SORRY MADAM (37)

0
SEHEMU YA THELATHINI NA SABA
ILIPOISHIA...
Nikatumia kama masaa mawili na kufika nyumbani kwake na kukuta ukimya mwingi ukiwa umetawala ila kitu kingine kilicho anza kunipa wasiwasi ni nyasi nyingi na ndefu zilizo oto nje ya geti lake na kwaharaka nikajua Sheila hayupo ndani ya nyumba yake kwa maana kama angekuwepo kusingekuwa na nyasi nyingi huku geti lake likiwa lemetawaliwa na vumbi jingi.

NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU

SASA ENDELEA...
Ikanibidi kuchungulia kwenye eti lake ili kujionea mwenyewe nikipingana na mawazo yagu ya kusema Sheila hayupo ndani ya nyumba yake.Giza lilitawala kwenye nyumba yake na hapakuwa na dalili yoyote ya mtu kushi na jinsi mlango tulivyo ufunga siku ya mwisho ndivyo jini ulivyo kwa sasa.Nikashusha pumzi nyingi huku nikitazama wapi nielekee na mbaya zaidi sikua na jirani yoyote wa Sheila ninaye mjua ambaye ninaweza kumuulizia habari za Sheila

Hali ya uchunu ikaanza kunitawala na kwa mbali machozi yakaanza kunilenga lenga na kujikuta nikitamani utokee muujiza Sheila kusimama mbele yangu,Wazo la kuwa na mama likaanza kunijia ila kutokana na kuchoka nikashidwa kujua kama nitaweza kwenda nyumbani ambapo tulikuwa tunaishi ila woga ukaanza kunijia kwani kumbukumbu ya baba siku alivyokuwa akinipiga ikanijika kichwani kama mkanda wa video ila ukakata gafla baada ya kusikia mnguruo wa mbwa ukitoka nyuma yangu. Nikageuka na kukutana na mbwa wakubwa wawili wakiwa wananguruma huku wakinitazama kwa macho yao makali kiasi kwamba nikajikuta nikiaanza kutetemeka.Nikatulia kwa muda huku mwili wangu ukishindwa kukimbia kabisa kutokana na njaa kali iliyopelekea nguvu za mwili wangu kuniiishia.Nikasikia mlunzi wa mtu akiwaita mbwa walio karibu yangu na wakaelekea walipo itwa na kumuona mlinzi wa nyumba ya jirani akiwa amesimama huku mbwa wake wakiwa wamenzunguka na mkononi mwake akiwa ameshika bunduki yake aina ya gobore

“Samahani kaka”
Nilimuita mlinzi kwa sauti ya kukwaruza kwaruza huku nikianza kupiga hatua za taratibu za kumfwata sehemu alipo na kabla sijamfikia akaikoki bunduki yake na kunielekezea
“Usipige atua nyingine ya kunfwata la sivyo nitakulipua”
Nikasimama huku nikiwa ninamwangalia mlinzi na sikua na cha kufanya zaidi ya kuwa mnyonge mbele ya mlinzi huyo
“Samahani kaka yangu kuna kitu ninaomba nikuulize”
“Uliza fasta fasta”
“Eti huyu dada aliyekuwa akiishi humu ndani yupo wapi?”
“Kwani wewe ni nani yeke?”
“Mimi nilikuwa ni mchumba wake?”

“Unaudhibitisho gani kwamba wewe ulikuwa ni mchumba wake?”
“Ninaweza kukutajia jina lake”
“Anaitwa nani?”
“Sheila”
“Sasa wewe itakuwaje usijue habari za mchumba wako?”
“Ni hstoria ndefu ndugu yangu”
“Sasa kwa ufupi huyo demu yupo jela”
“JELAA.....!!!?”
“Unashangaa nini sasa.........? Wewe si ulitaka kujua ni wapi alipo huyo demu?”
“Jela gani?”
“Sijui yupo gereza gani ila ukweli ni kwamba amefungwa”
“Amefungwa kwa kosa gani?”
“Kaka mimi sio hakimu bwana kama unataka nenda Kisutu kaulizie watakuambia”

Wasiwasi ukaanza kunijaa mwilini mwangu na kujikuta chozi likinitoka na sikutaka nilie mbele ya mlinzi
“Kwani leo ni tarehe ngapi?”
“Wewe jamaa umevurugwa na nini hata tarehe umesahau?”
“Naoma tu nijue ndugu yangu”
“Ni terehe 15 mwezi wa sita haya hadi mwezi niemkutajia unaweza ukachapa lapa kwani bosi wanu akitoka hapa akikuta ninazungumza na watu kibarua changu kinaweza kikaota mbawa bure”

