SEHEMU YA TANO
ILIPOISHIA...
Mida ya saa tano nikasikia mlango unagogwa nikanyanyuka nikaitazama suruali yangu nikaikuta imekauka nikavaa na kwenda kumfungulia mtu anayegonga.NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU
SASA ENDELEA...
Nikakutana na msichana wa kidato cha pili ilikuwa ni rahisi kumgundua kwani katika shule yetu kila kidato wanafunzi wanavaa sare zao
“Shikamoo”
“Marahaba vipi?”
“Safi wewe ndio kaka Eddy?”
“Ndio”
“Madam ameniagizanikuambie kuwa amelazwa katika hospitali ya shule ila anasema usiende mpaka atakapo kujulisha”
“ Sawa hali yake ipo vipi?”
“ Sio nzuri sana kwani alijisikia vibaya akiwa anatufundisha darasani kwetu ndio akapelekwa hospitali na Madam Rukia”
“Powa mdogo wangu nashukuru kwa taarifa yako”
“Sawa ila amesema usitoke toke kwenda kutembea kwani walimu wanajua umekwenda kwenu”
“Powa..Dogo unamjua jamaa flani wa kidato cha tano anaitwa Jonh Magati?”
“Hapana”
“Powa mdogo wangu siku njema”
“Na wewe pia”
Mwanafunzi aliye agizwa na Madam Mery akaondoka na na mimi nikarudi ndani huku moyo wangu ukiwa unajilaumu ni kwanini nilimzidishia dozi Madam Mery kwani kuna mara kadhaa aliniomba kupumzika.Kabla sijaingia chumbani kwa Madam Mery mlango ukagogwa tena nikajua moja kwa moja atakuwa ni yule mwanafunzi wa kidato cha pili.Nikafungua mlango na kijikuta nikirudia rudia kuyapandisha macho yangu kutoka chini hadi juu nikimtazama jamaa mrefu aliye jazia kifua chake huku akiwa amevalia nguo za jeshi zilizo kamilika kuanzia juu hadi chini huku akiwa na nyota moja begani mwake na mgongoni mwake akiwa amevalia begi kubwa la jeshi huku akionekana kutoka safari
“Shikamoo”
“Marahaba”
Jamaa akanijibu kiufupi kisha akapiga hatua za kuingia ndani ikanibidi kumpisha mlangoni huku nikiwa ninajiuliza jamaa ni nani kwani anaonekana kujiamini sana
“Samahani kaka sijui wewe ni nani mwenzangu?”
“Unaniuliza mimi ni nani ndani ya nyumba yangu?”
Moyo ukanipigwa paaaa kama jiwe lililotua juu ya bati tena la nyumba ya uswahilini.Nikajua jamaa anaweza akawa mume wa Madam Mery mapigoa moyo yakazidi kunienda mbio pale jamaa alipoanza kupiga hatua za kwenda chumbani kwa Madam Mery kwani boxer na tisheti ya shule vyote vipo ndani ya chumba hicho na vipo sehemu ya wazi kwa mtu yoyote anayeingi lazima ataviona,na kingine kilichozidi kunipagawisha ni kitanda nilivyo kiacha kimevurugika kwani kinaonyesha hivi hivi kilikuwa ni kiwanjwa cha mechi za wakubwa
Jamaa kabla hajafunua pazia ili aingie ndani simu yake ikaita.Akaitoa kwenye mfuko wa suruali kisha akaipokea na kuanza kuzungumza mazungumzo ambayo yalianza na ndio bosi.Jamaa akanitazama kisha akatoka nje nikahisi mazungumzo yake ni muhimu sana na niya siri sana ndio maana akatoka nje huku begi lake akilivua na kuliweka pembeni ya mlango wa kuingilia chumbani kwa Madam Mery.Ikawa nafasi kwangu kuingia chumbani nikachukua kila kilicho changu huku shuka lililo changungaka nikilitoa na kulisokomeza mvunguni mwa kitanda na kuliacha godoro likiwa na foronya yake tu pasipo kuwa na shuka,Nikarudi hadi sebleni na kumuona jamaa akirudi ndani kwani mlango aliuacha wazi kidogo.Ikanibidi boxer yangu niiweke mfukoni mwa suruali yangu huku tishet yangu nikiwa nimeishika mkononi huku nikitaka kuivaa
“Dogo unakenda wapi?”
“Ehee”
”Hujasikia…! Unakwenda wapi?”
“Kununua vitafunio vya chai”
“Dogo mbona unajifanya mjanja sana?”
Maswali ya jamaa yakazidi kunichanganya akili na kunizidisia presha ambayo sikuelewa kama inapanda au inashuka.
“Mjanja wa nini brother?”
