SEHEMU YA SITA
ILIPOISHIA...
“Nilikuwa nakusubiri ni wewe tu kupeleka posa kwetu”
Wote wakache natukatoka njee ya hospitali na kuelekea hadi shuleni.Moja kwa moja jamaa akanipeleka katika ofisi za mku wa shule hii ni baada ya kumuonyesha zilipo ofisi hiyo.
NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU
SASA ENDELEA...
Kwa bahati mzuri tukamkuta mkuu wa shule tena akiwa pamoja na mwalimu Kikole katika ofisi yake,akasalimiana nao kisha wakamkaribisha kukaa katika kiti ila kaka Lucka akasimama na kuniomba mimi nikae katika kiti hicho
“Samahani mzazi wa Eddy hatutoweza kuizungumzia kesi ya mwanao kwani muda wake wa kutumikia adhabu yake haujapita”
Head master alizungumza kwa suti ya upole huku akimtazama Lucka ambaye kwa jinsi sura yake alivyoiweka katika hali ya umakini nikahisi mkuu wa shule pamoja na Mr Kikole wakiogopa
“Sikuja kusikiliza kesi yake ila nimemleta aendelee na masomo sawa”
“Ila kijana wako ni mkorofi”
Mr Kikole alidakia na kumfanya kaka Lucka kumtazama kwa jicho la hasira
“Siongei na mbwa naongea na mwenye mbwa kwahiyo funga bakuli lako”
Jibu la Kaka Lucka alilomjibu Mr Kikole likanifanya nicheke na waalimu wote wakanitazama huku mwalimu mkuu akionekana kuto kupendezwa na jibu la Kaka Lucka
“Nimetoka jeshini nimeacha shughuli muhimu za kufanya na sijaja kupoteza muda cha msingi ni kumrudisha dogo darasani sawa”
Head master akatingisha kichwa akionekana kukubaliana na kaka Lucka japo Mr Kikole alionekana kukasirika
“Eddy yule mwalimu aliye kuchapa ni yupi.Nionyeshe ili niondoke naye nikamuhoji kambini?”
Moyo wangu ukaingia furaha huku nikimtazama Mr Kikole nikamuona jinsi anavyo haha haha huku akiwa anatamani kuondoka katika ofisi hiyo.Mr Kikole akaanza kunikonyeza pasipo Kaka Lucka kumuona ili nisimtaje
“Bro achana naye bwana”
“Si alikuzalilisha mbele ya wanafunzi wezako ngoja na mimi nikamzalilishe kambini”
Kusema kweli mwalimu Kikole anatetemeka hadi nikahisi kaka Lucka anaweza kumgundua ni yeye.Nikamtazama katika suruali yake nikaona jinsi inavyoanza kuchorra uwa lisilo na umbo maalumu kwani haja ndogo inaanza kumtoka hadi nikajikuta nikimuonea huruma.Kaka Lucka akatoa simu yake na kuiminya minya na kuiweka sikioni
“Ndio mkuu”
“Nimemfikisha dogo hapa shule hapa nasubiri anitajie huyo mwalimu aliyemdhalilisha na pia ningeuomba uwasiliane na mkuu wa hapa arusha ili aniletee vijana wawili na defender moja”
Mazungungumzo ya kaka Lucka yakazidi kumchanganya Mr Kikole hadi nikashuhudia haja ndoho ikianza kuchuruzika kwenye kapeti lililopo katika ofisi ya mkuu wa shule
“Eddy nionyeshe fasta fasta niondoke naye si unajua nipo kwa muda maalumu hapa”
“Kaka hembu tufanye kama umemsaehe kwani mmmmmm”
Nilizungumza huku nikicheka na kumfanya kaka Lucka kunitazama huku akinishangaa
“Dogo unacheka nini.Alafu mbona mzee unatetemeka kiasi hicho ni wewe nini?”
Kaka Lucka alizungumza haku akimpiga piga Mr Kikole kwenye bega lake cha kumshukuru Mungu hakumuangalia chini kwani Mr Kikole alikuwa amekaa kwenye kiti ambacho kanatazamana na mimi na hali yake ya hewa ilisha haribika muda mrefu.Nikamshika mkono Kaka Lucka na kutoka naye nje ya ofisi huku nikiendelea kucheka
“Eddy mbona unacheka kiasi hicho”
“Kaka nticha mwenyewe ni yule mzee pale uliyekuwa unampiga piga bega”
“Haaa sasa mbona hukuniambia nikamnyanyua nimchangamshe damu kwa kichura chura?”
“Ohhh mwenzako pale alipo kojo nje nje”
“Amejikojolea?”
“Ndio”
“Masikini mzee wa watu,nilikuwa nawachimba biti kumbe muhusika yupo pale?”