Nikajikuta nikizidi kufadhaika kwani nimiezi mine imepita tangu nilipo kutana na tatizo la kupigwa na walinzi wa uwanja wa ndage.Nikaondoka kinyone huku nikitazama tazama nyuma nikitamani nimueleze mlinzi njaa ninayo ihisi tumboni kwangu hata kama anaweza kunipatia chakula kidogo ila nikashindwa kwani tayari alishapandwa na hasira.Nikaendelea kutembea huku sijui ninapo elekea kwani mawazo mengi yanakizungusha kichwa changu kiasi kwamba ninajikuta nikiongea ongea mwenyewe.Nikakuta watu wapatao sita wakiwa wamelala kwenye maboksi nje ya baraza za maduka mengi na kujikuna mimi nikikaa kwenye moja ya baraza ambayo ukuta wake umechorwa picha za wasichana na kugundua ni saloon ya wanawake.Usingizi haukuweza kunijia na kila nilipo jaribu kuutafuta nikajikuta nikijipiga piga mwilini kuwaua mbu wanao ning’ata mwilini mwanu.Hadi kunaanza kupambazuka nikajikuta nikipitiwa a kausingizi kazito na kujikuta nikilala kwenye sakafu pembezoni mwa geti la salooni hii ya kike

Nikastukia mguu ukinigonga gonga begani nikayafumbua macho yangu na kukuta mwanga wa jua ukiwa uemshatawala eneo zima,Macho yangu yakakutana na msichana mrembo akiwa amevalia suruali nyeupe iliyo mbana vizuri na kuyafanya makalio yake makubwa kuonekana vizuri huku sura yake akiwa ameipamba kwa vipodozi vinavyo onekana ni vyagharama.Mkononi mwake akawa amezishika funguo nyingi na tukabaki tumetazamana

“Unanianaliangalia nini hembu nyanyua mindevu yako nahitaji kufnugua geti langu”
Nikanyanyuka na kusogea na kukaa pembeni kidogo,akafungua geti lake la saloon na kuingia ndani na kuanza kupana vitu vyake.Watu wengi wanapita mbele ya macho yangu huku kila mmoja akionekana kuwa na mihangaiko yake ya kutafuta chochote kwa siku hii.Nikapiga miyayo ya uchovu na kusimama ila nikashindwa kupiga hatau yoyote kutokana na kuchoka sana,Nikakaa chini na kuanza kutafakari ni nini nifanye ili kuweza kupata hata kifungua kinywa nikachungulia ndani ya saloon na kumuona dada wa saloon akiendelea kufanya usafi.

“Samahani dada ninaweza kukusaidia japo kufagia fangia”
“Kwani nilikuomba unisaidie?”
“Hapana ila nimeomba tuu kama ninaweza kukusaidia”
“Usije ukawa kibaka ukaniibia vitu vyangU humu ndani”
“Hapana dada mimi sio kibaka”
“Haya njoo unipigie deki”
Nikanyanyuka huku nikiwa na fauraha kidogo ya kuweza kupata chochote cha kula,akanipa tambara la deki pamoja na kindoo chenye maji kidogo na nikaanza kupiga deki taratibu huku nikijitahidi kusafisha kila sehemu ya salooni hiyo.Nikamaliza na kupiga deki kwenye eneo zima la Saloon

“Tayari dada yangu”
“Haya asante”
“Dada yangu naomba japo kajipesa nikanunue kifungua kinywa”
“Haaa kumbe ulikuwa unapiga deki ili nikulipe.......? Mimi nilidhani umenisaidia bure”
“Hapana mimi ninaomba japo kidogo tu niweze kupata kifungua kinywa”
Dada akafungua pochi yake na kutoa shilingi mia mbili na kunipa nikabaki nikiitazama kwa sekuende kadhaa pasipo kusema chochote na kwajinsi ya ugumu wa maisha ya Dar es Saalam yalivyo magumu kwa shilingi mia mbili siwezi kupata chochote nitakacho weza kula.

“Dada yagnu huwezi kuniongeza japo mia tatu ili iwe mia tani niweze kupata chochote tuu”
“Kaka yanu hiyo ndio hela niliyo nayo na kama unataka kifungua kinywa jana niliacha kiporo cha ubwabwa wa mchana unaweza kufungua hilo hotpot hapo juu ya meza utakiona chakula”
Sikuwa na jinsi nikalisoelea hotpot alilo nelekeza na kulifungua na kukutana na harufu kali ya ubwabwa ulio chacha ambao umepikwa na nazi huku ukiwa na maharage yake.Nikakitaama kwa muda kisha nikaanza kukila haraka haraka na kunya dada wa Saloon akibaki akiwa ananitazama kwa macho ya mshangao.Ubwabwa ukaanza kuniongea ila nikajikuta ukiwa unaelekea ukingoni kwani niliufakamia fakamia kwa haraka,nikajilamba vidole vyangu kwa utamu nilio upata kisha nikasima na kunawa mikono yangu kwa maji niliyo pigia deki

“Asante dada yangu”
Dada wa Saloon akabaki akiwa amenitazama huku akikiangalia kifua changu na kugundua kuwa anatakuwa amestushwa na mstari wa oparesheni niliyo fanyiwa
“Nakuomba utoke ndani ya Saloon yangu kabla sijakuitia polisi kwani unaonekana wewe ni jambazi”
“Kwa nini?”
“Usitake kujua kwa nini au unataka nikupigie kelele za mwizi?”

