SORRY MADAM (46)
JINA: SORRY MADAM Mwandishi: Eddazaria G Msulwa SEHEMU YA AROBAINI NA SITA ILIPOISHIA... Nikaendelea kutafuta habari nyingine na kukutana na habari nyingine ikesema {“HIZI NDIZO PICHA ZINAZO MUONYESHA WAZIRI BI MAGRET AKIWA MIKONONI MWA MAGAIDI WALIO TOA SIKU KUMI NA TANO KWA SETIKALI YA TANZANIA”} NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU SASA ENDELEA... Nikaanza kutazama picha moja baada ya nyengine na kumuona jinsi mama alivyo fungwa kitambaa cheusi machoni mwake huku kichwani mwake akiwa amewekewa mitutu kama sita ya bunduki aina ya SMG .Machozi yakaanza kunimwagika baada ya kuiona picha nyingine ya mama akiwa amechorwa maandishi ya kiarabu yenye rangi nyekundu kwenye kifufua chake huku mkono mmoja wa mtu ulio valia gloves nyeusi ukimshika kwenye sehemu ya chini ya kidevu chake huku akimminya mashavu yake kwa nguvu Nikajikuta mkono wangu ukielekea kwenye kitufe cha kuzimia computer na kurudi kitandani huku machozi yakinimwagika na hasira ikawa imenikaba kifuani mwangu hadi …