wako amepata ajali ya gari na hapa alipo hawezi kuzungumza vizuri”
“Mungu wangu ni mzima?”

Nikagundua ni sauti ya Sheila na kukumbuaka hali yeka aliyo nayo ikanibidi nimpokonye dada simu na kuiweka sikioni
“Baby sijaumia sana?”
“Eddy ni wewe?”
“Ndio mke wagu sijaumia sana na usiwe na presha”
“Baby usife....nitabaki na nini jamani mume wangu”
Sheila alizungumza huku nikimsikia akiwa analia
“Baby siwezi kufa nakuomba uache kulia si unajua hujapona vizuri utazifanya hizo nyuzi za kidonda kuachia”
“Baby kama haujaumia basi waambiea wakulete huku hospili”
“Sawa baby ila nyamaza kulia”

Nikakata simu na kuiweka mfukoni na kunyanyuka nikisaidiwa na baadhi ya watua na tukaingia kwenye moja ya taksi na nikawaomba wanipeleke kwenye hospitali aliyo lazwa Sheila na madaktari wakanipokea na kuniingiza kwenye chumba ambacho wakananishona kwenye jerala langu la usoni na kunifunga bandeji.Nikaelekea kwenye chumba alicholazwa Sheila na kumkuta akiwa yupo na nesi wakiomba huku mikono yao wakiwa wameiweka juu ya Biblia na macho yao wakiwa wameyafumba.Nikawaacha wamalize kuomba na wakafumbua macho na kuniona nikiwa nimekaa pembeni ya kitanda alicho lala Sheila na akaonekana kunishangaa huku machozi yakimwagika

“Eddy upo salama?”
“Nipo nipo mke wangu sawa”
“Pole mwanangu”
Nesi ambaye ni miongoni mwa masister wa kanisa la katoliki wanaofanya kazi katika hospitali hii alinipa pole na nikamuitikia kwa sauti ya upole na yenye unyonge ndani yeke
“Mwanangu hujaumia sana?”
“Sijaumia sana ni hapa usoni ndio nimechanwa na kiio cha gari”
“Eddy afandhali hujumia sana ila gari halina dhamani kwangu kuliko wewe”
“Sikwenda na gari yetu nilikuwa nimepnda taksi”
“Pole sana mwanangu.....ngoja niwaache ninakwenda kuendelea na shuhuli nyingine”

Nesi akatoka ndani ya chumba na kutuacha tukiwa kimya,Nikamsogelea Sheila na kumfuta machozi taratibu na ukimya ukatawala ndani ya chumba
“Eddy”
“Naaamm”
“Mbona unaonekana una mawazo?”
“Ni mama?”
“Amefanyaje?”
“Ametekwa kwenye ndege?”
“Weee”
“Ndio”
“Wewe umejuaje?”
“Nmesikia kwenye taarifa ya habari”
“Mmmm Eddy turudi Dar tukajue ni nini kinacho endelea”
“Tutarudi hadi wewe upone”
“Nmeshapona mume wangu?”
“Haujapona vizuri mpaka madaktari wakikupa ruhusa ndio tutarudi Dar”

Simu yangu ikaita na kukuta ni namba ngeni ndio inayopiaga tena ni namba ya mezani.Nikaitazama kwa muda kisha nikaipoke
“Habari yako Eddy”
Sauti nzito ya kiume ilisikika kutoka upande wa pili wa simu na kunifanya nistuke kidogo
“Salama nani mwanzangu?”
“Mimi ni mkuu wa upelelezi wa Taifa nimepewa jukumu la kukujuisha kitu kinachoendelea juu ya mama yako”
“Sawa”
“Nina taarifa ambayo sio nzur sana kwa mama,kwanza tunakuomba usiwe na wasiwasi kwa maana hali ya abiria wote waliomo kwenye ndege ya shirika la KLM tumegundua wanaendelea vizuri akiwemo mama yako na hapa tunafanaya juhudi za kuwaokoa na nitazidi kukujulisha kila kitakacho endelea”
“Sawa nashukuru kwa taarifa yako”

Nilizungumza kwa sauti ya unyonge na simu ikakatwa na nikairudisha mfukoni huku nikimtazama Sheila
“Wamewapata?”
“Bado”
“Ohoo Mungu wangu msaidie mama yangu mkwe anusurike na matatizo hayo”
Maneno ya Sheila yaliyojaa huzuni yakaamsha hisia zangu za kulia na kujikuta nikimkumbatia Sheila na akaanza kuniliwaza na maneno matamu

“Ni wapi nimekosea kwenye maisha yangu Mungu wangu kwa nini kila siku ni mimi..Likiiasha hili linakuja hili kama ni vipi ni bora nife kuliko kupitia kipindi hichi kigumu kwenye maisha yangu”
Nilizungumza huku machozi yakizidi kuni kunitiririka huku moyoni mwangu nikiwa nimekosa amanani na kukata tama ya kushi kabisa duniani
“Eddy kwanini unazungumza hivyo.....Unataka mimi niishi peke yangu? Unadhani wewe ukifa mimi nitaishije ninaamini kwamba wewe unaijua historia ya maisha yangu.Sina baba,Mama,kaka,dada wala jamaa wa karibu.Eddy wewe ndio mwanga wangu...wewe ndio baba yangu..wewe ndio mama yangu.Ukifa wewe na mimi nilazima nife”

Sheila akazidi kuniongeza uchumgu wa kulia kwani kusema kweli kila hatua ya maisha yangu ninayopitia kwangu inamikosi
“Sheila hata mimi nikifa nakuomba usijiue...Mimi ni mwaname natambua wewe utapata mwanaume mwengine wa kukuoa ila usije ukafanya hivyo kwa ajili yangu”
“Eddy hapana wewe ndio kila kitu kwangu kwa sasa..Japo tunamuda mfupi ila kwako nimepata tulizo la moyo wangu”

Nikanyanyuka kitandani na kufungua dirisha na kuchungulia kwa chini nikiangalia watu wanao ingia na kutoka ndani ya hospitalini hii.Mawazo ya ajabu yakaanza kunitawala akilini mwangu na gafla nikamuona mama kwa chini akiwa amekaa pembeni ya jeneza huku akiwa amevalia nguo yeupe huku puani akiwa na pamba na akaanza kuniita huku akilia kwa uchungu kiasi kwamba nikaanza kuchanganyikiwa

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI

KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)