“Huendi kununua vitafunio ila sema ninakwenda kununua vitafunwa kwani vitafunio ni hayo meno yako”
“Sawa bro nimekuelewa”
“Ehee kwanza hujaniambia wewe ni nani? Nakuona upo upo tu humu ndani?”
“Mimi ninaitwa Eddy”
“Yuko wapi Mery?”
Nkaanza kufikiria cha kumjibu huku maswali mengine nikijiuliza mwenyewe na kujijibu mwenyewe ndani ya moyo wangu hadi nikapata muafaka wa nijibu nini
“Amelazwa kwenye hospitali ya shule”
“Lini?”
“Leo asubuhi”
Lengo la kumjibu jamaa kiufasaha kila swali analo niuliza ni ili akienda kumuangalia Madam Mery iwe nafasi ya mimi kuondoka katika nyumba hiyo ili nikatafute hata sehemu ya sehemu ya kuishi nikisubiria siku zangu za kusimamishwa masomo ziishe
“Powa dogo vaa tisheti yako unipeleke huku alipolazwa”
Sikuwa na ujanja zaidi ya kuivaa tisheti yangu na kumalizia kuvaa viatu vyangu na kitu kilichozidi kuniweka mpole mbele ya jamaa ni pale alipoitoa bastola yake na kutazama kama inarisasi za kutosha kwenye magazine yake na kuirudisha kiunoni bastola yake huku akionekena kuridhika na risasi zilizomo.Safari ikaanza huko sote tukiwa kimya ila mimi nimetangulia mbele kama hatua moja huku yeye akifwatia kwa nyuma.Akili yangu ikawa inanituma nipige hatua za haraka haraka na kama kuna uwezekano nikimbie kwani ichochoro vyote ninavijua katika mji huo
“Dogo nasikia kuna majambazi sana wamezuka kipindi cha hivi karibuni?”
“Kusema ukweli bro mimi mwenyewe ninasikia ila sina uhakika kivile.Ila ni juzi kuna benki pale mbele ilivamiwa na pesa zote zikaibiwa”
“Dogo subiri ninunue P.K hapa dukani si utakula?”
“Ndio”
Jamaa akaingia kwenye moja ya duka,nikamchungulia kwenye duka hilo nikamuona yupo bize na muuza duka.Nikaanza kupiga hatua za taratibu huku nikizuga zuga watu waliopo katika eneo hilo wasistukie kitu chochote ili nikifika mbali na duka hilo nianze kukimbia.Kabla sijafika mbali kidogo gafla nikastukia nikiguswa bega kwa nyuma.Nikageuka na kukutana na muuza mahindi
“Oya broo yule jamaa pale mjeda ameniambia nikuletee maindi uchague”
Nikatamani nimtukane muuzaji wa watu ila nikaona hana kosa taratibu nikaanza kuyatazama mahindi yaliyo chomekwa kwenye spoke za baiskeli zipatazo kumi na kuunganishwa katika mti mmoja.Nikachangua indi laini laini kwani sikuwa nimekula kitu cha aina yoyote tangu asubuhi.Jamaa akaja hadi tulipo akatoa noti ya elfu kumi na kumpa muuza maindi na kumuambia chenchi akae nayo
“Aisee kamanda wangu Mungu akubariki sana”
Muuza maidi alizungumza kwa lafudhi ya kichaga huku akipiga saluti na kumfanya jamaa acheke ila mimi sikuwa na hata hamu ya kuyakenua meno yangu.Tukaendelea na safari ya kwenda katika hospitali ya shule ambayo haikuwa mbali sana na shule kwani ilikuwa pia inatoa msaada wa kuwahudumia wananchi wa kawaida tofauti na wanafunzi
Tukafika hospitalini na tukakutana na Madam Rukia akiwa nje ya wodi ya wagonjwa,nikamsalimia nikabaki nikiwatazama jinsi anavyo salimiana na jamaa huku wakicheka kwa furaha na kuonekana wakifahamiana kwa muda mrefu
“Huyo mwenzako anaendeleaje?”
“Kidogo joto lake limeshuka kwani asubuhi hali yake haikuwa nzuri kivile”
“Tatizo lake ni nini haswa?”
“Maleria alikutwa na vidudu sita ndio vimemlaza.”
“Sasa mbona umekaa huku nje?”
“Nilitoka mara moja kupunga punga hewa ila twende ukamuone”
Wakati wote wanazungumza nilikuwa kimya nimetulia kama maji ya mtungini huku moyoni nikifurahia jamaa aingie ndani na mimi niondoke .Jamaa na Madam Rukia wakaanza kuingia ila jamaa akasimama na kuniangalia
“Oya dogo twende ukamuangalie mgonjwa”
“Huyu mwalifu umemtoa wapi?”