“Ndio”
Sote tukajikuta tunacheka ila mimi nilizidi kucheka hadi machozi yakaanza kunimwagika.tukaagana na kaka Lucka akurudi zake hospitali kisha mimi nikaelekea darasani.Kabla sijafika darasani kuna mwanzafunzi akaja kuniita
“Head master anakuita”
“Yupo wapi?”
“Ofisini kwake”
Sikuwa na wasi wasi,nikaanza kwenda ofisni kwa mkuu wa shule nikamkuta yupo peke yake huku Mr Kikole akiwa hayupo,Nikakaa atika kiti ambacho nilikuwa nimekalia hapo awali na kutazamana na mkuu wa shule huku miwani yake akiiweka vizuri
“Kijana nataka kukuambia kitu kimoja tu na ukiweke akilini na ukishike……..Usione kuwa tumekukubalia urudi shule kabla ya muda wa azabu yako kuisha ukazani tumekuogopa.Sasa ni hivi utafanya kazi ya kuchimba mashimo 15 ya taka hadi jumamosi adhabu yako itakapokwisha na utafyeka kila eneo la shule lenye nyasi ndefu.SAWA”
Nikamtazama mkuu wa shule kwa macho ya dharau huku nikiwa ninajiamini na kumfanya mkuu wa shule kuikunja sura yake huku akianza kuhema kwa hasira.Nikajikuta ninamuuliza mkuu wa shule swali
“Mbona hukuzungumza hivyo wakati kaka yangu yupo hapa?”
Mkuu wa shule akasimama kwa hasira huku akiuvua mkanda wa suruali yake akitaka kunichapa
“Wewe ni mshenzi kweli lala chini”
Ikanibidi kuwa mnyonge nikamuomba msamahaa mkuu wa shule adi akanielewa na tukakubaliana adhabu ya kuchimba mashimo ianze kesho asubuhi.Nikafika darasani na kuwakuta wezangu wakijisomea.Wakanishangaa kuniona ninaingia darasani
“Oya Eddy si tumetangaziwa una Sas P ya wiki moja?”
John aliniuliza huku akinipisha kwenye kiti changu ninacho kalia darasani huku yeye akihamia kwenye kiti kingine
“Kesi imeisha juu kwa juu ila nimepewa adhabu ya kuchimba mashimo……Ehee nipe stori vipi yule Salome umebonga(Zungumza naye) naye?”
“Yule dogo anajisikia sana kama vipi kamdai zile pesa zako ulizo mpa”
“Hembu acha masihara ndugu vipi aliniulizi?”
“Akuulizie wewe ni nani?,Mbaya zaidi dogo nasikia anapigwa na yule jamaa aliye cheza naye ila sasa hii dogo tunapishana kama magari mabovu NO salamu”
“Nikumbushe baadaye nikusimulie kilicho mkuta Mr Kikole”
“Huyo msen** leo pia kanichapa zamu si yake ila ana kihere here kama amenyimwa penzi na mkewe”
“Yule si kihere here ngoja nitakuambia wewe mwenyewe utacheka hadi mbavu zikuume”
Tukaendelea kuzungumza na John hadi muda wa kutoka darasani mchana ukafika.Kendele ya chakula ikagongwa ikiashiria kidato cha tano wote tukachukue chakula.Tukaelekea katika sehemu ya kuchukulia chakula na tukapanga foleni kama walivyo panga wanafunzi wengine wa kidato chetu tulio wakuta
“Samahani ninaweza kukaa mbele yako?”
Nikageuka na kumkuta ni Salome ndio anaye niongelesha,nikasogea kidogo akapita mbele yangu kwa jinsi mstari wa chakula watu walivyo banana nikajikuta karoti yangu iliyoanza kusimama ikigusa makalio ya Salome na kumfanya ageuke geuke nyuma na kuniangalia usoni huku akitabasamu akionekana akifurahi kwa jinsi ninayo mgusa gusa na koroti yangu katika makalio yake yaliyo makubwa kiasi
Mstari wa chakula ukaanza kusogea taratibu kuelekea mbele huku mimi na Salome tukiwa kimya hakuna aliye msemesha mwenzake.Ikanibidi niukate ukimya
“Salome leo tunaweza kuonana?”
“Saa ngapi?”
“Kabla ya prepo”
“Sawa nitaangalia kama kuna uwezekeno”
“Nitashukuru sana.Ila vipi shemeji hajambo?”
“Hajazaliwa bado”
“Acha kuniongopea”
“Kweli shem wako bado hajazaliwa”
Kabla sijazungumza kitu chochote akaja kaka mkuu sehemu tuliyo simama katika mstari na kunifanya nikae kimya
“Ahaa Salome mbona umepanga mstari si ungepita mbele?”
“Naogopo yule prefect(kiongozi) anayesimamia pale mkali kama nini?”
