SORRY MADAM (37)
JINA: SORRY MADAM Mwandishi: Eddazaria G Msulwa SEHEMU YA THELATHINI NA SABA ILIPOISHIA... Nikatumia kama masaa mawili na kufika nyumbani kwake na kukuta ukimya mwingi ukiwa umetawala ila kitu kingine kilicho anza kunipa wasiwasi ni nyasi nyingi na ndefu zilizo oto nje ya geti lake na kwaharaka nikajua Sheila hayupo ndani ya nyumba yake kwa maana kama angekuwepo kusingekuwa na nyasi nyingi huku geti lake likiwa lemetawaliwa na vumbi jingi. NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU SASA ENDELEA... Ikanibidi kuchungulia kwenye eti lake ili kujionea mwenyewe nikipingana na mawazo yagu ya kusema Sheila hayupo ndani ya nyumba yake.Giza lilitawala kwenye nyumba yake na hapakuwa na dalili yoyote ya mtu kushi na jinsi mlango tulivyo ufunga siku ya mwisho ndivyo jini ulivyo kwa sasa.Nikashusha pumzi nyingi huku nikitazama wapi nielekee na mbaya zaidi sikua na jirani yoyote wa Sheila ninaye mjua ambaye ninaweza kumuulizia habari za Sheila Hali ya uchunu ikaanza kunitawala na kwa mbali …