Madam Rukia alimuuliza jamaa na kumfanya atabasamu ila kwangu nikazidi kuogopa,cha kumshukuru Mungu jamaa hakulijibu swali la Madam Rukia kwani tayari tulishafika ndani ya chumba alicholazwa Madam Mery.Jamaa akakaa kitandani na kumkumbatia madam na wote kwa pamoja wakawa wanatokwa na machozi ya furaha,sikujua kinacho waliza ni nini
Wakaachiana huku jamaa akianza kumfuta Madam Mery machozi kwa kutumia kitambaa chake na kunifanya roho yangu kuanza kuhisi maumivu ya wivu
“Lucka mdongo wangu ni wewe?”
“Ehee….!”
Nikajikuta nikihamaki hata kabla jamaa hajamjibu Madam Mery nikamfanya Madam Rukia kunitazama kwa jicho kali lililoashiria kunionya nifunge domo langu
“Ndio dada yangu ni mimi kwanza pole kwa kuumwa”
“Asante za huko Pakistani?”
“Dada huko kuseme kweli si kwema ni kudra za mwenyezi Mungu miaka yote saba tuliyokuwepo kule ni kwarehema za Mungu”
“Kweli hilo ni la kumshukuru Mungu mdogo wagu kwani kila siku nilikuwa nafwatilia taarifa ya habari kujua muna endeleaje ila sikuwa ninapata majibu kamili”
“Yaani dada maisha ya kule ni bunduki mkononi wakati wote.Kuisikia milio ya risasi ni kitu cha kawaida”
“Sasa mbona walikuongezea miaka miwili ya kuishi?”
“Dada jeshini ni kufwata amri tuu huwezi kujiamulia kuwa nataka hichi hichi sitaki”
“Basi miaka mitano ilipoisha nikawa kila mara ninakwenda makao makuu yenu.Basi wakawa wananizingu hadi baba yake huyo kijana ndio alinisaidia katika kujua taarifa zenu kidogo matumaini ya kukuona yakarudi upya kwani nilidhani umefariki ndio maana wakawa wanakataa kuniweka bayana”
“Baba yake Eddy ni nani pele makao makuu?”
“Ndio mkubwa wa sasa hivi katika makao makuu yenu,Baada yule muliye muacha si aliugua kansa ya damu na kufariki”
“Ahaa sasa Napata picha unajua nilipomkuta Eddy kule kwako sura yake nikwa ninaifananisha na sura ya Mzee Godwin yaani hadi ongea zao zinafanana”
“Tena wamefanana sana.Eddy huyo ni mdogo wangu wa damu baba mmoja mama moja na tupo wawili tu kwetu”
Hadi wakati huo sikuwa ninaamini kama jamaa ni mdogo wake Madam Mery mawazo na fikra zangu zote zilipelekea mimi kujua ni mume wake na kwajinsi alivyokuwa akini hoji hoji maswali yake yaliyokuwa yakinichanganya
“Nashukuru kukufahamu bro Lucka”
“Alafu mzee wako alinipigia ule muda niliokuwa ninazungumza naye akaniambia nimuandalie mazingira kwani kesho au kesho kutwa anaweza kuja kukutembelea”
Mawazo yakarudi upya,Tena ya safari hii yakazidi kunichanganya kabisa kwani mziki wa mzee ninaujua mimi mwenyewe na hapa nilipo ndio kwanza nina siku moja tangu nisimamishwe shule kwa wiki moja
“Alafu Madam Rukia uliniambia Eddy ni mualifu?”
“Tena mualifu sana mwambie mwenyewe akuadisie”
Madam Rukia kama kawaida yake ya kuwachochea wanafunzi ndivyo alivyofanya kwa Lucka .Ikanilazimu nimuadisie mkasa mzima kuanzia wakati wa sherehe hadi waliponipa barau ya kusimamishwa wiki moja
“Huyo mwalimu aliye kuchapa fala kweli kwani mtu ni lazima kukaa hadi mwisho wa sherehe?”
Kauli ya Lucka ikamfanya Madam Rukia kunyamaza huku akionekna kuto pendezwa na Lucka kunitetea mimi
“Hata mimi nashangaa yule Sir sijui anakisa gani na mimi”
“Haya Eddy amka twende nikupeleke shuleni.Dada zangu jamani nitakuja muda si mrefu ndoja huyu raia nikamkabidhi kwa waalimu wake walio msimamisha.Alafu Rukia vipi lile ombi langu la kukuoa?”
“Nilikuwa nakusubiri ni wewe tu kupeleka posa kwetu”
Wote wakache natukatoka njee ya hospitali na kuelekea hadi shuleni.Moja kwa moja jamaa akanipeleka katika ofisi za mku wa shule hii ni baada ya kumuonyesha zilipo ofisi hiyo.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI
KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger
Email: ZephilineEzekiel@Gmail.Com