“Twende nikupitishe wewe ni mtu mkubwa bwana hapa shule”
Jamaa akamshika mkono Salome na kumtoa kwenye mstari na kuondoka naye kitendo ambacho kimenikera kupita maelezo kwani kaka mkuu kanipeperushia ndege wangu.Nikiwa najifikiria kupita na mimi mbele ili niwahi kuchukua chakula na kumfwata Salome ili tuzungumze vizuri jamaa mmoja wa kidato cha tano akaja sehemu niliyo simama
“Oya Eddy unaitwa na mwalimu wa nidhamu”
“Yupo wapi?”
“Ofisini kwake”
Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio kwani katika waalimu ninao waogopo katika shule hii ni mwalimu wa nidhamu ambaye anaonekana kutokuwa na masihara na mwanafunzi wa aina yoyote.Nikampa vyombo vyangu John anishikie huku nikianza kujichunguza kuanzia miguuni hadi kwenye shati.Sikuwa nimevaa sare za darasani kwani tangu juzi sikwenda bwenini zili po nguo zangu.Niaanza kuelekea katika ofisi za nidhamu.Maigo ya moyo yakaanza kunienda mbio zaidi baada ya kuliona gari la baba aina ya Hammer wanayo tembelea wakuu wa jeshi huku dereva wake akiwa ndani ya gari hilo.Nikaenda kumsalimia dereva kutokana nina juana naye,
“Shikamoo brother P”
“Marahaba vipi Eddy?”
“Safi vipi home munaendeleaja?”
“Tunaendelea vizuri vipi masomo?”
“Safi,vipi mzee mbona kaja fasta fasta kwema”
“Kwema yupo huko ofisini kwenu’’
Nikajaribu kumchunguza dereva kuniambia juu yam zee kama amekasirika au laa ili niweze kujiandaa kwa chochote kwani mzee(baba) kurusha ngumi kwake ni kitu cha kawaida sana.Nikaachana na dereva na kwenda ofisini.Nikamkuta baba akiwa na Mwalimu wa nidhamu Mr Karata wakiwa wanazungumza maswala yao huku wakicheka .Nikawasalimi kwa pamoja wakaniitikia huku sura zao zikiwa na tabasamu
“Oohh my first born how you?”(Ooh mtoto wangu wa kwanza hujambo?)
“Am fine dady”(Nipo sawa baba)
“Why your looking so scare what’s wrong of you?”(Mbona unaonekana kuogopa,Una tatizo gani?)
“Nothing dady”(Hakuna kitu baba)
“Ok be happy my son”(Sawa kuwa na furaha mwanangu)
Nikaweka tabasamu usoni mwangu huku nikiwa ninashangaa leo baba anafuraha na mimi wakati katika vipindi vyote alivyokuwa akinitembelea shuleni alikuwa kauzu hadi waalimu wakawa wanashangaa ni maisha gani ambayo tunaishi na baba yangu na sheria nyingine ya baba akianza kuzungumza kingereza ni lazima na mimi nimjibu kwa lugha hiyo hiyo
“Hapa nilikuwa nazungumza na mwalimu wako akinielezea kisa chako cha kuvunja fimbo ya mwalimu”
Nikakaa kimya huku nikimtazama mwalimu wa nidhamu huku kimoyo moyo nikimlaani ni kwanini amemuadisia baba yangu juu ya mkasa huo kwani hashindwi kunichapa mikanda mbele yake
“Mwanangu usiwe mkorofi sawa first born”
“Sawa baba nimekuelewa”
“Mimi nilikuja kukutembelea mara moja kwani wiki ijayo ninakwenda Iraq kwa ajili ya kazi maalumu huko tunakutana wakuu wa majeshi wan chi mbali mbali nitakaa mmwaka mmoja na nusu”
“Sawa na mama anarudi lini?”
“Mama yako anarudi kesho kutwa”
“Atakuja huku kunitembelea?”
“Nitamwambia aje kukutembelea ila cha msingi hakikisha unasoma kwa juhudi matokeo yako mwalimu hapa nimempatia Email yangu kila ripoti yako ya masomo atakuwa ananitupia…Sasa kazana na kusoma sawa?”
“Sawa baba”
Baba akatoa pesa na kunipa laki tano za matumizi ya kipindi chote ambacho nitakuwepo shule.Mwalimu wa nidhamu akaomba anishikie laki nne ili kuepuka kuibiwa,Sikuwa na ubishi nikampatia laki nne na nusu nikabakiwa na elfu hamsi nikachananya na pesa nyinine nilizo kuwa nazo. Baba akanipa simu mbele ya mwalimu wa nidhamu japo sheria za shule haziruhusu mwanafunzi kuwa na simu
“Sasa Eddy uwe makini na simu yako ili waalimu wengine wasiione wakakupokonya kwa mimi ninakuruhusu kuwa nayo”
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI
KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger
Email: ZephilineEzekiel@Gmail.Com