Sikutaka makuu ya kubisha na dada wa Saloon nikaondoka huku nikiwa ninajisikia vibaya kwa jinsi maisha yangu yalivyo badilika.Nikaondokoka na kuelekea nyumbani kwetu huku nikijifariji liwalo na liwe.Nikiwa njiani nikajiku nikisimama na baadhi ya watu wanaosoma magazeti kwenye kibanda kidogo na gazeti moja lina pichwa kubwa ya Sheila huku pembeni yake kukiwa na kitanzi na juu yake kukiwa na maandishi makubwa yaliyo nistua na kujikuna nikianza kutetemeka yanayo someka
“MUUAJI WA MTOTO WA WAZIRI AHUKUMIWA KIFUNGO CHA KUNYONGWA HADI KUFA”

“Haaa...!!”
Nilishanga kwa sauti ya juu na kuwafanya watu walipo pembeni yangu kunishangaa kiasi kwamba nikajikuta nikitazamana nao huku wakinishangaa,Nikataka kuondoka ila dada muuza magazeti akaniita na kunifanya nirudi sehemu alipo
“Kaka nahisi nimesha wahi kukuona sehemu?”
“Labda utakuwa unanifananisha”
“Hapana wewe ndio Eddy?”

Moyo ukanistuka na kujikuta nikitaka kukimbia ila miguu ikaishiwa ujasiri wa kufanya hivyo na kujikuta nikianza kutetemeka.
“Huyu si ndio jamaa aliyesemekana kuwa ameuliwa?”
“Ndio huyu”
Watu wakaanza kubishana mmoja baada ya mwengine huku kila mmoja akionekana kunishangaa hadi wakanizunguka
“Jamani muacheni kaka wa watu aondoke munamshangaa hadi anajisikia vibaya”
“Sasa si tunataka kujua ni nini kilicho mpata”
“Jamani hembu acheni wanga mimi ndio nimemuita sasa kila mmoja akiwa anataka kujua ni nini kilicho mpata kaka wa watu ni umbea”

Watu wakaendelea kubishana wenyewe kwa wenyewe na dada mwenye kibanda cha kuuza magazeti akanishika mkono na kunivuta pembeni na tukaingia kwenye moja ya duka lililopo pembei ya kibanda hicho na kumuomba muhisika wa duka hilo kutupa nafasi kidogo ya kuzungumza na muuza duka hakuwa na lakupinga akatupatia viti viwili na tukakaa
“Najua utajiuliza ni kwani ni nimekutoa kule kukuleta huku ila ngoja kwani nijitambulishe....Mimi ninaitwa Judith na nimuuza maazeti pale kwenye kibanda ndio ofisini kwangu na mimi nimekuwa ni msomaji mkubwa sana wa stori ianyo endelea sasa kwa huyu dada Sheila kumuua mtoto wa waziri hadi jana alipo hukumiwa kunyongwa hadi kufa”
“Ina maana Sheila ndio ameniua mimi?”
“Kaka yangu mimi wala sijajua kama huyo dada ndio muhusika ila kwa msaada ngoja nimpiie mchumba wangu ambeye ndio muandishi wa habari yako aje hapa tujuae ukweli”

Judidh akatoa simu yake na kumpigia mtu aliye dai ni mpenzi wake na baada ya muda jamaa akafika sehemu tulipo akitumia usafiri wa pipipiki aina ya boxer.Judith akampisha mpenzi wake kwenye kiti alicho kaa na yeye akasimama pembeni na jamaa akanipa mkono huku akionekana kunishangaa kwa jinsi nilivyo
“Mimi ninaitwa John ni muandishi wa habari wa gazeti”
“Nashukuru kukufahamu”

Judidh wakabaki wakiwa wametazamana pasipo kuzungumza kitu cha aina yoyote kisha John akakohoa kidogo huku akiaachia tabasamu pana mdomoni mwake na kuanza kuzungumza
“Kaka mimi ni miongoni mwa watu walio tokea kuguswa na tukio lako la kusemekana kuwa umekufa ila nikaamua kulifwatilia kina ubaga hadi sasa hivi ninaanza kupata picha ambayo itaweza kumsaidia mpenzi mpenzi wako katika kuachiwa huru.......

Nilizungumza na Sheila akanielezea kisa kizima na alidai kuwa ameonewa kwa maana tangu siku ambayo wewe ulipelekwa katika chumba cha kufanyiwa oparsheni ndio siku ya yeye alipo kamatwa na polisi kwanza akashikiliwa kwa kosa la kutaka kumuua mkuu wa jeshi ila kutoka na ushaidi kutoka kwa manesi na madaktari ukamsaidia sana Sheila kuishinda kesi ya kumjerehi baba yako ambaye alitaka kukuua hadharani”

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI

KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)